Kikwete siyo safi! - yes I said it!

Wewe fanya SUBIRA kidogo. Ilimradi kinga ya mafisadi ameachana nayo; mimi nauona MWANGA ndani ya Kikwete siku sio nyingi zijazo. Tukiendelea kumsakama atarudi kulekule kumalizia muda wake.

Hiyo subira mpaka lini? ili haki mafisadi wanazidi kukamua kila kitu.. nayeye akizidi kuwaogopa na hata kuwakingia kifua kwamba waachwe waoumzike, ama kwa staili yake ya tume juu ya tume ya kuchunguza kazi ya tume...??
 
wahenga wanasema "hata roma haikujengwa kwa siku moja"...ila waroma wakawajibu "na haikuchelewa kama mnavyofikiria".

hata kwa mkapa mlisema hivyohivyo mwisho wa siku akamaliza muda wake na hakuna lolote alilolifanya

Kumlinganisha Mkapa na Kikwete nadhani sio sahihi; kwanza kama wanadamu wanatofautiana sana, pili, kama viongozi ndio kabisaaa! Watanzania tumeoza nje, ndani. Angalau uozo huu Kikwete ameuona na hatua anachukua. Tumpe support anayoihitaji sana kwa sasa.
 
mazingira hayamruhusu kikwete kuwa si fisadi.
kwa kuwaacha tu mafisadi watende wanayo yatenda inadhihirisha moja kwa moja kuwa yeye ni fisadi.
kwa kushindwa kutoa majibu kwa wananchi na kuchukua hatua mbali mbali panapotokea makashfa ya ajabu, kunadhihirisha kuwa kikwete ni fisadi.
 

support ipi?
orodha ya madawa ya kulevya tumempa.
ripoti ya richmond iko ofosini kwake
ripoti ya madini tumempa
wanaomiliki mabilioni nje ya nchi tumempa.
taarifa ya EPA na makampuni hewa halikadhalika.

sasa unataka tumpe support gani?
 
support ipi?
orodha ya madawa ya kulevya tumempa.
ripoti ya richmond iko ofosini kwake
ripoti ya madini tumempa
wanaomiliki mabilioni nje ya nchi tumempa.
taarifa ya EPA na makampuni hewa halikadhalika.

sasa unataka tumpe support gani?

Angalia sasa mambo yalivobanana na yote hakuna linalohitaji papara au uamuzi wa mtu mwingine isipokuwa yeye tu. Hatukuamka mapema kuwabana waliomtangulia hasa Mwinyi na Mkapa. JF ilichelewa kuanza na hata ilipoanza ilifahamika kwa wachache tu. Bunge lilikuwepokuwepo tu na WATUMISHI WA UMMA walikaa kimya wakiambulia makombo ya ufisadi wa viongozi wetu.
 

Kwa sababu ana shamba basi ni mwizi? Yaani wa-Tanzania wote wenye mashamba ndio kipimo cha wizi wao kwa taifa letu?

Unasema statement zangu sio sahihi, lazima ulikuwa na mana kuwa zako ni sahihi, au?
 
Kwa hiyo in short usicompare kabisa issue ya mwalimu na JK, wakati wa Mwalimu kila mtu alijua power iko wapi na hata kama mwalimu alifanya ka upendeleo kidogo sio issue kama kukumbatia majambazi wanaoua uchumi wa nchi yetu.


Ahsante sana mkuu, nimekusikia hoja nzito sana!
 
support ipi?
orodha ya madawa ya kulevya tumempa.
ripoti ya richmond iko ofosini kwake
ripoti ya madini tumempa
wanaomiliki mabilioni nje ya nchi tumempa.
taarifa ya EPA na makampuni hewa halikadhalika.

sasa unataka tumpe support gani?
Mkuu uemongea vizuri sana maana JK amejaribu kupoteza kwa kuunda tume (kwa kujidai hayajui hayo maasi), sasa tume nyingi zimeleta taarifa na amekaa kimya kwa zote. Hata hivyo tusisahau alisema mwenyewe kwamba aliletewa majina ya waleta unga wa kubwia hapa na amekaa kimya maana tunawaona wafungwa wakiwa huru na kuendelea kuagiza kufanya biashara kama yule aliyeunganisha hiyo biz na michezo yetu ya olimpiki. Mnataka kusema Kikwete ni safi kwa kukumbatia haya yote? ama anasubiri ayafanyie kazi kipindi cha pili? naombeni kama kuna mwenye data atushushie hapa.
 

