Kwa vile mpaka sasa hakuna takwimu na wachangiaji mada kuhusu kiasi gani cha barabara zilizojengwa kwa kila awamu, naogopa kusema ni awamu hii au ile ndiyo zaidi. Lakini dhana ya kwamba eti Rais anasafiri sana na kwa hiyo hawezi kuwa alijenga barabara nyingi kuliko watangulizi wake ni upungufu mkubwa katika uwezo wakujenga hoja. Ninavyofahamu mimi ni kwamba kumekuwa na hatua nzuri sana kuhusiana na maendeleo ya miundo mbinu katika awamu hizi mbili za uongozi. Kwa mfano barabara za Mbeya - Chunya mpaka Tabora, ile ya Singida mpaka Manyara, Somanga mpaka Ndundu, ile ya Mangaka Tunduru, na nyingine nyingi ni zao la awamu hii ya nne.[/QUOTE
Si kila kitu kinahitaji takwimu za kimaandishi,mambo mengine yanaonekana wazi,hizo barabara nyingi ulizotaja hata km 20 hazijafikisha kujengwa!,serikali hii inaongoza kwa ahadi au tuseme mipango ya makaratsi,tatizo la viongozi wetu uwa muda mwingi wapo kwenye propaganda za kisiasa,wanaropoka tu wakijua kuwa watanzania wengi tu wavivu wa kufikiri tunajaza kichwani kila kinachozungumzwa,nakumbuka kipindi cha kampeni JK aliulizwa mbona anamwaga ahadi nyingi alijibu bila wasiwasi kuwa watu wanapenda kusikia ahadi!!!
Tatizo hili limeota mizizi kwa watendaji wetu,kiongozi anaweza kuongea uongo hata kwa mtu mwenye akili ya kuvuka barabara tu atajua kuwa ni uongo lakini atabaki anatetea huo ujinga akifikiri kuwa watu hawajua,mfano juzi wakati akihitimisha hotuba yake Pinda alisema serikali ilishachukua maamuzi magumu bila haya akataja moja ya maamuzi ni serikali kuvunja baraza la mawaziri wakati ukweli ni kuwa serikali haikuvunja baraza kwani kitendo cha waziri mkuu kujiuzuru moja kwa moja baraza linavunjika siyo kuvujwa!!
Labda wa kumtetea bwana mkubwa wangesema kuwa mipango iliyopo kwenye makaratasi ikikamilika (na hizo ni ndoto kwani hata ya kwake bagamoyo-msata km 50 imemshinda) bwana mkubwa atakuwa amejenga barabara nyingi kwani muda bado anao wa kufanya marekebisho,ila kwa sasa ni uendawazimu kumlinganisha mkapa na kikwete kujenga barabara achilia mbali uongozi kiujumla