Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 2)

Mkuu Sikonge, umenikumbusha mbali, enzi za primary darasa la 5, kuna hesabu moja ya kutafuta eneo la kopo la chakula cha kuku jibu lake lilikosewa kwenye kiongozi cha mwalimu, mimi nikapiga hesabu ya kweli, matokeo darasa zima wakapata mimi peke yangu nikakosa!. Nikapiga tena hesabu nikapata jibu lile lile, nikanyoosha kidole kumuomba mwalimu tupigie hesabu ubaoni. Akachangua mmoja akaenda kupiga hesabu ubaoni kufikia jibu akaliandika jibu la kiongozi cha mwalimu, mimi nikanyoosha kidole kuwa hilo sio jibu sahihi, nikazomewa na darasa zima!.

Kumbe yule mwalimu Ramadhani (Mama Rama), alikwenda kuifanya mwenyewe. Kesho yake alipongia tuu akakumbushia hiyo hesabu, nikaitwa mbele kwenda kuifanya ubaoni, nikaifumua!. Mwalimu akatuma mitihani yote irudishwa darasa zima walikosa wakakatwa maksi na mimi nikapata nikaongezewa maksi.

Kwenye kupigania haki, nakiri mimi ni mbishi, ndio maana kwenye kuipigania haki ya Lowassa kuteuliwa nitapigana mpaka mwisho!.
 
Watanzania wenzangu,wazalendo wenzangu nashukuru kujua haya; Baada ya haya; Rostam popote ulipo 'YOU WILL SEE!! wee endelea tu kuchezea watanzania unavyojisikia, halafu kibaya zaidi juzijuzi tu wamerekani wamesaini mkatataba wa kuchimba Uranium na tanzania, ikumbukwe mtandao wa weak leakes ulisema Iran ilikuwa ikisaidiwa na tanzania kusafilisha uranium kutoka nchi jirani. Now you quickly can brainstorm uhusiano wa kinafiki kati ya ROSTAM-IRAN-MAREKANI kuizuru TANZANIA. MTIKILA ALILALAMIKA SANA KUHUSU ROSTAM kwamba sio mzawa,sio mwenzetu,uraia wake sio wa kizalendo,mlanguzi tu.
 


alilalamika baada ya rostam kuonyesha waandishi payments vouchers kutoka kwake alizozisaini mtikila..?
 
Kitimtim, pole!, tumeshikwa pabaya!.
 

Mkuu ngoja tupate fursa ya kutafakuri...lakini hapa nashindwa kuelewa,kwa hiyo RA na EL na mkuu wa kaya sio kambi moja kwa sasa? na kama ni hivyo kwanini inaonekana kama mkuu wa kaya anendelea kuwalinda RA na EL...?
 
Mkuu ngoja tupate fursa ya kutafakuri...lakini hapa nashindwa kuelewa,kwa hiyo RA na EL na mkuu wa kaya sio kambi moja kwa sasa? na kama ni hivyo kwanini inaonekana kama mkuu wa kaya anendelea kuwalinda RA na EL...?
Only 83, hawalindi bali anawaogopa kwa vile wao ndio wameshika mpini, wao ndio waliomuweka yeye na serikali yake yote iko mikononi kwao, hawezi kuwafanya chochote!. Hivyo ni hao ndio wataamua baada ya JK nani atafuatia!.
 
Pasco,
Wala sikuwa na maana ya wewe ni MBISHI kama nilivyoandika. Ila ulipoanza kuelezea EUREKA na ARCHMEDES, na kuangalia jina lako ni Pasco, ndipo nikaanza kurudisha kumbukumbu kwa hao akina Newton na adui yake Hooke, Pascal na wengine wengi na nikaamua kuweka hicho kichekesho kama muendelezo ya kitendo cha Archimedes kutoka nje uchi huku akipiga makelele "Eureka Eureka".

Vinginevyo, asante kwa hii habari ya jibu la hesabu. Anyway, nyie mlikuwa na bahati maana nasikia kuna darasa waliondolewa wote darasani ili wakafanye swali la 20 nje mtihani wa form 4, kisa tu limeandikwa "without using table (math table) solve equation....."

