Kikwete siyo safi! - yes I said it!

JOKOFU aka NYANI NGABU,
Two things will happen ktk hii battle you either WIN or you go home with lots of SHAME..........so far you'r in the "den of darkness." Kuna mtu alisema hapa kwamba NYANI NGABU = na JOKOFU KIWETE/KIKWETE. Seems like you want to win it all, two faces in one body na ndio Utanzania huo, shame on you!!!.
 

naona ushaanza kuanika mmoja baada ya mmoja, kweli huu mwaka kuna mengi JF ! naenda kwenye mapenzoooo kupumzika !
 

Now this is what I call flummery...!!!
 

Mimi sio Jokofu Kiwete. Get it? If you think I am him then I double dare you to prove it. Na wewe ES...you have been around for too long not to tell who's who? How come I know who he is and none of y'all can't? Pathetic...
 
Haya yamekwisha wajomba!
Sifa moja kubwa nayompa Kikwete hadi sasa ni uhuru huu wa waandishi..
Kusema kweli hapa sina mfano pamoja na kwamba yeye mwenyewe hujipunguzia kudos anapodai kuwa hizi ni KELELE za wapinzani hazimzuii kupata usingizi!...
 
Sifa moja kubwa nayompa Kikwete hadi sasa ni uhuru huu wa waandishi..

So far ninazimia sana na Adam Lusekelo, maana mkuu humkoma nyani kwenye Daily News, sasa nimeelewa kwa nini Mkuu wa kaaya, angekuwa na his way nasikia angetaka yafungwe,

yaani Daily News/Uhuru, na Mzalendo, ila it is a matter of time nasikia anayalia dip tu siku moja atayafunga, maana haya sio mtandao!
 
Mkandara, right on the mark.. kama kuna jambo moja ambalo Kikwete alilifanya mapema sana na kumzuia Seif Khatib kutumia nguvu yake ya kisheria, hasa pale watu walipomuita yeye msanii.. kucha ndefu zisizokatwa za vidole vya serikali zilikuwa tayari kuparua.. ni yeye alizuia..
 

Does he have an option? Kwani yeye hajui akifungia magazeti ndio hata hiyo sifa ndogo iliyobaki itapotea?

Yaani mnataka hata hao watu wa nje ambao bado hawajafahamu udhaifu wake nao waanze kumwona kuwa hafai?

This may be the only thing going for him this far; but not because of his own benevolent wish. He is forced to.
 
Umeanza tena! naona hujipendi. Waache wale wala wali wale wali wao!

Tanzania kila mtu yuko huru kusema kile anachojisikia.
Tusiposema sisi basi mawe yataongea
 

Sifikiri kama anaweza kuyafunga, hana huo ubavu. Waandishi makini kama Adam ndio wanatakiwa Tanzania sio wale wanaochukua bahasha halafu wanasahau wajibu wao. Chukua bahasha na piga nondo kama kawaida.
 
Kikwete had ten solid years kama waziri wa mambo ya nje. Na kabla ya hapo waziri wa fedha..and i dont know what else. Anahitaji miaka mingine mingapi ili kuweka mambo sawa?

Katika Mahojiano na BBC (1985) kabla mwalimu hajang'atuka, aliulizwa swali kwanini asiitikie wito wa wananchi wa kumtaka aendelee na urais? mnakubuka maandamano ya usiku kucha, wazee, vijana, etc..kwenda nyumbani kwa mwalimu kumuomba asisistaafu?

mwalimu alijibu kwamba alikuwa na miaka 'ishirini na tatu' ya kufanya mambo kama rais. hata akiongezewa miaka mingine mia (emphasis is mine) haoni kama inaweza kubadili kitu.

katika nchi kama marekani, issue ya conflict of interest ni issue kubwa. mtu anapokubali public service analazimika 'kuachia business interests'. actually kuwa mfanyakazi wa ngazi ya juu serikalini ni kukaribisha umaskini! Lakini si umechagua kuutumikia umma? basi ridhika!

Isue ni kwamba wanasiasa wetu wanaingia madarakani kuchuma! Ndio maana Kennedy (pamoja mna mpungufu yake) alitupa usemi wa karne katika nyanja ya utumishi wa umma " usiulize nchi yako itakuffanyia nini bali wewe utaifanyia nini nchi yako?