Asipofuata taratibu za tume na uchunguzi wa kina tutapiga kelele kwamba hafuati KATIBA yetu kwa kukiuka misingi ya UTAWALA BORA. Mambo yanayohitaji suluhisho la kudumu hayataki haraka.
 
Asipofuata taratibu za tume na uchunguzi wa kina tutapiga kelele kwamba hafuati KATIBA yetu kwa kukiuka misingi ya UTAWALA BORA. Mambo yanayohitaji suluhisho la kudumu hayataki haraka.
Kama ndivyo mkuu unahisi tunatakiwa kusubiri hadi lini ili ufumbuzi wa kudumu upatikane? nauliza hivyo maana nafasi aliyoiacha JK inaruhusu mafisadi kuendelea kutamba kwa nguvu zao zote. Ingekuwa hata amesimamisha kwanza trend iliyopo ningemwelewa kwa kiwango fulani. Sasa mambo ni kama kawaida na nadhani mafisadi wameongeza kasi ya kula kwa kilichopo kwenye line kabla mambo hayajaharibika, waliohisi noma basi wanafanya mabadiliko ya kuharibu ushahidi ili atakapokuja kusema tumchunguze tunaambiwa ni msafi kabisa. JK haendeshi nchi, nchi inamwendesha Mkulu.
 
Asipofuata taratibu za tume na uchunguzi wa kina tutapiga kelele kwamba hafuati KATIBA yetu kwa kukiuka misingi ya UTAWALA BORA. Mambo yanayohitaji suluhisho la kudumu hayataki haraka.

Tume siyo kanuni za kikatiba bali ni mamlaka ya rais kikatiba,kuunda tume siyo kutekeleza mamlaka ya kikatiba bali ni kutengeneza nyenzo ya kutumia mamlaka yenyewe,kwa hiyo kwa maana nyingine Kikwete alitengeneza nyenzo lakini anasita kuitumia na kushindwa huko kuitumia nyenzo aliyoiumba yeye mwenyewe ndiyo ufisadi unaosemwa, kwani alitumia rasirimali ya watanzania kuiumba nyenzo hiyo!!
 

I couldn't agree more, Zero. Bado sijaona strategy nzuri ya kuwawajibisha/kuwa-stopisha the so-called mafisadi guys. Unachokisema ni kweli kabisa, "tunajifurahisha tu hapa JF."

So here is what I'm suggesting:

Wanafunzi wa vyuo vikuu, shule za sekondari, wakulima vijijini, pamoja na tasisi mbalimbali nchini wanapaswa kuwa jasiri na kuanza rasmi kutetea maslahi ya taifa letu pasipokujali personal consequences za hapo baadaye.

Kama ilivyo kwa nchi za Magharibi, tunapaswa sasa kuanzisha vikundi vidogovidogo ( grassroots movement ) vitakavyo hakikisha kuwa viongozi tuliowachangua wanawajibika na kutumika kwa ajiri ya wananchi na si vinginevyo.

Grassroots movement hizo zipange na ku-organize mambo mbalimbali yanayowabana viongozi waliowachaguliwa ili kuhakikisha kuwa maslahi ya taifa zima, na sio ya watu wachache, daima yanawekwa mbele.

Mambo kama:

1.Ku-organize mikutano mikubwa ya hadhara na kuwakemea viongozi manafiki
wanaoweka mbele maslahi yao binafsi.

2.Kutundika mabango makubwa ya Billboard yenye ujumbe wa kushinikiza.

3.Kukusanya sahihi ku-petition jambo linalowakera.

4.Kuchangisha hela za kurusha matangazo ya kampeni kwenye Tv, Radio , na magazetini dhidi ya mafisadi ( I mean majimboni kwao).

