Kikwete Mbeya: Mgongano na wananchi na mwitikio wa serikali

Kikwete Mbeya: Mgongano na wananchi na mwitikio wa serikali

Ana mwaliko wa kutembelea Brazil. Halafu atapitia tena Marekani.
Habari ndiyo hiyooo!
rais atakuwa arusha kesho kumpokea mkulu wa botswana ambaye atawasiri mapema ya kesho
 

....kwani ratiba ya rais si inapangwa miezi kabla???..afteral safari ya dar mbeya kwa gulfstream haifiki masaa mawili...inakuwaje mikutano ya tangu asubuhi ifutwe??

Hawana ratiba wale. Rais angekuwa ana ratiba wasingesema wameshindwa kusimama uwanjani kwa sababu jua lilizama. Unapoandika itinerary ya Rais unatakiwa kujua mawio na machweo ya Jua ni saa ngapi.

Hata uki google sekunde tano utajua leo Mbea Jua limezama saa kumi na mbili na dakika 41 jioni na kesho litachomoza saa kumi na mbili na dakika 22 adhuhuri. Sasa Ikulu nzima imeshindwa ku google mpaka wakapigwa mawe??????

AccuWeather.com - Mbeya, TANZANIA - Weather Forecast - Local Weather Forecasts
 
Hii kuikimbia haijaa kaa sawa kwa mujibu wa ratiba si ilikuwa leo aondoke tu leo? sasa hii sensationalization kuwa jk "kuikimbia" ndio ushabiki mwenyewe huu.


Duh! Jamaa anasema kweli kwamba katika ratiba ya Kikwete ilikuwa awahutubie wananchi wa Mbeya na hata uwanja ambao alikuwa ahutubie ulikuwa unafanyiwa matengenezo na barabara zinazoenda katika uwanja huo pia zilikuwa zinafanyiwa matengenezo, wewe mjuaji unaona ni sensationalization!!!! Watanzania tuache ushabiki ambao hautusaidii kama wananchi Watanzania, nchi inayumba sasa kila kona na jamaa anaonekana kabisa hana uwezo wa kutatua lolote.

Alipoingia madarakani katika safari zake za nje alikuwa anakutana na makuindi ya Watanzania katika nchi zote alizotembelea, baadaye baada ya kuanza kuwekwa kiti moto akawa anachagua wachache tu wale ambao wameweka mbele umuhimu wa wao kupiga picha na JK badala ya kumuuliza mambo na matukio mbali mbali yanayoendelea nchini kwetu. Sasa naona mtindo huo wa kukutana na watu wachache anaanza kuutumia ndani ya Tanzania. Huku ni kuwakimbia Wananchi ambao wanausongo na mambo mbali mbali ndani ya nchi yetu. Kuwa kiongozi wa nchi siyo lelemama, kama JK anaona mambo yamemzidi kimo basi aachie ngazi kabla hali haijawa mbaya zaidi.
 
Duh! All over a sudden mambo ishakuwa hivi?

Yani Mh Rais ishakuwa mshike mshike, anaye anaye...

Nchi ni kweli iko kwenye hati hati na sasa naona ataharakisha ujenzi wa ile ikulu yake mpya.

Kuna wale wanaosema kuwa kuna washauri wake wanaotaka nguvu ya dola itumike zaidi.

Tanzania ni nchi yako Mh Rais unapowakimbia wananchi na wao wakimbilie wapi?

Wakukimbize?

Je walikuchaguwa kwa kishindo ili wakukimbilie,uwakimbie ama wakukimbize?

Noma.
 
Fidel
Kwa utaratibu huu 2010 magereza hayatatosha. Watafute chanzo grrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
 
Fidel
Kwa utaratibu huu 2010 magereza hayatatosha. Watafute chanzo grrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr

Sasa itakuwa vipi Rais awakimbie wananchi halafu wakichukia wakamatwe?
Sasa nani mwenye kujenga uadui?
Tunakoelekea si kuzuri kabisa kwasababu maisha viongozi wetu wanayoishi si rahisi kuwasikiliza wananchi...They are living large and the sense of money and power wanajiona kama miungu watu

Wananchi wagome nchi nzima halafu tuone kama hao viongozi na polisi watakula wapi.

Hivi utawanyanyasa vipi watu wanaokulipa kwa jasho la kodi zao?

Hii system si ile ile ya mkoloni na ndio tuliipiga vita kuwa watawala wanawanyonya wananchi,kuwanyanyasa na kuwakandamiza?


Ina maana sasa ukishapata madaraka unakuwa mkoloni?

