Mbu
JF-Expert Member
- Jan 11, 2007
- 12,752
- 7,861
...Sisi wananchi Wadanganyika kama sio waafrika wote huchagua viongozi wanaofanana na hulka yetu sisi wenyewe. Hulka ambayo imetokana na Umaskini wa kufikirii na ndio maana ELIMU kwa mtu mweusi ilikuwa ni elimu ya kujua kusoma na kuandika ktk lugha yao, hatukuhitajika kufikiri toka mkoloni kwani hiyo haikuwa kazi yetu.
Nitarudia kusema kizazi hiki kinanipa tumaini kubwa sana na pengine ktk miaka 10 ijayo wadanganyika wanaweza toka ktk lindi hili la elimu ya kusoma na kuandika. Watafungua bongo zao na kuanza kufikiri bila kumtegemea mtu mweupe.. hadi hapo tutaendelea kuwa watumwa na ndio maana hakuna haja ya Kushangaa kwa nini wananchi aslimia 80 walimchagua JK ama Mkapa kuwa rais. kazi ya kufikiri ilikuwa sii yao ila ya baadhi viongozi ambao kwa uzoba wetu tuliwaona wako karibu na mzungu kwa sababu hawa watawala weusi wamesoma Ulaya ama makuzi yao yalikuwa karibu na wazungu...na huwezi kupata hesabu kubwa ya Manyapala hawa isipokuwa toka chama tawala - CCM.
Big in capitol letters,YES!!!Tatizo ni wananchi, vijijini na mijini hawana xposure na/au elimu ya kutosha juu ya serikali yao na yale yanayojiri. Wajua kama Kenya, watu wengi wapo xposed so haiwi a up hill battle kama Tanzania, tia elimu vichwani mwa watanzania, then win majority of sits bungeni na mwisho kabisa ndio kuchukua ikulu....lakini sio kukurupuka tu, next time sisiemu wataweka mtu mbovu kuliko JK hapo ndio mtasema afwadhali ya kikwete. Wananchi wa Tzania ni JOKE!!.
Mkuu wangu Invicible,
Heshima mbele, unayosema ni kweli kabisaa, lakini bado hatuja-address matatizo yetu ya character, kutokana na kutokuwa na maadili ya uongozi, ambayo yataanzia kwenye level ya sisi wananchi pia kuwa na maadili ya kijamii, otherwise sisi wananchi haya mabadiliko hayatatusaidia kitu, bali viongozi wachache, maana hata kuanzishwa kwa vyma vingi walionufaika ni kina Mreema na Mtei, sio sisi wananchi, bila wanachi kuamshwa tutaishia kama Visiwani, wananchi wanamuaminia Seif tuu, mpaka sasa amenunuliwa hawaelewi cha kufanya maana kila kitu kilikuwa Seif tu,
Kama tusipokazana kuwaamsha wananchi, hata yanayoendelea sasa yataishia kuwanufaisha wachache tu, na sisi tutaendelea kupiga kelele tu hapa!
Lakini heshima kwa maneno yako mazito mkuu!
...Naam, kama Mkapa alikuwa chaguo la Nyerere, Kikwete ni chaguo la wapiga kura wa Tanzania walompa ushindi wa Tsunami, maana 80% si kidogo!
...Viongozi wa vyama vya upinzani Tanzania wanapaswa kutumia muda wa ziada 'kuwasomesha wananchi' ubora wa sera za vyama vyao na kujionyesha kweli wameiva kiuongozi, badala ya kukurupuka wakati wa kampeni kupigania Ruzuku tu.
...CHADEMA-Bara na CUF-visiwani vinajitahidi kwa kiasi fulani kuinyima usingizi CCM, ni matarajio vyama hivi vikifanya mabadiliko kidogo kiutendaji vinaweza kuwa tishio hapo siku si nyingi, Upinzani ambao utaweza kuipa shinikizo serikali ya CCM kufanya yale yaliyo tegemeo kwa Wananchi wa Tanzania nzima.
...2010 si mbali, kama kweli kilio kimesikika, ushindi wa tsunami nao utabakia historia, la sivyo ndio kama walivyonena wakuu hapo, wananchi wataendelea kuichagua CCM hata kama CCM wataleta mgombea ambaye 'atakuja kuonekana mbovu' kuliko BM au JK, wakati huo huo 'Maisha bora kwa kila mtanzania' yanazidi kudumaa. Ni matumaini yangu CHADEMA na CUF watajifunza kwa haya yanayojiri sasa Tanzania na kuchukulia advantage loopholes zinazojitokeza, na wakati huo huo CCM nao wakijitoa kwenye 'ndoto' walizonazo kwani wananchi wa Tanzania wanaanza kuchoshwa na 'ahadi za kununuliwa viatu', baada ya miaka mitano unaulizwa tena "ulitaka viatu gani vile?"