Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 1)

Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 1)

Pamoja na umuhimu wa mjadala huu kwetu kama vijana, lakini ni dhahiri kabisa kwamba wanasiasa wote hawa miaka 15 - 20 ijayo watakuwa wastaafu wakipumzika na familia zao, huku vijana wengi humu tukiwa bado hata kufikisha miaka 50, na wengine wengi tu chini ya miaka 40. Kwa mtazamo wangu ambao unaweza kuwa hafifu sana, ni muhimu tujikite katika mjadala huu huku tukitambua hilo, na muhimu zaidi, kwa vision ya miaka 15 - 20 kutoka sasa, ambapo na sisi tutakuwa mbioni kuwaachia watoto wetu na wajukuu zetu taifa lililo imara. Ni muhimu sana kwa vijana sasahivi, kuchagua upande sahihi wa historia ya nchi hii 2011 and beyond, kuliko kuja juta na kusaga meno baadae kwa kujikuta walichagua the wrong side kwa uzembe, tamaa, ama uwoga.

Jukumu la kuamua upande upi ndio upande ndio the right side of history ni wa kijana mwenyewe, mmoja mmoja, bila ya kuingiliwa na mtu yoyote kwani huo ni uhuru na haki ya kila mtu. Zaidi ya hivyo, ni kukumbushana tu kwamba, unlike safari ya hawa wanasiasa tunaowataja taja humu ambao safari yao kisiasa itafikia ukiongoni miaka sio mingi kutoka sasa, wakiwa wastaafu HAI au HOI, safari yetu sisi kama vijana bado ni ndefu sana, na ile ya watoto na wajukuu wetu ndio ndefu zaidi, na itategemea tunafanya maamuzi gani leo i.e. between 2012 and 2015.



Mchambuzi, hii ni take home message nzuri. Jambo moja muhimu ni kuwa lazima tuachane na hii culture ya impunity. Lazima tumshukuru "mletahabari" ili written evidences zihifadhiwe kwenye archives na hawa watu wapate haki yao inavyostahili kuliko kuwaaacha wastaafu huku familia za victims wao zikiteseka na vinyongo. Mfano mzuri ni organized killings and near death ya balozi wetu aliyekuwa SA na wengineo. Wewe binafsi huoni kuwa kuna umuhimu wa justice kwa yeyote aliyehusika?
 
Watanzania,

Hivi kweli mnapenda story za udaku namna hii?.

Kila siku huwa nasema na kusisitiza anzeni kufikiri kwa kutumia ubongo wenu acheni magazeti na mitandao kuwafikiria.

Ndio maana mnalialia kila kukicha maisha magumu, hayawezi kuwa raisi kama mnaamini story ya kutunga kama hiyo hapo juu.

wewe usiwe mvivu wa kufikiri, acha amalize story yote then great thinkers tu join it together and arrive into a logical conclision, ila hata mimi I can clearly see logical and connected trend in this thread, lets wait and see!! patience pays!!
 
Kwa hali ya sasa, wa kufanya maamuzi magumu sio viongozi bali vijana, na hapa sina maana ya UVCCM bali vijana wa Tanzania, haswa wale wenye bahati ya elimu na upeo, kuwaongoza wenzao waliokosa bahati hiyo, katika uelewa wa mambo; Ni bahati mbaya sana kauli mbiu muhimu kama hizi za 'maamuzi magumu', 'ukosefu wa ajira kwa vijana ni timing bomb', n.k. huwa tunaletewa na viongozi badala ya chimbuko lake kuwa ni vijana wenyewe, ikiwa sehemu ya msimamo na dira ya vijana; Badala yake, vijana tumekuwa tunashirikiana kwa kauli tu, huku tukielekeza nguvu na akili zetu zote kwenye ushabiki na ufuasi wa pande mbili au tatu zilizopo badala ya vijana wenyewe kutengeneza upande wa nne, kwa manufaa yetu wenyewe.
Afadhali umefikiri ktk angle nyingine kabisa! Umetoa suluhisho na ndivyo tunapaswa kufanya.mtoa habari ametudokeza kuwa Umma hauwezi kumzuia Lowasa kwenye masanduku ya kura bali maandamano tu! Thread hii imetufanya kufikiri tofauti kabisa.Clean system imekufa,waadilifu wachache waliobaki ndio hawa walioamua kuhamia mitaani kwa wananchi ili wajue ukweli wasihangaike na kura! Tuna kazi kubwa kuushinda mtandao huu nafikiri ndio maana Dr Slaa kidogo amekuwa wa baridi maana hakuna wa kumwamini tena! Umesikia ya Zitto na Mbowe(msome vizuri Mtoa habari!) Si hatari hii mkuu?
 
