Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 2)

Mkuu TR tofauti yako wewe na wengi waliomo humu ndani kama akina Nguruvi3, Mwanakijiji, nk. ni wewe kutokuchambua hoja, na hasa kila point anayoingelea mtoa mada na kuionesha ni kwa namna gani mtoa hoja yupo wrong. Mwenzetu mara nyingi unapinga tu, au unachukua uzi wa karibu page nzima unauweka tuusome bila kutuambia nini hakipo ok.

Mimi nadhani unakosa kabisa kuendana na culture ya JF ambayo tunapingana kwa hoja na sio kuwa mkali tu huku unakataa bila hoja. Hilo ndilo ambalo wenzangu wamekuwa wakikuomba ulifanye pasipo mafanikio. Na hiyo inasaidia kwa kiasi kikubwa kumpa credit mtoa hoja (HU) kwa sababu huna mantiki katika kupinga kwako.
Hilo ni tatizo kubwa sana, nadhani hii mambo ya majina fake humu bado tu wanashindwa kuficha hisia zao, kuna namna mtu anamtetea kiongozi flani ama kumpigia debe to the extent that there is no wa huyo mtu siyo yeye.
 
Hivi kumbe RA ni graduate wa LSE? Eee bwana eee..basi huyu jamaa namvulia kofia!
Nilisoma kwenye gazeti moja UK, nadhani inaweza kuwa The Observer,The Guardian or The Times kuliwa na kurasa kama mbili zilikuwa zinamwongelea JK na Rostam alitajwa kama amesoma Economics, Oxford university.

Kwa nini unamvulia kofia!! Mbona Seif Gaddafi alipewa Phd baada ya kutoa mchango wa milioni 1.5. Rostam inawezekana ata chuo cha Veta hajatia mguu,kwa nini anaficha ficha elimu yake.
 
Mkandara you have said it all! Mi nashangaa sana katika karne hii,watu kusoma na kutafsiri,kutafakari na kujadili,kuchambua na kuchangia masuala ukiwa na dhana ya udini kwenye mind yako. Inasikitisha..
 
mkuu hizo contradiction zake kwetu ni burudani ili tuweze kufikirisha vichwa vyetu, hata hesabu za MAGAZIJUTO mwisho wake utakuta ni 4-2 wakati zilizingirwa na minamba kibao ikiwamo ya kujumlisha, kugawanya na kuzidisha.

asante DSN kwa ufafanuzi hapo juu.

ok naheshimu mawazo yako na haki yako ya kupata burudani lakini burudani yako si lazima iwe yangu pia!na wewe inapendeza kama utaheshimu hilo japo si lazima sana kutokana na maumbile yetu binadamu m/mungu ametuumba kwa mapenzi makubwa sana lakini tofauti!
 
Mkuu wangu ebu turudi ktk mavuno kuangalia story nzima ya uzakishaji wetu. Yatazame mavuno vizuri sana grade yake kisha jiulize imetokana na nini?

1. Huoni kama nchi hii wapo watu ambao ni above the law?..
2. Huoni kama nchi hii inaendeshwa na mtandao zaidi ya serikali ikiwa wapo watu wanakiuka miiko na maadili lakini hawafikishwi mbele ya sheria?.
3. Huoni kama chaguzi za viongozi wetu ktk nyadhifa tofauti zinashangaza.. wapo mawaziri ambao hawafai kuwa mawaziri na uwakilishi mwingi unategemea kujulikana?.
4. Tazama madaraka hata ndani ya vyombo vya Usalama kwa nini vyeo havifuatwi badala yake wanachomekwa watu..
5. Tanzania leo bado nchi maskini sana na vyombo vingi vya kimataifa vinasema UFISADI (Grand Corruption) ni moja ya sababu kubwa kwa nini Corruptors wanalindwa?
6. Sii kweli kwamba mwandishi ame target RA bali yeye ndiye rubani hao ulowataka wapo ktk nafasi zao za viti vya abiria..safari yao ni moja hizi habari dini zinatoka wapi?..Hivi kweli unaamini JK anashindwa uongozi nchini kwa sababu ni Muislaam...hakuna sababu nyingine?..au hao kina Mkapa, EL, Mramba, Mwanyika, Chenge, Werema ulowataja ni wezi hatari kwa sababu wao ni Wakristu?... ndio source ya mahusiano ya matendo kweli?..
7. JK hana nguvu ya rais na anatuonyesha udhaifu ktk mikutano ya chama, kitaifa na uwajibikaji. Huhitaji Phd kuona kwamba JK ni abiria pia anaedeshwa sii dereva - Sasa dereva nani?.... ndio story zote hizi zinapotokea!

