Kikwete kuwa Gorbachev wetu?

Kikwete kuwa Gorbachev wetu?

Inachanganya kidogo kwamba Karume anatia saini lakini haionekani kwenye mkataba...naona picha hii imepigwa wakiuziana kiwanja sio muungano.

Kama ingelikuwa muungano basi hiyo saini ya Karume ni lazima ionekane kwenye mkataba.

hivi umewahi kuona mkataba wa Muungano? au unafikiria ile sheria ya kuridhia Muungano ndiyo mkataba wenyewe.. mnanifanya nicheke sasa maana yawezekana nina kazikubwa zaidi kuliko ya miaka minne iliyopita.
 
Muungano ulipigiwa kura na Bunge la Tanganyika na Baraza la Wawakilishi wa Zanzibar. Pande zote mbili zilijadili (najua wengi hawajui historia hiyo). Nyerere alileta hoja Bungeni na kuwaelewa wabunge wetu kwanini mataifa mawili haya yataungana. Wabunge wakaridhia na ni baada ya hapo ndio Muungano ukafanyika.
Kama ni hivyo ni jambo lililo bora na zuri wananchi wakayazungumza mambo haya aidha kupitia mabunge yote mawili au kwa kura ya maoni kwa sababu inavyo onekana hakuna taifa hata moja katika mataifa haya mawili yaliyoko kwenye huu Muungano aliyemlazimisha mwenziwe kuungana.

Na hakuna ubaya wowote wala dhambi kwa pande zote mbili kusikilizana nini mwenziwe anataka. Kama upande mmoja unafikiria kuwa jambo hili wakati wake umekwisha tulibadilishe, basi wasikilizane tu na sio kufanyiana vitisho.

Hivyo ni Muungano halali na ni jukumu la kila Mtanzania kuulinda. Katika kuulinda huko ni jukumu letu kuwapinga pasipo kuwapepesea macho wale wote wanaotaka Muungano uvunjike kwa sababu hawataki kufanya maamuzi magumu au kuzungumzia mambo yanayoleta utata katika Muungano. Wapo watu wa bara ambao kwa kawaida hatupendi sana migongano, tunapenda vitu lelemama kiasi kwamba tumekuwa kama tumedekezwa hivi!

Huu Muungano ni mali ya Tanganyika na Zanzibar kama kuna kero kutoka upande wowote ni busara kuelezana kupitia vyombo husika na si kufikiria kuwa upande mmoja mawazo yao ni ukoma au yule mwenye kuuliza mambo yaliyoko kwenye Muungano ni msaliti...! Nyerere na Karume walikuwa ni binadamu kama mimi na wewe, nao walikuwa na mapungufu yao.

Muungano unajadilika tena sana na bila wasi wasi wowote.
Serikali ikisema "hawa wanaleta mgawanyiko katika jamii" basi kama watoto tunakubali na kuwakimbia wenzetu kwa sababu "serikali imesema"; Serikali ikija na kusema wapinzani wanataka kuligawa taifa basi tunakimbia kama watoto huku tumenyanyua mikono tubebwe huku tunaonesha vidole "yule anataka kuligawa taifa mama!".
Watanzania wengi hawajazoewa kufikiria wenyewe, wakati wa zidumu fikra za mwenyekiti zishapitwa na wakati kwani sasa mfumo wetu si wa kijamaa tena... huu ni wakati wa fikra mbali mbali m-badara... Wakati wa kutishana tulisha uzika pale alipozikwa Nyerere kule Butiama... Tumekubali vyama vingi basi tukubari fikra mpya as long tunatumia vyombo husika tena bila kutishiana maisha.

Hatutaki kugonganisha mawazo na matokeo yake hata kwenye vikao vya kazi tumekuwa hivi hivi tu. Mtu anayebisha sana anaonekana "mbishi tu"; mtu anayetaka maelezo zaidi anaonekana kama anataka kujipendekeza. Tunataka mambo ya upole upole na taratibu.

