Kikwete na madhaifu yake yote ya kibinadamu hakufikia hii stage

Kikwete na madhaifu yake yote ya kibinadamu hakufikia hii stage

mcTobby

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2018
Posts
7,894
Reaction score
22,679
Siwezi sema hakukuwa na matukio ya matumizi ya vyombo vya dola kutumika visivyo kwa maslahi ya Ccm[ kwa state party yoyo duniani hiyo ni 3.14]. Na wala siwezi sema utawala wa kikwete haukuwa na makandokando kama ilivyo serikali zingine duniani lakini HAKUFIKIA STAGE YA KUPOTEZA WATU NA WAKAPOTEA ZII. mfano kwa Kwa case ya Dr. Ulimboka atleast walimbonyeza na kumuacha hai kama "KUMUONYA". Ila baada ya hapo sasa what come next.......... Anyway hata kama kuna ukosoaji unaofanywa usio na staha kwa wanaoipinga serikali kuna 1000+ ways za ku dili nao pasipo kuwapoteza au hata kuwaua. Tunajisifu kisiwa cha Amani ila deep down mikono ya watawala na viti vyao vya enzi vinanuka DAMU MBICHI ZA WATU... Lini tutastaarabika? Je , Mnadhani Suluhisho la pekee la kudumu dhidi ya wapinzani wa kisiasa wanaokosoa mlio kwenye viti vya enzi ni KUUA?
Nyie ndio mnatunga sheria. Kwanini msiwaweke vizuizini atleast basi hata muwafunge miezi hata 5 walime mashamba huko wakitoka hapo wameshika adabu ,kama ni adabu mnataka kuwashikisha. Mtaua wangapi na nyie mtaishi hadi Lini?...
Machozi ya ndugu wa Akina SOKA,SAA8 na akina mdude unadhani hayaanguki kwenye huu Udongo tunaokanyaga? Naamini ipo siku tu yatailoanisha ardhi na nyie mtahisi Ardhi imeloana na Matope..
Madaraka ni matamu sana lakini je ni matamu kweli huku mikono yenu inanuka damu?
 
IMG-20250816-WA0003.jpg
 
Aliwaweka ndani masheikh wa uamsho bila kosa lolote. Kesi ilipigwa kalenda kwa zaidi ya miaka 8.

Huyu ndo atakuwa kamfundisha Samia kutumia mahakama kama njia ya kudeal na mahasimu wa kisiasa
 
Mkuu unaweza kunitajia mwanahakati hata mmoja kutoka Zanzibar anaeikosoa serikali?
Binafsi sijawahi kusikia au kuona mzanzibar mwenye harakati hizo.
Unataka watekwe ingali wao wapo kimya wanapambana na uchumi wao wa blue
Umewahi kuona wazanzibar wanatekwa na kufungwa kama wabara?
 
Back
Top Bottom