Mr President jakaya mrisho kikwete: BE CAREFUL!:
Ningekuwa na muda ningekueleza mengi sana. Muda wangu ni kidogo sana ndiyo maana nashindwa hata kupost mambo mengi kuhusu taifa hili hapa JF. Ninatuma post hii si kwa lengo la kukutisha. Lengo ni kukukumbusha uwe makini ili usijefanya uamuzi wa hovyo na kuliingiza taifa katika machafuko na kuharibu timetable za watanzania. Machafuko ndiyo tunayoyakwepa lakini si wewe (I have to tell you the truth because you are not my breadwinner at all).
Mtandao
Ninachozungumzia hapa ni kundi kubwa na hatari linaloaminika kuongozwa na Edward, Rostam, Othman, Apson, Karume na Shein na Mkapa. Ninakufahamu vizuri sana na ungekuwa uwezo wako, hawa wote ungeweza kufanya uwezalo ili kumweka madarakani mtu unayemtaka kwa maana ya Asha au Nahodha. Huu ni mtandao unaofanya kazi kwa umakini wa hali ya juu sana. Ukitaka kuamini, jiulize swali la kipuuzi sana kuwa kwanini kila plans unazofanya (zisizo na faida) kwa kundi hili zote zimefail?
1. Shein ni nani?
Nataka nikukumbushe ''issue'' ya Omar Juma. Huyu alikuwa threat kubwa kwa kundi lenu kwa ajili ya 2005. Mtandao wake ukibebwa na Mkapa ulikuwa ni hatari sana. The only way ilikuwa ni ''kumwondoa'' na hilo liliwezekana. Siku nikiwa na muda nitaeleza mchezo wote ulivyofanyika. Wakati jina limeletwa tukiwa hotel moja maarufu hapa Dar, nakumbuka hukuweza kumfahamu Shein wala kulitamka jina lake vizuri. Ulikosea mara tatu kulitamka. Tukacheka wote. Hatimaye Shein akawa makamu wa rais.
Baada ya wenzako kukuweka madarakani (mgombea ndani ya CCM), kosa ambalo Shein hataweza kukusamehe katika maisha yake (Mimi sio Mungu, kwani anaweza kukusamehe vilevile) ni pale ulipo-attempt kumfanya Zakhia kuwa makamu wa rais. Asingekuwa Edward, Rostam, Mkapa na Karume, leo hii Shein angekuwa mwenyekiti wa TPDC au TANAPA!. Kitendo cha Shein kuletwa na kundi hili, kutetewa na kundi hili achilia mbali kushawishiwa na kundi hili agombee urais wa Zanzibar ili kummaliza nguvu Nahodha chaguo lako kinamfanya awe mtiifu kwao kuliko hata kwa Mwanamwema!. Unafahamu vizuri Shein alivyoshinda urais Zanzibar, rafiki zako walikuchezea akili wakikuambia kuwa wamemleta Shein ili kupunguza kura za Bilal na ulipomkubali Shein wao wakaenda kumpigia Bilal kampeni wakijua kazi ya kumweka Shein imekamilika. Baada ya hapo uliendelea kumng'ang'ania Zakhia kuwa makamu. Mkapa akishirikiana na Rostam (ambaye alikuwa akim-install Bilal kuwa makamu huku yeye akiwa South Africa kuangalia World Cup) walimweka Bilal hapo alipo.
Shein hakushinda uchaguzi Zanzibar. Kilichofanyika ni Mkapa, Rostam, Karume kumhonga pesa za kutosha sana Maalim kupitia kwa kijana wao hatari sana Jussa (kumbuka huyu aliletwa na Rosatm ili umteue awe mbunge). Today, umeshindwa kumweka mtu wako Zanzibar na makamu wa rais Muungano. Walichoweza kufanikisha ni kuiteka Zanzibar yote (Bilal na Shein). Nakukumbusha ya kwamba, ili uwe mgombea kupitia CCM, unahitaji Zanzibar na 'Lake Zone'. Kule 'Lake Zone' wamekushinda. Hilo unalifahamu vizuri. Hii ndiyo maana Wanzanzibar wamekutesa sana ndani ya CC iliyopita. Ili kukuonyesha kwamba hufai, Shein kampa udaktari wa heshima ''Baba yake'' mdogo Karume. Ninafahamu jinsi unavyojikosha kwa Anne kwa kumpa nishani ili kusiwe na vote of no confidence mwakani hasa kwa sakata la Richmond na Twiga. Napenda kumhakikishia Anne ya kwamba that's a strategy anayoitumia Mugabe ya kuwamaliza watu. JK ameiiga huko. Naomba Anne uwe makini sana. Waweza kufa kwa ''presha'' usipoangalia.
