Abdulhalim
Platinum Member
- Jul 20, 2007
- 17,215
- 3,076
Abadan asilanMpe heshima yake,Huyu Ni miongoni mwa viongozi wanaowaza kulingana na dunia ya Sasa inapoelekea
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Abadan asilanMpe heshima yake,Huyu Ni miongoni mwa viongozi wanaowaza kulingana na dunia ya Sasa inapoelekea
Hapo ni kesi moja tu unaongelea ambayo ana handle judge mmoja cha ajabu hapo nini? Muda wa kesi ule uleUwezo wako wa kufikiri ni mdogo sana.
Teknolojia inavyoenda, itafika mahali, kazi iliyokuwa inafanywa na majaji 20, itafanywa na jaji mmoja mwenye uwezo wa kutumia teknolojia ya kisasa. Jaji ataweza kuendesha kesi akiwa Dar, mshtakiwa akiwa Kigoma, shahidi akiwa Songea.
Mambo hayo hatuyaweziUmeshawahi kufanya interview kwenye taasisi za kimataifa kupitia electronic systems? Huyo anayetumia tablet ana nafasi kubwa ya kupita kuliko wa chaki. Tuwekeze kwenye elimu ya kisasa. Mambo ya A+ za makaratasi tuachane nayo yaani.
🤣Mambo hayo hatuyawezi
Mambo ya mdomoni tu
Sahv yenyewe siku ya 3 watu wana lala gizani
Ova
Mbona boss umenikamia sana kwenye jibu lako?CHATO.
vipi umefurahi
Akili kisado weweAjira zitatoweka vipi means panakuwa hamna Serikali, aache uongo Serikali hela ipo ya kutosha na tunataka kuona raia mnajenga nchi msiwe na wasiwasi.
Sisi hata tufike miaka 4000 sijui kama kutakuwa na mabadiliko[emoji1787]
Umeongea ukweli mchungu.
Huo mwaka 2050 utakapofika wakati wenzetu wakifanya hayo, sisi ndo tutakua tumefungua kiwanda chetu cha kwanza cha kutengeneza simu za tochi kwa msaada wa mabeberu.Ukweli mchungu by 2050 kila kitu kitabaki kwenye technology
Hivyo wanaitajika watu ambao wapo tayari kujiajiri, Machine na operators wa machine
Maroobot vile vile yatakuwa yakifanya kazi sehemu kama shelli na super market
So kazi zitakuwa chache au kutokuwepo kabisa
Kikwete ana hoja tuchukue hatua.
Elimu mbovu na matatizo yote chanzo chake ni CCM.Rais mstaafu wa awamu ya nne Dk Jakaya Mrisho Kikwete ameonya tusipobadilika namna tunavyofundisha watoto wetu basi ajira zote zitatoweka ifikapo mwaka 2050.
My take.
Hii elimu yetu ya kuwafanya chadema washangilie kila baya linaloipata nchi yetu ikiwemo kukamatwa ndege, miradi kukwama , tutashitakiwa MIGA etc bora ifutwe kabisa tuanzishe elimu mpya itakayowafanya chadema wajitambue.
====
Dar es Salaam. Rais mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete amesema kutokana na utoaji hafifu wa elimu nchini kuna hatari ya nusu ya ajira zilizopo kutoweka ifikapo mwaka 2050.
Ameyasema hayo leo Jumanne Mei 18, 2021 wakati akizindua kongamano la elimu linalojadili ufadhili wa elimu lililoandaliwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (Tenmet) jijini Dar es Salaam.
Akieleza utafiti uliofanywa na tume ya kimataifa ya elimu ambayo yeye ni mjumbe, amesema elimu inayotolewa barani Afrika ilitolewa miaka 50 hadi 70 iliyopita kwa nchi zilizoendelea.
"Sisi bado tunatumia chaki, wakati wenzetu wanatumia tablets. Tuliona kuwa kuna watu zaidi ya milioni 263 waliotakiwa kuwa shule lakini hawapo, kati yao milioni 100 wapo Afrika. Kwa waliopo shule wengi hawamalizi shule. Wengi wanaishia njiani. Asilimia 67 wamemaliza shule, asilimia 33 ni idadi kubwa," amesema Kikwete.