Ukisoma maelezo yako kwenye hii makala na HU, nimeanza kuunganisha dots kuhusu hawa wagombea Urais wa Tanzania mwaka 2015. Naona hadi ikifika mwaka 2014 watu watakuwa hoi utafikiri pambano la Raundi 14 heavy Weight Boxing kule Manila. Ukweli unabaki kuwa, pamoja na Lowassa au King Maker kuwa na Jeuri ya pesa na nguvu kubwa, hili group la HU na wenzake, linaweza kuwapaka sana kiasi cha kuchukiwa na hata hela zao zikakataliwa au kusahauliwa na makanisa wanayoyapa sasa hivi hela.

Ngoja tusubiri tuone hapo mwakani nani atashinda na kuwa Mwenyekiti wa CCM na hilo litaanza kuonyesha yupi anaelekea kushinda na nani aanze kutafuta pa kukimbilia.
 
Mambo unayoandika ni mazito sana sana, we don't know if we should believe what you say or not.Ila ktk unachosema inaoneka kuna elements za ukweli,but time will reveal.
 
Lah! Jamani balaa tupu, huyu RA anatisha kweli vileee....Haya nimesikia uvumi mwingine kuwa RA ni member wa Maison....ya kweli haya?
 
Lah! Jamani balaa tupu, huyu RA anatisha kweli vileee....Haya nimesikia uvumi mwingine kuwa RA ni member wa Maison....ya kweli haya?
Mkuu Mkandara, Freemasons ni secret society ambapo hakuna memba mwenye ruhusa ya ku reveal status ya member mwingine yoyote isipokuwa yeye mwenyewe akiamua kujireveal kama alivyofanya Sir. Andy Chande. Sasa baada ya kusikia uvumi RA ni freemason, hiyo itabaki ni uvumi tuu!.

Waandishi wetu nao kazi zao ni kuandika habari za mikutano, semina, warsha na kongamano tuu, ukipangisha chumba pale Kempinsiki na powerful infrared camera, unaweza kupata picha za masons wote wakiingia pale grand lodge yao, hiyo itanyamazisha tetesi na kuwaacha watu midomo wazi pale watakapo washuhudia hadi kina ....wakiingia na wakitoka!. Huingia usiku mkuu na kutoka kabla hakujakucha!
 
Nimetulia kwa makini sana, nafuatilia nyuzi hizi kwa utulivu wa hali ya juu bila kuchangia chochote. Najua hapa ntaibuka na boooonge la kitu.
 
Bila kupewa hiyo kazi, kuna wengine washajichukulia u campaign manager wa L! Kaazi kweli kweli! I believe in something else...and am sure the prevailing work would cease to be at some point....the unknown will lead us to the land of honey and milk.
 
Nionavyo miimi Usalama wa taifa umebaki jina tu kwani ni ukweli usiopingika kuwa Othman hamuungi mkono JK na ndio maana hamwambii ukweli wa hali hii na nyingine zinazoangamiza taifa
 
Bado nina mashaka sana na hilo la RA kuwa CIA, anyways ngoja nisome tu na labda given time, nitaitambua dhana nzima ya HU.
 
Mkuu ngoja tupate fursa ya kutafakuri...lakini hapa nashindwa kuelewa,kwa hiyo RA na EL na mkuu wa kaya sio kambi moja kwa sasa? na kama ni hivyo kwanini inaonekana kama mkuu wa kaya anendelea kuwalinda RA na EL...?

hapo kwenye red...not by choice.
i think.
 
kikwete ndio rais wa tanzania na ndio amiri jeshi mkuu na na ndio mwenyekiti wa chama cha mapinduzi,that is the reality na itabaki kuwa hivyo mpaka atakapomaliza muda wake 2015 kwa mujibu wa katiba,nyingine ni story tu za kuchangamshia gumzo hapa kijiweni pachangamke,ndio maana mnaona watu serious kama kina Fm Es,mzee mwanakijiji,WJ malecela,Invisible na vichwa vingine wameamua kuupotezea kiaina huu mjadala licha ya kuchokonolewa mara kadha hapa na baadhi ya wachangiaji wameona hauna maslahi wala mashiko lakini sisi tuendelee tu kuchangamsha kijiwe chetu kisiwe doro!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…