Kama hatutawatoa CCM madalakani au kupata upinzani wa nguvu au kuwawajibisha mafisadi Tanzania tusitegemee kwenda popote zaidi ya stories za kujifurahusha hapa JF. Natabiri 2010 hali itakuwa mbaya TZ karibu na ile ya 1980s lakini JK atapata 70 % ya kura na CCM watapata 80 % za wabunge!!!!
I couldn't agree more, Zero. Bado sijaona strategy nzuri ya kuwawajibisha/kuwa-stopisha the so-called mafisadi guys. Unachokisema ni kweli kabisa, "tunajifurahisha tu hapa JF."
So here is what I'm suggesting:
Wanafunzi wa vyuo vikuu, shule za sekondari, wakulima vijijini, pamoja na tasisi mbalimbali nchini wanapaswa kuwa jasiri na kuanza rasmi kutetea maslahi ya taifa letu pasipokujali personal consequences za hapo baadaye.
Kama ilivyo kwa nchi za Magharibi, tunapaswa sasa kuanzisha vikundi vidogovidogo ( grassroots movement ) vitakavyo hakikisha kuwa viongozi tuliowachangua wanawajibika na kutumika kwa ajiri ya wananchi na si vinginevyo.
Grassroots movement hizo zipange na ku-organize mambo mbalimbali yanayowabana viongozi waliowachaguliwa ili kuhakikisha kuwa maslahi ya taifa zima, na sio ya watu wachache, daima yanawekwa mbele.
Mambo kama:
1.Ku-organize mikutano mikubwa ya hadhara na kuwakemea viongozi manafiki
wanaoweka mbele maslahi yao binafsi.
2.Kutundika mabango makubwa ya Billboard yenye ujumbe wa kushinikiza.
3.Kukusanya sahihi ku-petition jambo linalowakera.
4.Kuchangisha hela za kurusha matangazo ya kampeni kwenye Tv, Radio , na magazetini dhidi ya mafisadi ( I mean majimboni kwao).
5.Ku-organize maandamano makubwa nchi nzima kupinga ufisadi.
7.Wananchi wawaandikie wabunge wao kuwaeleza kinachowakera.
8.Ku-organize " get out the vote", kwa kuwahamasisha watu kupiga kura, ikiwezekana kuwasafirisha kwenda kwenye vituo vya kura.
Kwamba, Dr. Harrison Mwakiyembe ataporudi kuomba kula Kyela, movement imuulize, "...mwaka huu unaahidi kuongeza vitanda vingapi katika hospitali ya wilaya?" Kadhalika wananchi wa Mbulu nao wamuulize Philipo Sangka Marmo, "...ni nini mikakati yako katika kutatua tatizo lililopo la upungufu wa wauguzi katika hospitali yetu ya wilaya?" Endapo kama wataahidi kutatua matatizo hayo na kutoa maelezo ya kueleweka, basi wapewe nafasi ya kurudi Dodoma; lau sivyo, wasipotoa maelezo ya kueleweka, movement itafute mbadala (alternative).
Kando na hayo, movement pia itoe kipaumbele kwenye suala la marekebisho ya katiba. Katiba ya sasa inampa Rais madaraka makubwa sana ya kiutendaji. Imefikia muda sasa kumpunguzia Rais madaraka hayo na badala yake Bunge na Mahakama ziwe na mamlaka makubwa zaidi ya kuidhibiti serikali.
Sambamba na hilo, wakati umefika pia kwa Mawaziri na Naibu Mawaziri wa Serikali kuchaguliwa kutoka nje ya Bunge kama ilivyo kwa nchi nyingi za Magharibi, mfano, Marekani. Haina maana kuwa na Bunge ambalo nusu ya wabunge ni viongozi wa serikali pia. (movement ifanye/ishinikize hili pia).
Last but not least, movement ishinikize kuwa: Lazima katiba mpya iweke bayana kwamba mawaziri wote watoke nje ya Bunge ili iwe rahisi kwao kuwajibika kwa wananchi kuliko ilivyo hivi sasa ambapo karibu nusu ya mawziri wanatoka ndani ya bunge (you know ile kitu inayosema, "waziri inabidi a-pledge loyalty kwa serikali." Si unafahamu? Sasa hao mabunge/mawziri wAnawakislishaji wananchi? Hebu tujiulize hilo. Na tukisha jiulize hivyo, then let's roll up our sleeves and get to work boys).
Hivyo ndivyo (kama wanaharakati) tunavyoweza kupunguza influence ya mafisadi nchini. Otherwise, tunajifurahisha tu.