PreGE2025 Kikwete: Nchi ni tulivu, mambo safi chini ya Rais Samia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Sasa kama yeye anamiliki mali adhimu za nchi hii na anakula na kunywa anachokitaka anaanzaje kusema hari ni mbaya bwana yule a.k.a boys2men? Aliyeshiba hajawahi kuwa rafiki na mwenye njaa hata iweje
 
"Nakupongeza sana kwa kazi kubwa unayoendelea kufanya nchini katika maeneo mbalimbali, katika nyanja mbalimbali. Mwenye macho haambiwi tazama na mwenye masikio haambiwi sikia na kwa hii ambayo tumeona leo, kwanza kuhusu uwanja wa ndege, uwanja wa ndege wa Msalato umekuwa ni dhima ya viongozi wote waliokutangulia tangu baba wa Taifa, akaja Rais wetu wa pili Mzee Mwinyi, akaja Rais wetu wa tatu Mzee Mkapa, nikaja mie, akaja Ndugu yetu Magufuli.

Jambo hili tumekuwa wote tukilitamani lionekane, lipatikane lakini safari hatua, imekamilika kwenye kipindi chako, tunakupongeza sana. Ndoto ya Viongozi wote waliokutangulia imetimia, hongera sana Mhe. Rais. Kwakweli nami nimepita pale, nimeshangaa shangaa lakini nimefarijika sana kuona mnajenga kiwanja cha kisasa kabisa, kiwanja ambacho kitakuwa na uwezo wa kupokea na kuhudumia ndege ya abiria iliyokuwa kubwa kabisa kuliko zote duniani. Hata uwanja wa ndege wa Dar Es salaam bado haijajengwa uwezo huo kwahiyo hongera sana Mhe. Rais kwa jambo hilo kubwa kwa manufaa ya nchi yetu.

La pili ni barabara hizi za mzunguko. Kwanza inajibu jawabu la tatizo maana siku hizi hata Dodoma kuna msongamano na jawabu la msongamano ni barabara zile za juu kwa juu (interchange) lakini kujenga hizi Ring road, barabara hizi za mzunguko na unaweza ukajenga tu lakini zile zilizojengwa nzuri sana na kama alivyosema waziri wa Ujenzi zinaupendezesha Mji wa Dodoma.

Ile interchange pale Ihumwa, Mtumba, namuomba Mwenyenzi Mungu anijalie kuniweka nami nije kuiona. Kwahiyo Mhe. Rais nikupongeze tena kwa kazi kubwa nzuri unayoendelea kuifanya, nikupongeze unao vijana wazuri, wachapakazi, vijana hodari - wanaiheshimisha serikali unayoiongoza, wanatoa matumaini kwa watanzania. Sisi wazee tuliokwisha staafu utake nini tena, nchi tulivu, mambo yanakwenda vizuri na Rais hayo tunayaona chini ya Uongozi wako, Mungu akujalie."- Rais mstaafu Jakaya Kikwete leo Juni 14, 2025 Jijini Dodoma kwenye Mkutano wa hadhara wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Baba muumba wa mbingu na aridhi ikikupendeza chukua na huyu anatuletea mateso zaidi.
 
Huyu baba ni mbinafsi huyu!!

Haoni utekaji, uonevu, siasa chafu na mauaji yanayoendelea nchini?
 
OKTOBA TUNA ✔️
 
Mzee wa Msoga ana karama ya Siasa ,Alizaliwa kwa ajili hiyo 😃
 
Huyu Masaju alikua AG pale serikalini ilikua na mabishano ya Kisheria Bungeni na Lisu nilibaki nacheka
Alikuwa anapelekeshwa mpaka aibu, refa (spika Anna Makinda) anamlinda ila bado anakula za uso.
Kuna mjadala mmoja wa jioni flani hivi refa ilibidi akubali hoja za Lisu zote; yaani Makinda anailiza Mh. Lisu hapo imekaaje? Apate mwongozo.
 
Kwenye sheria sio mzuri kiukweli kama Lissu alikua anasumbua Masaju vile kwenye sheria alafu leo anakua jaji mkuu safari bado ndefu
 
huyu akifa binafsi nitanza kuitambua siku aliyokufa kama sikukuu ya kitaifa
 
Inadaiwa kwamba Kikwete ameeondolewa kwenye nafasi ya kumshauri Samia. Inadaiwa Ushauri wake haujamsaidia chochote Samia ndo maana akachukuliwa Kiziga kuziba pengo.
Screenshot_20260510_173923_YouTube.jpg

Kwamba ushauri wake umesababisha Vijana kumchukia Samia

Hali hiyo imemfanya Kikwete kujiweka mbali na kazi za Samia. Kikwete hataki kuandamana tena na mtu kama Samia.

Na Watu wa Kikwete wote waliokuwa kwenye utawala wa Samia, wanaondolewa mmoja baada ya mwingine (wanatengwa).

Inadaiwa hata Paul Kagame alipokuja Tanzania, Kikwete alifungiwa uani🤣

Pia ikumbukwe, hadi leo Kikwete hajatoa pole kwa Vifo vya Watanzania waliopumzika kwa amani 29.10.2025..
 
Inadaiwa kwamba Kikwete ameeondolewa kwenye nafasi ya kumshauri Samia. Inadaiwa Ushauri wake haujamsaidia chochote Samia ndo maana akachukuliwa Kiziga kuziba pengo.

Kwamba ushauri wake umesababisha Vijana kumchukia Samia

Hali hiyo imemfanya Kikwete kujiweka mbali na kazi za Samia. Kikwete hataki kuandamana tena na mtu kama Samia.

Na Watu wa Kikwete wote waliokuwa kwenye utawala wa Samia, wanaondolewa mmoja baada ya mwingine (wanatengwa).

Inadaiwa hata Paul Kagame alipokuja Tanzania, Kikwete alifungiwa uani[emoji1787]

Pia ikumbukwe, hadi leo Kikwete hajatoa pole kwa Vifo vya Watanzania waliopumzika kwa amani 29.10.2025..
View attachment 3586673
Source ya habari mkuu? Au ni mtizamo wako JK na Samia there inseparable kwa taarifa yako.
 
Haya ni maigizo kama maigizo ya wale wafungwa wa juzi 😊😊
 
Back
Top Bottom