Kwa hali ya sasa, wa kufanya maamuzi magumu sio viongozi bali vijana, na hapa sina maana ya UVCCM bali vijana wa Tanzania, haswa wale wenye bahati ya elimu na upeo, kuwaongoza wenzao waliokosa bahati hiyo, katika uelewa wa mambo; Ni bahati mbaya sana kauli mbiu muhimu kama hizi za 'maamuzi magumu', 'ukosefu wa ajira kwa vijana ni timing bomb', n.k. huwa tunaletewa na viongozi badala ya chimbuko lake kuwa ni vijana wenyewe, ikiwa sehemu ya msimamo na dira ya vijana; Badala yake, vijana tumekuwa tunashirikiana kwa kauli tu, huku tukielekeza nguvu na akili zetu zote kwenye ushabiki na ufuasi wa pande mbili au tatu zilizopo badala ya vijana wenyewe kutengeneza upande wa nne, kwa manufaa yetu wenyewe.

Mtoa Habari amesema dawa ni UMMA tu ndio itaweza kuwatoa hawa wazee. Lazima tufahamu kwanza mpaka tumefikia hapa tulipo tatizo hasa ni nini? Binafsi naona tatizo hasa ni umaskini uliopitiliza kipimo na uchoyo/ubinafsi.Huo umechangiwa capitalism and globalization. Kila mtu anadream kuwa kama maisha mazuri kupindukia ndani ya kipindi kifupi. Hapo ndio tunadondokea kwenye mtego wa EL, RA & Co kiurahisi. Inasikitisha kuona vijana kama January, Zitto na vijana wengine wengi wakiwa wamenasa tayari. Joining Solution moja nionavyo mie ni kuwa nyie vijana mliondani ya system kudrive change from within kwa kuwa mnafahamu hizo kura zinaibwa vipi. Tukisolve hilo nadhani utakuwa ni mwanzo mzuri! Ni hayo tu kwa sasa
 
@ Mtoa Habari,

Vipi issue ya Prof. Mwaikusa kudaiwa kumuona/kukutana na Balali (sijui kwa bahati mbaya au kwa deisgn) huku USA na kupeleka kifo chake, je ni kweli tetesi hizo? Na ni nani mhusika na kifo hicho?
 
Hata mimi nilikuwa namkubali sana Dr OA Juma ambaye Mwalimu alimsifia sana kwa kutokuwa na uchu wa madaraka. Kama kweli alifanyiwa hivi utawala huu utakuwa na mwisho mbaya sana. Linalonishangaza ni kuwa wote waliohusika na Urais wa JMK wanadhani wataendelea kuwa marais tena ifikapo 2015. Na kuna watu humu wanakuwa kama hamnazo vile kwa kutokuona, kusikia wala kusoma madudu kama haya yaliyowaweka watu hawa madarakani.
KATIBA MPYA ihakikishe inatupatia mfumo bora kabisa wa kumpata RAIS wa NCHI hii. Vinginevyo tujiandae kuchinjana tu huko tuendako.
 
Hata mimi nilikuwa namkubali sana Dr OA Juma ambaye Mwalimu alimsifia sana kwa kutokuwa na uchu wa madaraka. Kama kweli alifanyiwa hivi utawala huu utakuwa na mwisho mbaya sana. Linalonishangaza ni kuwa wote waliohusika na Urais wa JMK wanadhani wataendelea kuwa marais tena ifikapo 2015. Na kuna watu humu wanakuwa kama hamnazo vile kwa kutokuona, kusikia wala kusoma madudu kama haya yaliyowaweka watu hawa madarakani.
KATIBA MPYA ihakikishe inatupatia mfumo bora kabisa wa kumpata RAIS wa NCHI hii. Vinginevyo tujiandae kuchinjana tu huko tuendako.

Chinjaneni wenyewe. Ukianza hivyo ujue umefikia mwisho (etc) - End of Thinking Capacity!.
 