2. Karume ni nani?
Huyu alipigiwa kampeni kubwa sana na Edward na Rostam mwaka 2000 licha ya CCM Zanzibar kumkata jina lake. Kwa hili Karume hawezi kuwasahau hawa jamaa mpaka anakufa. Karume alikupinga Butiama. Yeye, Edward na Rostam wakaenda ku-design ''mwafaka'' wao wanaoujua ambao leo hii unafanya kazi Zanzibar. Nataka nikukumbushe mara ya pili kuwa Jussa aliletwa kwako na Rostam ili umpe ubunge. Think twice! Karume ndiye rais aliyeleta maendeleo makubwa Zanzibar. Shein will do more than what Karume did. Usishangae ukisikia Karume kuwa makamu wa Lowassa 2015!. Karume ana msimamo. Hayumbi na bahati mbaya sana hakuogopi.
Karume na Jussa ni wamoja na wanafahamiana vizuri sana kuliko wewe unavyofikiri. Kundi hili linao uwezo wa kuvunja Muungano muda wowote linaoutaka na kuanzisha serikali tatu na baada ya malengo kutimia likaanzisha serikali moja!. Ni vigumu kuelewa ni yapi majukumu ya Karume ndani ya hili kundi na nani kampa majukumu hayo na wapi kiburi cha Karume kimeegemea. Ni swala la historia ndefu sana ambayo nitaiunganisha vizuri baada ya kumchambua Rostam ambaye nitachukua muda mrefu kumchambua kuliko mwingine yeyote katika kundi hili.
Hata hivyo Karume anaweza kweli kusahau mchezo mliotaka kumfanyia wewe na Nahodha kuhusiana na mwafaka kabla ya kipindi chake kuisha na kupelekea kumtishia Nahodha nafasi yake ya Waziri Kiongozi? Nahodha akabaki analia wakati wewe umemruka tayari baada ya kuona umezidiwa nguvu?. Mr President, unawafahamu waliokuwa nyuma ya mchezo huu? Basi hao hao kwa miaka mingi wangekwishakumaliza lakini Edward alionekana "kukupenda" zaidi na yeye amekuwa akiwawekea ngumu yaani kukulinda lakini kwa bahati mbaya sana, amewakubalia hivyo kufanya game kuwa kali. Edward anaweza kukulinda baadaye. Lakini hutaweza kufanya biashara yeyote ile na waweza kubaki na "njaa" kali sana baada ya kustaafu. Game hii ni hatari kwasababu lazima imuweke Karume kwenye nafasi za juu za uongozi wa taifa hili 2015. Mh Rais naomba umuulize Mama Maria Nyerere akwambie vitisho alivyopewa na Karume na Mkapa kuhusiana na mwanaye makongoro wakati wewe unaendesha kikao cha NEC. Hata hivyo ni vizuri ukajiuliza swali la kitoto kama hili: Je ni kwanini Karume na wenzake walikushinikiza sana umteue Tom Apson kuwa mbunge wao wakikudanganya kwamba Tom amefanya kazi nzuri ya kuiba siri za Apson na malecela na wengine? Think twice Jakaya!.
3. Rostam ni nani?
Licha ya kuwa rais wa nchi hii tena Kamanda mkuu wa vyombo vyote vya usalama, umeshindwa kumfahamu Rostam kwa undani zaidi. Nikiri kwamba, bado hujamfahamu Rostam vizuri na sidhani kama vijana wako wanamfahamu vizuri. Kabla sijamwelezea vizuri, naomba nikukumbushe kitu kimoja. Hivi ilikuwaje mwaka 1995 wakati kambi yako inaomboleza baada ya kushindwa urais, Rostam alionekana kwenye sherehe ya kumpongeza Mkapa tena akiwa na Mkapa na kwa mazungumzo marefu sana?. Je aliwasaliti nyie washirika wake?.
Nikiri tena kuwa, Rostam aweza kuwa mtu hatari, mwenye akili ya haraka sana lakini mwenye kuzichezea kwa akili ya juu sana siasa za Tanzania kuliko mtu yeyote aliye hai niliyeweza kumfahamu hapa Tanzania. Huyu akiwa pale LSE UK, alijenga urafiki mkubwa sana na binti wa mkubwa mmoja na muhimu katika Tehran (siasa za Iran). Haikufahamika kwa haraka ni nini alichokuwa akikitafuta kwa huyo binti na nani alimtuma ajenge huo urafiki ghafla kiasi hicho. Hili ninalolisema kwa sasa hata Lowassa hawezi kulifahamu, si wewe peke yako.
