Kwa maswali ya papo kwa papo kwa rais, naona tunadanganyana, kwa sababu hakuna mtu mwenye uwezo huo wa kukariri kila kitu asubiri tu kuulizwa papo kwa papo kisha ajibu. Tusishangae kusikia majibu mengi yakifanana na "nitafuatilia", "nimekusikia", "sina taarifa", "nasubiri taarifa kutoka kwa wasaidizi" nk. Au aanze kutoa majibu tata kama yale ya Mh Pinda ya kusema "Zanzibar si nchi", au kushabikia uchukuaji wa sheria mkononi (wauaji wa albino).
Kwa nini asijipe nafasi ya kufanyia utafiti maswali hayo, aje na majibu kamilifu kabisa, pengine asubiri tu maswali ya nyongeza ya kutaka ufafanuzi. Hayo ya nyongeza au ya ufafanuzi ndio yawe 'live', na wasaidizi wake wawepo kutoa details, yeye afanye tu kumalizia conclusions na uamuzi, yaani kuyatilia nguvu ya utekelezaji.