Kikwete: Kutokana na utoaji hafifu wa Elimu nchini, kuna hatari ya nusu ya ajira zilizopo kutoweka ifikapo mwaka 2050

Hapo ni kesi moja tu unaongelea ambayo ana handle judge mmoja cha ajabu hapo nini? Muda wa kesi ule ule
ina maana kutakuwa na jaji mwingine wa ku handle kesi ingine nk ambapo mshitakiwa aweza kuwa mtwara na shahidi japan!! nk
 
Umeshawahi kufanya interview kwenye taasisi za kimataifa kupitia electronic systems? Huyo anayetumia tablet ana nafasi kubwa ya kupita kuliko wa chaki. Tuwekeze kwenye elimu ya kisasa. Mambo ya A+ za makaratasi tuachane nayo yaani.
Mambo hayo hatuyawezi
Mambo ya mdomoni tu
Sahv yenyewe siku ya 3 watu wana lala gizani

Ova
 
Ajira zitatoweka vipi means panakuwa hamna Serikali, aache uongo Serikali hela ipo ya kutosha na tunataka kuona raia mnajenga nchi msiwe na wasiwasi.
Akili kisado wewe
Anamaanisha kushindwa kutumia elimu kununua njia mpya za maisha zinazotengeneza Ajira (mfano kwa sawa ni teknolojia ya mawasiliano imetengeneza ajira na uchumi) kushindwa huko kutapelekea janja la kukosa ajira
 
Labda kama ni walimu pekee ndo wataguswa hivi mtu kama daktari anakosaje ajira miaka hiyo mgonjwa atatibiwa mtandaoni
Tuchomwe sindano mtandaoni
 
Kukomaa na elimu ya bila ujuzi ni undezi,tuige hata wenzetu walioendelea wao wanachofanya
 
Huo mwaka 2050 utakapofika wakati wenzetu wakifanya hayo, sisi ndo tutakua tumefungua kiwanda chetu cha kwanza cha kutengeneza simu za tochi kwa msaada wa mabeberu.
 
Elimu mbovu na matatizo yote chanzo chake ni CCM.
References: Makonda na Sabaya.
 
Kwa hiyo Mabala the Farmer na Hawa the bus driver havitakuwa na maana tena.

Bora turudi kusoma shairi la 'Karudi baba mmoja'
 
Huyu huyu aliyewahi kusema "hajui kwanini nchi anayoiongiza ni maskini?
Mkuu mwanasiasa yeyote huwa ana akili ya utambuzi vizuri sana, yaani ana uelewa mkubwa kuhusu kipi kizuri na kipi kibaya, siyo kwamba hawa viongozi wa sasa hawaelewi hili alilolisema JK, wanaelewa sana ila tatizo ni wataendeleaje kula kama wakitoa siri kama hizi ilihali hata wao hiyo elimu iliwaumiza. So wao wanakuja kukuambia ujiajiri huku akitumia uwezo wake wa kujenga HOJA NADHARIA kuchambua na kukuambia yasiyowezekan katika uhalisia wa maisha.

Hawa viongozi wetu siyo kwamba madudu yote yanaoendelea kila sehemu hawayajui, la hasha! Wanayatambua vema sana, ila wanajifikiria wao kwanza na familia zao, maslahi ya taifa ni baadae na hayo maslahi ni yale yasiyoathiri maisha yao kiujumla.

Leo serikali ikae ianze kutengeneza syllabus mpya yenye kukidhi vigezo vyote, hao wataalamu wanao?? Tanesco leo luku mfumo unasumbua nchi nzima, mifumo yetu ya mitandao na teknolojia tunachukua nje kisha tunatumia kujifunzia halafu ndiyo tulete mfumo mpya.

Ukionekana unaleta mapinduzi hata yenye faida kwa maslahi ya nchi utawaiwa faster na kuulizwa swali dogo tu "tupe kibali cha wewe kufanya hili", mimi juzi ndiyo nimeanza hata mafanikio bado ila lengo ni kuifaidisha nchi yangu leo unakuja niuliza kibali tena ukiwa na sura ngumu na baadhi kujia na polisi na wanasheria juu wa kuanza kuchambua ibara.

