Elections 2010 Kikwete Kuzomewa na Kupigwa mawe?

Elections 2010 Kikwete Kuzomewa na Kupigwa mawe?

Watanganyika hamuwezi kuikataa CCM katika masanduku ya kura ,hilo kamwe halitasaidia kitu ,mbinu za kuishinda CCM ni mbinu zilezile zilizotumika Pemba ,mbinu ambazo ziliwafanya usa;lama wa Taifa wasipate usingizi mbinu ambazo ziliwafanya FFU wakimbie na masanduku ya kura mchana kweupe,mbinu ambazo zilivifanya vikosi vya SMZ na Polisi wa Muungano kufanya unyama usiosahaulika ,mbinu ambazo zimeilazimisha Serikali ya CCM Zanzibar kuamua na kukubali serikali ya umoja wa Kitaifa ,ni baada ya October kwisha kwa Uchaguzi mkuu ndipo hapo CUF itakapoingia kwenye serikali hio ,mawili ama awe ndio mshindi na CCM kuingia au awe ameshindwa na hivyo pia atakuwemo kwenye serikali tena kwa nafasi nyeti.

WaTanganyika walio wengi bado wanawaogopa polisi ufikapo uchaguzi hawawezi kuwaekea ngumu na kuhakikisha asiehusika hapigi kura ,na maboxi ya kura yanaisabiwa na kila mmoja anaona ,zaidi ni hawa mawakala wa vyama ambao roho zao bado hazijatosheka na kuweza kuibeba dhamana waliopewa kwa lolote litakalo kuwa ,akiekea hela ndogo kama milioni moja tu anawacha mawakala na watume wafanye na kupanga watakavyo. Hilo sio jambo dogo.

Jengine ni kuwa WaTanganyika hawawezi kuungana na kupinga matokeo kwa pamoja na kujumuisha wananchi ,mara utasikia akina Chadema hawaungi mkono wala mguu na si ajabu wakatoa pongezi ,kusema kweli hamuna musimamo ni mahodari wa kusema na kulipuwa mabomu pale bungeni lakini ukweli unapodhihiri huwa mnajitenga.

Mkuu nakubaliana na wewe watanganyika ni watu hewala. wanaibiwa kura na wanajua kabisa kuwa wameibiwa, kinachofanyika ni FFU wanawapiga mabomu na virungu wanakimbilia ndani, wachache wanakamatwa na baadae wanasamehewa wanafurahia kwelikweli. Vyama vingi vya siasa ni succus ya CCM wewe ukigoma wao unasikia sisi tunakubali. Zanzibar vyama imara ni CCM na CUF hapo ndipo unapoona kuwa mafahali wawili lazima pachimbike. Wanasiasa wetu kinawaua njaa akioneshwa bulungutu tu mate nje anasahau kama yeye ni mpinzani.

1.Jeshi la Polisi ni lake
2.Uhasama wa taifa ooooh am sore namaanisha Usalama wa Taifa wapo chini yake.
3.Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni yake
4.Zekomedi (Augustine Mrema et al) ni wakwake
5.Waongo,wanafiki,wazushi, wambea na wababaishaji(Muhingo Rweyemamu aliyezusha eti Dakta Slaa katumwa na Mzee Ratzinger) nae anaripoti kwake
6.Yeye ni kiongozi wa Chama cha watu waliofuzu digrii za juu zaidi za WIZI WA KURA
Kwahiyo hata akipigwa mawe au akizomewa haisaidii kitu

Mkuu upo sahihi kila siku mwizi anapokuwa anaiba na watu wanamuangalia tu anaona kuwa haibi bali anachukue kilicho haki yake. Ila akipata mkong'oto huwa anakuwa makini sana kuhakikisha ama haonekani kama kaiba au anaacha wizi kwa bara hili bado ni ndoto
 
Mkuu nakubaliana na wewe watanganyika ni watu hewala. wanaibiwa kura na wanajua kabisa kuwa wameibiwa, kinachofanyika ni FFU wanawapiga mabomu na virungu wanakimbilia ndani, wachache wanakamatwa na baadae wanasamehewa wanafurahia kwelikweli. Vyama vingi vya siasa ni succus ya CCM wewe ukigoma wao unasikia sisi tunakubali. Zanzibar vyama imara ni CCM na CUF hapo ndipo unapoona kuwa mafahali wawili lazima pachimbike. Wanasiasa wetu kinawaua njaa akioneshwa bulungutu tu mate nje anasahau kama yeye ni mpinzani.

Mkuu upo sahihi kila siku mwizi anapokuwa anaiba na watu wanamuangalia tu anaona kuwa haibi bali anachukue kilicho haki yake. Ila akipata mkong'oto huwa anakuwa makini sana kuhakikisha ama haonekani kama kaiba au anaacha wizi kwa bara hili bado ni ndoto

Nakubaliana na wewe tu kwa sababu unaujua ukweli jinsi ulivo ila nakupinga kwa kuendelea kusimamia mtazamo huo wakati ukijua kabisa una wajibu wa kuleta mabadiliko katika fikra za watanzani wanaoendelea kuaimini kuwa tanzania bila ccm haiwezekani. Ni nani ambae aliyewahi kuwaza kwamba dola ya roma ingeporomoka enzi za utawala wake? Ni wachache tu waliowaza hivyo ila katika uchache wao waliyafanyia kazi mawazo yao hadi kuidondsha dola kubwa ya roma. Suluhisho si kuendelea kusifia udhalimu huo bali kuchukua hatua madhubuti kubadili mtazamo wa watu, na hii haihitaji umwagaji damu. Amini nakwambia hata ndani ya usalama wa taifa, polisi, jeshi, tume ya uchaguzi na hata serikalini wapo wasiomkubali kikwete hata kidgo. Chukua hatua.
 