Amesema kutokana na utoaji hafifu wa elimu na maendeleo ya teknolojia kuna janga la ukosefu wa ajira linakuja.
"Ifikapo 2050 asilimia 50 ya kazi zitafutika, kwa sababu ya matumizi ya mashine. Kutakuwa na magari yasiyotumia dereva. Unataka usafiri, unaita Uba, unatumia simu yako inakuja inakupeleka sehemu husika labda Ubungo Plaza au Millennium Tower," amesema.
Amesema mbali na ukosefu wa ajira, idadi ya watu barani Afrika itafikia watu bilioni mbili, “kama watu hao hawana ujuzi unafanya nini? Sijui itakuwaje. Kutakuwa na athari kubwa za kiuchumi na kijamii."
Akisisitiza matumizi ya teknolojia, Kikwete ameshauri kuwepo na uwekezaji katika elimu ili vijana wa Afrika wasiwe watazamaji, wawe washiriki wa uchumi.
"Kunatakiwa kuwepo na matumizi ya sayansi na teknolojia katika ufundishaji. Kila shule inatakiwa kuunganishwa na intaneti," amesema.
Huku akitoa mfano wa janga la corona, Kikwete amesema limethibitisha jinsi ukosefu wa teknolojia unavyoathiri ufundishaji.
"Tumeona wakati wa corona, moja hatua zilizochukuliwa ni kufunga shule. Wanafunzi wetu hawakusoma, wanacheza rede, lakini nchi zilizoendelea shule zilifungwa na watoto wakaendelea kusoma.”
"Nilipokuwa Rais tulianzisha matumizi ya intaneti katika ufundishaji, tuliwekeza sana kwenye mkongo wa Taifa. Lengo langu lilikuwa ni kuhakikisha kila shule, hospitali ziunganishwe na intaneti. Mwalimu mmoja wa hisabati afundishe nchi nzima,” amesema.
Kuhusu Elimu jumuishi ameitaka Serikali na wadau kuhakikisha hakuna mtoto anayebaki nyuma kwa kukosa elimu.
"Wengine wanadhani msichana ni wa kubaki jikoni. Wengine wameachwa nyuma kutokana sababu za kisiasa.
Tunatakiwa kuhusisha mashirika yasiyo ya kiserikali kuchangia elimu," amesema.
Awali akimkaribisha Kikwete mwenyekiti wa Tenmet, Dk John Kalage ambaye pia ni mkurugenzi wa taasisi ya HaliElimu amesema kongamano hilo litajadili kwa kina njia za ufadhili wa elimu nchini.
Chanzo: Mwananchi
Mkuu mwanasiasa yeyote huwa ana akili ya utambuzi vizuri sana, yaani ana uelewa mkubwa kuhusu kipi kizuri na kipi kibaya, siyo kwamba hawa viongozi wa sasa hawaelewi hili alilolisema JK, wanaelewa sana ila tatizo ni wataendeleaje kula kama wakitoa siri kama hizi ilihali hata wao hiyo elimu iliwaumiza. So wao wanakuja kukuambia ujiajiri huku akitumia uwezo wake wa kujenga HOJA NADHARIA kuchambua na kukuambia yasiyowezekan katika uhalisia wa maisha.Huyu huyu aliyewahi kusema "hajui kwanini nchi anayoiongiza ni maskini?
Kila mwanasiasa ukimpa nafasi ya kujadili jambo fulani hatakosa la kuongea, kwa sababu wanasiasa wengi huwa hawaishiwi maneno mdomoni.Jamani nilichomuelewa mzee wetu Kikwete ni; creating brighter future kwa vizazi vyetu! Kwanza ukimsoma amezungumzia issue ya gender hasa kuondoa primitive nonsense kwamba watoto wa kike ni wa kufanya domestic roles (mapishi, mahunjumati na kulea wanaume na watoto). Katika hili anatambaa kwenye kuwezesha hadi watoto wa kike kujifunza ICT ambayo ni dunia inayokuja. Hata ITU wana siku maalum ya Girls in ICT. Kila April.