Ndio maana utaona watu wengi wa bara wanaotaka Muungano uvunjike wanafanya hivyo kwa sababu utaondoa "migongano" na kubishana bishana. Tunataka "utulivu, amani, na mshikamano" wa uongo. Ndio maana watu wa bara wanaona kama Zanzibar ni wakorofi kweli kumbe kule Zanzibar wao wameshazoea zile siasa za kujibizana, kubishana na serikali, na kutunishiana misuli.
Tatizo lipo uko uko kwa waliokamata madaraka, mbinu wanao tumia ni ile ya kumwita Mbwa jina baya ili haonekane mbaya apate kipigo toka kwa watoto mitaani.

Serikali inatakiwa kuondoa hizi choko choko za maneno kama nilivyoa andika hapo juu... dawa ni kukaa vikao husika tena ka kushirikisha vyama vyote vya siasa na kuwepo na kula moja mtu mmoja, kwa maana kila mwakilishi hawe na haki sawa na si kutumia hili bunge lililo jaa wabunge wa chama kimoja na kila jambo kuwa na maamuzi ya jazba bila kuangalia maslahi ya taifa.
Ninaamini athari kubwa sana ya ukoloni katika psyche ya watu wa bara ni unchecked docility ya ajabu sana. Na watawala wetu wanatumia sana hii kuwatuliza watu wa bara.

Muungano tutaulinda na tutaudumisha na kuuboresha. Tutawapinga watu wa bara wanaotaka kuuvunja kwa sababu hawataki kubishana na kulumbana na kugongana kifikra na tutawapinga watu wa visiwani wanaotaka kuuvunja kwa sababu wanaogopa kukubali ukweli wa umuhimu wa muungano.

Tutawaunga mkono wale wote majasiri ambao watasimama na kutoa hoja za jinsi ya kuudumisha, watakaokuwa tayari kutoa mapendekezo ya jinsi ya kuuboresha na wale watakaonesha uongozi wa kuboresha muungano wetu kwa uwazi na ukweli na ujasiri usio kikomo.

Natumaini hatutawafumbia macho wala kuwaonea haya kuwashughulikia pasipo kuwabembeleza watu wanaofanya njama za kuuvunja muungano wetu.

Muungano daima!

Tusiwazuie Watanganyika na Wazanzibar kuzungumza masuala ya Muungano na Katiba, kama kuna baadhi ya mambo yanatakiwa kufanyiwa marekebisho, yafanyiwe bila kuonekana wengine wachawi, serikali isiwatishe watu watu wanao hoji mustakabali mzima wa mambo ya Muungano kama katiba inafaa au haifai dawa ni kuangaliwa upya.

Hii katiba ina viraka kama nguo ya mwenda wazimu... Na hivyo viraka vimewekwa na hao walioko madarakani, wakati umefika sasa ya kushona nguo mpya...! Kama kweli serikali inataka umoja wa kitaifa ni bora kutengeneza katiba mpya.

Hali hii ya baadhi ya watu kutaka kuvunja Muungano ni matokeo ya serikali tawala kukaa kimya na kuwatisha wale wote wenye kuulizia mambo ya Muungano na katiba.

Hivi hao waliokuwa viongozi (marehemu Nyerere na Mzee Karume) hawakuwahi kuhitilafiana kwenye masuwala ya Muungano mbona tunawaona kama vile walikuwa malaika? Kama walihitilafiana nina uhakika kabisa walikaa na kuyazungumza yakaisha... basi nasema kuwa wakati huu si wa marais wawili kukaa peke yao na kuzungumza kero ya Muungano na katiba ni haki ya Watanganyika na Wazanzibar kukaa kitako na kuyazungumza hadi kukubaliana. Tatizo lililopo sasa ni kuwa viongozi hao wa juu hawataki kuzungumza na kila mwenye kusema anaonekana kuwa ni mwenye kutaka kuvunja Muungano.

Wakati ni huu sasa tuwe wakomavu wa fikra, hakuna lisiloweza au kuzungumzika.
 
..natamani Raisi ajaye wa Muungano atokee Zenj.

..huo ndiyo utakuwa mwisho wa Muungano kutokana na vurugu za wa-Tanganyika.

..kumbukeni kwamba Mwalimu hayuko tena kuipinga kwa mabavu hoja ile ya Wabunge wa Tanganyika.
 
