Kikwete siyo safi! - yes I said it!

Field Marshall Es,
Mapungufu ya uongozi kwa Rais, hayahusiani ni tabia ya wizi ya viongozi wachache walioko ndani ya CCM, that is my point!
Mimi nadhani mkuu hapa kidogo umenasa..
Kiongozi mzuri asiye na mapungufu ni yule ambaye kwanza hakubali tabia za wizi wa viongozi ambao huwachagua yeye mwenyewe na sio Wananchi. Sii Wananchi waliomchagua Rostam, Lowassa, Chenge, Karamagi, Meghji, na wengineo kushika nyadhifa zile...
Kuchaguliwa Ubunge wa hawa watu haina wananchi wote wa Tanzania walikubali watu hawa wawe viongozi.. Na kama unavyojua sheria za huku majuu, mkuu kama utampatia hifadhi mwizi basi wewe mwenyewe ni mhusika kwa njia moja ama nyingine..Unaweza kuwa arrested kwa kitendo hicho tu cha kumhifadhi jambazi!.

Kwa hiyo Kikwete anaweza kutokuwa mwizi lakini hadi sasa ametufanya wengi tujiulize maswali magumu kwa sababu NI wazi anafahamu kuwepo kwa wizi na wahusika lakini bado anawawekea kifua wezi wenyewe tena kwa Kauli yake mwenyewe...
Huyu ni rais wetu alikula kiapo cha kuitumikia serikali yetu kwa kuushika msahafu wa dini yake mwenyewe, leo anakuja fanya mambo nje ya kiapo bado kweli tunaamini hahusiki..
Mimi mkuu nimechoka na nimeshindwa kuvumilia pamoja na kwamba tumeombwa hivyo tka aingie madarakani lakini kwa usawa huu mkuu sidhani!
 
Mimi nadhani mkuu hapa kidogo umenasa..
Kiongozi mzuri asiye na mapungufu ni yule ambaye kwanza hakubali tabia za wizi wa viongozi ambao huwachagua yeye mwenyewe na sio Wananchi.

Mkuu Bob,

Ninakusikia tena sana, sasa kwa mwendo wako ina maana kuwa under Mwalimu viongozi wote walikuwa safi?

Kitendo chake cha kuwabadili na kuwapa ubalozi viongozi wabovu, kina tofauti gani na hiki cha Muungwana kuwakalia kimyaa?

Yote hayo ya Mwalimu na Muungwana, mimi nayaita ni mapungufu ya uongozi wao, lakini haina maana kuwa Mwalimu naye alikuwa mwizi kama Mr. 10%Bomani, kwa sababu alimbadilisha tu na kuwa balozi na baadaye kumrudisha kuwa waziri, angalau hata Muungwana amewatema waziri mkuu na mawaziri watatu,

Bado siwezi at this time kwenda kwenye njia ya kumuita Rais wa Jamhuri ni mwizi, kwa sababu kisiasa nitakuwa nina-declare kuwa Tanzania hatuna serikali, that is too strong of a political statement if you will, mapungufu ya uongozi ya kina Mwalimu, Mwinyi na Muungwana, yasichukuliwe kama ni mapungufu ya uwizi, hapana!
 
Field MarshalEs,
Kwanza kabisa ni lazima uelewe tofauti iliyopo kati ya Mwalimu na Kikwete mbali na kwamba sijasema kuwa Nyerere alikuwa SAFI... (Sasa nasema ALIKUWA SAFI)..Kwa maana kwamba viongozi wabovu hawakupata tena nafasi ya kuongoza ndani ya nchi.
Mkuu wakati wa Nyerere Balozi alikuwa hana kazi zaidi ya kusimamisha bendera ya taifa..Tulikuwa na Siasa za magharibi na Mashariki hivyo hakuna uhusinano wowote unaoweza kujengwa kama hujachagua Upande. Hivyo kazi kubwa alikuwa nayo Waziri wa mambo ya nje kuliko huyo balozi na kulikuwa hakuna biashara kabisa...Ubalozi ilikuwa ni ADHABU zaidi ya kuwa ni cheo... Hata wale aliowaona ni hatari na wanaweza ku challenge aliwatupa kuwa mabablozi..
Sasa labda kama unazungumzia USAFI wa matendo yaani hakutumia haki kuwapeleka baadhi ya viongozi nje kuwa Mabalozi hapo nakubaliana na wewe tena basi kama Kikwete ni Muungwana hivyo ampelke mtu kama Lowassa Ubalozi wa Vietnam au North Korea, Rostam - Iran, atakuwa SAFI kichizi..
Hata hivyo mkuu sii wewe siku zote hupendi kurusha madongo kwa mtu asiyehusika ktk mjadala. Hivi Usafi wa Kikwete unapimwa kulingana na Nyerere au yeye mwenyewe kama kiongozi na mazingira aliyopo?
 