Sote inatupasa tufahamu kuwa AFRIKA ni bara linalojumuisha mataifa zaidi ya hamsini [ 50 ]. Kwahiyo, Rais Mstaafu Mheshimiwa Mrisho Khalufani Kikwete anajapojaribu kujadili mataifa zaidi ya hamsini [ 50 ] kwa pamoja inakuwa haijakaa sawa kitaaluma.Pili, kasema elimu yetu ya Afrika iendane na dunia ya sayansi na teknoloji. Anatoa mfano, utafika wakati unaita gari halihitaji 'mpigadebe wala suka' bali ni teknoloji. Hivyo tunahitaji kuandaa vizazi vyetu viweze kukabili hili.
Ndio! Hapa nakubali, kuwa ni muhimu kwa wanafunzi wa shule za sekondari kuanza kujifunza masomo ya kompyuta na kuna baadhi ya shule za sekondari ziliisha anza kutumia na kusoma masomo ya kompyuta kama somo.Tatu, kuhusu kuunganisha shule na maeneo mengine ya kijamii kweli Mkongo wa Mawasiliano wa Taifa ulikuwa ndiyo moja ha malengo yake. I do remember! Sasa tusibeze kutumia tablets ndiko kujenga kizazi cha digital.
Na hili ni azimio la WSIS.
Huu mradi wa EDUCATION FOR ALL upo na upatikana sana kwa nchi za KENYA, UGANDA na RWANDA. Sijafahamu vizuri kwa upande wa TANZANIA hali ni ikoje.Nne, wanaodrop kwenye elimu. Huwezi kuingia kwenye dunia kijiji halafu bado ukawa na watu asilimia zaidi ya asilimia 30 hawamalizi shule. Ndiyo maana hata UN ina Azimio la Education For All ambalo ni la Dakar, Senegal (2000). Lilianzia Jomtie, Thailand.
Ni mada nzuri kwa wakati uliopita. Ilimpasa awe na mada hii kipindi yeye ni mtendaji mkuu na ni kiongozi wa serikali ya TANZANIA.Kimsingi, hii presentation ya JK siyo ya level ya kufikiri kwa kukurupuka. Inahitaji utulivu wa akili ujue kwanza hoja. Ni mada kubwa!😀😀😀
Ranger9 Magufuli kafikaje hapa wakati tunazungumzia Elimu ya Africa na mfumo duni tulio nao. Mheshimiwa Jakaya alikuwa Rais anazungumzia anayoyaona kama Mstaafu pia. Naona Magufuli anaitwa Mbulula. Chuki Binafsi hizi. Nchi huwa haisimami kila siku ndio maana tunauongozi muda wote.Wewe ni mtu mjinga uliyeripoti habari za mtu mwerevu.
Anyway, anachokisema Kikwete ndo hoja zinazopaswa kuzungumziwa na Viongozi Wakuu wa Kitaifa, haya mambo Magufuli alikuwa haelewi chochote sijui ilikuwaje tukawa na Rais mburula vile.
Cha msingi kinachoonekana hapo labda matumizi ya sayansi na teknolojia na hasa matumizi ya kompyuta.somo la kompyuta lifundishwe kuanzia shule za msingi mpaka vyuo vikuu kwa vitendo zaidi ili kuwafanya wawe wabobezi katika anga hiyo.lakin kama shule nyingine zitafundisha kwa umahili somo la kompyuta wakati shule zingine hasa hizi za kwetu hazitafundisha somo hili basi kutakuwa na umbwe kubwa kati ya watoto wa maskini na wale wa matajiri.JK amesahau matumizi ya teknolojia hayabadilishi mitaala, usome kwa kutumia tablet au mwenzio aende kayumba at the end of the day wote watafanya mtihani mmoja.
Labda yule wa tablet atamzidi mwenzie topic alizo-cover in case ikitokea issue kama ya Corona, ila pasipokuwepo na Corona tofauti yao itakuwa ndogo sana.
Kitakachomyima mtoto wa masikini ajira hata akiwa na ufaulu mzuri bado ni kujuana (nafasi kutolewa kwa upendeleo) lakini sio kwasababu ya teknolojia, na ajira bado zitakuwepo pale pale haziwezi kuondoka.
