Kikwete: Kutokana na utoaji hafifu wa Elimu nchini, kuna hatari ya nusu ya ajira zilizopo kutoweka ifikapo mwaka 2050

Mbona hata sasa ajira hakuna wakati tuna ardhi ya kutosha ambaye tungewekeza huko ajira zingepatikana nyingi. Tatizo kilimo kinadharaulika wakati ndio ajira nyepesi, ni vigumi kijna aliyemaliza chuo kikuu kupewa mkopo wa kilimo kwa kuwa serikali yenyewe ni kama haikithamini hivi.
 
Rais mstaafu wa awamu ya nne Dk Jakaya Mrisho Kikwete ameonya tusipobadilika namna tunavyofundisha watoto wetu basi ajira zote zitatoweka ifikapo mwaka 2050.

My take.
Hii elimu yetu ya kuwafanya chadema washangilie kila baya linaloipata nchi yetu ikiwemo kukamatwa ndege, miradi kukwama , tutashitakiwa MIGA etc bora ifutwe kabisa tuanzishe elimu mpya itakayowafanya chadema wajitambue.

====

Dar es Salaam. Rais mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete amesema kutokana na utoaji hafifu wa elimu nchini kuna hatari ya nusu ya ajira zilizopo kutoweka ifikapo mwaka 2050.

Ameyasema hayo leo Jumanne Mei 18, 2021 wakati akizindua kongamano la elimu linalojadili ufadhili wa elimu lililoandaliwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (Tenmet) jijini Dar es Salaam.

Akieleza utafiti uliofanywa na tume ya kimataifa ya elimu ambayo yeye ni mjumbe, amesema elimu inayotolewa barani Afrika ilitolewa miaka 50 hadi 70 iliyopita kwa nchi zilizoendelea.

"Sisi bado tunatumia chaki, wakati wenzetu wanatumia tablets. Tuliona kuwa kuna watu zaidi ya milioni 263 waliotakiwa kuwa shule lakini hawapo, kati yao milioni 100 wapo Afrika. Kwa waliopo shule wengi hawamalizi shule. Wengi wanaishia njiani. Asilimia 67 wamemaliza shule, asilimia 33 ni idadi kubwa," amesema Kikwete.

Amesema kutokana na utoaji hafifu wa elimu na maendeleo ya teknolojia kuna janga la ukosefu wa ajira linakuja.

"Ifikapo 2050 asilimia 50 ya kazi zitafutika, kwa sababu ya matumizi ya mashine. Kutakuwa na magari yasiyotumia dereva. Unataka usafiri, unaita Uba, unatumia simu yako inakuja inakupeleka sehemu husika labda Ubungo Plaza au Millennium Tower," amesema.

Amesema mbali na ukosefu wa ajira, idadi ya watu barani Afrika itafikia watu bilioni mbili, “kama watu hao hawana ujuzi unafanya nini? Sijui itakuwaje. Kutakuwa na athari kubwa za kiuchumi na kijamii."

Akisisitiza matumizi ya teknolojia, Kikwete ameshauri kuwepo na uwekezaji katika elimu ili vijana wa Afrika wasiwe watazamaji, wawe washiriki wa uchumi.

"Kunatakiwa kuwepo na matumizi ya sayansi na teknolojia katika ufundishaji. Kila shule inatakiwa kuunganishwa na intaneti," amesema.

Huku akitoa mfano wa janga la corona, Kikwete amesema limethibitisha jinsi ukosefu wa teknolojia unavyoathiri ufundishaji.

"Tumeona wakati wa corona, moja hatua zilizochukuliwa ni kufunga shule. Wanafunzi wetu hawakusoma, wanacheza rede, lakini nchi zilizoendelea shule zilifungwa na watoto wakaendelea kusoma.”

"Nilipokuwa Rais tulianzisha matumizi ya intaneti katika ufundishaji, tuliwekeza sana kwenye mkongo wa Taifa. Lengo langu lilikuwa ni kuhakikisha kila shule, hospitali ziunganishwe na intaneti. Mwalimu mmoja wa hisabati afundishe nchi nzima,” amesema.

Kuhusu Elimu jumuishi ameitaka Serikali na wadau kuhakikisha hakuna mtoto anayebaki nyuma kwa kukosa elimu.

"Wengine wanadhani msichana ni wa kubaki jikoni. Wengine wameachwa nyuma kutokana sababu za kisiasa.

Tunatakiwa kuhusisha mashirika yasiyo ya kiserikali kuchangia elimu," amesema.

Awali akimkaribisha Kikwete mwenyekiti wa Tenmet, Dk John Kalage ambaye pia ni mkurugenzi wa taasisi ya HaliElimu amesema kongamano hilo litajadili kwa kina njia za ufadhili wa elimu nchini.

Chanzo: Mwananchi
Yeye alipokuwa namba 1 alichangia nini kuelekea huko anapopatamani! Huyu mzee naye mbona anatuingiza majaribuni! Hata kuitoa hiyo elimu ilipitwa na wakati bure alishindwa ati yakhe😜! Talking is cheap eeh😜!
 