Mimi nadhani tusome kujifunza, kupima na kuunganisha vitu kama walivyosema wengine. yapo utakayo yakubali na mengine yatakupa mashaka, haikatazwi kutokubaliana lakini sii kuyaweka maneno mdomoni mwa mtoa mada. Haya yachukue kama mawazo yako wewe na yawakilishe kama yako wewe sio kutafsiri mawazo ya mwingine upendavyo.

Binafsi siongopi RA ni mtu hatari sana nchini kwa sababu ya WATU na MAZINGIRA tuliyopo. Watanzania kwa ujumla maskini sana wanaweza kuuza hata binti zao kwa fedha, sio siri na tunaogopa sana kupoteza nafasi za ulaji. Simba sii mnyama mbaya hata kidogo tena anavutia sana lakini ukimweka ktk kundi la Swala utamtazama kwa hukumu tofauti..Sisi ni ombaomba toka mtu mmoja mmoja hadi Taifa huru lisilo huru, hivyo yaliyosemwa yote pande zote yanawezekana..Haramu ikisha halalishwa huwezi ona ubaya kuifanya sana sana ukiipinga ni Makuruh.

1. Kama nani yuko above the law? una uhakika kwamba Rais ndio anatakiwa kuwapeleka mahakamani?

2. Nchi inaongozwa na mtandao according to who? chadema? what do you expect from them? anything positive NONE. Nchi inaongozwa kwa mujibu wa katiba, anayeona kuna mtu ana makosa ampeleka mahakamani au afuate sheria??

3. Chaguzi hazifai huo ni mtazamo tu; hamuwezi kuwa mnafanana kimtazamo mbona ww umetofautiana kuhusu JJ mnyika kupewa nafasi hiyo, sijaona tatizo la teuzi. ulitaka nani achomokwe wapi na kwanini? tutakuamini vipi kama na wewe siyo vilevile una kundi lako..

4. Mwandishi ukisoma between the lines ana-mtarget RA kama vile ni hatari kupita chenge, lowassa etc.. anachotaka kukiaminisha jamii ni kwamba unajua rostam ndio mbaya sana kupita hawa wenzetu wakristo; angekuwa hayuko biased angezumgumzia issue ya SYMBION thubutu hiyo ni wakristo..

5. JK haendeshwi na mtu anawaendesha nchi, kila mtu na style yake; you may like or not; tunampima rais si kwa watu wangapi wameadhibwa kama atakavyo Slaa (hiyo ni yardstick yake) sisi tunampima kwa huduma za jamii; barabara, maji, vyuo (enrollment), shule na matibabu period..

Ni ujinga wa hali ya juu kuamini hawa waandishi ambao wanampenda ku-potray kwamba jamii fulani ya watu ndio wabaya zaid ata least jamii fulani ni afadhali ndicho anachofanya huyu ..kwa mbaali anawasafisha kina chenge na lowassa huku akimtuhumu RA ambaye at least amewajibika tayari kisiasa ..kupita hata hao wenzake..

Anayedanganywa ni wewe unayeamini kuwa huyu mtoa mada yuko hayuko biased; uko deceived na wengi wako deceived hivyo hivyo wanalenga mbali sana hawa watu..
 
Mkuu TR tofauti yako wewe na wengi waliomo humu ndani kama akina Nguruvi3, Mwanakijiji, nk. ni wewe kutokuchambua hoja, na hasa kila point anayoingelea mtoa mada na kuionesha ni kwa namna gani mtoa hoja yupo wrong. Mwenzetu mara nyingi unapinga tu, au unachukua uzi wa karibu page nzima unauweka tuusome bila kutuambia nini hakipo ok.