Hapa anaongelea jumla. Wanaosoma hayo masomo ni wengi kuliko wa science. Na wana impact kubwa sanaUongo hayo ni yale ya kukariri ,ni kwa masomo ya arts ambayo Kikwete mwenyewe ndio aliyasoma nafikiri hayo ya kukariri aliyosoma yeye ndiyo anaongelea yeye alisoma digrii ya kukariri ya uchumi
Mainjinia,madaktari,hata makenika tu watoka VETA hakuna kukariri
Masomo ya sayansi hayana huo ujinga wa kukariri kama wa ARTS
Mkuu asante sana kwa darasa zuri ulilonipa....majuzi nasikia yale marekebisho ya katiba maarufu kama BBI ya majirani zetu wanataka kuongeza majimbo mengine ya uchaguzi.....wanasiasa wapo kwa aijili ya matumbo yao tu!Mkuu mwanasiasa yeyote huwa ana akili ya utambuzi vizuri sana, yaani ana uelewa mkubwa kuhusu kipi kizuri na kipi kibaya, siyo kwamba hawa viongozi wa sasa hawaelewi hili alilolisema JK, wanaelewa sana ila tatizo ni wataendeleaje kula kama wakitoa siri kama hizi ilihali hata wao hiyo elimu iliwaumiza. So wao wanakuja kukuambia ujiajiri huku akitumia uwezo wake wa kujenga HOJA NADHARIA kuchambua na kukuambia yasiyowezekan katika uhalisia wa maisha.
Hawa viongozi wetu siyo kwamba madudu yote yanaoendelea kila sehemu hawayajui, la hasha! Wanayatambua vema sana, ila wanajifikiria wao kwanza na familia zao, maslahi ya taifa ni baadae na hayo maslahi ni yale yasiyoathiri maisha yao kiujumla.
Leo serikali ikae ianze kutengeneza syllabus mpya yenye kukidhi vigezo vyote, hao wataalamu wanao?? Tanesco leo luku mfumo unasumbua nchi nzima, mifumo yetu ya mitandao na teknolojia tunachukua nje kisha tunatumia kujifunzia halafu ndiyo tulete mfumo mpya.
Ukionekana unaleta mapinduzi hata yenye faida kwa maslahi ya nchi utawaiwa faster na kuulizwa swali dogo tu "tupe kibali cha wewe kufanya hili", mimi juzi ndiyo nimeanza hata mafanikio bado ila lengo ni kuifaidisha nchi yangu leo unakuja niuliza kibali tena ukiwa na sura ngumu na baadhi kujia na polisi na wanasheria juu wa kuanza kuchambua ibara.
Kiufupi hata hao tunaotaka wabadili mfumo wao wenyewe hawajui wataubadili vipi maana wataalamu kwanza hawapo na wanaoaminika kuwa wataalamu wanaishi kwa copy and paste, no creativity at all.
Kuna kozi unasoma Tanzania, practical unaeenda jifunzia nje tena baada ya kuitwa graduate.
Shida ni kwamba tunaishi kimazoea na tunafanya mambo yaleyale. Yaani mechanical engineer kashakaririwa kuwa kazi zake ni zilezile naye anaishi humohumo, yaani hakuna kujiongeza.
Wajanja wengi hata makazini ni wale waliojiongeza na kujifunza vingi nje ya masomo yao na hao huwa wengi wao wanatafuta sehemu zenye kujua na kuthamini thamani zao. Ukimnyima kazi hapa anatoka anaenda nje huko unasikia baada ya miaka kadhaa tuna mtanzania anafanya kitu fulani huko nje na anafanya vizuri sana.
Hii nchi ukiwa tajiri, ukiwa na uwezo mzuri wa kufikiri, ukiwa na msimamo kusimamia haki na ukijitambua sana unageuka kuwa ADUI. Maana wengi hawapendwi wanaharabu kazi za wanasiasa ambao hawajui chochote zaidi ya kukesha kukariri vifungu vya sheria na kufuata taratibu ambazo zipo outdated so unapokuja na kitu kipya unawachanganya na kuona una nia ya kuwaharibia.