Kiufupi hata hao tunaotaka wabadili mfumo wao wenyewe hawajui wataubadili vipi maana wataalamu kwanza hawapo na wanaoaminika kuwa wataalamu wanaishi kwa copy and paste, no creativity at all.

Kuna kozi unasoma Tanzania, practical unaeenda jifunzia nje tena baada ya kuitwa graduate.

Shida ni kwamba tunaishi kimazoea na tunafanya mambo yaleyale. Yaani mechanical engineer kashakaririwa kuwa kazi zake ni zilezile naye anaishi humohumo, yaani hakuna kujiongeza.

Wajanja wengi hata makazini ni wale waliojiongeza na kujifunza vingi nje ya masomo yao na hao huwa wengi wao wanatafuta sehemu zenye kujua na kuthamini thamani zao. Ukimnyima kazi hapa anatoka anaenda nje huko unasikia baada ya miaka kadhaa tuna mtanzania anafanya kitu fulani huko nje na anafanya vizuri sana.

Hii nchi ukiwa tajiri, ukiwa na uwezo mzuri wa kufikiri, ukiwa na msimamo kusimamia haki na ukijitambua sana unageuka kuwa ADUI. Maana wengi hawapendwi wanaharabu kazi za wanasiasa ambao hawajui chochote zaidi ya kukesha kukariri vifungu vya sheria na kufuata taratibu ambazo zipo outdated so unapokuja na kitu kipya unawachanganya na kuona una nia ya kuwaharibia.
 
Kila mwanasiasa ukimpa nafasi ya kujadili jambo fulani hatakosa la kuongea, kwa sababu wanasiasa wengi huwa hawaishiwi maneno mdomoni.

Hivyo basi inapofika hatua ya wananchi kujadili jambo fulani kwa masilahi ya taifa, kila mwananchi atazungumza lake kulingana na nafasi aliyopo kwa wakati huo.

Lakini binafsi kama mwananchi wa kawaida na niliyesoma elimu ya TANZANIA, kuanzia chekechea hadi chuo kikuu, maoni yangu ni haya:

Kwanza kabisa, ingetupasa kama taifa la TANZANIA tuwe na sheria za wanafunzi wa shule za msingi yaani PRIMARIES ACTS na sheria za wanafunzi wa shule za sekondari yaani SECONDARIES ACTS kama muongozo na kanuni za wanafunzi wawapo shuleni.

Suala lingine, ni kuwepo na uwazi katika matokeo ya wanafunzi wa shule za msingi na shule za sekondari. Hii itasaidia kuondoa udanganyifu na upendeleo katika upangaji wa matokeo ya wanafunzi wote kwa ujumla.
Pili, kasema elimu yetu ya Afrika iendane na dunia ya sayansi na teknoloji. Anatoa mfano, utafika wakati unaita gari halihitaji 'mpigadebe wala suka' bali ni teknoloji. Hivyo tunahitaji kuandaa vizazi vyetu viweze kukabili hili.
Sote inatupasa tufahamu kuwa AFRIKA ni bara linalojumuisha mataifa zaidi ya hamsini [ 50 ]. Kwahiyo, Rais Mstaafu Mheshimiwa Mrisho Khalufani Kikwete anajapojaribu kujadili mataifa zaidi ya hamsini [ 50 ] kwa pamoja inakuwa haijakaa sawa kitaaluma.

Na kwa upande wa ubora wa elimu, huwa kuna taasisi ya kimataifa inayoshughulika na masuala ya ubora wa elimu, taasisi hii inaitwa UNESCO.

Kwa taarifa za UNESCO kwa miaka kadhaa iliyopita ni kuwa, ubora wa elimu ya TANZANIA umeshuka ukilinganisha na mataifa mengine.

Ubora wa elimu ya TANZANIA umeshuka kwa sababu gani? Sababu kubwa ni UDANGANYIFU WA MADARAJA YA UFAULU YA WANAFUNZI - kwa lugha ya kiingereza wanaita ni "REPLACEMENT OF PASSMARKS [ GRADES ]".

