Kikwete kainua uchumi wa Tanzania

 

Mkuu kama kweli hiki ndio unachokiona pole sana. Una aamini kweli waalimu ni asilimia 100? madai yao wameshughulikiwa, ajira mpya? pole sana mkuu. Naona bado Mkapa was far better than JK. Miaka 5 ya kwanza ya Ben tuliona mengi tangible lakini sasa ya JK wewe ndio unayaona.
 
Angalia hapo nilipoweka wino mwekundu ktk quate. Utagundua kwamba hata hizo takwimu ulizotoa zinakubaliana na kichwa cha habari. Yaani GDP ni $1300, ukilinganisha na ile niliyoiandika $1400. Tofauti sio kubwa na katika takwimu, hiyo hukubalika na ndio maana ameadika EST( kadirio). Hivyo uchumi umepanda na unaendelea kupanda kama takwimu zako zinavyoonyesha. Na hilo ndilo la msingi.

Ukweli ni kwamba kila utapojaribu kwenda kutafuta vyanzo vingine, ni moja utakutana nalo, hili la kupanda kwa uchumi. Jamani tumpe sifa zake huyu raisi kijana, angalau katika hili. Ndio, kama binaadam ana udhaifu wake lakini hapa kaonyesha ujasiri. Kikwete anaweza!!!!
 
Unajua, ndugu Bongo lander nikwambie kitu kimoja ambacho bado hujakifahamu. Ikitokea vita, utafunzwa kuendesha gari masaa 5, na kukabidhiwa Scania kupeleka chakula kwenye uwanja wa mapambano. Askari atafundishwa silaha na ujanja wa porini kwa siku 5, na kukabidhiwa bnduki na kwenda mapambanoni. Hivyo ndivyo ilivyo popote duniani.

Sasa kitu usichokifahamu ni kuwa Tanzania tupo katika VITA. Vita ya kumuondoa adui ujinga. Hii ni vita kubwa kuliko ya kumtoa Idd Amin. Maana si vita utayoimaliza kwa mwaka au miaka10, bali ni vita endelevu. Tunawasiliana mimi na wewe kwa sabau tulikwenda shule. Lakini kwa mtindo ule, kati ya wanafunzi darasa la saba 100 eti wanafaulu 2 tu, ni aibu kubwa sana. Katika hilo hakukua na jinsi ila kutangaza vita.

Ikiwa vijana hawajui kusoma na kuandika, hata kama ukaweka matangazo ya kukomesha ukimwi lakini vijana hawajui kusoma unapoteza pesa yako tu. Lakini kwa sasa hivi, angalia hata magazeti wanunuaji ni walala hoi ambao zamani walikuwa hawajui kusoma. Hii itaturahisishia hata katika ukuaji wa Demokrasia nchini. Hivyo tuunge mkono hali iliyopo, angalau moja tumetatua, hili la madarasa. Kuwa hatutaonyeshwa tena kwenye CNN vijana wetu wkisomea kwenye miti. Sasa tuje kwenye hili la walimu. Ninahakika kabisa kuwa linawezekana. Tumuunge mkono Rais wetu Kikwete.
 
Kwanini usituandikie GDP ya Tanzaini toka cia.gov? Ukazunguka maneno Mengi! Unajua kwanini! Gues! Kwa sababu unajua kuwa haitofautiani sana na hiyo niliyoiandika.

Hata hivyo, ndugu Interested Observer #8 ametusaidia. ANGALIA MAANDIKO YALIYO KATIKA wino mwekundu. Hata huko mambo si mabaya kwa Kikwete. Kama macho yangu hayanidanganyi, inasoma GDP $1300. Si tofauti kubwa ($1400], inakubalika katika takwimu. KWA HIYO UCHUMI UNAPANDA. tUMSIFU HUYU RAIS KIJANA.

"Why don't you go and get direct figures www.cia.gov; these are correct figures just released: Create Date: Sep-17-2009 08:51
GDP (Purchasing Parirt); there are no current estimates for 2009

GDP (purchasing power parity):
$54.25 billion (2008 est.)
country comparison to the world: 88 $50.65 billion (2007 est.)
$47.27 billion (2006 est.)
note: data are in 2008 US dollars
GDP (official exchange rate):
$20.72 billion (2008 est.)
GDP - real growth rate:
7.1% (2008 est.)
country comparison to the world: 36 7.1% (2007 est.)
6.7% (2006 est.)
GDP - per capita (PPP):
$1,300 (2008 est.)
country comparison to the world: 204 $1,300 (2007 est.)
$1,200 (2006 est.)
note: data are in 2008 US dollars
GDP - composition by sector:
agriculture: 27.1%
industry: 22.5%
services: 50.4% (2008 est.)"
 