5.Ku-organize maandamano makubwa nchi nzima kupinga ufisadi.

7.Wananchi wawaandikie wabunge wao kuwaeleza kinachowakera.

8.Ku-organize " get out the vote", kwa kuwahamasisha watu kupiga kura, ikiwezekana kuwasafirisha kwenda kwenye vituo vya kura.

Kwamba, Dr. Harrison Mwakiyembe ataporudi kuomba kula Kyela, movement imuulize, "...mwaka huu unaahidi kuongeza vitanda vingapi katika hospitali ya wilaya?" Kadhalika wananchi wa Mbulu nao wamuulize Philipo Sangka Marmo, "...ni nini mikakati yako katika kutatua tatizo lililopo la upungufu wa wauguzi katika hospitali yetu ya wilaya?" Endapo kama wataahidi kutatua matatizo hayo na kutoa maelezo ya kueleweka, basi wapewe nafasi ya kurudi Dodoma; lau sivyo, wasipotoa maelezo ya kueleweka, movement itafute mbadala (alternative).

Kando na hayo, movement pia itoe kipaumbele kwenye suala la marekebisho ya katiba. Katiba ya sasa inampa Rais madaraka makubwa sana ya kiutendaji. Imefikia muda sasa kumpunguzia Rais madaraka hayo na badala yake Bunge na Mahakama ziwe na mamlaka makubwa zaidi ya kuidhibiti serikali.

Sambamba na hilo, wakati umefika pia kwa Mawaziri na Naibu Mawaziri wa Serikali kuchaguliwa kutoka nje ya Bunge kama ilivyo kwa nchi nyingi za Magharibi, mfano, Marekani. Haina maana kuwa na Bunge ambalo nusu ya wabunge ni viongozi wa serikali pia. (movement ifanye/ishinikize hili pia).

Last but not least, movement ishinikize kuwa: Lazima katiba mpya iweke bayana kwamba mawaziri wote watoke nje ya Bunge ili iwe rahisi kwao kuwajibika kwa wananchi kuliko ilivyo hivi sasa ambapo karibu nusu ya mawziri wanatoka ndani ya bunge (you know ile kitu inayosema, "waziri inabidi a-pledge loyalty kwa serikali." Si unafahamu? Sasa hao mabunge/mawziri wAnawakislishaji wananchi? Hebu tujiulize hilo. Na tukisha jiulize hivyo, then let's roll up our sleeves and get to work boys).

Hivyo ndivyo (kama wanaharakati) tunavyoweza kupunguza influence ya mafisadi nchini. Otherwise, tunajifurahisha tu.
 
Benki Kuu sasa, kuliko wakati mwingine wowote, kumetulia. Waliomo mle wanatuambia hivyo. Hatuna sababu ya kutowaamini WaTZ wenzetu hawa. Naamini na Mawizarani nako kutatulia. Tukidhani Kikwete peke yake ataiweza VITA hii kwa muda mfupi kiasi hiki, tunajidanganya.
 
Baada ya kupitia hizi posting za hapa na kuangalia ukweli ulioandikwa na kusemwa hapa nimeridhika kwamba kweli JK si msafi hata kidogo. 2010 kura yangu sahau.
 
Baada ya kupitia hizi posting za hapa na kuangalia ukweli ulioandikwa na kusemwa hapa nimeridhika kwamba kweli JK si msafi hata kidogo. 2010 kura yangu sahau.

kidatu cha kufanya sio kura yako tu, bali sasa tunatakiwa kupambana ili kupata na kura za wengine ili mapambano yaendelee na hapa ndo tutaweza kuwakimbiza hawa jamaa.
so amka sasa na uwaamshe waliolala
 
kidatu cha kufanya sio kura yako tu, bali sasa tunatakiwa kupambana ili kupata na kura za wengine ili mapambano yaendelee na hapa ndo tutaweza kuwakimbiza hawa jamaa.
so amka sasa na uwaamshe waliolala


Sawa mkuu.
 
Back to basics!!! Yes I said and I will say it again... Kikwete si safi!
 
I've a hunch -- the issue that will prove that he's not clean is the Dowans issue. Just you wait!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…