Tetesi: Kikwete kumrithi Ban Ki-Moon

Tetesi: Kikwete kumrithi Ban Ki-Moon

Wazungu wanampenda JK kwa sababu ni kuwadi wa ubepari. Hawawezi kamwe kumpa mtu kama yule nafasi ya uboss wa UN. Salim A Salim alikubalika sana na ni mweledi sio kama JK lkini alipigwa veto isivyoelezeka.
 
Nchi ya watu milioni 47 aliigeuza ghala la wachuuzi na wapiga dili atawezaje UN? labda tumpe awe makamu wa nkurunziza BURUNDI
Mkuu huo ndio ukweli kabisa maana kama aliamua kutumia mamilioni ya walipa kodi kwa kununua magari ya washawasha ili kuhakikisha wapinzni hawaingii ikulu
 
Nami imani yangu ipo kwake ndugu jakaya kikwete kwa umahiri wake mkubwa wa kidiplomasia na siasa ya dunia yeye anatosha kuwa katibu mkuu wa umoja wa Mataifa , kupitia yeye afrika itanufaika na mambo mengi ikiwa na kumalizika kwa migogoro ya mataifa ya afrika ,kukuza umoja na mshikamano kwenye bara la afrika kiasi kwamba itapelekea bara la Afrika kupaa kiuchumi
Akili ya mchwa hiyo uliyonayo
 
Hizi nafasi zinakwenda kwa mzunguko na wala si kwa propaganda, baada ya katibu wa sasa nadhani anae fuatia anapaswa kutoka Ulaya kwa maana naibu wake wa sasa nadhani ametoka Argentina kama sikosei..endeleeni kubwabwaja JF na FB.. haitokaa itokee!
Mkuu super Handsome nakupa heko kwa kutoa ukweli, salute mkuu
 
Kikwete anapendwa sana na wazungu zaidi ya waswahili!! mnyonge mnyongeni Ila haki yake mpeni!! Jk tunakuombea uzidi kujitangaza Tanzania
Kwakuwa aliwauzia nchi yetu bila kuwajali watanzania na kila aliyejitokeza kupinga kufukuzwa kutoka kwenye ardhi yake alipigwa mijeredi bila huruma
 
HUYU NDIYE MRITHI WA BAN KI-MOON
_________________________________________________
Dr. Jakaya Mrisho Kikwete Rais mstaafu wa Tanzania kwa awamu ya nne (2005 – 2015) ni miongoni mwa wanadiplomasia wakubwa duniani wenye ushawishi na uwezo wa utatuzi wa matatizo mbalimbali duniani, sio tu kwa sababu viongozi wa mataifa mbalimbali duniani wanamkubali bali kwa uwezo wake katika masuala ya kidiplomasia.

Alizaliwa mwaka 1950 Oct katika mkoa wa Pwani Wilaya ya Bagamoyo katika kijiji cha Msoga katika familia ya kisiasa na kilimo. Baba yake Mzee Mrisho Kikwete alikuwa ni Mkuu wa Wilaya (DC) ya Pangani na babu yake naye ambaye alikuwa ni Chief wa Wakwere, Chief Kikwete.


Alipata elimu ya Msingi Msoga kabla ya kujiunga na shule ya sekondari Kibaha akiwa pia ni mwenyekiti serikali ya wanafunzi na vijana wa TANU 1966 na Baadaye Tanga school. Ambapo alijiunga na chuo kikuu Dar es salaam, ambapo pia alikuwa mwenyekiti wa serikali ya wanafunzi na kuhitimu Shahada ya uchumi 1975 alipojiunga na Jeshi.

Aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Singida 1977 na baadae kuhamishiwa Zanzibar kwa kazi maalum baada ya muungano wa TANU na ASP mpaka kufikia mwaka 1980 aliporudishwa makao makuu ya chama (CCM).

Mwaka 1988 aliteuliwa kuwa mbunge na pia NaibuWaziri wa Nishati na Madini chini ya uongozi wa MH. Al Ahsan Mwinyi mpaka kufikia mwaka 1990 ambapo aliteuliwa kuwa Waziri kamili wa maji nishati na madini.

Mwaka 1994 aliteuliwa kuwa waziri wa uchumi akiwa na umri wa miaka 44 ambapo alikuwa ni waziri mwenye umri mdogo kuwahi kuteuliwa. Kufika mwaka 1995 alitueliwa kuwa waziri wa mambo ya nje chini ya uongozi wa Rais Benjamin W. Mkapa na kuongoza wizara hiyo kwa miaka 10 mpaka kufikia mwaka 2005 ambapo alichaguliwa kuwa Rais wa Tanzania.