Wasitake mapinduzi hawa.
 
Mbeya wana Rais wao.Nashangaa kwanini Jk alikuwa hajua kipindi chote hiki!
This is not true kwenye jukwaa la siasa. Hii haina tofauti na wale wanasiasa wanaodanganya kupata kura. Bro acha uchochezi weka vitu vya maana sio kama hiyo kauli. Election gani ilifanyika kuchagua raisi wa mbeya? watake radhi waTZ na wananchi wa Mbeya kuwaondolea haki yao waliyoipata ktk uchaguzi mkuu kwa kumuweka JK kama raisi wao na wana haki ya kumuhoji japo anawakimbia.
 
Nikiwa mwanadamu na mtanzania mwenzangu naomba niseme hivi!

Maskini Jakaya Mrisho Kikwete, nchi hii ya kishindo imekosa nini? Ee Baba yetu ulie Mbinguni mpe ujasiri Kikwete wa kuwa na moyo wa kuchukua hatua na kutupeleka kwenye nchi ya ahadi.

Asante
 
Haya ndio matokeo ya kuwa na washauri kama.....................January Makamba
 
Haya ndio matokeo ya kuwa na washauri kama.....................January Makamba

exactly exacatly!!! kama baba yake anachemsha kiasi hicho je huyu JANUARY KWELI SI NDIYE NA JINGA BOMUUUUUUUU! LA KUTUPWA!

SIJUI NAYE KASOMEA MAREKANI! NA INAONEKANA VIJANA WENGI WALIOMZUNGKUKA JK NI WALE WALIOSOMEA MAREKANI WANAZALISHA ZIRA ZA MAREKANI ZISIZO NA KICHWA WALA MIGUU, NI AIBU KWA KUMPELEKA RAIS WA NCHI MAREKANI JKWA FREQUENCE KUBWA KIASI HICHO.
 
mkuu wa wilaya ya mbeya, ambaye aliwatangazia wanachi wote wa jiji la mbeya kuhudhuria kwa wingi pale mwanjelwa wakati rais anakabidhi cheli ya 13bn kujenga soko mpya sijui atawaambia nini wananchi, kwa kuwa hata jukwaa lilikuwa tayari limejengwa na liko pale hadi saa hizi. ukweli ni kuwa wananchi wengi wa mbeya wanadhani amewakimbia. na hata alipokuwa anaondoka jana jioni, hakupata watu wa kawaida kuagana naye airport zaidi ya misafara ya magari ya serikali na viongozi wenzake.

bila shaka kukimbia kwake kuna jambo, ameogopa kuzomewa? kupigwa mawe? kupongezwa kwa kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa? hilo wanalijua zaidi wana usalama wake waliomshauri afute mikutano ya wananchi na kwenda kujifungia naye kwenye ukumbi wa mkapa wenye uwezo wa kuchukua si zaidi ya watu 300! tena kwa masaa 3.

swala la kukosa nafasi ebu tuliangalie tena kwa siku yake ya mwisho jana

asubui kama saa tatu anaondoka ikulu mbeya kwenda eneo la songwe kudungua kiwanda kidogo cha kutotolea vifaranga kinachomilikiwa na mtu binafsi, mr and mrs johansens. inasemwa kuwa yeye na mrs johansens walikuwa pamoja oljoro jkt miaka hiyo, huyu mama ameolewa na raia wa norway ndo wako mbeya (kufungua kiwanda cha kutotolea vifaranga na kushindwa kuhutubia wananchi wa mwanjelwa aliowahidi yeye mwenyewe siku walipozuia msafara wake wapi na wapi?

toka songwe kwa bwana johansens anaenda kujifungia ukumbi wa mkapa, barabara zote zinazoingia na kutoka eneo la sokomatola ulipo ukumbi huo zinafungwa, anamaliza mkutano wake huo saa tisa kisha anakimbilia airport kuwahi dsm!
 
Hii kuikimbia haijaa kaa sawa kwa mujibu wa ratiba si ilikuwa leo aondoke tu leo? sasa hii sensationalization kuwa jk "kuikimbia" ndio ushabiki mwenyewe huu.


sawa hajakimbia, bali kalala mbeya, hii sasa imekaa sawa?
 
Hii kuikimbia haijaa kaa sawa kwa mujibu wa ratiba si ilikuwa leo aondoke tu leo? sasa hii sensationalization kuwa jk "kuikimbia" ndio ushabiki mwenyewe huu.

