Kikwete kumalizia kumsafisha Lowassa

Kikwete kumalizia kumsafisha Lowassa

Lowasa nafasi iliyobaki kwa yeye kuwa Rais Tanzania labda ni kujaribu kumvaa Kikwete mwakani.Vinginevyo ni kujidanganya.Pamoja na uzezeta wa wapiga kura wa Tanzania lakini Lowasa hatokuja kuwa Rais wa Tanzania 2015 au baada ya hapo.Ana nguvu ya pesa,ana nguvu CCM lakini ajue kwamba laana ya ufisadi inayomwandama haiwezi kumwacha kamwe na haiwezi kutoka vichwani mwa watanzania hata kama atasafishwa vipi.Na kama anajua kupima nyakati basi pia ajue kuwa wakati wake umeshapita wa kuwa Rais wa Tanzania.
 
Kabla ya kuletwa tena na serikali ripoti ya utekelezaji wa maamuzi ya bunge juu ya richmond Lowassa atakuwa amesafishwa rasmi-siyo na bunge, siyo na magazeti bali na rafiki wa siku nyingi na mshirika wake katika safari ya siasa. Si kwamba JK ana uchaguzi katika hilo; hana. Na wana CCM wote (hamaanisha wote) watasema "amina". Na bomu la wapiganaji ccm litakuwa limeteguliwa kitaalam. EL ametambua kuwa : mlete rafiki yako karibu lakini adui yako karibu zaidi.
Ameiga mambo ya Don Corleon. Siasa za TZ zinataka umakini mkubwa sana kuzifuatilia maana kusema kweli wahusika wengi wakubwa picha wanazo potray sio zao halisi. Ni wanafiki wa kupindukia. Siwezi shangaa hili likitokea
 
Njaa bwana, ninaamini kama vya vya upinzani vingejiunga pamoja kama walivyo fanya Kenya CCM ingetoka, shida wataanza kugombania madaraka.


Usiwape watu jina ambalo hawana .Hakuna cha njaa . Kam tunataka mabadiliko jamnbo moja dhahiri na la kusimamiwa ni Tume ya Uchaguzi kuwa huru . Tume ikisha kuwa ya watu wote nakueleza CCM itaisha hata bila ya kuunganakwa Upinzani.Tume huamua kutangaza matokeo kwa nguvu wale returnig officers wote wanakuwa na maelekezo maalumu. Mchawi ni tume ya Uchaguzi wapinzania waende mahakamani sasa iwe huru .
 
Vinginevyo haya yoote tunayoongea ni kelele za mlango, sisiM wanajua wanachokifanya kwani style yao ni kuwa, Jeshi la wananchi, UWT, Polisi na kila chombo kilicho katika serikali ni lazima kijue kuwa masilahi yao ni masilahi ya CCM, kushindwa kwa CCM ni kupoteza kwaoa maslahi hayo. Hivyo wamekula viapo vya mioyoni kuwa watailinda CCM mpaka tone la mwisho.
Mkuu, sioni jinsi majeshi hayoyavyoweza kufanya kinyume na matakwa ya Rais. Maana Rais/Mwenyekiti wa CCM ndie amiri jeshi mkuu wa majeshi yote ya ulinzi na usalama, nchini. Vile vile, kwa wao kufanya kinyume ni sawa na uasi.

Inabidi mwenyekiti wa chama asiwe Rais wa nchi.
 
sentensi nzito sana hiyo. Kuna hidden message hapo. Nadhani wanaJF tungependa ufafanuzi zaidi...

Kwa maelezo mafupi tu ni kwamba, JK anahitaji wapiganaji wake wote waliomuwezesha kushinda 2005 ili aweze kushinda tena na kwa urahisi 2010. Na anadhani EL ndie mpiganaji mwenye mbinu zote za ushindi na ndie anaeweza kuwaunganisha upya wapiganaji wote wa 2005. Anajua pia kuwa, wanamtandao wa ushindi wa JK wako kwa EL. Na wanamtandao wote bado wanamuamini sana EL. Hii inathibika zaidi kwa jinsi wanamtandao wanavyojaribu kumkwepesha na tuhuma za ufisadi na kumsafisha kwa uwezo wao wote.
 
kwa maelezo mafupi tu ni kwamba, jk anahitaji wapiganaji wake wote waliomuwezesha kushinda 2005 ili aweze kushinda tena na kwa urahisi 2010. Na anadhani el ndie mpiganaji mwenye mbinu zote za ushindi na ndie anaeweza kuwaunganisha upya wapiganaji wote wa 2005. Anajua pia kuwa, wanamtandao wa ushindi wa jk wako kwa el. Na wanamtandao wote bado wanamuamini sana el. Hii inathibika zaidi kwa jinsi wanamtandao wanavyojaribu kumkwepesha na tuhuma za ufisadi na kumsafisha kwa uwezo wao wote.