Hapo Bob, unaharibu the ishu ni kwamba waliendelea kuwa viongozi pamoja wizi wao kwa taifa kama viongozi wa sasa, nafikiri ndilo hasa wengi wetu tunamlalamikia muungwana, au?

Ukisema ubalozi haukuwa na manufaa unakosea sana maana Bomani, aliacha ameajiri ndugu zake watupu pale ubalozini, sasa huwezi kusema ubalozi haukuwa na manufaa, huku watoto wa kiongozi ambaye ni proven mwizi walikuwa wanasoma nje kwa gharama ya hela zetu walipa kodi unajua enzi zile watoto wa mabalozi walikuwa wanalipiwa na serikali!
 
Field Marshall Es,
Bomani alikuwa nazo hata kabla ya kupewa Ubalozi as a fact enzi za mwalimu utasikia uchungu ukiingia ofisi za balozi wetu yaani ilikuwa aibu tupu acha hizo nyumba walizokuwa wakikaa, maisha yao wenyewe na kadhalika - huwezi kabisa kulinganisha balozi wa wakati wa Mwalimu na leo hii..Siku hizi Ubalozi wanakata deal tu ndio maana Mkapa na JK wamepeleka watu wao zaidi ili kuvuta ma deal.. Mitikasi siku hizi ipo nje nje tofauti kabisa na siasa zile za kijamaa.

Kisha hao ndugu zake Bamani ambao wewe unadai waliajiriwa Ubalozini mkuu nakuhakikishia wewe usingechukua nafasi zao hata kidogo kwa sababu nafasi zote kubwa huchaguliwa toka wizarani ama Ikulu, Bomani hakuwa na nguvu ya kuwapa wadhifa ndugu zake zaidi ya kuwaweka wajibu simu na kuwa madereva..Labda wanakuficha tu.
Mkuu wewe mwenyewe unafahamu kuwa mzee wetu sisi Wakerewe Marehemu Lukumbuzya kupewa kwake Ubalozi Canada ndio ilikuwa mwisho wa nguvu zake na pamoja na kwamba aliichukua familia yake yote huko lakini ndio imetoka mkuu he was nobody hadi katuondoka!..
FMES, Nyerere alitumia balozi kama adhabu na hili huwezi kunambia kitu kwa sababu najua vizuri wale wote walioathirika ikiwa ni pamoja na Sarakikya!... hana kisu wala sauti tena!
Hilo la watoto wao kusoma mkuu ulitaka watoto pia waadhibiwe?...Ni afadhali kulipia gharama za elimu yao tukifahamu kwamba zinatoka mfuko wa serikali kimahesabu sio kuibiwa mikataba ili watoto wa mkulu apate elimu..huu ni wizi mkuu. Ipo tofauti kubwa sana..
 
Mkuu Bob,

Unasema maneno mengi sana kinyume na hii ishu ambayo ni ndogo sana, nayo ni kwamba hata Mwalimu aliwakumbatia viongozi wachafu, Bomani alikuwa mmoja wapo, alikuwa mchafu tena sana pamoja na kuwa na hela toka zamani,

Kuwakumbatia viongozi wachafu ninasema ni dalili za unyonge wa Rais aliyeko kwenye power, lakini haina maana kuwa huyu Rais ni mwizi au mchafu kama viongozi anaowakumbatia, ila ni moja ya mapungufu ya Rais, ndiyo hasa point yangu, na ninasema hivi bado siwezi at this point kumuita Rais wa sasa mwizi just because anawakumbatia viongozi wachafu, kwa sababu siwezi kumuita Mwalimu kuwa alikuwa mchafu kwa sababu aliwakumbatia kina bomani,

Huwezi kumuita Rais ailyeko madarakani mwizi bila ya kuwa hard evidence, au angalau dataz nzito sana, ndiyo hasa point yangu, kama ni ubalozi hakuna wakati wowote ungeweza kuwalinganisha viongozi waliobaki nyumbani na mabalozi walokuwa nje, maana hata sasa hivi ukija bongo, utakuta waloikuwa mabalozi wote wako safi tena sana, kulinganisha hata na mawaziri waliobaki nyumbani kuanzia then mpaka sasa, ingawa sio point muhimu sana hii,

Hapa ni wewe kuamini kuwa Rais wa sasa ni mwizi na mimi kutoamini bado kwa kukosa kuona ushahidi mzito, that is all mkuu!
 