Pasco,

Mtandao wa ENL, RO, una nguvu kubwa sana, kifedha na kimkakati, ndani na nje ya nchi, kwani hata mwaka 1995, Kikwete alimshinda Mkapa Chimwaga chini ya mwenyekiti wa mikakati, ENL, licha ya ENL kuchafuliwa jina na Nyerere kama fisadi.
Je, Nyerere alimuonea ENL? Ni wazi kwamba ENL alikuwa na utajiri mkubwa sana na wa ghafla, na Nyerere angefanya yaleyale kwa mwana CCM yeyote ambae angekuwa na hali hiyo ya kifedha, kitu ambacho Nyerere aliona hakiendani na maadili ya uongozi. ENL alikuwa na utajiri mkubwa katika kipindi kifupi – 1989 – 1995. Ni mwaka 1989 ambao ENL aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa AICC Arusha. Kabla ya hapo, alikuwa na maisha ya hali ya chini sana akitokea Chuo Kikuu miaka ya mwisho ya 70, ambapo baada ya kipindi kifupi jeshini, aliamua kuingia kwenye siasa na kuwa Mbunge wa Taifa kupitia viti vya UVCCM mwaka 1985, na mjumbe wa NEC UVCCM (1987). Huko ndiko alipokutana na Kikwete, nae akiwa mbunge wa taifa (uvccm) na Mjumbe wa NEC UVCCM. Tofauti na sasa, miaka ya nyuma, hata wanaume walikuwa wakigombea nafasi hizi. Lakini nafasi hizi hazikuwa na maslahi yoyote kifedha zaidi ya kujijenga kisiasa.

Tangia amalize Elimu yake Chuo Kikuu DSM miaka ya katikati ya 70, ambako pia ndiko alipokutana na Mkewe Regina, na baadae kwenda Nottingham, Uingereza kwa elimu ya juu zaidi mwishoni mwa miaka ya 70, ENL hakuwahi kushika wadhifa wowote mkubwa au kiutendaji ndani ya serikali. Kabla ya mwaka 1985, ENL aliwahi kuwa Katibu msaidizi wa CCM mikoa ya Shinyanga (ambako mtoto wake Fred ndiko alipozaliwa) na pia kushikilia nafasi hiyo hiyo Arusha miaka ya mwanzo ya 80.
Katika kipindi cha 1980 hadi mwaka 1988, ENL hakuwa anamiliki nyumba ya aina yoyote, na alikuwa na gari moja tu aina ya Volkswagen namba TAP 180, kwa miaka mingi sana. Nyumba ya kwanza ya ENL, mbali na ya kwa wazazi vijijini ilikuwa ni flat ya Msajili wa Majumba pale Sanawari Arusha kama mpangaji, akiwa CCM Arusha. Miaka michache baadae, alibahatika kupata nyumba nyingine ya msajili kama mpangaji, mtaa wa mahando, Masaki Dar-es-salaam. Mambo yakaanza kubadilika kuanzia Mwaka 1989 baada ya Mzee Mwinyi kumteua kuwa Mkurugenzi wa Kitu cha kimataifa cha mikutano Arusha (AICC). Nafasi hii aliitafuta mwenyewe. Mwaka 1990, aliteuliwa kuwa Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, baada ya Waziri Mkuu mteule (1990), John Malecela, kumuomba Mzee Mwinyi. Mawaziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu mara nyingi wanapatikana baada ya Rais kushauriana na waziri mkuu.

Mwaka 1991, Mwinyi akamhamishia ENL Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo Mijini, na hapo ndipo alipokutana na Haruna Masebu kama Mkurugenzi Mkuu wa NHC, na kuanza urafiki mkubwa sana wa kikazi na kimaslahi. Mwaka muhimu kukumbuka ni ule wa 1992 ulioruhusu viongozi wa CCM na Serikali kumiliki mali. Kufikia mwaka 1994, ENL akawa mmoja wa viongozi wa kizazi kipya kuwa na nyumba za kupanga, moja wapo ikiwa makazi ya Balozi wa Afrika Kusini Tanzania, kule masaki ambapo alikuwa analipwa $5,000 kama kodi ya mwezi kuanzia mwaka 1994. Mandela alipokuja Tanzania, alitembelewa na Nyerere pale kwa Balozi, na kufanya Press Conference pale pale. Ni katika hafla ile ndio Nyerere akaambiwa ile ni nyumba ya ENL, kitu kilichomsononesha sana. Ndipo Nyerere akatumia nafasi ile kufanya uchunguzi zaidi na kubaini mengi. TISS walimtengenezea Mwalumu Faili maalum juu ya hilo. Mwaka 1995, Mwalimu alikuwa anatembea katika vikao vyote vya maamuzi alipokuwa anaalikwa kutoa msimamo wake juu ya wagombea. Alipomfuta ENL, mtandao wote ulifyata, na aliebakia kumtetea ENL alikuwa ni Sitta ambae alimweleza Mwalimu waziwazi kwenye vikao kwamba sasa ni zamu ya vijana, na wamechoka kuendelea kuchaguliwa na wazee. Mwalimu alibishana sana na Sitta, na baadae Mwalimu akamwambia “Wewe ni waziri wa sheria na katiba, sasa kwa nafasi yako, nimepewa faili juu ya mtu huyu, naomba uchukue faili hili la ENL, na kwa nafasi yako kama waziri wa sheria, utusaidie kufafanua yaliyomo humo ili tubaini kama ENL anaonewa.” Sitta akakaa chini na hakusimama na wala kuzungumza tena.