Sina uhakika kama hoja yake ipo sawa. Ukienda Mlimani city japo kuna automated machines za car park bado utakuta kuna mtu ameajiriwa kubonyeza machine kutoa card na mwingine kutoa change kwenye machine ya kulipia. Huku Tanzania tunafanya vitu tofauti kidogo.
 
Mhhh! Hii ni hatari ssna. Mwanafunzi anamaliza form six hajui Microsoft Word. Power points, au excel. Huyu anaenda kuajiriwa na nani. Hajui hata kutengeza CV ya kuombea kazi. Atakuwa mgeni wa nani huyu?
 
Duh
 
Ukweli mchungu by 2050 kila kitu kitabaki kwenye technology

Hivyo wanaitajika watu ambao wapo tayari kujiajiri, Machine na operators wa machine

Maroobot vile vile yatakuwa yakifanya kazi sehemu kama shelli na super market

So kazi zitakuwa chache au kutokuwepo kabisa

Kikwete ana hoja tuchukue hatua.
Binafsi nimeshindwa kumuelewa Kikwete; anataka ajira ziongezeke au zipungue? Kwanini anahimiza matumizi ya teknolojia ambayo anafahamu matokeo yake ni kupunguza ajira?

Kama mwalimu mmoja tu wa hisabati ndo ataajiriwa kufundisha nchi nzima, huku si ndo kupunguza ajira? Sasa tuchague kutumia teknolojia au tuongeze ajira za walimu?
 
JK amesahau matumizi ya teknolojia hayabadilishi mitaala, usome kwa kutumia tablet au mwenzio aende kayumba at the end of the day wote watafanya mtihani mmoja.

Labda yule wa tablet atamzidi mwenzie topic alizo-cover in case ikitokea issue kama ya Corona, ila pasipokuwepo na Corona tofauti yao itakuwa ndogo sana.

Kitakachomyima mtoto wa masikini ajira hata akiwa na ufaulu mzuri bado ni kujuana (nafasi kutolewa kwa upendeleo) lakini sio kwasababu ya teknolojia, na ajira bado zitakuwepo pale pale haziwezi kuondoka.
Hao unaowaita masikini na wenyewe wabadilike wawe matajiri
 
Technology is a reality na inabadilika kila kukicha. Sasa ombi kwa Madame President. Unavyosema rukhsa kwa vibali vya kz left, right and centre jaribu kuingia mikataba ya wazi na haya makampuni na vijana wetu waenda hizo nchi zao kwa ajili ya sponsorship/secondment nk ili wapate exposure na experience ya technology. Ratio hata ya for every 10 expat 1/2 TZ siyo mbaya. Ifike hatua tukipewa tatizo walete na viable solutions...2050 tuna muda wa kijiandaa.
 
JK amesahau matumizi ya teknolojia hayabadilishi mitaala, usome kwa kutumia tablet au mwenzio aende kayumba at the end of the day wote watafanya mtihani mmoja.

Labda yule wa tablet atamzidi mwenzie topic alizo-cover in case ikitokea issue kama ya Corona, ila pasipokuwepo na Corona tofauti yao itakuwa ndogo sana.

Kitakachomyima mtoto wa masikini ajira hata akiwa na ufaulu mzuri bado ni kujuana (nafasi kutolewa kwa upendeleo) lakini sio kwasababu ya teknolojia, na ajira bado zitakuwepo pale pale haziwezi kuondoka.

Elimu yetu haitoi kipaumbele kwa wanafunzi kuwa creative. Ina heshimu wanaoweza kukariri.
Anachosema JK ni kuwa hizi kazi zilizopo leo zinapungua kadri technology inavyoenda mbele.
Bila kuwa na elimu itakayoweza kutengeneza kazi za aina mpya, wengi watakuwa hawana kazi. Sio Tanzania tu, hii ni Dunia nzima. Artificial intelligence inaanza kubadili mambo taratibu. Ni lazima elimu yetu ibadilike ili iweze kuwajengea wanafunzi uwezo wa kuhimili changamoto mpya zinazotokana na muda kubadilika
 
Kuzeeka kuna mengi keshaanza kupoteza kumbukumbu

Kwa hiyo ikifika hiyo miaka serikalini na mahakamani tutaajiri wazungu kufanya kila kazi ya ajira iliyoko serikalini na kwenye mahakama zetu?
Aher JK aliyezeeka mwili kuliko wewe uliyezeeka akili.
 
Mleta mada una nyege za sehemu za duara.
Hapo CHADEMA imekujaje?
Nyie si ndio mmeleta elimu duni ili muendelee kuwatawala Wadanganyika?
 
Kwa hiyo ikifika huo mwaka majeshi yetyu yote iwe polisi au JWTZ watakuwa wanaajiriwa wazungu wenye elimu bora?
Tatizo ni kwamba akilini na uwezo wenu wa kufikiri unaishia mita 2.

