Kikwete 'live' TBC1 Sept 9, 2009

Kikwete 'live' TBC1 Sept 9, 2009

Status
Not open for further replies.
Kwa maswali ya papo kwa papo kwa rais, naona tunadanganyana, kwa sababu hakuna mtu mwenye uwezo huo wa kukariri kila kitu asubiri tu kuulizwa papo kwa papo kisha ajibu. Tusishangae kusikia majibu mengi yakifanana na "nitafuatilia", "nimekusikia", "sina taarifa", "nasubiri taarifa kutoka kwa wasaidizi" nk. Au aanze kutoa majibu tata kama yale ya Mh Pinda ya kusema "Zanzibar si nchi", au kushabikia uchukuaji wa sheria mkononi (wauaji wa albino).

Kwa nini asijipe nafasi ya kufanyia utafiti maswali hayo, aje na majibu kamilifu kabisa, pengine asubiri tu maswali ya nyongeza ya kutaka ufafanuzi. Hayo ya nyongeza au ya ufafanuzi ndio yawe 'live', na wasaidizi wake wawepo kutoa details, yeye afanye tu kumalizia conclusions na uamuzi, yaani kuyatilia nguvu ya utekelezaji.
 
Good move mheshimiwa Rais! Yahoo address??, wamechemsha, ila safi sana kwa ujumla
 
Huko ndio kufulia kisiasa. 2005 alituahidi maisha bora kwa kila mtanzania. hayo maisha bora yako wapi? Tumechoka na siasa, Hatuli wala hatuinywi siasa na wala hatulali wala kuishi kwa siasa. Tuhahitaji hali nzuri za maisha , maendeleo na si siasa na kutafuta cheap popularity. Atuambie maisha Bora aliyohahidi amepora nani? kama ni siasa poa si kwa watanzania wa sasa
 
Mi nadhani tumpe (tuwape) rais na wasaidizi wake "benefit of a doubt" tuone watatuletea nini leo. Tusianze kuwa pre-empt! Huo muda ni mdogo sana na hataweza kujibu hayo maswali yote, lakini tuone watasawazisha vipi, na hakika kesho tutaweza kujadili zaidi.
 
Mi wala sina la kuchangia zaidi ya kufurahi kwa kuwa leo ntapata burudani mpya. Si mnajua original comedy wamefulia, futuhi wanajikongoja? Ngoja nione hili kundi jipya kama lina jambo jipya. Nashauri hili kundi liitwe ZE IKULU COMEDY. Salva ndo Seki wao..... JK atakuwa mkandamizaji wao sijui nani atakuwa Joti? hahahahahaha! tehetehetehe!!
 
Walitakiwa wafikirie kwanza kabla ya kuanzisha mpango huu,kwasababu wananchi wengi wana hasira na nchi yao,kwahiyo na hakika maswali mengi yatakuwa ya kumdiscredt mheshimiwa kutokana na utendaji wa serikali yake,na hii inaweza msababishia stress na hasira ambazo amezitengeneza mwenyewe,ukizingatia kuwa huyu mheshimiwa hana system ya kujibu vyema since day one!!
 
Huko ndio kufulia kisiasa. 2005 alituahidi maisha bora kwa kila mtanzania. hayo maisha bora yako wapi? Tumechoka na siasa, Hatuli wala hatuinywi siasa na wala hatulali wala kuishi kwa siasa. Tuhahitaji hali nzuri za maisha , maendeleo na si siasa na kutafuta cheap popularity. Atuambie maisha Bora aliyohahidi amepora nani? kama ni siasa poa si kwa watanzania wa sasa

Nadhani swali la msingi atupe kwanza jibu, anayaelewaje maisha bora? Unaweza kukuta tuongelea vitu tofauti? Labda watu (kwa miaka hii 4) wamekuwa wakitegemea kitu tofauti na alichoandaa yeye, na inawezekana keshatoa hayo maisha bora (kwa mtazamo na uelewa wake)!
 
Mimi naona ingefaa apewe maswali ya wananchi kupitia njia alizotaja in advance kisha maswali hayo ayafanyie utafiti halafu atafute muda wa kutoa majibu yenye uhakika! Hayo maswali ya papo kwa hapo amwachie Waziri Mkuu Pinda akiwa Bungeni. Otherwise anaweza akajishushia hadhi kwa utaratibu huu kwa kuwa kunaweza kuwa na maswali ambayo ni embarassing!

Hilo linaweza kujitokeza na nadhani baada ya maswali 2-3 hivi simu zitaondoka hewani!
 
Mimi naona ingefaa apewe maswali ya wananchi kupitia njia alizotaja in advance kisha maswali hayo ayafanyie utafiti halafu atafute muda wa kutoa majibu yenye uhakika! Hayo maswali ya papo kwa hapo amwachie Waziri Mkuu Pinda akiwa Bungeni. Otherwise anaweza akajishushia hadhi kwa utaratibu huu kwa kuwa kunaweza kuwa na maswali ambayo ni embarassing!

na mimi nacho amini maswali mengine hata jibu lakini atakukatisha tamaa, kama kusema mwacheni mkapa apumzike, sijui kwanini Tanzania ni maskini na majibu ya kufanana kama hayo.
 
