Tetesi: Kikwete kumrithi Ban Ki-Moon

Tetesi: Kikwete kumrithi Ban Ki-Moon

HUYU NDIYE MRITHI WA BAN KI-MOON

Mbona kama nafasi yetu Afrika Kofi Anan kamaliza majuzi tu, itawezekanaje mkuu. Najiuliza tu.
 
mtoa uzi anashindwa kutofautisha ccm na Un pili hajui utaritibu wa uteuzi wa katibu....
hizi tetesi akamsimulie mkewe tu huwezi kumpaisha mtu ambaye ameleta hasara nchini na kutuachia majipu chungu nzima.
hizo tetesi zako ziishie chumbani
 
Nafasi ya ukatibuu mkuu wa umoja wa mataifa sio cheo cha umonita kila mtu anaweza . kama ulidhani hivyo Umepotea
 
kama tulikosa kipindi cha Dr. Salim ndiyo basi tena tusubiri kizazi kijacho.
 
Kikwete anapendwa sana na wazungu zaidi ya waswahili!! mnyonge mnyongeni Ila haki yake mpeni!! Jk tunakuombea uzidi kujitangaza Tanzania
Ukiona kiongozi yeyote wa Africa anapendwa na Wazungu, jiulize sana Why him??????? Yaani juilize sana!
 
Huyu Jamaa namdharau sana kwa alivyoendesha hii nchi :
Tanzania imeliwa sana na watu Wa ulaya.....hizi rasilimali zimepigwa sana...

My Take;;
Jakaya kikwete ni mtu hatari sana, huyu jamaa yaelekea ni mzuri kwao na wanalipa fadhila kwa mkwere baada ya kuwaachia wakaiba Tembo na blaa blaa zingine
 
....post to u.n .......
if you think he qualify....
hapa ni helpless.....
n.b
****
as chair of ccm he should finalise a [HASHTAG]#znz[/HASHTAG] saga 1st.
**Total disqualifications.
that post means "usuluhishi kwa mataifa mbalimbali hapa kwako znz ni shida tafrani haki inapokwa.
Heshima kwako mkuu huyu umempa za uso na kumkata maini,JK arithi kiti cha nani??kwa uwezo upi???amuulize Migiro atamweleza UN panavyowaka moto yule mama ni msomi mzuri tu lakini palimpeleka puta hadi akaondolewa.
 
Hivi wadau hamsikii harufu yoyote?
Huu uzi,una harufu ya bangi bangi tu

Mtu hajui methodologies zipi zinatumika kumchagua mwenyekiti wa UN

Na sifa zipi zinaangaliwa,

Jitu linakurupuka tu.
 
endeleeni na ndoto..naona ni mwendelezo wa jk kutaka kuwa hot kweny media...
hawez u GS,.na bora asiwe2 ataenda kutuaibisha tu uko Kufisadi....
nchi imemshinda sembuse un,.tukumbuke aliomba poo akasema naomba mda wangu uishe wa urais maana ni mgumu sana..akae tu ccm2 azeekee pale...,...
alafu mnasema wazungu wanampenda,...wazungu watakupenda ukiwa connector wa dili zao,..mbona mugabe hawampendi,...7bu hawapi dili,..kikwete kawapa dili wazungu za kuhujumu nchi......
lo2.jpg


mfalme wa anga.......
 
kura Tanzania ya kumchagua Ban Kimoon ni kama iltolewa ili kupata fadhila kwa kuwa haya yalifanyika kupitia Ban na nchi yake baada ya uchaguzi
1. Korea kusini ikajitolea kujenga daraja kule Kigoma
2. Ikajitolea msaada wa kusaidia ICT UDSM
3. akampa Migiro Unaibu katibu mkuu UN
4. Inaendelea na ujenzi wa barabara Arusha
Tunajuliza hizi propaganda zenu ni kwa kuwa mtukufu ameshauza vitalu vya gesi na kumaliza madini yetu ardhini au kunakingine anataka kufanya japo kutuuza kabisa sisi wananchi tusio na hatia?
waje wajibu hapa wa lumumba wanaosifa kila kitu.....
wanjiita team kusifia
 
Kuwa katibu mkuu UN aingalii tu uanadiplomasia Wa MTU Bali pia uwezo Wa MTU ki akili. Nina wasiwasi uwezo Wa Kikwete upstairs haumpi nafasi ya kuichukua nafasi hiyo. Uwezo Wa kujieleza Na kutiririka kwa kiingereza Kikwete Hana pia

Tiba
 
HUYU NDIYE MRITHI WA BAN KI-MOON
_________________________________________________
Dr. Jakaya Mrisho Kikwete Rais mstaafu wa Tanzania kwa awamu ya nne (2005 – 2015) ni miongoni mwa wanadiplomasia wakubwa duniani wenye ushawishi na uwezo wa utatuzi wa matatizo mbalimbali duniani, sio tu kwa sababu viongozi wa mataifa mbalimbali duniani wanamkubali bali kwa uwezo wake katika masuala ya kidiplomasia.