Katika Nyanja za kimataifa Mh. Jakaya Kikwete ni miongoni mwa wanadiplomasia ambae amefanya mambo mengi katika bara la Afrika na Dunia, kama vile kutatua migogoro katika nchi za maziwa makuu, jumuiya ya Afrika Mashariki akiwa kama Mwenyekiti wake (EAC) baadhi ya mambo ambayo dunia inampongeza ni pamoja na Mwaka 2005 akiwa kama Mwenyekiti mwenza wa mikutano wa Helsinki (Helisinki process on Globalization and Democracy) aliweza kuongoza mikutano huo kwa mafanikio makubwa.

2013 akiwa ndiye kiongozi pekee kutoka Afrika aliyeshiriki katika mkutano nchi za umoja wa Ulaya EU wa Alpbach Austria aliliwakilisha bara la Afrika vyema katika kutafuta fursa za maendeleo na ushirikiano kimataifa.

Dr. Jakaya Kikwete pia amekuwa Mjumbe tume ya Elimu Duniani ikiongozwa na waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown katika kutafuta namna ya kugharamia Elimu duniani (TICFGEO) kwa mwaka 2015.

Kwa mwaka huu 2016 Dr. Jakaya Kikwete ameteuliwa kuwa Mjumbe wa kamati ya Amani nchini Libya katika kusaidia kurudisha amani nchini Libya
Pia amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mwenza kwa tume ya kusaidia afya ya Mama na motto duniani kwa mwaka huu 2016 ikiwa ni katika jitihada zake kuhakikisha Afya na mama na motto duniani kote zinalindwa.

Kwa mtazamo huo nina imani kubwa kwa kipindi ambacho Mh. Ban Ki-Moon ataachia ofisi, Mwanadiplomasia huyu ndiye atakayechukua viatu vyake .

Hizi ni baadhi ya tuzo za heshima alizowahi kupata toka nchi mbalimbali...

2007: Sullivan Honor
2007: The AAI African National Achievement Award (on behalf of Tanzania).
2009: US Doctors for Africa Award.
2011: Social Good Award from the United Nations Foundation
2011: South-South Award for Global Health, Technology and Development
2012: FANRPAN Policy Leadership Award from the Food, Agriculture and Natural Resources Policy Analysis Network.
2013: Africa's Most Impactful Leader of the Year by the Africa Leadership Magazine
2013: ICCF Mengha Award by the International Conservation Caucus Foundation
2014: Icon of Democracy Award, from The Voice Magazine (Netherlands)
2015: Leadership Excellence Award by the Pan-African Youth Union.
2015: African Achievers Award by the Institute for Good Governance in Africa.
2015: African Statesman of the Year by the The African Sun Times.

View attachment 325689 View attachment 325692 View attachment 325693 View attachment 325694 View attachment 325695 View attachment 325696 View attachment 325697 View attachment 325698
itabaki kuwa tetesi
 
endeleeni na ndoto..naona ni mwendelezo wa jk kutaka kuwa hot kweny media...
hawez u GS,.na bora asiwe2 ataenda kutuaibisha tu uko Kufisadi....
nchi imemshinda sembuse un,.tukumbuke aliomba poo akasema naomba mda wangu uishe wa urais maana ni mgumu sana..akae tu ccm2 azeekee pale...,...
alafu mnasema wazungu wanampenda,...wazungu watakupenda ukiwa connector wa dili zao,..mbona mugabe hawampendi,...7bu hawapi dili,..kikwete kawapa dili wazungu za kuhujumu nchi......
lo2.jpg


mfalme wa anga.......
Fast jet
 
ana uzoefu mkubwa wa mambo ya kimataifa tangu akiwa waziri wa mambo ya nchi za nje..
ni tofauti na yule boya alielopoka eti SADAM alikua rais wa Quwait.
 
Hata mbingu zikipasuka jina lake sio tu kupita lakini hakitafikiriwa. Ni bora hata Asha-Rose Migiro.

Kwanza uzoefu hana zaidi ya kuwa chimbuko la migogoro. Burundi alimbeba Nkurunziza mpaka mishono ya operation kutaka kufumka.

Zanzibar aliibeba CCM kwa kutuia jeshi kukandamiza haki, na kuleta mfarakano, leo eti afikiriwe kukalia kiti cha watu wadilifu, haiwezekani! Nafasi pekee iliowahi kupata Tanzania ilikuwa kwa Dr. SALIM Ahmed Salim.
 
Nami imani yangu ipo kwake ndugu jakaya kikwete kwa umahiri wake mkubwa wa kidiplomasia na siasa ya dunia yeye anatosha kuwa katibu mkuu wa umoja wa Mataifa , kupitia yeye afrika itanufaika na mambo mengi ikiwa na kumalizika kwa migogoro ya mataifa ya afrika ,kukuza umoja na mshikamano kwenye bara la afrika kiasi kwamba itapelekea bara la Afrika kupaa kiuchumi
labda hamsini kwa hamsini... na si mengine
 
hivi hii tetesi bado haijawa confirmed tu , inakuwaje pale tetesi inapozidi mwezi ?
 
Back
Top Bottom