Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Ukiona mtu amechafuka na tope na maji yanayomzunguka ni ya matope ujue kwamba yeyote atakayejaribu kumsafisha kwa maji hayo naye atajikuta amechafuka na tope.
Kabla ya kuletwa tena na serikali ripoti ya utekelezaji wa maamuzi ya bunge juu ya richmond Lowassa atakuwa amesafishwa rasmi-siyo na bunge, siyo na magazeti bali na rafiki wa siku nyingi na mshirika wake katika safari ya siasa. Si kwamba JK ana uchaguzi katika hilo; hana. Na wana CCM wote (hamaanisha wote) watasema "amina". Na bomu la wapiganaji ccm litakuwa limeteguliwa kitaalam. EL ametambua kuwa : mlete rafiki yako karibu lakini adui yako karibu zaidi.
Ukiona mtu amechafuka na tope na maji yanayomzunguka ni ya matope ujue kwamba yeyote atakayejaribu kumsafisha kwa maji hayo naye atajikuta amechafuka na tope.
No walikuwa na uwezo wa kuchukua nchi 2015, 2020 kama strategy zao zingekuwa makini zaidi.
Japo umesema kwa ku-conclude,still I hope wanachance kubwa ya kushika nchi, if and only if they will face reality na kupata wapiga kura
Maana kazi si kutetea maamuzi yao, kazi ni kwa jinsi gani kila wanachofanya wanaathiri wapiga kura.
siasa is a game though,
Ukiona mtu amechafuka na tope na maji yanayomzunguka ni ya matope ujue kwamba yeyote atakayejaribu kumsafisha kwa maji hayo naye atajikuta amechafuka na tope.
Vyama vya upinzani visahau kuchukua nchi kwa njia ya kura unless mambo yafuatayo yafanyike kwanza.
1. Waongeze nguvu zao katika kudai mabadiliko ya Katiba ili kuwe na Tume huru ya uchaguzi itakayodhibiti mbinu zote chafu za wizi wa kura na kumanipulate final tallies of election results- Kwa hili sisiM imejipanga vilivyo kulizima.
2. Wakiisha pata Tume huru ya Uchaguzi, wagombee ubunge kwanza si Mbowe, Lipumba et al ili kulichukua bunge yaani wawe na filibuster majority ya kupitisha agenda za mageuzi, hili nalo kwa sisiM ni bora punda afe mzigo ufike wapo tayari kwa lolote.
3. Kukiisha kuwa mazingira ya usawa na haki na uhuru katika chaguzi, na baada ya kuwaonesha wananchi kuwa wapinzani wanaweza tena zaidi ya sisiM hapo tunaweza pata rais wa kwanza wa kidemokrasia halisi katika historia ya nchi.
Vinginevyo haya yoote tunayoongea ni kelele za mlango, sisiM wanajua wanachokifanya kwani style yao ni kuwa, Jeshi la wananchi, UWT, Polisi na kila chombo kilicho katika serikali ni lazima kijue kuwa masilahi yao ni masilahi ya CCM, kushindwa kwa CCM ni kupoteza kwaoa maslahi hayo. Hivyo wamekula viapo vya mioyoni kuwa watailinda CCM mpaka tone la mwisho.
Ukweli ni kwamba Tanzania ilitakiwa ifikirie kuingia kwenye siasa za vyama vingi labla mwaka 2080. VINGINEVYO KUWE NA WA KUFANYIWA KAFARA KWA AJILI YA UKOMBOZI WA KWELI WA KULETA DEMOKRASIA- Un-option which is not recommended by any one unless you feel useless and stranded for you life is no difference to death because of "POVERTY"
Kabla ya kuletwa tena na serikali ripoti ya utekelezaji wa maamuzi ya bunge juu ya richmond Lowassa atakuwa amesafishwa rasmi-siyo na bunge, siyo na magazeti bali na rafiki wa siku nyingi na mshirika wake katika safari ya siasa. Si kwamba JK ana uchaguzi katika hilo; hana. Na wana CCM wote (hamaanisha wote) watasema "amina". Na bomu la wapiganaji ccm litakuwa limeteguliwa kitaalam. EL ametambua kuwa : mlete rafiki yako karibu lakini adui yako karibu zaidi.
Hasa ukizingatia kuwa Six naye alishapigwa bit la nguvuMkuu Mwanakijiji,
Na inasemekana ktk mkutano wa bunge ujao mwezi Novemba, wabunge wote wa CCM watakaa kama kamat ya chama na kukubaliana kuanza upya na kusahau yaliyopita na hapo watatangaza rasmi kuwa hoja ya ufisadi imefungwa ndani ya chama na yaliyobaki yashughulikiwe na vyombo vya dola.
Baada ya hapo itafuata ripoti ya utekelezaji ya masuala ya richmond (iliyofanyiwa marekebisho na mkulu) na hapo itatamkwa wazi kwamba EL hakuwa na kosa kisheria bali alishauriwa vibaya na wataalamu ambao wamekwisha onywa.
Serikali kupitia waziri mkuu itatoa taarifa ya kuufunga mjadala wa richmond ndani ya chama na nje ya chama. Huu ndio utakuwa mwisho wa kikundi cha akina Mwakyembe na EL atakuwa huru rasmi baada ya kikao hicho cha bunge.