hivi el kampa limbwata jk,anamg'ang'ania wa nini,hata kama ni fadhili kwa kumsaidia kuukwa uraisi 2005 lakini sio kwa mtaji wa kuimaliza nchi,hivi jk mshauri wake wa mambo ya siasa ni nani mulipata kumjua naomba nifahamishwe kwa sababu anaonekana ni mtu hana akili hata moja ya kuamua mambo yake na kusimamia maamuzi yake aachane na lowassa mwizi huyo
 
Mkuu Mwanakijiji,

Na inasemekana ktk mkutano wa bunge ujao mwezi Novemba, wabunge wote wa CCM watakaa kama kamat ya chama na kukubaliana kuanza upya na kusahau yaliyopita na hapo watatangaza rasmi kuwa hoja ya ufisadi imefungwa ndani ya chama na yaliyobaki yashughulikiwe na vyombo vya dola.

Baada ya hapo itafuata ripoti ya utekelezaji ya masuala ya richmond (iliyofanyiwa marekebisho na mkulu) na hapo itatamkwa wazi kwamba EL hakuwa na kosa kisheria bali alishauriwa vibaya na wataalamu ambao wamekwisha onywa.

Serikali kupitia waziri mkuu itatoa taarifa ya kuufunga mjadala wa richmond ndani ya chama na nje ya chama. Huu ndio utakuwa mwisho wa kikundi cha akina Mwakyembe na EL atakuwa huru rasmi baada ya kikao hicho cha bunge.

Mkuu nakusoma sana.....kama kuna asiye kuelewa basi tena.....CCM inapokuja kwenye uchaguzi...ndio utajua how serious they are......nafikiri mifano tumeiona kwenye chaguzi ndogo zilizopita........

........huko nyuma nilishawaambia kuwa matatizo ya kufichuka kwa siri za ufisadi ni confusion iliyokuwepo kati ya outgoing utawala Vs incoming utawala........sasa baada ya vikao virefu ambavyo mwana JF mmoja hapa aliwahi gusia........mambo yanaelekea kuwa mswano on the side of CCM.........kwa hilo CCM nawapa........a thumb up.......

......in addition Rais kishaanza kupiga bao la kisigino mapemaaaa.........
 
Let us be serious, Huyo EL hana akili ya kufanya hayo unayozungumza he is not bright!! yeye ni mwizi tena jambazi maana kuna wezi wenye akili nyingi kwamba wanasumbua hata kuwakamata au kuwang'amua kwa huyu jamaa kama unakumbuka vizuri ilikuwa akitoa maagizo ya Richmond alikuwa anaandika vimemo ndo vikampa shida kama unakumbukumbu nzuri utakumbuka hata mama Kilango wakati wa mjadala alisema EL "ukome kuwa unatutishia kwa vijimemo vyako" yeye being a senior civil servant wa siku nyingi alitakiwa kujuwa kuwa vijimemo vinaweza kufire back!! kwa hivi had he been smart asingekuwa anaandika hii ni proof tosha kwamba jamaa is a dull nguvu nyingi kuliko akili na busara!! kwa mantinki hiyo I don't see him akifanya move ya kumrudisha tena katika top post no matter who says what !! He can just forget. lakini kama kweli ana mpango huo mimi binafsi nafikiri mzee Ndesamburo wakati akichangia mjadala wa Richomond alikuwa amependekeza hivi "Hawa watu wapigwe risasi hadharani kama China wanavyofanya" that was the best solution, hii kelele yote ingeishia hapo sijui kwanini Bunge alikukubali pendekezo hilo!! I don't believe in capital punishment, lakini kwa watu wasiokuwa na roho ya kujuta, na kujinyenyekeza wakaomba msamaha na kujutia makosa yao !! Mzee Ndesamburo had the best solution.Mungu Ibariki Tanzania
 
Well, vyanzo vingine vya karibu vinadokeza kuwa kambi ya EL ilishtushwa na kauli ya JK kuwa la Kagoda litashughulikiwa bila ya kujali urafiki. RA na EL hawakupendezwa na kauli hiyo. Hivyo EL akatumwa kumbipu Jk kuwa afikirie mara mbili kwani wametoka "mbali"
 
kazi sana, ndio siasa ztu waafrika, maana ni kulindana tu, sijui mzalendo wa kweli atakuja lini?
 
Well, vyanzo vingine vya karibu vinadokeza kuwa kambi ya EL ilishtushwa na kauli ya JK kuwa la Kagoda litashughulikiwa bila ya kujali urafiki. RA na EL hawakupendezwa na kauli hiyo. Hivyo EL akatumwa kumbipu Jk kuwa afikirie mara mbili kwani wametoka "mbali"

Undugu na urafiki unatumaliza jamani. Ndo maana wengi wamesema Kikwete si mssafi hata kidogo. Kama anataka kupambana na mafisadi aanze na nafsi yake. Ajisafishe na kutangaza kuwa sasa hana rafiki. Ajitoe kama sacrifice kwa ajili ya Taifa. Then tutamuona ndio kiongozi jarisi na bora.
 
