Elections 2010 Kikwete on ITV, maswali na majibu toka kwake

Elections 2010 Kikwete on ITV, maswali na majibu toka kwake

halafu huyu jamaa mbona anajibu km ameshakuwa rais tayari? eti...oooh!! miaka 5 ijayo tutafanya hiki.....!!! si angesema tukipata ridhaa tena tuta..........!! mie simuelewi!!! halafu alivyo mpumbavu katoa hadi siri namna wanavyo iba kura, mara oooh....mawakala wawe waangalifu, data zikiingizwa kwenye computer wazihakikishe za JK zisiongezwe...oooh.....!! yaaani bla bla nyingi, kumbe ndo wanavyotuibia kura zetu ee!!!!
 
JK yuko live ITV... Swali la kwanza ameulizwa na mshereheshaji kuwa anaonaje hali ya nchi baada ya kuizungukia takriban majibo yote... akajibu kisanii kuwa atashinda kwa kishindo kwakua wananchi wanahamasa kubwa

swali la pili ameulizwa na susan mungi kuwa anawapigia kampeni wabunge wenye kesi mbaya mahakamani ... Jk anajibu kuwa pengine hao watuhumiwa watashinda kesi...

Swali na tatu ameuli Rainfred masako kuwa 80% ya watanzania wamejiajiri ktk kilimo je ktk miaka mitano iliyopita amewafanyia nini? JK anajibu kuwa vyama vya ushirika vimekufa, na kuwa kilimo cha kutegemea mvua haifai na kuwa amejikita kuwasaidia... serikali itabeba madeni ya vyama vya ushirika!!! inaonekana swali alipewa mapema kwani anaelezea issue za masoko ...

Acha UONGO wewe. Hayo maswali yamejibiwa kwa urefu na upana zaidi mpaka muda ulikuwa unalalamikiwa. Sasa wewe kutuandikia majibu ya sentensi moja maana yake nini? Kawadanganye wajinga wajinga wengine (wengine wamejaa humu!) teh teh teh!
 
halafu huyu jamaa mbona anajibu km ameshakuwa rais tayari? eti...oooh!! miaka 5 ijayo tutafanya hiki.....!!! si angesema tukipata ridhaa tena tuta..........!! mie simuelewi!!! halafu alivyo mpumbavu katoa hadi siri namna wanavyo iba kura, mara oooh....mawakala wawe waangalifu, data zikiingizwa kwenye computer wazihakikishe za JK zisiongezwe...oooh.....!! yaaani bla bla nyingi, kumbe ndo wanavyotuibia kura zetu ee!!!!

Acha blah blah nyingi na jikumbushe rais wako sasa hivi ni nani. Utake usitake, ujinyonge ama uamue kuishi, rais wako ni Mheshimiwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete!
 
Hivi wangwana,

kuna mtu mwenye link ya youtube ambayo imerekodi huu mdahalo wa kikwete?
 
Vipi jamani sikuweza kupata muda wa kuangalia,umeme ulikatika jana au ndo mwenye nchi hakuna kukata umeme?
 
Mkuu tusisubiri ushindi, let us work for it at this very time mkuu.
naona baada ya vita ndefu ndugu yetu mwanakijiji anajipumzisha kivulini simwoni tena na cheche za fikra hasa kwenye kipindi hiki kigumu.


wewe.... vita ninavyopigana mimi ni vya mstari wa mbele kabisa! Nijipumzishe wakati ndio tumeingia masaa 48 kabla ya ushindi? sijipendi...? Ukiangaza angaza macho kuanzia J'pili hapo Dar.....
 
jamani huyu ndie RAIS wa nchi yenu, anae jisifia kwa kuboresha maisha ya mtanzania alie maskini na anae tarajia nafuu kwa kupata maisha ya baadae kuwa mazuri...

1. rais ni msanii..
2. hana competence katika kujitetea kama rais wa nchi
3. majibu yake hayana umakini na anaonesha kutojiandaa kutetea taifa letu
4. anatoa story badala yakuelezea kinacho takiwa na watanzania

Majibu mtu anayotoa inategemea hadhira (audience) yenyewe jamani! JK anajibu kwa wepesi huo kwa vile wengi wa umma wa watanzania ukiacha asilimia ndogo kama nyinyi hapa JF wana tatizo la kuchambua na kuelewa.Rais ameshalijua hilo... tumpongeza kwa kushuka chini na kuwa sawa na wananchi wake. Mtz wa kawaida anachotaka ni vitu vyepesi na laini ameze tu bila kutafuna!
 
Jinsi alivyomalizia (kwa maoni yangu) ni kama vile amesusa afu anasema "..kamchague unayemtaka.." lakini mwisho wa siku ntakuwa kiongozi wako...,kwa hali hii napata wasiwasi wa huo 'uongozi' wake (kama akishinda) utakuwa wa namna gani;sidhani kama ataongoza kwa minajili ya kuleta maendeleo na ustawi kwa wote rather ni visasi kwenda mbele..Let wait and see
 
Naomba mnisahihishe, wakati kamera zikiwa zimemwelekea muuliza swali, Muulizwaji alikuwa anaandika maswali au anasoma? Maana nilichoona kamera ikirudi kwake kuna kitu anaweka mezani mkono wake wa kulia na kuanza kujibu swali
 
Back
Top Bottom