jk lazima ataulizwa maswali magumu sana. Mojawapo yatakuwa haya yafuatayo:-
(i) Mhe. rais, serikali yako imejitahidi sana kupambana na mafisadi ikilinganishwa na serikali zingine zilizopita. wananchi tumeshuhudia serikali ikiwafikisha mahakamani watuhumiwa wazitowazito, jambo ambalo ni nadra sana. hongera sana mhe. rais. sasa watanzania wengi wangependa kujua, je, umejipangaje kuendeleza vita hii nzito dhidi ya mafisadi katika awamu yako ya pili ya uongozi.
(ii) Mhe. rais, katika eneo ambalo serikali imeliwekea mkazo ni ukuzaji wa uchumi. wananchi wengi wameshuhudia hali ya maisha ikiboreka japo siyo kwa kasi kubwa sana kutokana na kuyumba kwa uchumi duniani. Sasa, labda wananchi wangependa kupata maelezo yako namna utakavyoongeza kasi ya kukuza uchumi.
(iii) Mhe. rais, baadhi ya wananchi wanasifu sana uungwana wako wa kuwaruhusu watuhumiwa na fedha za EPA kurejesha fedha walizokwapua kwenye akaunti ya madeni ya nje. hongera sana mhe. sasa labda tungependa utufahamishe japo kwa ufupi, fedha hizo zimewanufaishije wakulima wetu.
(iv) Mhe. maeneo mengi uliyotembelea umekuwa ukitoa ahadi nyingi kwa wananchi na sisi kama waandishi wa habari kwa kuzingatia umakini wako tuna imani unaweza kutekeleza zote. lakini baadhi ya wananchi wana mashaka. je, unaweza kutoa maelezo mafupi tu namna utakavyohakikisha ahadi zote, ukiondoa sababu zilizo nje ya uwezo wako.
(v) Mhe. rais kwanza nikupongeze kwa juhudi na bidii zako za kusafiri mara kwa mara nje ya nchi kwenda kuhemea misaada kwa ajili ya wananchi. tunajua ni safari za kuchosha lakini unafanya kutokana na uchungu wa wananchi wako maskini. tungependa utufahamishe faida ulizopata kutokana na safari hizo.
(vi) Mhe. rais kumekuwa na tetesi na malalamiko ya chinichini kwamba wewe ni mdini. vyeo vingi serikalini umejaza waislamu wenzio bila kujali uwezo na inasemekana hata suala la mahakama ya kadhi na nchi yetu kujiunga na oic umeamua kunyamaza lakini umewaahidi waislam wenzio kwamba utaishughulikia kimya kimya. tetesi hizi zimewashtua sana viongozi wa dini zingine hususani wakristo. je, unasemaje kuhusu suala hili.
(vii) Mhe. rais utafiti umeonesha kuwa watanzania wengi bado wanakuunga mkono. lakini baadhi inaonekana wameanza kupata mashaka ya kukuunga mkono. je, hao walio na mashaka unapenda kuwaambia nini ili wasiwe na mashaka.
(viii) Mhe. rais una ujumbe gani unaotaka kuwaeleza watanzania waliojiandikisha kupiga kura