Kikwete kwanini hataki kujaza nafasi hizi? hakuna wanaofaa?

msimlaumu JK nadhani tatizo mnalijua analo nani na liko wapi

kwa nini hatutaki kuambiana ukweli?
 
Inasemekana TEUZI nyingi alizifanya EL alipokuwa WM. JK atafanya teuzi zake mwenyewe baada ya uchaguzi wa mwaka huu.
 
Nyerere hata baada ya robo karne tangu aondoke madarakani? Hivi woote tulifanya kazi na Mwalimu?
Ndo hapo sasa. Sioni kama hili la Nyerere lina ukweli wowote. Kwangu naona kama hatujapata mtu mwenye uwezo wa kufanya zaidi ya yale aliyofanya Nyerere ndio maana tunamlaumu. Kama ujamaa waliweza kuugaragaza, haya mambo mengine wanashindwa nini? Nyerere ameenda kaburini hawaelewi kwanini wamelitema Azimio la arusha! Nafikiri kama tunataka kubadilika we have to take ownership of our destine.
 

WildCard, bora hata huyo Mama Albino ambaye amesahau wajibu wake wa kuwatetea Malbino wenzake mpaka wanachinjwa kama mbuzi wa kafara. Mpaka Seneta wa Kimerikani (soma gazeti la The Citizen ya tarehe 3 February 2010) amemuomba Rais Obama amuwekee mbinyo Kikwete ili amalize mauaji ya Albino hapa Tanganyika. Je Askofu Getrude Lwakatare wa Mikocheni assemblies of God anafanya nini kule Bungeni? Kuna ibada ya uponyaji anaendesha huko?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…