Wanafunzi wengi wanapewa madaraja tofauti na ufaulu wao. Pale Baraza la Mitihani [ NECTA ] huwa wanasema hivi - "UNAPEWA UNACHOSTAHILI, SIO KILE UNACHOPATA KWENYE KARATASI LAKO LA MITIHANI" na kwa lugha ya kiingereza huwa wanasema hivi - "YOU SCORE WHAT YOU DESERVE, NOT WHAT YOU GET ON YOUR ANSWER SHEETS".

Hii inatoka na kupika matokeo ya wanafunzi wa shule za msingi na shule za sekondari kwa pamoja. Madhara yake taifa linapata wahitimu wasiokuwa na sifa za kitaaluma na sifa za kuajiriwa au kujiajiri wenyewe.

Sababu nyingine iliyopelekea elimu ya TANZANIA kushuka ni "KUTOKUWA NA UWAZI KATIKA KUTANGAZA MATOKEO YA WANAFUNZI". Kwa lugha ya kiingereza huwa wanasema hivi - "LACK OF TRANSPARENCY ON ANNOUNCEMENT OF PUPILS AND STUDENTS ACADEMIC RESULTS".

Sote tunafahamu kuwa, matokeo ya wanafunzi wote wa shule za msingi na shule za sekondari yalianza kutangazwa rasmi kipindi cha HAYATI RAIS JOHN POMBE MAGUFULI, mwaka 2016.

Je, tukiuliza orodha ya wanafunzi bora waliofanya vizuri kitaifa kwa mwaka wa 2015, iwe kwa darasa la saba, kidato cha nne na kidato cha sita tutazipata? Jibu ni hakuna?

Je, tukiuliza orodha ya wanafunzi bora waliofanya vizuri kitaifa kwa mwaka wa 2007, iwe kwa darasa la saba, kidato cha nne na kidato cha sita tutazipata? Jibu ni hakuna?

Kwahiyo, taifa la TANZANIA lilikuwa linazalisha wahitimu wasiokuwa na ufahamu wa sifa zao za kitaaluma mpaka mwaka 2016, ambapo HAYATI RAIS JOHN POMBE MAGUFULI alipoamua kuweka wazi kila kitu hadharani. MWENYEZI MUNGU amrehemu huko alipo!!

Kwahiyo suala la KUTOKUWA NA UWAZI KATIKA SEKTA YA ELIMU lilichangia ubora wa elimu ya TANZANIA kushuka ukilinganisha na ubora wa elimu ya mataifa mengine. Na madhara yake ni makubwa sana kwa wahitimu waliosoma elimu ya TANZANIA.

Kwa wale Watanzania waliobahatika kufanya kazi nje ya nchi au kwenye makampuni ya kimataifa watakubaliana na mimi kuwa - WATAALAMU KUTOKA TANZANIA HUWA HAWAAMINIKI KWA MATAIFA YA NJE. Na hii iko wazi kabisa, watalaamu kutoka TANZANIA huwa wanaitwa ni INCONSISTENCY PERSONEL, kwa lugha ya kiswahili sijui imekaaje hii.

Na kwa upande wa WAHANDISI yaani ENGINEERS huwa wanaanzia hatua ya TECHNICAL OPERATION kwa kipindi cha miaka miwili [ 2 ] hadi miaka mitatu [ 3 ] hata muhitimu awe na Shahada ya Uzamili au Shahada ya Uzamivu. Na hii ipo hata kwa upande wa MADAKTARI WA AFYA yaani DOCTORS OF MEDICINE, huwa wanaanzia kuwa CLINICAL OFFICIAL kwa kipindi cha miaka miwili [ 2 ] hadi miaka mitano [ 5 ].