Kwa nini wampige mawe? hakuna sababu wala ya kumzomea, wamnyime kura zao wakitaka inatosha.

Kupigwa mawe ndo inamfaa, akinyimwa kura wataiba kwa hiyo haitasaidia. Mi nimeipenda hiyo ya Mbeya kama watanzania wote tungeweza kufanya hivyo ingekuwa bomba mbaya.
 
Ukiona watu wanakuwa kama Interahamwe ujue hamna akili.Unahamasisha watu wampige mawe Kikwete,unajua hicho ni chanzo cha kuanzisha vurugu?
Unadhani hisia zako zinaishia hapo?Hujui kama kuna watu watakaotaka kukurudishia hapo mawe?Fikiria kabla ya kuandika utumbo wako.Haiwezekani kuleta sera za Interahamwe hapa.
 
Nitampiga mawe na kumzomea kwenye polling ballots hapo OCT 31
 
Nakubaliana na wewe tu kwa sababu unaujua ukweli jinsi ulivo ila nakupinga kwa kuendelea kusimamia mtazamo huo wakati ukijua kabisa una wajibu wa kuleta mabadiliko katika fikra za watanzani wanaoendelea kuaimini kuwa tanzania bila ccm haiwezekani. Ni nani ambae aliyewahi kuwaza kwamba dola ya roma ingeporomoka enzi za utawala wake? Ni wachache tu waliowaza hivyo ila katika uchache wao waliyafanyia kazi mawazo yao hadi kuidondsha dola kubwa ya roma. Suluhisho si kuendelea kusifia udhalimu huo bali kuchukua hatua madhubuti kubadili mtazamo wa watu, na hii haihitaji umwagaji damu. Amini nakwambia hata ndani ya usalama wa taifa, polisi, jeshi, tume ya uchaguzi na hata serikalini wapo wasiomkubali kikwete hata kidgo. Chukua hatua.

wakati umefika mwaka huu haziibiwi kura mim nitakuwa tayari kwa lolote
 
Je ugumu wa maisha yao umeanza wakati wa kikwete? na kama siyo wakati wa kikwete walifanya nini mwaka 2005? Wambie hao wenye fikra za kuzomea na kupiga mawe kuwa wakitaka mageuzi wajitokeze kupiga kura. Vile vile hakuna rais atakaye wapelekea pesa majumbani au mifukoni kwao bila kufanya kazi. Tamaa ya pesa za haraka haraka ndiyo iliyowafanya hao jamaa wa mbeya kuishia kuchuna watu ngozi na kupigana nondo hovyo.

Ni vigumu kuwazuia watu kuzomea, hali ni ngumu ya maisha, Mbeya walishindwa kujizuia si kuzomea tu, wakatupa mawe. Mimi natoa ushauri wa upendo, ili kuzuia hali hiyo kutokea ni bora raia wema wa nchi hii wasihudhurie mikutano ya CCM, ili kudumisha amani na utulivu, vinginevyo watazomea tu.
 
I dont think kama atapigwa mawe badala yake atapokelewa kwa shangwe as usual kwani hakuna sababu ya msingi ya mtanzania wa kawaida kumpiga mawe especially pale ambapo amejitahidi kuwapa matumaini watanzania... japo kwa mtu mmoja mmoja unaweza usione maisha bora aliyoyaahidi coz maisha yanapanda kila kukicha na hata akijitahidi kuwapa nafuu bado hali ya soko huria itawafanya wajanja wachache wawaumize watanzania wengi.
........KUZOMEWA???? well,hiyo nayo itakuwa ngumu kwa mtazamo wangu coz he didnt do that bad..so kama utaniuliza if atazomewa au kupigwa mawe mi nadhani watanzania wenye busara ya kupembua mambo hawatamzomea au kumpiga mawe..ikitokea hivyo basi ujue ni watu wachache wenye kuongozwa na itikadi za kisiasa watafanya hivyo kwa manufaa yao binafsi na vyama vyao na si kwa manufaa ya wanajamii wenzao kwa ajili ya kampeni tu.
ni hayo tu.
 
Assume ....,

Just assume ... mawe yamerushwa na mwitikio ulikuwa ni mkubwa!!

So?

That means what?

Kikweti is a good person ... He doesnt deserve those stones!

But what suprise me is why does he "GIVE IN" and yield to the "TYRANTS" who are controling him and the country down the bottomless pit?

Mr President dont you see that can be a bad fate to you?

Dont you think this can .... drive anybody to re think .... of throwing those stones ....!!
 
Ni vigumu kuwazuia watu kuzomea, hali ni ngumu ya maisha, Mbeya walishindwa kujizuia si kuzomea tu, wakatupa mawe. Mimi natoa ushauri wa upendo, ili kuzuia hali hiyo kutokea ni bora raia wema wa nchi hii wasihudhurie mikutano ya CCM, ili kudumisha amani na utulivu, vinginevyo watazomea tu.

WATU wamechoka na maisha DR Dr Kikwete atapata wakati mgumu katika kampini zake
 
Back
Top Bottom