Baada ya uchaguzi mkuu wa 1995, ENL alitupwa nje ya baraza la mawaziri kutokana na shinikizo la Nyerere. Kikwete ilikuwa ngumu kumuacha kwenye baraza kwani alikuwa namba mbili kule chimwaga (akiwa namba moja katika matokeo ya awali). Njia pekee ya kuumaliza Kikwete ikawa ni kumpa uwaziri wa mambo ya nje ili asiwe na wizara yenye mashiko na wapiga kura (mfani kilimo n.k), lakini pia kumtoa katika mizunguko/ziara ndani ya nchi, hivyo kupunguza nguvu yake katika grassroots level. Walichokosea kina Mkapa ni kwamba kwa ENL kuwa nje ya baraza, ilimpa muda mwingi sana kuendelea na mikakati ya 2005. Lakini ENL pia aliumia sana, na aliyemrudisha kwenye Cabinet ni Abson, baada ya kumuombea sana msamaha kwa Mkapa.

ENL hakuacha kuendelea kujijengea mtandao kwa ajili ya mwaka 2005 na baadae. ENL hajijengei mtandao kwenye siasa tu bali kwenye vyombo vya usalama, taasisi za Umma, Binafsi n.k. Ana mtandao mkubwa sana kwenye sekta za Umma kama Ewura ambako alimweka ndugu yake Haruna Masebu ambae alikuwa NHC, ENL alipokuwa waziri wa ardhi. ENL pia ana mtandao mkubwa sana TRA, Tanesco, kampuni za mawakili, wamiliki wa ma-baa, taasisi mbalimbali za kidini (dini zote), polisi, TISS, taasisi za kimataifa zenye wawakilishi wake Tanzania, n.k.

Mkapa hakuwa mtu wa JK tokea mwanzo. Lakini pia Mkapa hakuwa na chaguo lolote la wazi. Je ni Kwanini? Ni kwasababu, Nyerere miaka yote amekuwa anamtaka Salim kuwa Rais. Nyerere aliposhindwa kuamsha tena jina hilo chini kwa chini mwaka 1995, Mkapa ndiye akawa “his fallback position” (yani kwa Nyerere). Kwahiyo Mkapa kumbeba mtu mwingine nje ya yule ambae Nyerere alimpenda, ingekuwa kama usaliti kwa mtandao wa Nyerere. Lakini chini kwa chini, Mkapa alimtaka Hassy Kitine kumpokea mwaka 2005. Alianza kwa kuunda nafasi mpya kabisa tangia uhuru ya Uwaziri wa nchi utawala bora (Usalaam wa taifa), na kumfanya kitine kuwa waziri wa kwanza, ili ajijengee mazingira ya 2005. Lakini kina ENL, RO, waliligundua hili mapema sana na hivyo kummaliza Kitine bungeni kwa kashfa ya kutumia dola elf 60 kwa ajili ya matibabu ya mkewe Canada. Baada ya hayo, Mkapa alibakia anaelea, asijue la kufanya. Isitoshe, hata mabalozi wa Marekani, Uingereza, na nchi nyingine kubwa walikuwa wanamuonya sana Mkapa kwamba Kikwete hafai, ataingiza nchi katika matatizo. Pia walikuwa wanalalamika sana kwamba hawapati kabisa muda na Waziri wa Mambo ya Nje, na hivyo katika kipindi cha miaka kumi (1995 – 2005), kuishia kuwa na ukaribu zaidi na manaibu mawaziri wan je, katika nyakati tofauti, Balozi Shariff na Mwambulukutu.