Hizo ndizo zilizoitwa kero za muungano,zilishindwa kujadiliwa muda muafaka tukasema muungano ni jambo nyeti halijadiliki nani alitudanganya? hatuwezi kulibana tena lazima liishe kama tuendelee na muugano na tujue umesimamia wapi au tuachane nao, tuuache vipi wakati tunafikiria kuingia kwenye East African federation, kwanini tusitengeneze mazingira ya kushindana na wanyarwanda na wakenya pindi tukiingia humo? bado watu wetu skuli ndogo, wafanyabiashara mitaji hakuna na waliokua na pesa sio wamezipata kwa biashara bali kwa kukwapua somewhere,
na pamoja na kukwapua kwao wameenda kununua nyumba dubai na sasa hazikaliki wala haziuziki!hivi Black skinny kuna shida gani?
 
Si ndio wanafuata wanatumia kikao cha wawakilishi kilicho halali kikatiba kuomba kibadilishwe ili kiwafae watu na mahitaji yao...

tatizo kwanini watu wa bara wanataka kuwahadaa wazenj wasitumie fursa hiyo kubadilisha katiba?

Muungano unatakiwa uwe kwa manufaa ya wananchi na sio watawala. Kuendelea kuwepo kwa muungano pia kunatakiwa kupimwe na wananchi wa pande zote mbili kama wanauhitaji au la, hivyo yanayoendelea sasa kwa Wazanzibar ni haki yao kabisa, na sioni taabu yoyote, madamu wao wana serikali yao wanakila sasabu ya kutathmini na kuona kama nafasi yao ndani ya muungano iko je? Wakiona kuna haja ya kuendelea sawa, na pia wakiona hawauhitaji huu muungano basi wapewe nafasi yao! Hata ndo zinakuwepo pale wawili wanapokubaliana na kila mmoja kuona umuhimu wa mwenzie.

Muungano wa kuwapa watawala madaraka tu wa nini?
Muungano wa kuwanyima watu maamuzi juu ya rasilimali zao wa nini?

Kama sisi wabara hatuoni taabu na muungano huu, isiwe kisingizio cha kuwanyima wenzetu wa Zenj kuutathmini upya! Kwanza huu muungano sio wa watanganyika na wazenj kama wengi wanavyotaka tuamini.
 
wajukuu zangu, mie naungana na nyie juu ya ulinzi wa katiba yetu na wazo la kuwa makini juu ya utawala wa kikatiba maana huu ndiyo msingi wa muungano wa nchi hizi mbili.

lakini yapo mengine ambayo yataharibika baada ya muungano huu kuvunjika.ni dhahiri kwamba hali ya amani na utulivu iliyopo na tafsiri ya mshikamo iliyopo baina ya mataifa yetu ,kwa upande wa biasharana hata mahusiano binafsi yanatia moyo.kuvunjika kwa hili kutaathiri sana haya.

lakini pamoja na haya yapo mambo mengine mengi ambayo kwa kweli tutayapoteza kama hali hii itatoweka.

suala la kulinda muungano ni letu wote na nisingependa tulipuuze. watu wa kwanza kuchukiwa ni wale wanaopinga muungano huu.

1. Amani ya nani tunayoiongelea Tanzania? polisi kuwajambazi wananchi kwa kutumia silaha za moto,
2. au kukomesha mauwaji ya wenzetu albino waisio na hatia?
3. kuuza haki za wananchi kama ardhi yenye rutuba na maeneo ya wanachi yenye madini nao kuhamishiwa nyikani
4. uuzaji wa mali asili, mbuga wanyama, samaki na mafuta bila kujali haki mtanzania?

amani ya kutokuwa na huduma za msingi kwa watanzania? shule afya, usafiri, lishe n.k. Labda ndio amani unayoongelea. Kweli Wazanzibar/watanganyika ndio chanzo cha haya yote. Nadhani kila upande una mambo yake ya msingi, ila hili la amani huku wanatanganyika/wazanzibar wanakosa mahali pa kudai haki zao silioni.