Wadau...

Ni Maswali yapi ungependa kumuuliza Rais?

Ameshakuwa madarakani kwa miaka 4 kati ya 5 aliyotuomba (80% ya muda aliopewa). Tunategemea awe ametekeleza angalao 80% ya ahadi au malengo au ilani iliyomweka hapo. Swali: Je ni kweli ametekeleza 80%? Katika masuala gani? Kama bado, kwa nini?

Natumaini pia atatoa nafasi ya kuya-challenge majibu atakayotoa, ili akijibu kwa namna isiyoridhisha tuibuke kama Zito tupige simu tuseme "Mheshimiwa umetoa majibu ya hovyohovyo!"
 
+255-22-2772448 direct call
+255-22-2772452
+255-22-2772454 pia 0714-591589 (sms) kuna voda na celtel but sijazipata.
swalikwarais@yahoo.com-tuma ujumbe kuanzia leo

Jamani huu ufisadi utaisha lini?nani anayelipia au kufaidika na mapato yatakayopatikana kwa watakao uliza maswali kwa kupiga simu?ni serikali au mitandao husika( voda,tigo,au zain au TTCL? au JK kaingia ubia na haya makampuni kutafuta hela za uchaguzi mwakani?

Ukweli ni kwamba hana huo uwezo wa kujibu papo kwa papo!!

hizi namba ni toll free au?

Jamani jamani mi nimeishiwa nguvu na sitamani hata kuona?auuuu
 
Si lazima kama huna cha kuchangia ukatoa mawazo kwani huenda ikawa pumba kuliko uliyemkusudia
 
Rais wa nchi hii (kwa maana ya anayeongoza) ni nani hasa?

Hii nimeipenda zaidi, thanks DC. Kwa kweli kabisa rais kwa maana ya mtendaji (Executive President) kama katiba yetu inavyosema, mtu kama Kibaki anaweza kumtimua "Mwema" wao kazi, I doubt kama sisi tunaye ninahitaji msaada kwenye hili. Mimi nadhani angefanya kazi kwanza ndio atupe nafasi tumuulize maswali. Kazi aliyoahidi kufanya hajaifanya mwaka wa 4 sasa tutapata wapi cha kumuuliza?
 
Mimi naona ingefaa apewe maswali ya wananchi kupitia njia alizotaja in advance kisha maswali hayo ayafanyie utafiti halafu atafute muda wa kutoa majibu yenye uhakika! Hayo maswali ya papo kwa hapo amwachie Waziri Mkuu Pinda akiwa Bungeni. Otherwise anaweza akajishushia hadhi kwa utaratibu huu kwa kuwa kunaweza kuwa na maswali ambayo ni embarassing!

Buchanan, Hakuna sababu yoyote ile ya kupewa maswali in advance. Mambo yanayokera watanzania yanajulikana sitegemei kama kuta kuwa na swali ambali Rais JK atakuwa hajawahi kulisikia. Kama kweli hapa rais ameamua kuongea live na wananchi tunatahadharisha tusije kukakosa line kwa sababu ya JAM kwenye mawasiliano...
 
JK kama anataka discussion aanzishe thread humu JF!
 
Wana JF tusisahau kuuliza maswali maana tuna upeo mkubwa wa mambo!!! Watuhakikishie tu usalama wa maisha na visimu namba vyetu ambavyo tumeregister!!!

Unaweza kukuta tiyari wamesha andaa watu wa kuuliza maswali!
 
Jamani huu ufisadi utaisha lini?nani anayelipia au kufaidika na mapato yatakayopatikana kwa watakao uliza maswali kwa kupiga simu?ni serikali au mitandao husika( voda,tigo,au zain au TTCL? au JK kaingia ubia na haya makampuni kutafuta hela za uchaguzi mwakani?

Ukweli ni kwamba hana huo uwezo wa kujibu papo kwa papo!!

hizi namba ni toll free au?

Jamani jamani mi nimeishiwa nguvu na sitamani hata kuona?auuuu

Ni kweli Chaku umeongea, alitakiwa atumie namba za toll free. Vinginevyo itakuwa ni ubaguzi wa kimapato, wanyonge hawataweza kuuliza chochote. Kumbuka watanzania wengi wanatumia simu za mkononi ambazo ukipiga kwa landline ni ghali sana. Hata hizo tigo, voda nk ni ghali sana kupiga na kuuliza swali redioni. Unaweza kupiga ukapangwa kwenye foleni, wakati huohuo unaishiwa credit. Na watangazaji hawaoni aibu kusema 'msikilizaji wetu naona ameishiwa kiwese'. Watangazaji wakati mwingine wanadhihaki "msikilizaji kabla hujapiga simu hakikisha simu yako ina credit ya kutosha!".
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom