mkuu wa wilaya ya mbeya, ambaye aliwatangazia wanachi wote wa jiji la mbeya kuhudhuria kwa wingi pale mwanjelwa wakati rais anakabidhi cheli ya 13bn kujenga soko mpya sijui atawaambia nini wananchi, kwa kuwa hata jukwaa lilikuwa tayari limejengwa na liko pale hadi saa hizi. ukweli ni kuwa wananchi wengi wa mbeya wanadhani amewakimbia. na hata alipokuwa anaondoka jana jioni, hakupata watu wa kawaida kuagana naye airport zaidi ya misafara ya magari ya serikali na viongozi wenzake.
bila shaka kukimbia kwake kuna jambo, ameogopa kuzomewa? kupigwa mawe? kupongezwa kwa kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa? hilo wanalijua zaidi wana usalama wake waliomshauri afute mikutano ya wananchi na kwenda kujifungia naye kwenye ukumbi wa mkapa wenye uwezo wa kuchukua si zaidi ya watu 300! tena kwa masaa 3.
swala la kukosa nafasi ebu tuliangalie tena kwa siku yake ya mwisho jana
asubui kama saa tatu anaondoka ikulu mbeya kwenda eneo la songwe kudungua kiwanda kidogo cha kutotolea vifaranga kinachomilikiwa na mtu binafsi, mr and mrs johansens. inasemwa kuwa yeye na mrs johansens walikuwa pamoja oljoro jkt miaka hiyo, huyu mama ameolewa na raia wa norway ndo wako mbeya (kufungua kiwanda cha kutotolea vifaranga na kushindwa kuhutubia wananchi wa mwanjelwa aliowahidi yeye mwenyewe siku walipozuia msafara wake wapi na wapi?
toka songwe kwa bwana johansens anaenda kujifungia ukumbi wa mkapa, barabara zote zinazoingia na kutoka eneo la sokomatola ulipo ukumbi huo zinafungwa, anamaliza mkutano wake huo saa tisa kisha anakimbilia airport kuwahi dsm!