Alizaliwa mwaka 1950 Oct katika mkoa wa Pwani Wilaya ya Bagamoyo katika kijiji cha Msoga katika familia ya kisiasa na kilimo. Baba yake Mzee Mrisho Kikwete alikuwa ni Mkuu wa Wilaya (DC) ya Pangani na babu yake naye ambaye alikuwa ni Chief wa Wakwere, Chief Kikwete.


Alipata elimu ya Msingi Msoga kabla ya kujiunga na shule ya sekondari Kibaha akiwa pia ni mwenyekiti serikali ya wanafunzi na vijana wa TANU 1966 na Baadaye Tanga school. Ambapo alijiunga na chuo kikuu Dar es salaam, ambapo pia alikuwa mwenyekiti wa serikali ya wanafunzi na kuhitimu Shahada ya uchumi 1975 alipojiunga na Jeshi.

Aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Singida 1977 na baadae kuhamishiwa Zanzibar kwa kazi maalum baada ya muungano wa TANU na ASP mpaka kufikia mwaka 1980 aliporudishwa makao makuu ya chama (CCM).

Mwaka 1988 aliteuliwa kuwa mbunge na pia NaibuWaziri wa Nishati na Madini chini ya uongozi wa MH. Al Ahsan Mwinyi mpaka kufikia mwaka 1990 ambapo aliteuliwa kuwa Waziri kamili wa maji nishati na madini.

Mwaka 1994 aliteuliwa kuwa waziri wa uchumi akiwa na umri wa miaka 44 ambapo alikuwa ni waziri mwenye umri mdogo kuwahi kuteuliwa. Kufika mwaka 1995 alitueliwa kuwa waziri wa mambo ya nje chini ya uongozi wa Rais Benjamin W. Mkapa na kuongoza wizara hiyo kwa miaka 10 mpaka kufikia mwaka 2005 ambapo alichaguliwa kuwa Rais wa Tanzania.

Katika Nyanja za kimataifa Mh. Jakaya Kikwete ni miongoni mwa wanadiplomasia ambae amefanya mambo mengi katika bara la Afrika na Dunia, kama vile kutatua migogoro katika nchi za maziwa makuu, jumuiya ya Afrika Mashariki akiwa kama Mwenyekiti wake (EAC) baadhi ya mambo ambayo dunia inampongeza ni pamoja na Mwaka 2005 akiwa kama Mwenyekiti mwenza wa mikutano wa Helsinki (Helisinki process on Globalization and Democracy) aliweza kuongoza mikutano huo kwa mafanikio makubwa.

2013 akiwa ndiye kiongozi pekee kutoka Afrika aliyeshiriki katika mkutano nchi za umoja wa Ulaya EU wa Alpbach Austria aliliwakilisha bara la Afrika vyema katika kutafuta fursa za maendeleo na ushirikiano kimataifa.

Dr. Jakaya Kikwete pia amekuwa Mjumbe tume ya Elimu Duniani ikiongozwa na waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown katika kutafuta namna ya kugharamia Elimu duniani (TICFGEO) kwa mwaka 2015.

Kwa mwaka huu 2016 Dr. Jakaya Kikwete ameteuliwa kuwa Mjumbe wa kamati ya Amani nchini Libya katika kusaidia kurudisha amani nchini Libya
Pia amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mwenza kwa tume ya kusaidia afya ya Mama na motto duniani kwa mwaka huu 2016 ikiwa ni katika jitihada zake kuhakikisha Afya na mama na motto duniani kote zinalindwa.

Kwa mtazamo huo nina imani kubwa kwa kipindi ambacho Mh. Ban Ki-Moon ataachia ofisi, Mwanadiplomasia huyu ndiye atakayechukua viatu vyake .

Hizi ni baadhi ya tuzo za heshima alizowahi kupata toka nchi mbalimbali...

2007: Sullivan Honor
2007: The AAI African National Achievement Award (on behalf of Tanzania).
2009: US Doctors for Africa Award.
2011: Social Good Award from the United Nations Foundation
2011: South-South Award for Global Health, Technology and Development
2012: FANRPAN Policy Leadership Award from the Food, Agriculture and Natural Resources Policy Analysis Network.
2013: Africa's Most Impactful Leader of the Year by the Africa Leadership Magazine
2013: ICCF Mengha Award by the International Conservation Caucus Foundation
2014: Icon of Democracy Award, from The Voice Magazine (Netherlands)
2015: Leadership Excellence Award by the Pan-African Youth Union.
2015: African Achievers Award by the Institute for Good Governance in Africa.
2015: African Statesman of the Year by the The African Sun Times.

View attachment 325689 View attachment 325692 View attachment 325693 View attachment 325694 View attachment 325695 View attachment 325696 View attachment 325697 View attachment 325698
Save your MBs mkuu, cheo cha ukatibu mkuu UN ni rotational kwa mabara yote, baada ya Afrka (Koffi Annan), then Asia (Ban Ki Moon) sasa hivi ni zamu ya nchi za Ulaya kutoa katibu mkuu UN, nafasi kubwa zaidi zikipewa nchi za ulaya mashariki. So, forget about it man. Omary Kipingu
 
JeiKei kaharibu Tanzania vya kutosha, yaani wampe na Dunia aiharibu? hamna kitu kama hiko
 
Back
Top Bottom