Kikwete: Kutokana na utoaji hafifu wa Elimu nchini, kuna hatari ya nusu ya ajira zilizopo kutoweka ifikapo mwaka 2050

Jamani nilichomuelewa mzee wetu Kikwete ni; creating brighter future kwa vizazi vyetu! Kwanza ukimsoma amezungumzia issue ya gender hasa kuondoa primitive nonsense kwamba watoto wa kike ni wa kufanya domestic roles (mapishi, mahunjumati na kulea wanaume na watoto). Katika hili anatambaa kwenye kuwezesha hadi watoto wa kike kujifunza ICT ambayo ni dunia inayokuja. Hata ITU wana siku maalum ya Girls in ICT. Kila April.

Pili, kasema elimu yetu ya Afrika iendane na dunia ya sayansi na teknoloji. Anatoa mfano, utafika wakati unaita gari halihitaji 'mpigadebe wala suka' bali ni teknoloji. Hivyo tunahitaji kuandaa vizazi vyetu viweze kukabili hili.

Tatu, kuhusu kuunganisha shule na maeneo mengine ya kijamii kweli Mkongo wa Mawasiliano wa Taifa ulikuwa ndiyo moja ha malengo yake. I do remember! Sasa tusibeze kutumia tablets ndiko kujenga kizazi cha digital.
Na hili ni azimio la WSIS.

Nne, wanaodrop kwenye elimu. Huwezi kuingia kwenye dunia kijiji halafu bado ukawa na watu asilimia zaidi ya asilimia 30 hawamalizi shule. Ndiyo maana hata UN ina Azimio la Education For All ambalo ni la Dakar, Senegal (2000). Lilianzia Jomtie, Thailand.

Kimsingi, hii presentation ya JK siyo ya level ya kufikiri kwa kukurupuka. Inahitaji utulivu wa akili ujue kwanza hoja. Ni mada kubwa!😀😀😀
 
Vipi na yale mazombie kule mjengoni yanayoshangilia mambo ya kipuuzi hakuna Chadema kule wamejaa nyumbu wa kijani toka mitaa ya Lumumba. Kinuju bila kuitajataja Chadema kigololi chako hakitulii
 
Wewe ni mtu mjinga uliyeripoti habari za mtu mwerevu.

Anyway, anachokisema Kikwete ndo hoja zinazopaswa kuzungumziwa na Viongozi Wakuu wa Kitaifa, haya mambo Magufuli alikuwa haelewi chochote sijui ilikuwaje tukawa na Rais mburula vile.
Bila Corona kuingilia kati tungeteseka sana na yule kiumbe
 
Ajira zitatoweka vipi means panakuwa hamna Serikali, aache uongo Serikali hela ipo ya kutosha na tunataka kuona raia mnajenga nchi msiwe na wasiwasi.
soma vizuri umuelewe JK mfumo wa elimu yetu leo unatuandaa kuwa watazamaji wa mapinduzi ya kiteknolojia baadaye.
 
Hapa tunapaswa kumlaumu mzungu kwa ushetani aloufanya wa kutumezesha dini badala ya kutumezesha elimu anachokizungumza JK ni kitu cha kweli kabisa ukiangalia provision ya elimu waliyoipata karne ya 15-16 imeanza mwanzoni mwa miaka ya 1910 na hiyo effect imeanza kuonekana miaka ya 60.
 
Alicho
2050 dunia itakua ktk elimwengu mwengine Wa sayansi, elimu ya "sikuile akaenda, shambani kutembelea, akayaona matunda, mtini yamejaa" haitokuwa na matumizi tena miaka hiyo! Tubadilishe mitaala!
sahau ni kuwa wengi tutakuwa tushakufa so tutakuwa tumeepukana na kadhia hio
 
JK ameongea ukweli mtupu !angeshauri tu kwamba , kwakuwa tunakoenda dunia inakuwa ni finest digital , kila kitu dogital , tungeanza kuwekeza kwa watoto wa shule zetu , mfano hata kilimo chenyewe miaka. Ijayo kitakuwa digital tu , kila. Kitu ni digital , tusipobadilika tutaajiri wataalaumu watufanyie haya mambo
 
Tutaletewa vitendea kazi kwa gharama nafuu kutoka kwa hao waliotumia muda huu kubadilika na hizo kazi zitapungua kwa mtindo huo na zile zitakahitaji maarifa zaidi watakuja kuzifanya wao sisi tukiwa tumepigwa doro.
 
Ajira zitatoweka vipi means panakuwa hamna Serikali, aache uongo Serikali hela ipo ya kutosha na tunataka kuona raia mnajenga nchi msiwe na wasiwasi.
Kati ya vijana zaidi million ishirini Serikali inajiri watu wangapi ? Hizo Ni fikra za kiongozi mwenye maono ya mbali,
Tusipobadili elimu yetu ,tukubali kutawaliwa kiteknojia,
Swala halitakuwa kujuana isipokuwa mwenye maarifa sahihi ya wakati huo,
 
kwani... huyu hakua raisi wa hii nchi?

this fooker never stops to amuse me!
 