Haba tukubalitu tu yaishe!!!

Uchumi umependa, full stop, whether aliyepandisha ni Kikwete, au Mkapa au mimi na wewe? We don't care... Ukweli Uchumi umependa.
 

Umeshawahi kufika china weye au unaandika tu kwa sababu unaweza kufanya hivyo?!muwe mnaandika vitu mlivyo na uhakika navyo..,hakuna program ya afya,elimu,malazi, kama unavyoongea wewe kutoka kwa serikali ya china kwenda kwa wananchi wake..,iwe masikini au matajiri..,

information mnazoweka hapa ni elimu kwa baadhi ya watu..,go a little further to verify them kabla ya kuziweka hapa..,ni hayo tu.

FYI:much of what you read on the internet is incorrect..,usitegemee sana Google.🙂
 
Tena tunapenda sana watu kama nyie, Sasa tupe uhondo wa hayo ya China, maana mwenzetu umesoma na kuishi huko. Wana JF wanakusubiri, mbona una kanusha tu bila kutoa takwimu zako zitazoonyesha tusemayo si kweli.

Vibaya hivyo, si unajua hapa ni pahala pa kuelimishana. Tupe elimu na ulinganishe kati ya India na China. Kwa muono wangu huwezi kulinganisha China na India katika hilo.
 
Ninafura kusema kuwa kumbe wote ukweli tunaujua kuwa Serikali ya Kikwete imefanya kazi kubwa sana ya kuinua uchumi wa Taifa. Kwa sababu hakuna hata mmoja aliyekuja na Data tofauti, ama aliyekataa moja kwa moja kuwa uchumi haukui.

Na tunajua kuwa uchumi hauwezi kukua wenyewe tu, au sijui ushuke toka Mbinguni. Kwa hilo ninafuraha sana, na nitazidi kuleta mafanikio ya awamu ya 4. Kwa vile kilio cha wengi huko nyuma kilikuwa : Hivi huyu Kikwete kafanya nini cha maana? Kuna wengi wameingia mtini baada ya kupata hoja dhahir. Ukibisha. lete takwimu na chanzo. Hii ndio kanuni ya mchezo huu.

Huu ni uwanj wa mafanikio, wa kufeli utakuja baadaye.
 
Tabasam la Kikwete lina bahati, ngekewa na linazivuta nchi zote duniani kuiona Tanzania kama Tumaini la uwekezaji.

Ee bana kweli kabisa Zawadi Ngoda! Kikwete haitaji kufanya lolote zaidi ya kutabasamu tu, na Voila! Uchumi wa nchi "unapaa" wenyewe kwa miujiza.

Kulingana na takwimu za CIA, uchumi wa Tanzania unakadiriwa kupaa kwa asilimia 0.00000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000001
kila Kiwete anapotabasamu!
 

Ee bana Dar es Salaam sawa kabisa! Imebaki Kikwete kujenga misikiti ya Ijumaa kila mkoa Tanzania. Nadhani akifanya hivi, uchumi utakuwa 100%! Kipato kitapanda 100% kwa kudra ya Allah na tabasamu ngekewa ya Kikwete! Watu tutakuwa tunaishi mbinguni!
 
DAR-ES SALAAM KASEMA
Ahsante JMK, toka umeingia madarakani, takwimu zote zinaonyesha ukuaji, mashule ya sekondari zaidi ya asilimia 100 juu, vyuo vikuu zaidi ya asili mia 100, mazahanati zaidi ya asilimia 100, kazi mpya zaidi ya asilimia mia moja, uchumi ndio kama hiyo report hapo juu inavyojieleza, kesi zinazosikilizwa na kumalizwa mahakamani zaidi ya asilimia 200, na, na, na, Yote hiyo kwa muda mchache wa kuanzia 2005.

Ni Rais gani mwingine wa Tanzania aliyeweka rekodi inayokaribia hii? = HAKUNA!

JE NI SHULE GANI MPYA YENYE HADHI YA ILBORU AU MZUMBE!SHULE SI IDADI BALI KIWANGO. ni bora ujenge shule tatu kama Ilboru ya Arusha kuliko kujenga shule 20 zenye hadhi ya chini na hazina walimu. Kwanini wasikuze shule zilizopo!
 
no social mobility

poor programmes to reach the poor

no encouragement to grow internal bussinessess

no self help programmes to increase the government income

still looking for doners on his budget

begging investors to rob us (by the way this is where the GDP inakuongopea)

lastly poor kilimo, kilimo strategy looh! ebu nendeni mka waulize wa-russia, romania etc kilimo kiliwapeleka wapi zaidi ya kuishia kuwacha vyakula vinaoza kwenye ma-warehouse. You need all you can get to advance. Na si kuangalia projection or facts ambazo zina base na government income through foreign investment.