Wewe ndio mshabiki unayeona ratiba yake ya kuondoka tu. Tuambie yale Majukwaa ya muda yaliyojengwa pale Mwanjelwa kwa fedha za walalahoi nani atawalipa? UFISADI mwingine! Tuambie vumbi lililotimuliwa pale Sokoine na magreda eti kumsafishia njia Mkuu na hatimaye KAINGIA MITINI nani atalipa? Kipindi hiki pale Mbeya si cha kutifua barabara kabisa! Soma magazeti ya leo yeye mwenyewe KAKIRI kuwa Mbeya si SHWARI!
 
kiongozi jasiri ..na anayeamini ugumu wa maisha hautokani na UFISADI...huwa haogopi kukutana na wananchi......ikiwa rohoni ugumu wa maisha unamuumiza na anatumia mbinu zote kukabliliana nao...na hashindwi kwa ajili ya kuelemewa na ufisadi....

mwalimu nyerere hakuona haya wala aibu kukutana na wananchi wakati wa njaa ,1974....au hata kile kipindi cha ugumu wa maisha cha miaka ya 80 - 84.....kamwe alipokuja mikoani hakusita kuitisha mikutano ya hadhara na kuwaambia wananchi hali halisi...

rais kikwete anawahitaji wananchi wamliwaze wakati huu kuliko wakati wowote ule....kama ulivyo utamaduni wetu wa kumpokea rais mikoani kwa ngoma,mikutano mikubwa ya hadhara,maandamano etc etc

tatizo linakuja pale anapokosa maelezo ya kina ya ugumu wa maisha ..kwa kuona haya kwani rohoni anajuwa ...mafisadi waliomuweka madarakani ndio chanzo cha kutetereka kwa utawala wake..........kama isingekuwa hivyo angekuwa na ujasiri wa kukutana na wananchi wake ....ili pamoja na yeye kuwaeleza ..nao wampe moyo...

ukiwa kamanda hakuna jambo jema na zuri kama kujua unao wapiganaji nyuma yako.........sasa kamanda tulie naye anashindwa kututia morali .....
 
This is not true kwenye jukwaa la siasa. Hii haina tofauti na wale wanasiasa wanaodanganya kupata kura. Bro acha uchochezi weka vitu vya maana sio kama hiyo kauli. Election gani ilifanyika kuchagua raisi wa mbeya? watake radhi waTZ na wananchi wa Mbeya kuwaondolea haki yao waliyoipata ktk uchaguzi mkuu kwa kumuweka JK kama raisi wao na wana haki ya kumuhoji japo anawakimbia.

Kwani kuna tatizo gani Mbeya wakiwa na 'rais' wao? Mbona huhoji Yanga, TFF, Chama cha Walimu kuwa na Marais wao?
 
Bila kuathiri ushabiki unaoendelea hapa!

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania... Mh. J.M. Kikwete alikuwepo Dar es Salaam kupokea maandamano ya albino kupinga kuuawa kwao ovyo!!!!

Ni matumaini yangu kuwa Ma-alibino walikuwa na ratiba yao na mh. Rais alikuwa na ya kwake... sasa sijui nani alistahili kufuata ya mwenzake.

Akili zangu ndugu nilizojaliwa na mola... nadhani Rais alitakiwa kufuata ya wananchi wake... especially hawa ambao wana-protest kutouwawa ovyo.
Nawasilisha!
 
sawa hajakimbia, bali kalala mbeya, hii sasa imekaa sawa?

Its true leo alikuwa amalize na kesho ndio aondoke na huko kukimbia na kufuta baadhi ya mikutano kulianza jana alipoufuta ule wa Rujewa ghafla bila taarifa sijui wali smell nini?
 
Bila kuathiri ushabiki unaoendelea hapa!

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania... Mh. J.M. Kikwete alikuwepo Dar es Salaam kupokea maandamano ya albino kupinga kuuawa ovyo!!!!

Ni matumaini yangu kuwa Ma-alibino walikuwa na ratiba yao na mh. Rais alikuwa na ya kwake... sasa sijui nani alistahili kufuata ya mwenzake.

Akili zangu ndugu nilizojaliwa na mola... nadhani Rais alitakiwa kufuata ya wananchi wake... especially hawa ambao wana-protest kutouwawa ovyo.
Nawasilisha!

Ratiba ya JK ilijulikana toka mwanzo ikiwa ni pamoja na majumuisho ya hiyo ya albino.. something somewhere must be wrong! tusubiri tuone
 
Kwani kuna tatizo gani Mbeya wakiwa na 'rais' wao? Mbona huhoji Yanga, TFF, Chama cha Walimu kuwa na Marais wao?