Ni vigumu kuamini kuwa, Serikali ya Marekani imegharamia masomo ya Rostam LSE (baada ya hii task) na hii serikali kupitia Prof mmoja anayefundisha chuo kikuu kimoja UK huku akiwa ni mfanyakazi wa CIA iliweza kufanikisha urafiki mkubwa wa Rostam na huyu binti huku yeye (Prof) akiwaachia maelekezo vijana wa CIA baadhi kum-monitor Rostam na hatimaye urafiki ukawa mkubwa sana kiasi kwamba ukaweza kumfanya Rostam akubalike na Tehran.
Kwa udhamini na wito kutoka serikali ya US, Rostam akawa anakwenda mafunzo mahsusi ya ki-usalama marekani na huko alikutana na watu wengi sana muhimu wakiwemo wamiliki wa Symbion. Kwa kukudokezea tu, pesa za Kagoda ni msamaha wa deni lililofanikishwa na ushawishi wake pale Tehran. Kwa bahati mbaya sana hata Mariam (mke wa Rostam) hakuufahamu uhusiano ule akifikiri ni mapenzi mpaka pale alipojua vinginevyo (ingawa hawezi kujua behind the scene kuna nini). Malengo ya Marekani na huu urafiki (Rostam-Tehran) bado yako palepale na nilipokutana na rafiki yangu (huyu aliweza kufanya kazi nzuri sana na Shah Riza kule Middle East) wa siku nyingi sana pale Boston, akanihakikishia kuwa lengo lilipangwa kutimia 2018 au 2022 hivi!. Ni hatari sana na mtandao wa Rostam na wenzake unaweza kukufanyia lolote watakalo kama usipokuwa makini!. Kule Saudi Arabia na sehemu nyinginezo ameweza kutumiwa sana na hawa mabosi wake kwenye masuala ya biashara.
Rostam anafanya kazi kubwa na nyingi za kibiashara na kisiasa na CIA kama agent wao muhimu sana Afrika huku yeye akisaidiana na mtandao wa CIA kule South Africa na ku-control sehemu kubwa Afrika Mashariki na Kati na sehemu nyingine za afrika ambazo US itakuwa na maslahi nazo. Mambo machache aliyoweza kufanikisha ni pamoja na kumfikisha Raila hapo alipo, mikataba ya kimaslahi na Salva Kiir achilia mikono ya Rwanda na Uganda kule Congo, Madagascar, mwafaka wa Zanzibar, kujivua gamba though kosa mojawapo ni wewe kukosea implementation hivyo kum-cost na kupelekea US kumwambia ajiuzulu ubunge na kuacha siasa kitu kinachomfanya afanye siasa mara kumi ya aliyokuwa akiifanya awali.
Mr President, muulize Othman akueleze ukweli kwa kuwa hili alilifahamu ingawa hajui ni kwanini lilitokea. Kumbuka vizuri wakati Bush amekuja Tanzania. Kule Arusha, viongozi wa makampuni makubwa yanayomiliki migodi mikubwa ambayo Bush, US na CIA ina maslahi nayo kutoka karibu kila kona ya dunia walikusanyika na walielezea ni kwanini biashara haiendi vizuri. Hakuna mtanzania yeyote Yule hata Deo aliyehudhuria except Rostam. Nani alimwalika na alihudhuria akitokea wapi?! Pale waliazimia mambo makubwa na ya hatari sana. Rostam anajua vizuri what happened na maazimio yale yalilenga nini.
US imeona wewe huna shida nao kabisa kwa kuwa nchi umeweza kuiendesha vizuri sana na bado una mvuto wako kwa wananchi na hii si hatari kwa maslahi yao hasa mafuta ya Zanzibar ambayo imeshayalia timing kwa maana ya kwamba imeshirki kikamilifu kucheza game ya Rostam-Jussa-Karume-mkapa kwa haraka sana. Nimekwambia kwamba, Muungano waweza kuvunjwa na baada ya muda ukarudi tena nakuwa serikali moja. Jiulize ni kwanini lowasa anakudharau kiasi hicho?. Hicho kiburi anakitoa wapi?. Mr President, usikurupuke, cheza karata vizuri!.