$1,300 GDP hiyo ni kusema bongo over 1.5mil (lowest estimate) bongo shillings, monthly ni karibu laki 140,000 uoni hadithi tupu on what transactions tumetengeneza hiyo GDP. It does not reflect the income of 36million people nor the government revenue for that period year so how did you come up with those figure pleeease.

Na education in terms of literacy nyerere katuacha na almost ninety percent the decline ni walio fuatia hana shughuli JK.

Even the society ina msuta with the amount of poverty watu walionayo. Aende badilisha sheria na kujipunguzia madaraka kwanza kama kweli ana nia na maendeleo.

Na si kuja kuwacha watu waendelee na ignorance sijui za kuja na project nini wala nini ambazo ni malumbano yasiokuwa na muelekeo ni yeye kipenzi chako ndio anaweza kuleta mabadiliko. Kwa kuanza na kuimarisha sheria zifanye kazi yake na kuangalia uchumi ulivyo vinginevyo mta corrupt jamii nzima iseme miafrica ndivyo ilivyo.

na watu wengine waje hapa kutuhamasisha na project zao zisizo kua na vichwa wala miguu sijui project Y sijui nini pumba tupu. wengine atuko intrest na politics but social mobility na kuweza kuleta changamoto nyumbani na sheria za Tanzania zina kwamisha na ufisadi wa chini pia unakwamisha sort that mess.

na wenye personal vendetta na serikali sijui baadhi ya watu serikalini waendelee but sort the mess and open the economy channels sisi wengine ndio tunachokitaka.
 
Last edited by a moderator:
Zawadi,

Kwa nini Deni la Taifa limeongezeka marudufu?

Ikiwa Deni hili ni 33% ya GDP kwa mwaka wa pesa 2008, si kweli kuwa true GDP basi si $1300 bali ni $910?

Je kwa nini Matumizi ya Serikali kuu yameongezeka na ile Surplus aliyotuachia MKapa imepotea kabisa?

Je kukua huku kwa uchumi kuna factor rushwa katika Baeti ya nchi ambapo kwa kauli yake mwenyeke Kikwete ni kuwa mwaka jana wa fedha, rushwa, ubadhirifu, hujuma na matumizi mabaya ya fedha kwenye bajeti ilikuwa ni 30% ya Bajeti ya 2008 ikiwa ni ongezeko la 10% kutoka kiwando cha rushwa cha 20% kwenye bajeti ya 2007?

Je ikiwa kila sarafu ya Dunia ilipata nguvu dhidi ya Dola ya Marekani kutokana na Uchumi wa Marekani kuporomoka, ni kwa nini sisi bado tunachechemea na hatukuona ahueni?
 

ni kweli mkapa anahitaji hongera ya kuuwa na kuiba mali ya umma
 
Ee bana Dar es Salaam sawa kabisa! Imebaki Kikwete kujenga misikiti ya Ijumaa kila mkoa Tanzania. Nadhani akifanya hivi, uchumi utakuwa 100%! Kipato kitapanda 100% kwa kudra ya Allah na tabasamu ngekewa ya Kikwete! Watu tutakuwa tunaishi mbinguni!


Mkapa si alijenga makanisa kila kipembe kule Zanzibar , mpaka kwenye vile visiwa vidogodogo ambako hakuna mkristo hata mmoja kumejengwa makanisa . Aliuwa Watanzania na kuhujumu uchumi na kuuza nchi . uchumi ulikuwa kwa 100000%
 

Watanzania haifai tuwe kama mbwa koko, amezoea kulala njaa basi akiona vimifupa ana kenua hadi jino la mwisho…tunatakiwa kuona mbali mkuu Zawadi, nchi hii imejaa minofu kila upande…hivi Tanzania ni nchi ya kuwa na GDP ya dola1300 kweli? kwa nini tuwe na GDP ya 1300?? Kwa nini tufurahi na kujivunia kuulinganisha uchumi wetu wa miaka 5 ijayo na Djibout ya sasa? nchi ambayo hao hao CIA wanasema ni nchi yenye ukame na inaimport sehemu kubwa ya chakula na ina mali asili chache, ukosefu wa ajira karibu 60% nk nk…

Kama GDP imepanda maradufu toka 600 hadi 1300 ina maana na maisha ya watanzania walio wengi kule vijijini yangekuwa na ahueni sana tu…lakini mbona mambo hayako hivyo?
sawa Kikwete ana mazuri na mapungufu yake lakini leo hii sidhani kama anaweza kusimama kifua juu mbele ya watanzania na kuwaambia ameukuza uchumi..
 
