Watanganyika hamuwezi kuikataa CCM katika masanduku ya kura ,hilo kamwe halitasaidia kitu ,mbinu za kuishinda CCM ni mbinu zilezile zilizotumika Pemba ,mbinu ambazo ziliwafanya usa;lama wa Taifa wasipate usingizi mbinu ambazo ziliwafanya FFU wakimbie na masanduku ya kura mchana kweupe,mbinu ambazo zilivifanya vikosi vya SMZ na Polisi wa Muungano kufanya unyama usiosahaulika ,mbinu ambazo zimeilazimisha Serikali ya CCM Zanzibar kuamua na kukubali serikali ya umoja wa Kitaifa ,ni baada ya October kwisha kwa Uchaguzi mkuu ndipo hapo CUF itakapoingia kwenye serikali hio ,mawili ama awe ndio mshindi na CCM kuingia au awe ameshindwa na hivyo pia atakuwemo kwenye serikali tena kwa nafasi nyeti.
WaTanganyika walio wengi bado wanawaogopa polisi ufikapo uchaguzi hawawezi kuwaekea ngumu na kuhakikisha asiehusika hapigi kura ,na maboxi ya kura yanaisabiwa na kila mmoja anaona ,zaidi ni hawa mawakala wa vyama ambao roho zao bado hazijatosheka na kuweza kuibeba dhamana waliopewa kwa lolote litakalo kuwa ,akiekea hela ndogo kama milioni moja tu anawacha mawakala na watume wafanye na kupanga watakavyo. Hilo sio jambo dogo.
Jengine ni kuwa WaTanganyika hawawezi kuungana na kupinga matokeo kwa pamoja na kujumuisha wananchi ,mara utasikia akina Chadema hawaungi mkono wala mguu na si ajabu wakatoa pongezi ,kusema kweli hamuna musimamo ni mahodari wa kusema na kulipuwa mabomu pale bungeni lakini ukweli unapodhihiri huwa mnajitenga.
Mkuu nakubaliana na wewe watanganyika ni watu hewala. wanaibiwa kura na wanajua kabisa kuwa wameibiwa, kinachofanyika ni FFU wanawapiga mabomu na virungu wanakimbilia ndani, wachache wanakamatwa na baadae wanasamehewa wanafurahia kwelikweli. Vyama vingi vya siasa ni succus ya CCM wewe ukigoma wao unasikia sisi tunakubali. Zanzibar vyama imara ni CCM na CUF hapo ndipo unapoona kuwa mafahali wawili lazima pachimbike. Wanasiasa wetu kinawaua njaa akioneshwa bulungutu tu mate nje anasahau kama yeye ni mpinzani.
1.Jeshi la Polisi ni lake
2.Uhasama wa taifa ooooh am sore namaanisha Usalama wa Taifa wapo chini yake.
3.Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni yake
4.Zekomedi (Augustine Mrema et al) ni wakwake
5.Waongo,wanafiki,wazushi, wambea na wababaishaji(Muhingo Rweyemamu aliyezusha eti Dakta Slaa katumwa na Mzee Ratzinger) nae anaripoti kwake
6.Yeye ni kiongozi wa Chama cha watu waliofuzu digrii za juu zaidi za WIZI WA KURA
Kwahiyo hata akipigwa mawe au akizomewa haisaidii kitu
Mkuu upo sahihi kila siku mwizi anapokuwa anaiba na watu wanamuangalia tu anaona kuwa haibi bali anachukue kilicho haki yake. Ila akipata mkong'oto huwa anakuwa makini sana kuhakikisha ama haonekani kama kaiba au anaacha wizi kwa bara hili bado ni ndoto