Mkuu Fairplay,
Huwa ninaheshima sana na michango yako alyways hapa JF, lakini not this one, kwa sababu umenikumbusha siku nilipomliza Mkapa na maswali akiwa rais akakasirika na kuvunja mkutano na kukataa chakula, huku akimshambulia balozi kwa maneno kama yako kwamba eti kwa nini alitayarisha mkutano na wananchi huku akijua fika kuwa watu kama mimi ni wapinzani, mawazo kama haya ni pathetic na ni low IQ indeed!
I mean what RC has to do na mawazo ya wananchi? Hivi hatukuwaarifu mapema hapa kwamba kipigo cha Mtikila Tarime ni ujumbe mzito kwa viongozi wetu kuwa wasipowasikiliza wananchi kwa maneno na hoja watakula vipigo kama cha Mtikila? Sasa unasema kwamba RC alitakiwa kujua kuwa wananchi waliochoshwa na ufisadi watafanya nini rais asiyewachukulia hatua mafisadi na anayeruhusu kufungiwa kwa gazeti la wananchi Mwanahalisi atakapokuja kuwatembelea watafanya nini kweli inapaswa kuwa ni brainer au unahitaji kuwa professor kuelewa kuwa atapigwa mawe kama walivyofanya hawa wananchi? Are you serious au unatania mkuu?
Eti wakulaumiwa hapa ni RC are you kidding me? Yaaani ujumbe wa Tarime haujafika tu mpaka leo kuwa wananchi wamechoka na ujinga? Yaani tunawapa utabiri hapa kila siku na wanatuuliza kila siku tu-clarify tunachosema tunawafanyia kumbe yanaingia sikio moja na kutoka la pili? Sasa mkuu wangu unashangaa na kumlaumu RC? Yaani unasema kuwa tunamuona mwizi hapa anaiba tumuache maana ni tatizo la shetani sio Mungu?
Eti ajiuzulu RC? Kwa kosa gani? Kwa kosa la kutoingia vichwani mwa wananchi in advance na kujua kwamba watarusha mawe? I mean unasema tuwafukuze kazi polisi wote bongo kwa kutokujua mapema ni lini majambazi wataiba does that make a sense to you? Mimi sio a fan wa RC wa huko wala sikubaliani na mwendo wa kusua sua wa rais on mafisadi, I do not like it period, siwezi kumpiga mawe kwa hilo la mafisadi, lakini siwezi kuwa-prejudge wananchi wote wenye hasira kama yangu na ufisadi watafanya nini mbele ya mkuu wa nchi,
Tunashukuru sana kwamba rais hakuumizwa na hayo mawe, lakini nimesikia kuwa huenda waziri wa Miundo Mbinu alikula some of it, tunawapa pole sana, lakini ninaomba watafakari the message behind hayo mawe ni kwamba wananchi wamechoshwa na siasa za ujinga na zinazotabirikia kirahisi, yaani ukiona wananchi wamefikia mahali wanatabiri mapema kua Lowassa ataachiwa tu si rafiki wa rais na kweli anaachiwa kutanua hela za ufisadi za kodi ya wananchi, basi ujue kuna ujumbe mzito unakuja soon kutoka kwa hawa wananchi na this could be one of the ujumbes, yaani mawe!.
Na hata wakubwa wa dunia wanaelewa maana ya vita na ufisadi, ndio maana leo waliwaita wakuu wa gazeti moja kubwa nchini, balozi karibu nane leo ziliamua kutaka kujua hasa kilichotokea na kupelekea kufungwa kwa gazeti la wananchi Mwanahalisi, balozi kama za EU, UK, Canada, Sweeden, na Holland leo wamekutana na vigogo wa habari Dar kuwapa nafasi ya kuwaeleza wakubwa dunia kilichojiri na Mkuchika, na wamewaahidi kwamba katika hela wanazoji-commit katika ufadhili wao kwa serikali yetu, kwa mgawo huu bado hawajatoa 12%, kwa hiyo huenda wasiitoe iwapo hawataridhika na hii ishu,
Sasa mkuu Fairplay, kila mtu na nafasi yake hapa kwenye vita na mafisadi, anayerusha mawe anayeweza kuandika, anyeweza kuzuia ufadhili, I mean anything kumkosesha tembo usingizi! ni fair deal! kama sio politics! Mkuu ungana na wananchi kulilia utawala wa haki na sheria
Ahsante Mkuu!