Kikwete kajenga barabara nyingi kuliko awamu zote tatu?

Kaa la Moto

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2008
Posts
7,904
Reaction score
1,064
Jana nilimsikia huyu waziri mdogo wa biashara anaitwa Nyalandu katika kipindi cha Tuongee Asubuhi tar TV akisema kuwa awamu ya nne ambayo inaongozwa na Kikwete wamejenga barabara nyingi au niseme kilometa nyingi kuliko awamu zote tatu zilizotangulia kwa pamoja.

Hivi ni kweli? Je, ni barabara zipi?
 
barabara nyingi za nchi hii zimejengwa na serikali ya awamu ya tatu
kuna ambazo kikwete alikuta zinaendelea kujengwa lakini pesa yake ilikuwa tayari

hao wanataka kupiga cross na kufunga wenyewe
 
barabara nyingi za nchi hii zimejengwa na serikali ya awamu ya tatu
kuna ambazo kikwete alikuta zinaendelea kujengwa lakini pesa yake ilikuwa tayari

hao wanataka kupiga cross na kufunga wenyewe

Umesema vyema kabisa .JK amekuja anakuta kila kitu kwenye programu na yeye hana pesa za kujenga ila za kutalii Duniani .Hana muda but Mkapa ndiye apewe sifa kaacha zinajengwa na prog ilikuwa tayari so Nyalangu anajikomba tu kwa komba ili apate kamkate kake mnafiki mkubwa huyu .
 
Pengine kwa akili za baadhi ya watu wanaotetea unga wa familia zao si kosa lao kusema hivyo ni kosa la tumbo lisilojua kushiba. Tamaa nyingi. Mwanaume gani kusimama mbele ya wanaume wengine jasiri, akimsifu mwanaume mwingine; Bunge ovyo kama nini makofi kilo; Hata kama umetendewa vyema kiasi gani huwezi kunena eti kiwete kajenga barabara nyingi. HIZO BARABARA KAZIJENGA WAPI? LABDA ANGANI. MAANA HUYU JAMAA HATULII NCHINI. ANAKATA SANA ANGA. Kama hizo barabara zimejengwa angani nakubaliana na hoja. Mawaziri njaa, kila mtu njaa. Utu ni zaidi ya unga.
 
Walishamsoma huyo Mkere wakamjua. Anapenda kusifiwa sana. We jitokeze tu msifu hata mkewe ataweza kukupa.
 
barabara nyingi za nchi hii zimejengwa na serikali ya awamu ya tatu
kuna ambazo kikwete alikuta zinaendelea kujengwa lakini pesa yake ilikuwa tayari

hao wanataka kupiga cross na kufunga wenyewe

hapa pia nakataa, bara bara nyingi zilijengwa enzi za nyerere, labda mseme bara bara za kiwango cha lami ni mzee mkapa, lakini pia njia nyinge muhimu za uchukuzi km reli zimekufa enzi za mkapa.
 
Kabla ya Kikwete, awamu zote chini ya 10,000Kms, miaka 6 ya Kikwete zaidi ya 10,000Kms na bado zaja.
 
Sema wao wanaongoza kwa kuzindua barabara zilizoanzia awamu ya tatu! hakuna awamu hii inachofanya zaidi ya kutangaza udini na kuzurula nje ya nchi
 
Kikwete hajafanya chochote kwa muda wote wa uongozi wake!
Tazama shule ngapi za sekondari wakati wake na awamu zote zilizopita. Tazama zahanati. Tazama vyuo vikuu. Tazama barabara. Tazama viwanda. Halafu urudi useme uyasemayo.
 
Tazama shule ngapi za sekondari wakati wake na awamu zote zilizopita. Tazama zahanati. Tazama vyuo vikuu. Tazama barabara. Tazama viwanda. Halafu urudi useme uyasemayo.

kuna uwezekano wewe ni miongoni mwa zao la hizo shule. mbona mpango wa MMES na MMEM ulianza kabla ya kikwete?
 
Kabla ya Kikwete, awamu zote chini ya 10,000Kms, miaka 6 ya Kikwete zaidi ya 10,000Kms na bado zaja.
sema zimemlizikia msimu wa jk na kitu anachofanya jk ni kuendeleza yalioanzishwa na kibaya zaidi anamalizia vitu kwa magumashi mengi..nampongeza kwa kuleta pantoni kubwa na bovu kupita hata lile la mkoloni ndani ya miaka 3 panton linatoa moshi ka mabomba ya viwandani..
 