Labda Tanganyika wenye siri za muungano huu watuambie siri iliyopo! Kuna visiwa vingi tu kuanzia mashariki hadi magharibi ya bara la afrika, sijui vinathhiri vipi amani ya nchi husika. Labda, lakini sijui!
 
Soma kwa makini ibara ya 104 ya katiba ya JMT. Utafanyaje mabadiliko ya Kiongozi wa Zanzibar bila kuiathiri ibara hii? Katiba ya JMT inayo mapungufu yake, hatukatai. Lakini, ndio tuliyo nayo kwa sasa na ndio iliyowaweka madarakani viongozi tulionao. Wote waliapa kuilinda na kuitetea. Kama wanashindwa waondoke.

Unanichekesha kweli,
Mbona sasa kunakuwaga na mabadiliko ya katiba? kwa sababu hiyo katiba inayobadilishwa tayari kuna watu waliokwishaapa kuitekeleza, hivyo kubadilisha kifungu chochote ni kwenda kinyume na kiapo ambacho tayari ulikula kukilinda. Katiba inabadilishwa kwenda na wakati na kulingana na mahitaji ya wakati husika.
 
@Kuchanganya Mchanga
Mchanga uliochanganywa ni wa Tanganyika tuu...naye ni Nyerere pekee ndie aliechanganya mchanga huo wa mikoa tofauti kutoka Bara.

Ukitizama hii picha, utaona Karume hajagusa mchanganya huo..kwasababu si mchanga wa visiwani.

@Mwanakijiji
Ukitizama nyaraka ya muungano ni saini za Nyerere tuu na Msekwa hakuna saini ya Baraza au bunge la Zanzibar.Sasa huu msimamo wako kuwa Zanzibar walipitisha na kukubali muungano ulitokea wapi?Lete ushahidi kama huna basi unazungumza pumba tupu...

Nyaraka ya muungano iliyopo kwenye public http://www.scribd.com/full/24823426?access_key=key-1dlp0tnzt4n91utuby5c

Kwi kwi kwi, unachekesha kweli unapoleta habari za mchanga! yaani ndicho kizuizi cha muungano? kwi kwi kwi! kule horohoro, namanga na kwingineko miguu inabeba mitope kupeleka kenya na kuleta tanzania, na kwingineko lakini hakuwi kenye wala tanzania!
 
Kuna msemo unasema "usilolijua ni kama usiku wa kiza".

Ulichoambatanisha kuwa ni "nyaraka za Muungano" ukweli ni sheria iliyopitishwa na Bunge la Tanganyika kuridhia muungano; sheria kama hiyo ilipitishwa Zanzibar vile vile. Utaona kuwa ni kwa sababu hiyo unaona sahihi ya Nyerere kukubali mswada wa sheria kuwa sheria kamili; sahihi ya Katibu wa Bunge (wakati huo Msekwa) na chini kuna sahihi ya Chief Mkwawa (ambaye alikuwa ni Spika).

Wale wanaodai Muungano ulifanywa kwa siri ni wakanaji wa historia. Sheria ya Muungano iko wazi (kama ulivyoiweka hapa). Na mjadala wa Bunge la Tanganyika kuhusu Muungano unaweza kupatikana kwenye ofisi za Bunge. Hakuna cha siri ni tatizo la watu ambao hawataki kufanya uchunguzi wao wenyewe kwenda kutafuta ukweli.

Kwa maana hiyo katika huo mkataba wa muungano walisema kuwa utaratibu upi utakaotumiaka kuuvunja muungano?

Kama Zanzibar ni nchi ndani, lakini sio nje, basi wanaweza kufanya mmamuzi yooooote watakayo ikiwa ni pamoja na kujadili hatima ya muungano, na bila shaka wakati ukifika watayawakilisha. Hapo unaonaje?
 
Kama mafuta yako muungano ubaki,kama hakuna uvunjike,option nyingine labda Zanzibar iwe mkoa.
 
Ulichoambatanisha kuwa ni "nyaraka za Muungano" ukweli ni sheria iliyopitishwa na Bunge la Tanganyika kuridhia muungano; sheria kama hiyo ilipitishwa Zanzibar vile vile.

Tupatie waraka bro...kama nilivyosema awali, kama huna ushahidi hoja zako haziwezi kuwa na makalio.

