Rais mstaafu, Jakaya Mrisho Kikwete, amesema hana pingamizi lolote kwa mkewe, Salma Kikwete kuendelea kufanya kazi za uwakilishi bungeni
Amewataka wananchi wa Jimbo la Mchinga, lililopo mkoani Lindi, kumpigia kura ili aendeleze alipoishia katika kipindi kilichopita. Salma amelitumikia jimbo hilo kwa miaka mitano kuanzia 2020 hadi 2025
Kikwete amesema hayo Jumapili, Septemba 7, 2025, wakati wa uzinduzi wa kampeni za Chama cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Mchinga uliofanyika katika Uwanja wa Rutamba, mkoani Lindi
“Mimi sina tatizo na mke wangu Salma Kikwete. Nimevumilia miaka mitano na safari hii tena nitavumilia. Namuacha aendelee na kazi zake za ubunge ili awatumikie wananchi wa Mchinga,” amesema Rais huyo mstaafu
Amewaomba wananchi wa jimbo hilo, ikifika Oktoba 29, 2025, wampigie kura Mama Salma ili amalizie changamoto zilizobaki na kuwatumikia wananchi kwa ufanisi zaidi katika kipindi cha miaka mingine mitano ijayo
Soma pia
Chanzo: Mwananchi_official

- GE2025 - Salma Kikwete achukua barua ya utambulisho CCM, kuelekea INEC kuchukua fomu ya ubunge Mchinga
- GE2025 - Familia ya Kikwete yakosa upinzani CCM mbio za ubunge majimbo ya Mchinga na Chalinze
Chanzo: Mwananchi_official