Mimi nadhani unakosa kabisa kuendana na culture ya JF ambayo tunapingana kwa hoja na sio kuwa mkali tu huku unakataa bila hoja. Hilo ndilo ambalo wenzangu wamekuwa wakikuomba ulifanye pasipo mafanikio. Na hiyo inasaidia kwa kiasi kikubwa kumpa credit mtoa hoja (HU) kwa sababu huna mantiki katika kupinga kwako.

kama umenifuatilia mimi nimekua nikimchallenge huyu jama yenu azitolee ufafanuzi contradictions zilizopo kwenye maandishi yake yeye mwenyewe kutokana na makala zake tatu alizozibandika hapa,lakini bahati mbaya sana yeye hasemi chochote mnamsemea nyie,there are so many unanswered questions kwenye haya machapisho yake,but tukijaribu kuuliza u guyz u alwayz try to shut down questioning kwa kisingizio chenu kile maarufu but very weak "ur not a great thinker/this is not ur forum etc.." jamaa anakua ni kama mwalimu wa chekechea,anafundisha bila kuulizwa maswali,na watu wanatakiwa ku copy notice zake tuuuu basi!bahati mbaya sana mimi sio mwanafunzi wa hivyo,lakini sikukatazi wewe kufanya kinyume changu,mi huwa sijali kama namfurahisha mtu ama la cuz i didn't come here to win applause...
 
CDM haiwezi kuchukua hii nchi. Hizo ni story za JF tu!
Na huo mtandao haujakaa kihivyo ...... ni mchina ndiye atayemweka rais 2015.
Haya maongezi yataisha baada ya uchaguzi wa CCM.
He!Mkuu mbona mnazidi kunichanganya sasa?kumbe na China pia ina kamtandao kake?Ama kweli nipo gizani aisee!!Enhe hebu nijuze SOBY na China anahusikaje naye hapa?
 
Mkuu ... tofauti yako wewe na wengi waliomo humu ndani kama akina Nguruvi3, Mwanakijiji, nk. ni wewe kutokuchambua hoja, na hasa kila point anayoingelea mtoa mada na kuionesha ni kwa namna gani mtoa hoja yupo wrong. Mwenzetu mara nyingi unapinga tu, au unachukua uzi wa karibu page nzima unauweka tuusome bila kutuambia nini hakipo ok.

Mimi nadhani unakosa kabisa kuendana na culture ya JF ambayo tunapingana kwa hoja na sio kuwa mkali tu huku unakataa bila hoja. Hilo ndilo ambalo wenzangu wamekuwa wakikuomba ulifanye pasipo mafanikio. Na hiyo inasaidia kwa kiasi kikubwa kumpa credit mtoa hoja (HU) kwa sababu huna mantiki katika kupinga kwako.
Chesty, nakushukuru umeliona tatizo hapa, kuna watu wanafikiri kuandika sana ndio kuonyesha nao ni magreat thinkers au kujibu karibu kila post kwa maelezo marefu pointless.

Sio kila mtu anaweza kuwa Mwanakijiji, Nguruvi 3, Mkandara etc kwa kuwainga kuandika post ndefu, hao wako deep na post zao ni full mass nondo na sio post ndefu empty!.

Nawashauri sio lazima kujibu kila post wala sio lazima kuandika maelezo marefu, unaweza kuwa great thinker hata kwa kusoma tuu na kuelewa bila kujibu chochote!.

Ni afadhali kikaa kimya watu hawatakuelewa uelewa wako kuliko kujibu pumba na kuonyesha upumbavu wako!.
 
Usiku ulikuwa mreeefu sana sasa kunakaribia kucha watu waliozoe KUKESHA wanachanganyikiwa!!
 
1. Kama nani yuko above the law? una uhakika kwamba Rais ndio anatakiwa kuwapeleka mahakamani?

2. Nchi inaongozwa na mtandao according to who? chadema? what do you expect from them? anything positive NONE. Nchi inaongozwa kwa mujibu wa katiba, anayeona kuna mtu ana makosa ampeleka mahakamani au afuate sheria??

3. Chaguzi hazifai huo ni mtazamo tu; hamuwezi kuwa mnafanana kimtazamo mbona ww umetofautiana kuhusu JJ mnyika kupewa nafasi hiyo, sijaona tatizo la teuzi. ulitaka nani achomokwe wapi na kwanini? tutakuamini vipi kama na wewe siyo vilevile una kundi lako..