Wastaafu wana washwawashwa (in Mwendazake's Voice).

Hajatoa suluhisho zaidi ya kubwabwaja tu.

By the way yeye hatokuwepo duniani by 2050...aache kiherehere.
 
Teknolojia ikifanya kazi hakutakuwa na mambo ya wizi na rushwa. Roboti litaiba pesa lipeleke wapi. Kwenye vituo vya mafuta hakutakuwa na wizi wa mafuta kwakuwa roboti atafanya kazi otomatikali. Watakaokuwepo watafurahia maisha sana. Imajini saiv kakibwengo kanakuambia unanijua mi nani? Sa ngapi roboti litakuambia hayo. What a soft life that will be!
 
Vikao vya kulipana posho tu hamna concrete measure yeyote hapo.

Maswahibu yatakayowakuta watanzania watakaokuwa wanaishi miaka hiyo kwa kiasi kikubwa yatakuwa yamechangiwa na ufisadi tu.

Wewe unasema kutakuwa hamna kazi lakini mmekazana kuwanyang'anya ardhi wakulima wadogo vijijini halafu eti unashangaa kuwa 2050 hawatakuwa na ajira!

Itakapifikia hali hiyo nchi haitakalika kwa ujambazi na kila aina ya uhalifu maana lazima watu wale, sasa watakula vipi ndio issue.
 
Ukweli utabaki kuwa ukweli tu. Tanzania inabidi tuamke. Swala la ajira bado ni tatizo na hatiwezi kubaki kuendelea kulijadilitu mitandaoni na kwenye mijadala mbalimbali...tunatumia gharama kubwa sana kuandaa mijadala ya kujadili kuhusu tatizo la ajira. Lkn tunasahau kuwa maneno matupu hayavunji mfupa.

1. Inabidi serikali iingie kwenye utekelezaji wa maadhimio yote yenye tija kuhusu tatizo la ajira.

2. Mtaala wa elimu yetu inabidi ibadilike mara moja ili kwendana na mabadiliko ya dunia. Masomo kama ya ujasiria mali, na uwekezaji, yafundishwe mashuleni kuanzia ngazi ya shule ya msingi hadi chuo kikuu ili kutoa uelewa mpana kwa wasomi wetu na kupunguza struggle kubwa iliyopo kwenye soko la ajira nchini.

3. Serikali iongeze uwanda mpana wa utengenezaji ajira kwamaana ya kwamba, itengeneze sera madhubuti ambazo zitajikita kwenye uwekezaji kwenye viwanda zaidi na kutengeneza room kubwa ya ajira kwa wananchi wake.

4. Uadilifu katika taifa letu umepungua sana....watu siku hizi wanapewa ajira kwa kujuana( technical know who) na sio kwa kuangalia mtu anajua nn ( technical know how). Heria zetu bado ni butu sana na sekretarieti yetu ya ajira bado haijafanya kazi kama inavyo takiwa.

Watu wengi walio officen hawana proffesional bali wanaujuzi ambao pia wameupata kwa kupitia ndugu zao
 
Waachane tabia ya kuwekeza pesa kwenye vitu vya ovyo kama mwenge, jengeni vyuo vya veta vingi
 
Kuzeeka kuna mengi keshaanza kupoteza kumbukumbu

Kwa hiyo ikifika hiyo miaka serikalini na mahakamani tutaajiri wazungu kufanya kila kazi ya ajira iliyoko serikalini na kwenye mahakama zetu?
Pamoja na kuzeeka lakini ana fikra na maona yanayopaswa kuwa ya vijana,
Tusipoendana na teknolojia ya wakati ,itafika mahali ajira zitatukataa kutokana na maarifa yanayotokiwa kwenye ajira husika,
Hata usimamizi itabidi tutafute wasimamizi wa nje wenye teknolojia husika,
Hiyo miradi mikubwa kwanini tunawapa wazungu, ina maana hutuna mafundi wa kujenga miaka 50 ya uhuru ?
Kwanini tusichimbe migodi sisi wenyewe ?
Tubadili fikra zetu kiukweli tutakwama pakabwaa
 
Nakubali jambo kubwa si tablet wala ubao ukutani, ni
1) idadi ya wanafunzi darasani
2) elimu ya walimu wenyewe
3) mbinu wa elimu usiolenga kukariri lakini kutafakari
4) shule isiyotaka mwanafunzi aitikie bali awe tayari kupinga akiwa na sababu zake
5) mazingira inayoheshimu watoto badala ya kuvumilia kiboko...

nani ataongeza?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…