juzi juzi tu mtoto anayetegemewa kuwa rais wa hili taifa amelalamika kuwa kuna mbinu za kumuua mzazi wake, hivi huyo mzazi angekuwa na nguvu zote hizi malalamiko yangetoka wapi. lowassa hawezi kuwa rais wa JMT bila msaada wa kikwete, halafu 2015 ni mbali mno, kuna mengi tu yanaweza tokea, kila mtu anatumai kufika huko, mwenye uhakika wa kufika huko hakuna.
Mkuu Mkandara, kwa hiyo na mimi umeniweka kwenye kundi hili la "nani hapendi kuweka vogue barabarani na hekalu by the beach?, Get Rich or Die Trying!"Weee Pasco mhuni sana yaani... uwe karibu unukie manukato au sio?.. unajua kusema kweli una point nzuri sana maana maisha ya leo na umaskini huu unapopiga kelele za mlangoni au kunadi salaa alfajiri ambyo kwao ni usiku wa manane unawachosha waliolala.. Kubakia peke yako inakupa wakati mgumu sana pengine kweli inabidi watu tujipange nyuma ya Lowassa maana kufa maskini nako kazi!!!! Haaa! haaa! haa!
Hutaki Unaacha!
Hapo kazi ipo 2015 kuna kila dalili za umwagikaji damu ktk nchi hii
Huu mzunguko mbona nimeshindwa kuuelewa? Aliyesoma akaelewa ajaribu kunisaidia ili na mimi nisiachwe nyuma. Nini chimbuko la waraka huu?
Tiba
OOH my dear friend EMT, how wrong you are and it definitely looks like you are forgetting one very important point, this is Bongo !
Kigarama, mmiliki halisi wa Richmond yupo, sio Rostam wala sio Lowassa!. Hata Adam Gire aliyeisajili ni boya tuu!. Rostam na Lowassa wao waliingia ili kumnusuru mmiliki halisi, na ndipo ilipojigeuza Dowans, RA na EL wakatia mkono!, ukumbuke wao wametia tuu mkono, baada ya tume ya Mwakiembe, Zitto alipendekeza serikali iitaifishe, watu walipinga sana, sasa imechange hands to Simbion na inaendelea na kazi, na mmiliki ni mmiliki tuu, juzi, (richmond), jana (dowans) na leo (simbion)!.RA naye tunaambiwa kwamba anamiliki mali nyingi lakini si kwa jina lake. Hata Richmond ina mikono yake.
Hii inatoka kule kwenyewe kunako!. Kuna vijana wa Othman, wamelishwa sumu, sasa wanatapika nyongo humu ili madhara ya ile sumu yawapungue!hata kama ni stori ya kutungwa ina chembe ya kaukweli fulani kumbukeni kuwa hata wale watunzi wa riwaya maarufu huwa wana ujumbe fulani kwa hadhira
Heee! vogue ngapi unataka zijipange...lakini nadhani nakusoma vizuri sana kuliko wengi wanavyokuchukulia. Ni kaukweli kanakouma na kama vile unasema - Jiandaeni na mafuriko wabishi sisi tunapinga tu oooh haiwezekani kuhama! tuende wapi..Na humalizia kwa kusema shauri yenu mimi natangulia juu mlimani..Mkuu Mkandara, kwa hiyo na mimi umeniweka kwenye kundi hili la "nani hapendi kuweka vogue barabarani na hekalu by the beach?, Get Rich or Die Trying!"
Heee! vogue ngapi unataka zijipange...lakini nadhani nakusoma vizuri sana kuliko wengi wanavyokuchukulia. Ni kaukweli kanakouma na kama vile unasema - Jiandaeni na mafuriko wabishi sisi tunapinga tu oooh haiwezekani kuhama! tuende wapi..Na humalizia kwa kusema shauri yenu mimi natangulia juu mlimani..
Haya wingi ndio linafunga hivyo!
Mchunguzi nenda kwenye PM nikueleze kwanini namkubali Lowassa, tujadiliane huKo mpaka mwisho. achana na magazeti kaka na mtandao.
hivyo ni muhimu sana kuangalia ni gari gani unadandia ili ufike hiyo safari,
Karibu sana Mkuu Mkandara, kwenye gari letu linaloendeshwa na dereva bingwa mzoefu, Edward Lowassa