Usiwape watu jina ambalo hawana .Hakuna cha njaa . Kam tunataka mabadiliko jamnbo moja dhahiri na la kusimamiwa ni Tume ya Uchaguzi kuwa huru . Tume ikisha kuwa ya watu wote nakueleza CCM itaisha hata bila ya kuunganakwa Upinzani.Tume huamua kutangaza matokeo kwa nguvu wale returnig officers wote wanakuwa na maelekezo maalumu. Mchawi ni tume ya Uchaguzi wapinzania waende mahakamani sasa iwe huru .

Sawa mkubwa, siana nia ya kuwapa watu majina ambayo hawana, ila nia yangu ni kuonyesha hali halisi kuwa hata wale ambao wanaonekana kuwa mstari wa mbele ktk kutetea wananchi,inafika mahali unashanga speed inapungua kama vile wamefungwa peed cavana. Ukifuatilia sana unakuta kapewa kitu kidogo au cheo fulani na huo ndo unakuwa mwisho wake, hutamsikia tena akitetea kama mwanzoni.
 
Well, vyanzo vingine vya karibu vinadokeza kuwa kambi ya EL ilishtushwa na kauli ya JK kuwa la Kagoda litashughulikiwa bila ya kujali urafiki. RA na EL hawakupendezwa na kauli hiyo. Hivyo EL akatumwa kumbipu Jk kuwa afikirie mara mbili kwani wametoka "mbali"
JK is on diveded kingdom then. He wants to clean EL at the same time he wants to pursue Kagoda issue. hapo hawezi kuchagua yote..kuna atakalolitupa chini.
 
EL anaishi na kupumua hadharani kwa huruma ya JK. JK hawezi kumsafisha EL kwa viwango alivyochafuka hata kama ataamua kusimama mbali na kumrushia maji kwa bomba. Tusubiri tu JK amalize ngwe yake ya Urais na Rais ajaye kama hatatokana na kundi lao EL atapelekwa mahakamani tu.Akina Mramba wanashtakiwa kwa makosa waliofanya wakati wa utawala wa Mkapa kwa nini isiwe hivyo kwa EL?
 
Weli at the end wote watachafuka. Swala la msingi ni jee mmoja au wote wakichafuka SISI tunafanya nini? Baada ya kuona uchafu no one cares. By the way ni lini huyu msafishaji aliwahi kuwa Msafi ndo sasa tuseme atachafuka??
well said kiongozi.tuko ukurasa mmoja.hakuna aliyewahi kuwa masafi kati ya hawa
 
Hili wala halinishangazi sana JK kuamua kumsafisha EL, siasa za tanzania zimejaa unafiki! si mmemsikia Makamba eti sasa anajifanya kumsifia SS, huyu mzee hana hata aibu anayakana maneno yake mwenyewe eti wau wanajaribu kuwagombanisha na SS, hata Guninita nae sasa anamuunga mkono SS, yote hii ni baada ya kumsikia bosi wao JK kasema hana ugomvi na wanaopinga ufisadi. Unafiki! unafiki! unafiki! mtupu umejaa ndani ya CCM. aaah haya tusubiri tamthilia nyingine hii ya richmond inaanza kupoteza mvuto sasa. ndio nasema tamthilia sababu CCM wote ni wasanii.
 
well said kiongozi.tuko ukurasa mmoja.hakuna aliyewahi kuwa masafi kati ya hawa

Ni kweli usemayo. lakini Wadanganyika wengi tu vipofu. Njaa na Ujinga unawafanya watanzania waone Viongozi ni wasafi japo UCHAFU wao juu ya miili yao unachukua 20% ya uzito wao.
 
Ni muda muafaka pia kuanza kufikiria kama kuna haja ya ofisi ya WAZIRI MKUU kuendelea kuwepo wakati tuna MAKAMU wa RAIS. Angalia jinsi EL alivyoitumia ofisi hiyo kuingilia kazi za waziri wa nishati na mwanasheria mkuu.
 
Kazi ipo hapo,mimi naona kwa mtazamo wangu kazi iko kwetu wananchi,wanaweza kufanya lolote katika utashi wao lakini hawawezi kununua ufahamu wetu...kwa hoja zetu za nguvu tunaweza kuanza na hao wabunge( Mafisadi ) kuwanyima nafasi ya kurudi bungeni..wataanza kujua tuko serious
 
Well, vyanzo vingine vya karibu vinadokeza kuwa kambi ya EL ilishtushwa na kauli ya JK kuwa la Kagoda litashughulikiwa bila ya kujali urafiki. RA na EL hawakupendezwa na kauli hiyo. Hivyo EL akatumwa kumbipu Jk kuwa afikirie mara mbili kwani wametoka "mbali"

Kweli anapib tena kaweka loudspeaker. Ngoja tusikie kama jamaa atapokea au vipi? Ila Mwanahalisi imeshabonyeza kuwa ni kwa nini atakiwa assign NUMBER BUSY....
 
Back
Top Bottom