Ndio maana nimesema mkuu Ubalozi ilikuwa ni ADHABU, hivyo hakuwakumbatia....Kuwakumbatia viongozi wachafu ni lazima iendane na uchafu wenyewe..
Nitakupa mfano hai wa uchafu tofauti.. Kwa mswahili, mwanamke asojua kupika anaweza kuitwa mchafu hawa ndio viongozi wa Nyerere ambao walikuwa hawajui kuongoza wizara ama mashirika..Kila siku watoto tulikuwa tukishinda njaa na hilo sote tunalikubali kwamba Nyerere aliharibu uchumi wa nchi hii kutokana na kuweka viongozi WABOVU ktk nyadhifa muhimu, huyu mkuu anaweka viongozi wezi akijua kwamba ni wezi na wanaendelea kuiba na anawapa hifadhi kwa kauli yake kuwa hawa watu ni safi!..
Uchafu wa mwalimu ni tofauti na mwanaume anayemkumbatia mwanamke Malaya akielewa umalaya wake na bado amekolea ktk ndoa.. Hapo watu hujiuliza KULIKONI?...
 
Mkuu ES, Jk tunamtegemea lakini kadri siku zinavyokwenda anazidi kufanya makosa makubwa kupita kiasi na sasa hivi tuna serikali ndani ya serikali.

Jk yeye ni safari tu kama sio Japan, basi Africa, Europe au N America. Akirudi Bongo anatunga safari ya 10 days Tanga na mikoa mingine!! Really?? Jamani kuna viongozi dunia ya leo wanatembelea mkoa, jimbo au state kwa zaidi ya wiki nzima???

Nchi imekuwa kama haina mwenyewe, na Rostam na Lowassa wanatumia upenyo kuleta mtarafuku kila kona na karibuni wataingia hata kwenye dini yaani Uislam vs Ukristo. Kisa Mkuu wa Kaya anashindwa kuelewa kuwa usipokata mzizi mapema mbuyu itakuwa kazi kuukata huko mbeleni.

Kwa hiyo in short usicompare kabisa issue ya mwalimu na JK, wakati wa Mwalimu kila mtu alijua power iko wapi na hata kama mwalimu alifanya ka upendeleo kidogo sio issue kama kukumbatia majambazi wanaoua uchumi wa nchi yetu.

sorry kwa kuandika all over the place sababu naanza kuogopa mno kitakachotokea TZ, wengine we can clearly see nashangaa Mkuu wa Kaya yeye anadhani mambo ni lelemama wakati wenzake usiku na mchana wanapanga kucripple nchi kwa kuweka Bunge rehani, Jeshi, wizara mbalimbali.
 
Wakati wa Mwalimu miaka 15 ya kwanza tulikuwa na wahasibu wangapi, madaktari wangapi, na wahandisi wangapi? Tulikuwa na watu wangapi waliosomea mambo ya ushauri wa miraji mbalimbali?
 
Jamani mada tunayoijadili ni hii - Kikwete siyo safi-yes I said it. Usipoafiki sema na utoe sababu na kama unaafiki pia sema ni kwa nini.

Ukiogelea kwenye uchafu kumbe haujui hata kuogelea, kadiri unavyotapatapa unazidi kumeza uchafu. Sasa uchafu unakaa ndani yako - utajitakasa vipi.
 

I dont think some statement zako ni sahihi. Kikwete hana mashamba wala majumba are you sure? hata magazeti husomi? mwanzoni mwa mwaka huu alipigwa picha akinusa nanasi kutoka katika shamba lake muda mfupi kabla hajaruka kwenda USA. na comment ya picha alikuwa anaahakiki kuwa nanasi limeiva kabla hajachukua kama sample kutafuta wanunuzi wa nje!!!!
 

...tatizo la muungwana ni uswahili wake tuu kuweka ushkaji na mafisadi bila kujua wanamzunguka na hata kama anajua ni soft sana kuwafanya chochote,angalia lowassa bila pressure na mambo kuwa wazi angeendelea tuu kuwa PM ingawaje mungwana nina uhakika alijua uchafu wa Lowassa ,huyu mtu simjui kiundani lakini sijui kama anatuibia chochote pale hazina kama mafia wengine wanaojulikana,huyu jamaa naturally anaonekana ana roho nzuri na hana ubaya na mtu(maoni yangu tuu) lakini hii tabia yake ndio inajenga serikali ya mafisadi na nchi inaumia.
 
