BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Akizungumza kwenye hafla ya Miaka 10 ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC), Rais Mstaafu amesema ni muhimu kuhakikisha kunakuwa na sera nzuri zisizobagua na kuwanyima watu uhuru wao kwasababu hiyo ni njia nyingine kuu ya kulinda usalama wa nchi.
Amefafanua kuwa usalama wa nchi unahusisha mambo mengi, na kutolea mfano majukumu ya JWTZ kulinda mipaka, Idara ya Usalama wa Taifa kufanya upelelezi na kupekua mambo yanayotokea duniani kote lakini kipengele kikubwa ni nchi kuwa sera nzuri za ndani.
Kikwete amesema "Nchi ikiwa na sera nzuri za ndani na mahusiano mazuri na nchi nyingine haitalazimika hata kununua vifaru vya jeshi kwa sababu hakutakuwa na matishio ya usalama na hivyo hakutakua na wa kupigana naye".