Ameiga mambo ya Don Corleon. Siasa za TZ zinataka umakini mkubwa sana kuzifuatilia maana kusema kweli wahusika wengi wakubwa picha wanazo potray sio zao halisi. Ni wanafiki wa kupindukia. Siwezi shangaa hili likitokeaKabla ya kuletwa tena na serikali ripoti ya utekelezaji wa maamuzi ya bunge juu ya richmond Lowassa atakuwa amesafishwa rasmi-siyo na bunge, siyo na magazeti bali na rafiki wa siku nyingi na mshirika wake katika safari ya siasa. Si kwamba JK ana uchaguzi katika hilo; hana. Na wana CCM wote (hamaanisha wote) watasema "amina". Na bomu la wapiganaji ccm litakuwa limeteguliwa kitaalam. EL ametambua kuwa : mlete rafiki yako karibu lakini adui yako karibu zaidi.
Njaa bwana, ninaamini kama vya vya upinzani vingejiunga pamoja kama walivyo fanya Kenya CCM ingetoka, shida wataanza kugombania madaraka.
Mkuu, sioni jinsi majeshi hayoyavyoweza kufanya kinyume na matakwa ya Rais. Maana Rais/Mwenyekiti wa CCM ndie amiri jeshi mkuu wa majeshi yote ya ulinzi na usalama, nchini. Vile vile, kwa wao kufanya kinyume ni sawa na uasi.Vinginevyo haya yoote tunayoongea ni kelele za mlango, sisiM wanajua wanachokifanya kwani style yao ni kuwa, Jeshi la wananchi, UWT, Polisi na kila chombo kilicho katika serikali ni lazima kijue kuwa masilahi yao ni masilahi ya CCM, kushindwa kwa CCM ni kupoteza kwaoa maslahi hayo. Hivyo wamekula viapo vya mioyoni kuwa watailinda CCM mpaka tone la mwisho.
sentensi nzito sana hiyo. Kuna hidden message hapo. Nadhani wanaJF tungependa ufafanuzi zaidi...
kwa maelezo mafupi tu ni kwamba, jk anahitaji wapiganaji wake wote waliomuwezesha kushinda 2005 ili aweze kushinda tena na kwa urahisi 2010. Na anadhani el ndie mpiganaji mwenye mbinu zote za ushindi na ndie anaeweza kuwaunganisha upya wapiganaji wote wa 2005. Anajua pia kuwa, wanamtandao wa ushindi wa jk wako kwa el. Na wanamtandao wote bado wanamuamini sana el. Hii inathibika zaidi kwa jinsi wanamtandao wanavyojaribu kumkwepesha na tuhuma za ufisadi na kumsafisha kwa uwezo wao wote.
Mkuu Mwanakijiji,
Na inasemekana ktk mkutano wa bunge ujao mwezi Novemba, wabunge wote wa CCM watakaa kama kamat ya chama na kukubaliana kuanza upya na kusahau yaliyopita na hapo watatangaza rasmi kuwa hoja ya ufisadi imefungwa ndani ya chama na yaliyobaki yashughulikiwe na vyombo vya dola.
Baada ya hapo itafuata ripoti ya utekelezaji ya masuala ya richmond (iliyofanyiwa marekebisho na mkulu) na hapo itatamkwa wazi kwamba EL hakuwa na kosa kisheria bali alishauriwa vibaya na wataalamu ambao wamekwisha onywa.
Serikali kupitia waziri mkuu itatoa taarifa ya kuufunga mjadala wa richmond ndani ya chama na nje ya chama. Huu ndio utakuwa mwisho wa kikundi cha akina Mwakyembe na EL atakuwa huru rasmi baada ya kikao hicho cha bunge.
Well, vyanzo vingine vya karibu vinadokeza kuwa kambi ya EL ilishtushwa na kauli ya JK kuwa la Kagoda litashughulikiwa bila ya kujali urafiki. RA na EL hawakupendezwa na kauli hiyo. Hivyo EL akatumwa kumbipu Jk kuwa afikirie mara mbili kwani wametoka "mbali"
Usiwape watu jina ambalo hawana .Hakuna cha njaa . Kam tunataka mabadiliko jamnbo moja dhahiri na la kusimamiwa ni Tume ya Uchaguzi kuwa huru . Tume ikisha kuwa ya watu wote nakueleza CCM itaisha hata bila ya kuunganakwa Upinzani.Tume huamua kutangaza matokeo kwa nguvu wale returnig officers wote wanakuwa na maelekezo maalumu. Mchawi ni tume ya Uchaguzi wapinzania waende mahakamani sasa iwe huru .
JK is on diveded kingdom then. He wants to clean EL at the same time he wants to pursue Kagoda issue. hapo hawezi kuchagua yote..kuna atakalolitupa chini.Well, vyanzo vingine vya karibu vinadokeza kuwa kambi ya EL ilishtushwa na kauli ya JK kuwa la Kagoda litashughulikiwa bila ya kujali urafiki. RA na EL hawakupendezwa na kauli hiyo. Hivyo EL akatumwa kumbipu Jk kuwa afikirie mara mbili kwani wametoka "mbali"
well said kiongozi.tuko ukurasa mmoja.hakuna aliyewahi kuwa masafi kati ya hawaWeli at the end wote watachafuka. Swala la msingi ni jee mmoja au wote wakichafuka SISI tunafanya nini? Baada ya kuona uchafu no one cares. By the way ni lini huyu msafishaji aliwahi kuwa Msafi ndo sasa tuseme atachafuka??
well said kiongozi.tuko ukurasa mmoja.hakuna aliyewahi kuwa masafi kati ya hawa
Well, vyanzo vingine vya karibu vinadokeza kuwa kambi ya EL ilishtushwa na kauli ya JK kuwa la Kagoda litashughulikiwa bila ya kujali urafiki. RA na EL hawakupendezwa na kauli hiyo. Hivyo EL akatumwa kumbipu Jk kuwa afikirie mara mbili kwani wametoka "mbali"