Guys guys
hastle down pls, ina maana kura yangu nilimpigia swahiba wa lowasa?? anyway nimejishikia kichwa changu hapa najaribu kufikiria what best i can do 4my country....
halafu bado marafiki zangu wa TISS wanaendelea kuwalinda hawa washkaji huku wakijua wanahatarisha usalama wa taifa ktk kila nyanja tukianzia uchumi.....

Wenye Mungu na wapige magoti waiombee nchi maana wale dogs aliowasema nyerere wameshashika patamu
 
Tanzania: Taifa maskini lenye jamii iliyokosa maadili kwa kiasi kikubwa ... lakini inaoyaka Rais awe malaika... lakini Rais huyo atokee kwenye jamii hiyo hiyo iliyooza.

Kwa mazingira ya Tanzania, Afrika, Dunia kwa ujumla, kwa upande wa maadili, narudia upande wa maadili au relatively usafi. Kikwete ana alama za kutosha hata kama sio wa Kwanza Afrika, Afrika Mashariki etc.

Hiyo ni haki yake JK, hakuna anaweza mpokonya... atakuwa nayo forever.
 

Hakuna mtu anayetaka Rais Malaika! hakuna mtu anayetaka kiongozi asiye na madoa au asiyeweza kukosea.. Kama kuna mtu anawaza hivyo mtu huyo anaishi katika nchi ya kufikirika.

Lakini ni wa hatari zaidi wale ambao hawataki kuwawajijibisha viongozi wao au kutaka kiwango fulani kinachokubalika cha kuwajibika. Hawa ndio ambao wamewapa kichwa watawala kuwa tusitake kiwango bora cha uongozi na tukubaliane na uzembe, wizi, kushindwa madaraka, kutumia madaraka vibaya, rushwa n.k kwa sababu tukitaka bora, tutaonekana tunataka malaika.
 
ukijipaka mafuta na kujipulizia marashi utasifiwa sana na majirani lakini mkeo ndiye atakayejua siri yako kuwa haujaoga
 
Uchafu wa Rais wetu ulianzia kwenye MCHAKATO wa kumtafuta mgombea Urais kwa TIKETI ya CCM mwaka 1995. Wajumbe wengi wa CC ya CCM walionekana kutomtaka Kikwete kwenye nafasi hiyo isipokuwa UVCCM. Ikabidi atafute "MARAFIKI na WAFADHILI" wengine wenye nguvu kifedha na ushawishi ndani ya NEC ya CCM. Mafisadi wakagundua mvuto aliokuwa nao Kikwete kwa vijana na wananchi wa kawaida ambao ni masikini wa vipato (na fikra?). Lowassa, baada ya kushtukiwa na Mwalimu, akawa miongoni mwa watu mwanzo kabisa kumkumbatia Kikwete na kumuongezea idadi ya MAFISADI kwenye mchakato wa kuusaka Urais itakapofika 2005. Nadhani Kikwete atamalizana na MAFISADI hawa katika awamu hii ya kwanza ya utawala wake. Tumtegemee Kikwete halisi kuanzia 2010.
 


wahenga wanasema kama haikufaa rangi basi haitaweza chokaa, so kama kikwete kashindwa sasa hivi ataweza vipi baadae?
 
[/COLOR][/B]

wahenga wanasema kama haikufaa rangi basi haitaweza chokaa, so kama kikwete kashindwa sasa hivi ataweza vipi baadae?

Wewe fanya SUBIRA kidogo. Ilimradi kinga ya mafisadi ameachana nayo; mimi nauona MWANGA ndani ya Kikwete siku sio nyingi zijazo. Tukiendelea kumsakama atarudi kulekule kumalizia muda wake.
 
Wewe fanya SUBIRA kidogo. Ilimradi kinga ya mafisadi ameachana nayo; mimi nauona MWANGA ndani ya Kikwete siku sio nyingi zijazo. Tukiendelea kumsakama atarudi kulekule kumalizia muda wake.

wahenga wanasema "hata roma haikujengwa kwa siku moja"...ila waroma wakawajibu "na haikuchelewa kama mnavyofikiria".

hata kwa mkapa mlisema hivyohivyo mwisho wa siku akamaliza muda wake na hakuna lolote alilolifanya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…