4. Mwandishi ukisoma between the lines ana-mtarget RA kama vile ni hatari kupita chenge, lowassa etc.. anachotaka kukiaminisha jamii ni kwamba unajua rostam ndio mbaya sana kupita hawa wenzetu wakristo; angekuwa hayuko biased angezumgumzia issue ya SYMBION thubutu hiyo ni wakristo..

5. JK haendeshwi na mtu anawaendesha nchi, kila mtu na style yake; you may like or not; tunampima rais si kwa watu wangapi wameadhibwa kama atakavyo Slaa (hiyo ni yardstick yake) sisi tunampima kwa huduma za jamii; barabara, maji, vyuo (enrollment), shule na matibabu period..

Ni ujinga wa hali ya juu kuamini hawa waandishi ambao wanampenda ku-potray kwamba jamii fulani ya watu ndio wabaya zaid ata least jamii fulani ni afadhali ndicho anachofanya huyu ..kwa mbaali anawasafisha kina chenge na lowassa huku akimtuhumu RA ambaye at least amewajibika tayari kisiasa ..kupita hata hao wenzake..

Anayedanganywa ni wewe unayeamini kuwa huyu mtoa mada yuko hayuko biased; uko deceived na wengi wako deceived hivyo hivyo wanalenga mbali sana hawa watu..
Now you attacking me, playin a mind game eeeh!
Kwa nini wewe usinambie ulochokiona tofautina mimi badala ya ku judge mawazo na maamuzi yangu mimi.. Hivi lini Wadanganyika mtajifunza kujadili mijadala kule nimekuuliza tu yatazame mavuno kisha nambie huyaoni kadhaa wa kadhaa wewe umenirukia mimi kulikoni?..Unashindwa kujibu hoja mkuu wangu!..Hata hivyo nitakujibu moja baada ya jingine. Sikimbii maswali mimi kama wewe kwa kuuliza maswali zaidi juu ya maswali ulopewa wewe..

1. Kama nani yuko above the law?... - Kuna List of Shame na wengine umewataja wewe mwenywe huko nyuma.. Kama hawa unajua ni wezi unaweza nipa sababu kwa nini hawashtakiwi?..soma pia majibu yako namba nne.. kwa hiyo wapo watu above the law.

2. Nchi inaongzwa na Mtandao kutokana na kile nilichosema MAVUNO tulonayo -umeshindwa kuelewa unarudi kutafuta mchawi -Chadema! Maadam unasema wapo wezi na mafisadi kina Mkapa, EL na hawapelekwi mahakamani wakati ni wezi utasema je nchi inaongozwa kikatiba!.. Haya unayatunga sasa hivi..

3. Sina uchaguzi wowote juu ya viongozi wa Chadema wala sina list yangu hivyo ushauri wako unajipotosha wenyewe.. siwezi kukuchagulia mke ila naweza kupendekeza haina maana namtaka mkeo.. Swala la Mnyika ni none issue kabisa yeye sii fisadi wala mtandao na pia ni uongozi wa habari ktk chama.

4. Rostam ana Uislaam gani na wewe? kitu gani kinakufanya useme huyu ni Muilsaam kwa sababu ya jina au mwarabu? nipe vishawishi vya Rostam na uislaam kisha nionyeshe amepigwa vita kwa Uilslaam wake..vipi ustaadh hujui hata maana ya Uislaam?

5. Na bila shaka ktkm upimaji wako ndio maana nchi maskini hivyo sintokushangaa mtu anayepima umaskini kwa kiwango cha umaskini.. Unajua hata ktk hesabu unapokwenda negative na kila namba zinavyozidi ndivyo upo ktk hali mbaya zaidi, wewe na washabiki wengine mkiambiwa leo imepanda kuwa minus 6 toka -3 mnajua hali ni bora zaidi... Ama kweli Kila mtu ana staili yake..