Mimi nakubali kama hiyo niliyoleta hapa kutoka kwenye maktaba yangu ya scribd ni sheria iliyopitishwa na bunge...lakini huo mkataba wa muungano umo ndani yake kama ni attachment.

Wewe kama unayo original copy yenye saini kutoka Zanzibar, basi tuekee hapa...mie nasubiri 🙄
 
Hakuna Muungano wa Mungu na Shetani ukamnufaisha Mwanadamu
Wala Muungano wa Simba na Yanga kujadiri washinde vipi michezo yao
Wala Muungano wa paka na panya kujiwezesha kudumisha ushirikiano wao
Wala Simba na Swala kukaa pamoja na kujadiliana leo nani amle mwenzie

Ili Kikwete aonekane ana akili auachilie mbali Huo Muungano wa kihuni na
kushughulikia taifa katika maendeleo, usio kuwa na faida kama BONGO FLAVOUR kanisani au KITIMOTO msikitini
 
Tupatie waraka bro...kama nilivyosema awali, kama huna ushahidi hoja zako haziwezi kuwa na makalio.

Mimi nakubali kama hiyo niliyoleta hapa kutoka kwenye maktaba yangu ya scribd ni sheria iliyopitishwa na bunge...lakini huo mkataba wa muungano umo ndani yake kama ni attachment.

Wewe kama unayo original copy yenye saini kutoka Zanzibar, basi tuekee hapa...mie nasubiri 🙄

sasa si uende baraza la wawakilishi Zanzibar wanao. Muungano siyo siri.
 
Sasa nawaombeni wana JF muwe wakweli munapo jadili masuala mazito ya nchi.Sio munaleta zile kasumba za kisiasa kama alivyofanya Nyerere baada ya kupata uhuru.

Muungano umefanyika na kumekuwa na debate kubwa kuhusiana na uhalali wake.Kuna vitabu ambavyo watu ni specialists katika masuala ya politics, na wote hao wanaonesha uhalali wa muungano ni issue ya kudebate.

Mimi sikuwapo wakati huo, lakini honestly naweza kumfahamu hayati Karume kwanini alifanya muungano.Huu muungano inawezekana sana kwa Tanganyika ulipita sheria zote za kuuhalalisha, kama tunavyoona kwenye nyaraka niliyotoa awali.Kwa upande wa Zanzibar sheria hazikufuatwa, ni Karume tuu akisaidiwa na Nyerere walifanya hivyo.Hata kama kuna saini ya Karume, bado hii issue ina utata kwani huyo Karume hakuwa raisi halali wa Zanzibar.Halali si kwa maana ya kuwa hakuwa na maji ya uarabu, bali kupitia njia za demokrasia au uchaguzi.

Serekali iliyopinduliwa 63 ilikuwa ni serekali halali.Nitaihalalisha sio kwasababu mie nilikuwa ni supporter wao, bali hii serekali ilipata ridhaa au kuwekwa madarakani kwa kupitia uchaguzi.Sasa uchaguzi ulikuwa haki chini ya muingereza, hilo ni suala jengine.

Motives za kuunganisha nchi?Tuweke akilini kuwa hawa viongozi walikuwa ndio kwanza wachanga katika masuala ya siasa (akiwemo Nyerere).Wote walikuwa kwa mara ya kwanza wanapewa uhuru, hawajatulia vizuri kwa upande wa visiwani kukatoja mapinduzi.Maisha hayakaliki, ndio Nyerere akampa tough Karume kuleta muungano.Lakini kama nilivyosema awali Karume hakuwa raisi halali wa Zanzibar na juu ya hayo pia hakufuata sheria na kanuni za kuunganisha nchi.Hakupitisha kwenye baraza la mapinduzi ambalo lilikuwa ndio kama bunge la Zanzibar kwa kipindi hicho n.k

Sasa munapokuja hapa na hoja zenu ati bunge la Zanzibar lilipitisha, ndio na mie huwa natoa kikwazo lete ushahidi.Hii hoja imeungwa mkono na Dourado ambae alikuwa ndie mwanasheria mkuu Zanzibar.