Huna habari kuwa mpaka sasa kuna attacking choppers na hata ndege ambazo zinashambulia bila hata ya kuwa na rubani ndani? Idadi ya waongozaji kwenye kituo cha kuongozea haiwezi kuwa sawa na idadi ya marubani.

Kama umesafiri, nadhani umeona siku hizi katika mataifa yaliyoendelea ambapo kuna treni za umeme ambazo hazina madereva. Lakini zinafanya kazi masaa 24.
 
Kwa hiyo mahakimu na majaji watakuwa ni hayo maroboti ,mapolisi watakuwa ni hayo maroboti,Leseni za biashara zitakuwa zinatolewa na hayo maroboti,madaktari na manesi watakuwa ni hayo maroboti,WAtoto mashuleni na vyuoni watafundishwa na hayo maroboti au?
Uwezo wako wa kufikiri ni mdogo sana.

Teknolojia inavyoenda, itafika mahali, kazi iliyokuwa inafanywa na majaji 20, itafanywa na jaji mmoja mwenye uwezo wa kutumia teknolojia ya kisasa. Jaji ataweza kuendesha kesi akiwa Dar, mshtakiwa akiwa Kigoma, shahidi akiwa Songea.

Nenda nchi zilizoendelea uone polisi wanavyofanya kazi. Huoni polisi wa usalama barabarani akiwa barabarani, lakini ukikiuka tu sheria, umenaswa. Kazi ambayo zamani ilifanywa na polisi 50, leo wanafanya polisi 5.

Wewe sijui unaishi Ulimwengu gani!! Hivi hujaona leseni zinazotolewa mitandaoni. Unajaza kinachohitajika, system ina-collerate, kisha leseni inatoka au inakataliwa.

Tatizo ni kwamba mmezeeka akili, huku miili yenu ikionekana bado ni vijana.
 
JK amesahau matumizi ya teknolojia hayabadilishi mitaala, usome kwa kutumia tablet au mwenzio aende kayumba at the end of the day wote watafanya mtihani mmoja.

Labda yule wa tablet atamzidi mwenzie topic alizo-cover in case ikitokea issue kama ya Corona, ila pasipokuwepo na Corona tofauti yao itakuwa ndogo sana.

Kitakachomyima mtoto wa masikini ajira hata akiwa na ufaulu mzuri bado ni kujuana (nafasi kutolewa kwa upendeleo) lakini sio kwasababu ya teknolojia, na ajira bado zitakuwepo pale pale haziwezi kuondoka.
Umeshawahi kufanya interview kwenye taasisi za kimataifa kupitia electronic systems? Huyo anayetumia tablet ana nafasi kubwa ya kupita kuliko wa chaki. Tuwekeze kwenye elimu ya kisasa. Mambo ya A+ za makaratasi tuachane nayo yaani.
 
Population itakuwaje mwaka huo? Population ikiongezeka ajira zinaongezeka pia haziwezi kushuka zaweza shuka eneo moja zikaongezeka eneo lingine mfano population ikiwa itaongezeka ajira za madaktari na manesi lazima ziongezeke,pia za walimu,Maaskari na watendaji wengine.Huwezi tu kusema tu kwa sababu kiwandani zitashuka haina maana sekta nyingine kuwa nako zitashuka

Kuongelea kushuka au kutoweka kwa ajira unatakiwa kuangalia vitu vingi kimojawapo ni population je itakuwaje kipindi hicho na itahitaji nini kutoka soko la ajira wa kuwahudumia?
Mawazo finyu sana.

Hujui leo hii kutokana na maendeleo ya teknolojia, hospitalini, specimen ambazo zamani zilikuwa zinapimwa kwa kutazamwa kwa macho, moja baada ya nyingine, lakini kutokana na maendeleo ya teknolojia, kwa sasa unaweza kuzipima hata 400 kwa wakati mmoja? Kama zamani ulikuwa na wagonjwa 100, sasa una wagonjwa 200, zamani ulikuwa unapima specimen moja moja, sasa anazipima kwa mara 1 specimen 400, bado utasema kutokana na ongezeko la wagonjwa, na ajira za upimaji zitaongezeka?

Wenzetu, kwa sasa, ni kuwa specialist ambaye zamani ulihitaji kila hospitali iwe na wa kwake, leo anaweza kuwa Mwanza, akamsikiliza na kumhudumia mgonjwa wa Namabengo. Lakini pia huyo specialist amerahisishiwa sana kazi yake kwa sababu diagnosis ya awali inafanywa na instruments. Hata prescription ya tiba inafanywa na mashine.
 
Elimu yetu haitoi kipaumbele kwa wanafunzi kuwa creative. Ina heshimu wanaoweza kukariri.
Uongo hayo ni yale ya kukariri ,ni kwa masomo ya arts ambayo Kikwete mwenyewe ndio aliyasoma nafikiri hayo ya kukariri aliyosoma yeye ndiyo anaongelea yeye alisoma digrii ya kukariri ya uchumi

Mainjinia,madaktari,hata makenika tu watoka VETA hakuna kukariri

Masomo ya sayansi hayana huo ujinga wa kukariri kama wa ARTS
 
Back
Top Bottom