Na haya ndio madhara ya mfumo wa elimu ya TANZANIA. Baraza la Mitihani la TANZANIA yaani NECTA ni taasisi ya HOVYO sana, kuna uchafu mwingi sana pale. Imefikia hatua hata mataifa mengine yanaita TANZANIA ni "GARBAGE FROM PUERTO RICO" yaani "TANZANIA IS NO LONGER A BANANA REPUBLIC, IT'S A GARBAGE FROM PUERTO RICO".
Tatu, kuhusu kuunganisha shule na maeneo mengine ya kijamii kweli Mkongo wa Mawasiliano wa Taifa ulikuwa ndiyo moja ha malengo yake. I do remember! Sasa tusibeze kutumia tablets ndiko kujenga kizazi cha digital.
Na hili ni azimio la WSIS.
Ndio! Hapa nakubali, kuwa ni muhimu kwa wanafunzi wa shule za sekondari kuanza kujifunza masomo ya kompyuta na kuna baadhi ya shule za sekondari ziliisha anza kutumia na kusoma masomo ya kompyuta kama somo.
Huu mradi wa EDUCATION FOR ALL upo na upatikana sana kwa nchi za KENYA, UGANDA na RWANDA. Sijafahamu vizuri kwa upande wa TANZANIA hali ni ikoje.

Lakini huu mradi wa EDUCATION FOR ALL una malengo wezeshi kwa wanafunzi kuweza kusoma katika mazingira mazuri na rafiki ili kupata elimu iliyo bora.

Malengo ya EDUCATION FOR ALL yanaweza kabisa kufanana na malengo ya MMEM na MMES kwa upande wa TANZANIA.
Kimsingi, hii presentation ya JK siyo ya level ya kufikiri kwa kukurupuka. Inahitaji utulivu wa akili ujue kwanza hoja. Ni mada kubwa!πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
Ni mada nzuri kwa wakati uliopita. Ilimpasa awe na mada hii kipindi yeye ni mtendaji mkuu na ni kiongozi wa serikali ya TANZANIA.
 
Wewe ni mtu mjinga uliyeripoti habari za mtu mwerevu.

Anyway, anachokisema Kikwete ndo hoja zinazopaswa kuzungumziwa na Viongozi Wakuu wa Kitaifa, haya mambo Magufuli alikuwa haelewi chochote sijui ilikuwaje tukawa na Rais mburula vile.
Ranger9 Magufuli kafikaje hapa wakati tunazungumzia Elimu ya Africa na mfumo duni tulio nao. Mheshimiwa Jakaya alikuwa Rais anazungumzia anayoyaona kama Mstaafu pia. Naona Magufuli anaitwa Mbulula. Chuki Binafsi hizi. Nchi huwa haisimami kila siku ndio maana tunauongozi muda wote.

Kipindi cha Jakaya Mwenyewe hatukusomea Tablet. Lakini anatuonesha kuwa nini tufanye. Why? Kwasababu anaelewa Dunia inaenda Mbele. Tatizo la Elimu halitatuliwi na mtu mmoja ndani ya siku moja. Inatakiwa tujipange twende huko kwenye Technolojia. Kutukana viongozi haisaidiii. Hayati Magufuli kakaa miaka mitano tu na miezi 3 madarakani. Kakutana Madawati hakuna. Akapambana kweli kweli, unakumbuka MA DC walivyo washiwa moto watafte madawati. Wametafta madawati lakini haimaanishi Madawati yatatosha tukikaa tu maana watoto wanaongezeka.

Changamoto hazisimami. Serikali ianze pole pole kwenda kwenye technology huko.
 
Cha msingi kinachoonekana hapo labda matumizi ya sayansi na teknolojia na hasa matumizi ya kompyuta.somo la kompyuta lifundishwe kuanzia shule za msingi mpaka vyuo vikuu kwa vitendo zaidi ili kuwafanya wawe wabobezi katika anga hiyo.lakin kama shule nyingine zitafundisha kwa umahili somo la kompyuta wakati shule zingine hasa hizi za kwetu hazitafundisha somo hili basi kutakuwa na umbwe kubwa kati ya watoto wa maskini na wale wa matajiri.
 
Hapa anaongelea jumla. Wanaosoma hayo masomo ni wengi kuliko wa science. Na wana impact kubwa sana
 
Mkuu asante sana kwa darasa zuri ulilonipa....majuzi nasikia yale marekebisho ya katiba maarufu kama BBI ya majirani zetu wanataka kuongeza majimbo mengine ya uchaguzi.....wanasiasa wapo kwa aijili ya matumbo yao tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…