Vyovyote iwavyo huu muungano hauna faida, kwa upande wa visiwani umekuwa ni kero na kikwazo cha kila unapotaka kutia mkono.Sasa tokea Jumbe huko watu walikuwa na harakati za kutaka mjadala wa muungano.Lakini Nyerere again, akajifanya smart akaona bora apeleke muda mbele kwa kufunika shuka zito kwa wale wana harakati.

Ukweli huwezi kuuficha utakacho fanikiwa ni kununua muda tuu, ili muungano usivunjikie mikononi mwako kwa vile wewe ndio rais wa kipindi hicho.Lakini ukiondoka mjadala unarudi tena.

Suala jee kuna faida kuendelea kila siku kupigizana kelele na kuwekana roho juu.Au huku ndio kudumaza maendeleo na kupotezeana muda?

Nitawaachieni mujadili...
 
Munaijua hekima ya Nyerere kudai Mseto baada ya 1995?Nyerere alikuwa anaijua vizuri siasa ya Zanzibar.

Alifahamu vizuri kama Zanzibar siasa ni kama dini inaambatana na maisha ya mzanzibari kila siku.Na alijua fika ASP haikuwa na 100% support kama kilivyokuwa chama chake cha TANU.Hii inaweza kuwa ni moja ya motive za kuunganisha TANU na ASP, kuvunja makali ya maamuzi ya mzanzibari kisiasa.

Hapo utaona kama Nyerere aliposema Mseto hapo 1995 alishajua na alishasoma huko 1964 sababu ya Mapinduzi.Mapinduzi yalikuwa ni tukio moja ya "winner takes it all".

Sasa watanganyika huheshimu maelekezo yote ya Mwalimu, lakini kwenye Mseto ambao muasisi wa Tanganyika na mtu anaeheshimika kwao alikubali kuwa hili ndio suluhisho la umwagaji damu visiwani...leo wanampinga hadharani.

Hivi Msekwa na Makamba pamoja na puppets wao, hawa si ndio wanatakiwa kumuenzi Mwalimu? 😀
 
"Without any question, the manner and the implications of the union between Tanganyika and Zanzibar is the most misunderstood aspect of Tanzania's political development. It may not matter very much when foreigners get confused, but unfortunately there are many times when Tanzanians themselves appear to misunderstand it."


[FONT=Times,Times New Roman]Former Tanzanian President Julius Nyerere.[/FONT]
[FONT=Times,Times New Roman]Dar es Salaam Government Printer, July 1970. p. 3.[/FONT]​
 
Mi nadhani tunatakiwa kujua kwanini tunaungana, tunaungana katika maeneo yapi na kwa jinsi gani. Vinginevyo tutakuwa tunaahirisha matatizo tu, ukweli lazima siku moja muungano utavunjika sababu hakuna anaejua thamani yake. Kwa mfano Umoja wa Ulaya walichukua muda mrefu kufikia walipofikia, na hawakuanza na hatua za juu za muungano, walianza kuungana katika maeneo machache baada ya majadiliano, kwa hiyo kila mwanachama anajua kwanini amekubali kuungana na atanufaika vipi, changamoto ni zipi na namna ya kuzikabili.


Annina
 
Mi nadhani tunatakiwa kujua kwanini tunaungana, tunaungana katika maeneo yapi na kwa jinsi gani.

Id bet even your so called president is not fully aware of these critical subjects 😀
 
Kuna mtu yeyote anakumbuka hotuba ya Nyerere Bungeni kuelezea Muungano kabla hawajapitisha sheria iliyoridhia mkataba wa Muungano (ambayo MrFroasty ameiweka hapa)? Au ndio tunazungumza na vijana watupu humu jamani?
 
Unauliza swali halafu unakisia jibu mwenyewe?

ofcourse unaweza kukisia kutegemeana na historia yako ya "blind" follower of nyerere!

Kwa kuna hoja zaidi ya hiyo ya kutaka muungano ulindwe! siyo wewe wala ccm wanaweza kutuambia zaidi ya kuogopa eti mizimu ya wafu (nyerere/karume)

kama wanayo waseme na tujadili!
 
Back
Top Bottom