Mwaka 2005, mkakati wa mkapa inasemekana ulikuwa ni kuwatosa wagombea wote ambao walikuwa na nguvu kubwa kwenye jamii, ili kuepuka mfarakano iwapo kundi moja litaonekana limeonewa. Kwa mfano, Sumaye alikuwa na kundi kubwa la wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, na viongozi wengi wa halmashauri za wilaya. Malecela alikuwa na kundi kubwa sana viongozi wa CCM kitaifa, lakini pia wenyeviti na makatibu wa CCM mikoa na wilaya. Kikwete alikuwa na kundi kubwa sana la viongozi wa kitaifa wa UVCCM, UWT kutokea mwaka 1995 hadi 2005, huku akidokoa dokoa wengine wengi kutoka katika makundi hayo hapo juu. Mikakati ya Mkapa ikaingia dosari pale ENL, JK, RA, walipotoa msimamo kwamba iwapo Kikwete atatoswa, watahamia Chadema. Ndipo Mkapa akaunda timu ya kutembea nchi nzima kutafiti hilo, chini ya Absom, ambae whether ni kutonana na utafiti wa kweli au uliokwisha andaliwa mapema na kina EL, RA, akamletea taarifa Mkapa kwamba Kikwete akiachwa, CCM itapasuka, na nchi itaingia katika machafuko. Huu ndio ukawa mwanzo wa Mkapa kulibeba jina la Kikwete kwa mtindo wa kura moja badala ya tatu Dodoma.

Kuhusu Kikwete kujiunga na kina Lowassa, swali la kujiuliza ni je, kama Nyerere alishindwa kuwazuia mwaka 1995, na baadae Nyerere kufanikiwa kwa mbinu za kiintelejensia, Mkapa atawezaje kuwa kambi tofauti na ENL katika mazingira ya sasa?
Suala lingine la kujiuliza hapa - nini kilibadili msimamo wa Sitta (mwaka 2007) juu ya ENL - ikifananishwa na misimamo yake huko nyuma juu ya ENL - mwaka 1995 na mwaka 2005? Msimamo wake (Sitta) Sitta ulimgharibu sana kisiasa kwani alitoweka kabisa katika nafasi ya uwaziri kwa kipindi chote cha Mkapa 1995 – 2005, huku ENL na Kikwete wakiendelea kupeta.

Join Date : 27th December 2011??
Thanks...lete zaidi mkuu
 
Fair player naona maii yako yanaruka ruka kwa furaha..maana umepanda ELairline nawengine wamepanda membecoac iliyokata difu ya mbele....jf kiboko
 
Sema ni tetesi basi wapeleke huko kwenye tetesi usitake kuvuja amani ya uongozi wetu
 
Fair player naona maii yako yanaruka ruka kwa furaha..maana umepanda ELairline nawengine wamepanda membecoach iliyokata difu ya mbele....jf kiboko

Edson,

Sio kuwa Lowassa kanipatia chochote! masikini EL wa watu wala hanifahamu wala familia yake hainifahamu na sitaki wanifahamu!
Mie ni mtazamo wangu tu kwa kuzingatia usemi huu:

".............Na ASIYE NA DHAMBI AANZE KUMTUPIA MAWE"

Kumbe basi wote wameoza basi mwenye unafuu na anayethubutu na anayeweza ni Lowassa!. Hayo ni mapenzi yangu binafsi baada ya kutafakari.

ELairline na Sixbajaj na Sumaline na Membecoach na AshCoach....

Lol kwa majina nyie!
 
tuache massihara wakuu, kwa yoooote haya, bado tunataka huyu mtu awe Rais wa TZ? Huyu ni mtu mwenye tamaa za kupitiliza
 
Chinjaneni wenyewe. Ukianza hivyo ujue umefikia mwisho (etc) - End of Thinking Capacity!.
FP,
Ina maana fujo zote wakati wa kumtafutia Urais JMK tangu mwaka 1995-2005 hazikutikisi hata kidogo! Unadhani kundi hili lililoratibu na kufanikisha Urais wa JMK bado linastahili kupewa tena nafasi hiyo? Uchaguzi wa CCM ni mwaka huu. Tutajua tu la kufanya kama WATANZANIA baada kuona watakavyojipanga.
 
Mkuu Ogah,

Mie la dharau sijui maana ni perception. Unajua mtu ukiwa maarufu ni taabu kidogo.