Unajua, ndugu Kamundu nikwambie kitu kimoja ambacho bado hujakifahamu. Ikitokea vita, utafunzwa kuendesha gari masaa 5, na kukabidhiwa Scania kupeleka chakula kwenye uwanja wa mapambano. Askari atafundishwa silaha na ujanja wa porini kwa siku 5, na kukabidhiwa bnduki na kwenda mapambanoni. Hivyo ndivyo ilivyo popote duniani.

Sasa kitu usichokifahamu ni kuwa Tanzania tupo katika VITA. Vita ya kumuondoa adui ujinga. Hii ni vita kubwa kuliko ya kumtoa Idd Amin. Maana si vita utayoimaliza kwa mwaka au miaka10, bali ni vita endelevu. Tunawasiliana mimi na wewe kwa sabau tulikwenda shule. Lakini kwa mtindo ule, kati ya wanafunzi darasa la saba 100 eti wanafaulu 2 tu, ni aibu kubwa sana. Katika hilo hakukua na jinsi ila kutangaza vita.

Ikiwa vijana hawajui kusoma na kuandika, hata kama ukaweka matangazo ya kukomesha ukimwi lakini vijana hawajui kusoma unapoteza pesa yako tu. Lakini kwa sasa hivi, angalia hata magazeti wanunuaji ni walala hoi ambao zamani walikuwa hawajui kusoma. Hii itaturahisishia hata katika ukuaji wa Demokrasia nchini. Hivyo tuunge mkono hali iliyopo, angalau moja tumetatua, hili la madarasa. Kuwa hatutaonyeshwa tena kwenye CNN vijana wetu wkisomea kwenye miti. Sasa tuje kwenye hili la walimu. Ninahakika kabisa kuwa linawezekana. Tumuunge mkono Rais wetu Kikwete.
 
Nchi zote hizo toka 1.Zimbabwe..........21.Uganda....24.Mali......28.Tanzania. zimechukua mikopo kama hiyo ya Tanzania, na bado hawakutupiku. Mfano Deni la Tanzania ni Takriban $5bilioni, naa Kenya ni $6bilion. Hivyo hiyo sio ajenda.

Matumizi ya serikali kuu yameongezeka kwa sababu, Serikali kuu imeongezeka kutokana na kuongezeka kwa kazi husika. Kuhusu Surplus, hiyo sina uhakika kama imepotea. Na kama imepotea ni kwa kiasi gani, au yote. Jaribu kuthibitisha maneno yako kwa kutumia vyanzo vinavyoaminika.

Si kweli kuwa kila sarafu ya dunia ilipata nguvu dhidi ya Dola, Mfano rahisa Zimbabwe.
 
Umeandika mengi sana, lakini ya muhimu ni matatu.
1. kwa mwenzi ni sh 140000 kwa kili mtanzania, kutokana na mahesabu ya GDP.
2. Jamii inamsuta kwa umasikini
3. Fungua milango ya uchumi

Nikianza na hili la GDP. Kwa lugha nyepesi ni kwamba, GDP ni kiwango cha pesa ilichonacho Nchi gawanya kwa idadi ya wananchi wake. Mfano, kama Zawadi nina sh 1000 na mwenzaqngu Juma contena una 10,000, kama sisi ndio tunafanya nchi basi GDP = (1000+10000)/2 =5500 sh. Huu ndio utaratibu unaotumika. Kama unaona utaratibu huu unamakosa basi lazima uje na ule mpya unaodhani uafaa. Lakini mpaka leo huu ndio utaratibu unaotumika.

Pengine nikusaidie kitu usichokijua kimoja na kikubwa sana. Ni vipi mgawanyo wa pesa hiyo iliyomkononi mwa matajiri itawafikia walala hoi? SWALI HILI NDIO LA KUTATULIWA NA NDIO SUALA LA WANASIASA. Na hapa ndio hutofautiana kati ya komunisti, wasocialist, liberal, mabepari wenye mlengo mkali kama Republican au wale waingereza maconservative. CHA MSINGI NA CHA AWALI NI KUWA PESA YENYEWE IPO NCHINI, MGAWANYO NI NYINYI KATIKA UCHAGUZI NDIO MNAAMUA.

Ufunguzi wa milango ya uchumi, hilo halina mjadala. Si kitu cha kuomb li nni wajibu wakee kufanya hivyo. Ameanza, lakini mwendokasi ni mdogo mo. Mfano, ukinunua kiwanja Mbezi toka kwa Zawadi, unaweza kubadili jina moja kwa moja. Sio kama zamani mpaka ujene kwanza.

Kifupi nawez kuseaa kuwa eneo hili la kutoa sheia za kirasimu katika biashara a maswala mengine ni lazim lishughulikiwe. Na litasaidia sana kwenye kuondoa rushwa na kuongeza uchumi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…