Mkuu JK kama kumpenda tulimpenda sote lakini katika hili la kujaza pakacha linalovuja huwezi nambia kitu. Tumemwambia toka 2006 hadi kesho na tutaendelea kumwabia kwamba anachokifanya ni kuuiingiza nchi ktk madeni zaidi na zaidi..Kama tulikwama ktk tope basi hii nguvu kubwa anayotumia kuliendesha gari ndio kwanza analididimiza zaidi.. Sina chuki naye wala simkubali maana tatizo lipo analiona kalifumbia macho na masikio sasa tusema karogwa?... huyu sii dereva hata kidogo bana acha kutetea vitu ambavyo viko wazi kabisa..
 
mkuu ...kumbe hoja zako dhaifu unataka watu wazichukue kwa uzito hata km ni nyepesi. kuna mengine nakubaliana na ww lakini mengi unayokosoa inaonekana km unayakosoa kutokana na wivu kwa mtoa mada HU au mtoa tetesi/mtoa habari, sasa sijui anagusa na maslahi yako kiaina au pengine ungependa habari km hizi uzitoe ww umewahiwa!! twende taratibu mkuu, nchi hii ni yetu sote, hata tetesi na udaku tunauchukulia kwa uzito wa juu endapo unagusa maslahi ya taifa letu.
Mkuu Zumbemkuu, hakuna ubishi HU na MH ni vichwa na wamemwaga humu nondo za kufa mtu, sisi tunao appreciate let us appreciate na wanakandia acha wakandie ndio essence ya any healthy debate, tatizo labda ni kwa wakandiaji ambao hawana hoja zaidi ya kukandia upupu ili kujikomba komba kwa watawala dhalimu hawa waliotufikisha hapa!. Natamani 2015 ifike kesho tuifagie nyumba yetu kwa kuondoa takataka zote tutupe jalalani na kuzichoma moto zishije kutuachia uvundo!.
 
Pasco wiki hii naona presha itakuua. Punguza hasira ndugu yangu hawa watu wako kazini. Huoni Circle yao ni ile ile? Ila ring leaders wao siku mbili hizi wamepumzika, nadhani wanataka kuja na hoja nyingine kuhusu Mwalimu na kutangazwa kwake kuwa "mtakatifu".
 
1. Kama nani yuko above the law? una uhakika kwamba Rais ndio anatakiwa kuwapeleka mahakamani?

2. Nchi inaongozwa na mtandao according to who? chadema? what do you expect from them? anything positive NONE. Nchi inaongozwa kwa mujibu wa katiba, anayeona kuna mtu ana makosa ampeleka mahakamani au afuate sheria??

3. Chaguzi hazifai huo ni mtazamo tu; hamuwezi kuwa mnafanana kimtazamo mbona ww umetofautiana kuhusu JJ mnyika kupewa nafasi hiyo, sijaona tatizo la teuzi. ulitaka nani achomokwe wapi na kwanini? tutakuamini vipi kama na wewe siyo vilevile una kundi lako..

4. Mwandishi ukisoma between the lines ana-mtarget RA kama vile ni hatari kupita chenge, lowassa etc.. anachotaka kukiaminisha jamii ni kwamba unajua rostam ndio mbaya sana kupita hawa wenzetu wakristo; angekuwa hayuko biased angezumgumzia issue ya SYMBION thubutu hiyo ni wakristo..

5. JK haendeshwi na mtu anawaendesha nchi, kila mtu na style yake; you may like or not; tunampima rais si kwa watu wangapi wameadhibwa kama atakavyo Slaa (hiyo ni yardstick yake) sisi tunampima kwa huduma za jamii; barabara, maji, vyuo (enrollment), shule na matibabu period..

Ni ujinga wa hali ya juu kuamini hawa waandishi ambao wanampenda ku-potray kwamba jamii fulani ya watu ndio wabaya zaid ata least jamii fulani ni afadhali ndicho anachofanya huyu ..kwa mbaali anawasafisha kina chenge na lowassa huku akimtuhumu RA ambaye at least amewajibika tayari kisiasa ..kupita hata hao wenzake..

Anayedanganywa ni wewe unayeamini kuwa huyu mtoa mada yuko hayuko biased; uko deceived na wengi wako deceived hivyo hivyo wanalenga mbali sana hawa watu..

makaka wakuu wa jf watakupachika jina muda si mrefu,hawataki jamaa aguswe bwana,tunatakiwa kumsoma tu na kudumisha fikra zake bila kuhojii chochote,atakaemgusa huyo sio great thinker wala hana hoja!wao kwao hoja na wewe uje na hadithi za kufunga mtaa ndio wanazipenda hata kama ni ya kutunga poa tu!ukiwa mtunzi mzuri utaitwa GREAT THINKER!
 