Ninachomaanisha ni kua EL alitumia nafasi zilizopo kuweka biashara halali.

Money laundering ina apply kwenye biashara kubwa kubwa ambazo ni capital intensive, biashara za airtime voucher au laundry hazihitaji capital kubwa. Labda real estate business.

Lakini si tuna takukuru? Mbona tuhuma nyingi lakini hamna uthbitisho? Isije ikawa ya HIZBU ya SAS!


FP mkuu wangu..normally mabandiko yako ni objective lakini kwa hili bandiko ume demonstrate ulivyo biased kabisa and Iam sure hata nafsi yako inakusuta kwa sababu unajua unasema kitu ambacho in practice kwa siasa zetu za Tanzania ni ngumu kutekelezeka. Unaturudisha enzi za Mkapa kulalamika kwamba tuhuma dhidi yake na wala rushwa wenzake zipelekwe mahakamani wakati anajua mtuhumiwa ni YEYE na katiba na sheria zinamlinda asipelekwe mahakamani! Strange?? Mkuu kupambana na rushwa kwenye vinchi vyetu vya kimasikini it takes more than laws na akina Takukuru! It needs political will-something we badly lack, maana wanasiasa ndo wezi wakubwa! Kwa wote wenye nia na mapenzi mema na taifa letu tunalijua hili ndo maana tunaitafuta katiba mpya.

Otherwise, mkuu kama kawaida nitaheshimu michango yako hata kama sikubaliani na wewe mara nyingi..maana naamini ni mitazamo kama hii inatufanya tuwe na majadiliano tukitafuta suluhisho la matatizo yetu. Lakini kwa kauli yako hapo juu, I can safely say..umekuwa mnafiki: Pole kwa kutumia neno hilo maana nimekosa neno mbadala mkuu! Ushauri wangu hata kama tunawasupport hawa jamaa kwa sababu zetu mbali mbali..lakini tujitahidi kubakia objective kwenye hoja zetu (atleast kwa wale wengi wetu ambao bado tunaamini objectivity ya hoja). Maslahi ya taifa letu mbele daima.

Happy new year!

Masanja,
 
Huna mtiririko wa hoja na mpaka sasa umeshashindwa kuwadanganya watu.... unaleta upupu hapa... na hata hizo parts zingine ukizileta ni kujisumbua tu. Hazina mashiko hizi.
 
Teh teh teh.
Mto mada huyu alikuja na mada flani wakati wa uchaguzi mwaka jana na kutuweka roho juu kupita kiasi, kwa mliokuwa mnafuatilia JF kipindi hicho nadhani mnakumbuka vema sana. Nasoma kwa tahadhari sana habari zake
 
Mtoa habari,

Ukichunguza kwa umakini utajiri wa EL ameuongeza sana kwa UHALALI kuliko tunavyoambiwa. Na pia hajashiriki deals kubwa kubwa kama magazeti na wengi tunavyoamini. Miradi yake halali inatosha kumfanya awe tajiri.

Vipi biashara ya mauwa kupeleka nje ya nchi?

Vipi hujataja biashara ya ng'ombe kupeleka nje ambayo kwa sasa imesitishwa (sijui kama imefufuka)?
Kwahiyo utaona mengi ni majungu. He is a self made millionaire!
Biashara pekee ya Lowasa ambayo ni kubwa tu na hamtaki kuitaja ni ile ya kutafuna Idara na mashirika ya UMMA yaliyokuwa kwenye wizara alizowahi kuongoza:
-Kitengo cha Maafa ofisi ya WM kilimpa fedha nyingi sana wakati ule.
-Mamlaka za Maji Mijini zikiongozwa na DAWASA ya Mutalemwa zimemchangia sana tu.
-Ule mradi mzima wa maji wa ziwa Victoria-Shinyanga-Kahama ametafuna ni balaa.
-Alipoanza tu Uwaziri Mkuu akahakikisha anateua wakurugenzi wake wa halmashauri/Manispaa wengi tu ili atafune.
-NHC akiwa waziri wa ardhi na Haruna Masebu akiwa DG wakati huo ni balaa.
-EWURA ya Masebu nayo iliendelea kumneemesha LOwasa isivyo kawaida.
Mchezo huu unafanywa na mawaziri wengi tu sasa ingawa muasisi na kinara wake ni Lowasa.
 
Back
Top Bottom