Kwa vile mpaka sasa hakuna takwimu na wachangiaji mada kuhusu kiasi gani cha barabara zilizojengwa kwa kila awamu, naogopa kusema ni awamu hii au ile ndiyo zaidi. Lakini dhana ya kwamba eti Rais anasafiri sana na kwa hiyo hawezi kuwa alijenga barabara nyingi kuliko watangulizi wake ni upungufu mkubwa katika uwezo wakujenga hoja. Ninavyofahamu mimi ni kwamba kumekuwa na hatua nzuri sana kuhusiana na maendeleo ya miundo mbinu katika awamu hizi mbili za uongozi. Kwa mfano barabara za Mbeya - Chunya mpaka Tabora, ile ya Singida mpaka Manyara, Somanga mpaka Ndundu, ile ya Mangaka Tunduru, na nyingine nyingi ni zao la awamu hii ya nne.
 
Kabla ya Kikwete, awamu zote chini ya 10,000Kms, miaka 6 ya Kikwete zaidi ya 10,000Kms na bado zaja.

@FaizaFoxy, kwenye red: Is is possible that awamu zilijejenga barabara 9,999km? na hivyo Kikwete kwa miaka sita (5 1/2 yrs) akawa amejenga 1km?

Kikwete hajafanya miradi mikubwa yoyote, mingi alikuta tayari imeshanza na malipo yake yalikuwa tayari. Yeye amekuwa 'mfunguzi' au tuseme mzindizu wa hii miradi: Mliman City, Uwanja wa Taifa, Daraja la Mkapa. Hata chuo kikuu cha Dodoma kama sio Mkapa kisimamia tungekuwa tunaongea lugha ya Daraja la Kigambano! Mkapa aliweza kutafuta 'sources' of funds na akasimamia ujenzi.

Muda wa Kikwete madarakani unazidi kuyoyoma, walio karibu naye wamsaidie ili afanye kitu kimoja cha maana, lakini hiii tabia ya 'wapambe' ya kutaka kuanika mapungufu ya marais waliopita haiwezi kumjenga. By the way tumesikia mengi kuhusu Mwl Nyerere, sasa Mkapa. Ni lini tutasikia kuhusu Mwinyi?
 
Kabla ya Kikwete, awamu zote chini ya 10,000Kms, miaka 6 ya Kikwete zaidi ya 10,000Kms na bado zaja.

Mimi ni urban planner hvyo najua vizuri hatua za kuwepo barabara.Ili uwe na barabara lazima uwe na plan ya hizo barabara ambazo either zitajengwa kwa lami,changalawe au vumbi.Barabara tulizonazo zimekuwa planned na Mwl Nyerere nyingi ya hizo zikajengwa kwa changalawe na vumbi,Mkapa ndiye aliyeanzisha kuzipandisha hizi barabara kuwa za lami Kikwete ameendeleza alichokianzisha mkapa.BUT TANZANIA BADO HAIJAUNGANISHWA KWA KIWANGO KINACHOTAKIW,Hebu ona mtu wa Dodoma,Iringa akitaka kwenda Mtwara lazima aje Dar and viseversa.Ukiwa Dodoma unataka kwenda Iringa Mbeya,Ruvuma lazima uende Morogoro.Hebu fikiria Mtu akitaka kwenda Mara akiwa Dar,lazima apitie Shy. n.k.BARABARA ZINAZOSIFIWA KUJENGWA MNAZIJUA WAKUU!
 
huyu mzee mwinyi ndo gurudumu lilipoanzia la kwenda mrama mpka jk senior(nyerere) alisema ikulu sio sehemu ya walanguzi..na kuhusu jk kashangia world gueness record kuwa ni rais wa kwanza kuudhuria misba na sherehe nyingi kuliko marais wote duniani na anayedhurula dunia kiasi cha kulingana na vasco da gama..
 
 
Tazama shule ngapi za sekondari wakati wake na awamu zote zilizopita. Tazama zahanati. Tazama vyuo vikuu. Tazama barabara. Tazama viwanda. Halafu urudi useme uyasemayo.
Akili za huyu dada zimekaa vyp sijui' viwanda?' kikwete amejenga kiwanda kipi? Shule- hebu angalia elimu inayotolewa angalia ufaulu, tangu 2006 alivyoingia ufaulu fm 4 iliku zaidi ya 60% leo wanafunzi 51% wanafeli,shule ya msingi eti kati ya watoto 10 wanaomaliza la saba watatu hawawezi kusoma kitabu cha darasa la pili, sita kati yao hawawezi kusoma kitabu cha kiingereza cha darasa la tatu....Chuoni wanafunzi wanamaliza bila kwenda field pia hawana walimu wa kutosha.Afya kumbuka kilichotokea kwa babu Loliondo na matokeo ya ziara za wataalamu wizara wa afya wanavyofungia hospitali na zahanati...Ntarudi baadaye.
 

Hivi tangia tupate uhuru wa bendera kweli tumeweza kujenga barabara zetu wenyewe au tunabebwa na wahisani kwa mikopo nafuu na misaada lukuki..............isiyo na kikomo...............unapoona bajeti ya maendeleo inafadhiliwa na wahisani wa ulaya kwa asilimia 80 hivi tuna lolote lile la kujivunia.................................kweli mwenye macho haambiwi tazama................
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…