Kwani unadhani utunzi ni kitu rahisi namna hiyo? Bila kuwa great thinker huwezi kuwa mtunzi hata kidogo, kwani lazima ujue kuwa utunzi mfano wake ni Uumbaji na kazi ya kuumba ni kuomba majaaliwa ya mwenyezimungu. Kama Utunzi ni kitu rahisi kama unavyotaka tuamini unadhani mpaka leo tungekuwa tunasoma vitabu vya kina Shakespeare au Shaaban Robeto?
 
kuna mchangiaji mmoja huko huko nyuma unaweza kuwa GREAT THINKER hata kwa kusoma na kuelewa tu bila kutunga hadithi ndeeefu au kujaribu kujibu killa jambo!
 
Mkuu Zumbemkuu, hakuna ubishi HU na MH ni vichwa na wamemwaga humu nondo za kufa mtu, sisi tunao appreciate let us appreciate na wanakandia acha wakandie ndio essence ya any healthy debate, tatizo labda ni kwa wakandiaji ambao hawana hoja zaidi ya kukandia upupu ili kujikomba komba kwa watawala dhalimu hawa waliotufikisha hapa!. Natamani 2015 ifike kesho tuifagie nyumba yetu kwa kuondoa takataka zote tutupe jalalani na kuzichoma moto zishije kutuachia uvundo!.

....Yes! and only one!.......and one only! LOWASSA will take us through this mess......haki ya nani!
 
Ogah, mwanzo nilipigania sana Lowassa awe mgombea wa CCM!. Baada ya kuisoma hii kitu na kujua where real powers lies!. Sasa nimeamua kujinyamazia kwanza and watch how this man, King Maker, plays our mind away!. Hivyo kama haya humu ni kweli!, then JK is nothing!, CCM is nothing!, na sisi Watanzania wote we are nothing!.

The only thing that is something, according to this, then its the "King Maker"!. Ndiye aliyemuweka JK na VP wake!, akamuweka Spika!, akamuweka CJ. Hii ndio mihimili yenyewe ya dola!. Akaja kumuweka CDF!, IGP! na Chief wa TISS!, where true powers lies, usikute hata Hosea na kina DPP wanawajibika kwake!. Sasa who are we kukataa chaguo lake?!.

Kama ni kweli chaguo lake ni Lowassa, sasa kazi nitakayoianza kipindi kifupi kijacho, ni kuwahamasisha wapinzani kama EL ndiye atasimamishwa kuwa mgombea wa CCM, wasithubutu kuchukua fomu za urais!, wamuache apite bila kupingwa ili Tanzania iwe ile nchi ya ahadi!. Nchi ya maziwa na asali!. Mabomba yatatoa maji, maziwa na asali nchi nzima!. Kumpinga ni wastage of time and money!.

Then Yes Indeed, for 2015, Lowassa is The One and Only!.
 
mixed feeling!!, lack of power from within and above all captivitity of negativity!!!....Pasco; is frustration killing you?!!.....

Lowasa will never be the president of Tanzania...Markmy words...halafu usitishwe na nguvu ya hawa watu ..ni kweli wana nguvu sana tena ya pesa lakini nakwambia safari hii hawatacheza na akili za wazawa.....tatizo tunaloliona kwa nchi hii ni wsomi wa nchi hii hasa vijana wanakubali kirahisi sana na wananunulika sana kirahisi.....pingeni kwa nguvu nchi hii kuingia tena mikononi mwa wanyang'anyi
 
RA anakuzwa mno kwenye siasa za nchi hii bila sababu kama baadhi yetu tunavyomlaumu Mwalimu kwa kila tatizo la sasa miaka zaidi ya 25 tangu ang'atuke. Kama haya anayoandika HU ni kweli na mpo mnaoyafahamu tangu yanaanza kwa nini mmeendelea kuwatumikia watu hawa?
Kwa nini bado mnamtaka Lowasa ambaye mnajua hawezi kufurukuta kabisa kwa RA? Nguvu za RA zimeanza lini hasa na zinatokana na nini. Hivi kweli RA wa mwaka 2005 ndiye huyu wa sasa? Msitupagawishe WATANZANIA bwana.
 
Back
Top Bottom