Wewe una akili sana ila umeongezea kusoma, infact hao ma Rais uliowasema wa Yanga, TFF na CWT wanamzidi Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwanini? Nani ambae hajui jinsi Rais wa Yanga Imani Madega alivyosimama kuinusuru timu anayoingoza na wanachama waliomchagua kuweza kufanikisha kufutiwa adhabu ya kutoshiriki mechi za kimataifa?
Nani ambae hajui kuwa Rais wa TFF kuwa ni mchapakazi muungwana na si fisadi kamawaliowahi kukabidhiwa hicho chama hapo awali?
CWT si meona joto lake?au niseme tena kilichofanywa na CWT?aaah ina maana mmeshasahau?wabongo kwa kusahau haraka!Si ndio hiki chama kilichoitisha mgomo na serikali kujibu kwa kuuzuia mgomo kwa njia ya kukivizia hiki chama cha waalimu?
Haya JK sasa, mitihani imevuja mpaka humu tumepostiwa sisi yeye wala J4 waliotoa tamko!Waalimu wanamgomo baridi na mgomo moto upo waja hakuna juhudi zozote mpaka sasa. Mafisadi nao bado kawakumbatia juu ya yote hayo anacheka cheka tu huku akijua kuna migomo ya tughe na wanafunzi wa vyuo vikuu inakuja!

JK anakazi asipo uanika aangalie asije akautwanga mbichi!
 
Bila kuathiri ushabiki unaoendelea hapa!

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania... Mh. J.M. Kikwete alikuwepo Dar es Salaam kupokea maandamano ya albino kupinga kuuawa ovyo!!!!

Ni matumaini yangu kuwa Ma-alibino walikuwa na ratiba yao na mh. Rais alikuwa na ya kwake... sasa sijui nani alistahili kufuata ya mwenzake.

Akili zangu ndugu nilizojaliwa na mola... nadhani Rais alitakiwa kufuata ya wananchi wake... especially hawa ambao wana-protest kutouwawa ovyo.
Nawasilisha!

Kama wewe hizo ndizo akili zako ulizojaliwa na Mola bora uhamie kwa shetani!Kwa hiyo sasa umeamua kupimanisha NANI zaidi kati ya WANANCHI wa Mbeya na Maalbino? Rais anapokea Maandamano leo, jana alikuwa anafanya uzinduzi wa NGO ya Mama Kweggir. Hizo ishu ya Maalbino imeanza leo? Wanauwawa yeye anakatiza mitaa ya Holywood! Eti leo kawakimbilia Dar! Ebwana eh! Au ndio staili nyingine ya 'kumuosha' MKULU? Kama ni USHABIKI, wewe NDIO shabiki Nambari one, nyuma yako yuko Makamba na John Komba.

Kumsaidia MKULU kwa sasa ni kumwambia UKWELI ulio UKWELI. BASI! Haya ya kusema alikimbilia Maalbino Dar es Salaam mara waliompiga mawe ni walevi ni UTOTO! Mnamchanganya huyo Jamaa matokeo yake anaishia kusema wale wanaosema yeye haipendi Mbeya wameshiba Ugali na Maharage! Hivi wakati anasema hivyo yeye alikuwa ameshiba nini? Au alikuwa na njaa! Na kama alikuwa ameshiba WALIOMPA shibe hiyo ni kina nani? kama sio hawa anaosema wameshiba Ugali na Maharage ambao sasa anawasimanga kwa sababu yeye 'anashinda' kwenye migahawa ya Macdonald na Kuku wa Kentucky akitafuna 'Makuku ya Kukaanga na Watoto Hawajali'

MKIAMBIWA UKWELI mnasema USHABIKI! Tunafahamu hiyo ishu ya jana ya ufunguzi wa ile Taasisi ya Maalbino ilikuwa ni ya kifamilia zaidi kuliko Kitaifa. Yule mama Kweggir ambaye ni Mwenyekiti wa ile Taasisi ni Mke wa Kaka yake Bernad Membe. Tumbo moja. Si umesikia jana kawatosa wananchi kaenda kufungua 'kamtambo ka kutotolea vifaranga' ka kuruta mwenzie kule Oljoro!Rais angeweza kumuachia kazi ile hata Mke wake halafu leo kama ilivyopangwa ndio angepokea yale maandamano!

HIVI NIKUULIZE WEWE! Ziara ya Rais JK Mkoani Mbeya IMEFANA?
 
Back
Top Bottom