Ni wanasiasa wa ngapi Tanzania ya leo wana jeuri ya kujibu swali la Kennedy???
 
Ni wanasiasa wa ngapi Tanzania ya leo wana jeuri ya kujibu swali la Kennedy???

Mkuu Prince,

Heshima mbele kaka, maneno mazito, ila pia yanatushitaki na sisi wananchi, kwamba je tunayo jeuri ya kujibu swali la Kennedy, na in our case ni rahisi as wananchi ni kutowapigia kura tu viongozi wabovu, na kuwaelimisha na wananchi wengine pia on that!

Are we ready for that? Lakini you have a strong point, kwamba time should not matter kwa Muungwana, baada ya miaka mingi serikalini, well said!
 
Thanks for your analysis yakinifu. Lakini kwa wafuatiliaji wa masuala ya nchi wnajua hu is clean and who is not. Majority wa top layer ya uongozi wa ngazi za juu wa nchi are 'CORRUPT'. Wale wote waliokuwa tangu enzi ya Ruksa wamekuwa ni wabadhirifu wa mali ya umma na kuuza rasilimali ya nchi. I will go back 10 years. Uchaguzi wa 1995 ni nani alikuwa akiwika? Alikuwa ni Lowasa. walikodisha ndege kutafuta wadhamini katika mikoa. Pesa walipata wapi? Ndoa ya kikwete na Lowasa haijaanza leo. Lowasa tarack down Tangu AICC, Wizara ya Ardhi Loliondogate. Alikuwa waziri wa Ardhi. Baada ya Uchaguzi 1995 Lowasa alikwenda Msasani kumuuliza mwalimu 'mbona umenichafulia jina' Julius aliwaita vijana wake wakmpa fail la LOWASAGATES. Akamwambia openly Lowasa you are Corrupt. Aliondoka kimyakimya. Muulize Butiku he must have some information on that. Mkapa akaingia madarakani wakaanza ndoa na Sumaye huku Kikwete na Lowasa wakiendlea kutesa na kujiandaa kwa 2005. JE U safi wa Kikwete Uko wapi. Kwa wenzetu huku ughaibuni Kiongzi wa chini yako akituhumiwa kwa anything mkubwa aliyemweka madarakani inabidi ajipange vingenevyo anaondoka. Kwa hiyo ni wachache wakio wasafi. Kuanzia watumishi wa kawaida mamesenger mpaka huko juu. watu wanachozidiana ni kiwango cha ufisadi. Mafisadi ni wengi. sababu ikiwa ni umaskini uliokithiri, wivu wa maendeleo, tamaa ya kujitajirisha na kujiona. Je ni wabunge wangapi wanaweza kusema walishinda kama enzi za Julius yaani kura halali. PCB Polisi mahakama wote mafsadi wamejaa. Kwa hiyo kilichobakia ni nguvu ya wananchi. 2010 iko mlangoni. Wananchi watumie Kura. Lakini kama urubuni utaendelea wa kutumia technical campaign za pesa tutarudi palepale. Vitendo vya zomeazomea HOYEEEEE, ZOMEENI ZOMEENI ili waone Aibu. Ila sishauri wananchi kutumia nguvu au silaha. Mungu ibariki Tanzania na Wazalendo wake.
 
Do we really have the time to talk about Dirty Politics instead of developmental issues ?

Kuongea dirty politics kutaturudisha nyuma tu na hata target yetu ni kusonga mbele, so lets start to kusonga mbele jamani !
 
Mkuu Mwanakijiji, mbona naona watu wa vyama vya upinzani wanampango wakumuomba JK masamaha kwa kumsingizia kuwa yeye ni fisadi na kumweka kwenye list ya mafisadi ya Dk Slaa? Sijui wewe kwa hilo unamaoni gani kama yalioyoandikwa na Rai ni ya kweli. Nawepia utajitokeza kuomba msaamaha kama watakavyofanya vyama vinee vya upinzani?
 
kwani mimi niko kwenye vyama vya upinzani? wao wamejitwisha mzigo wao, na waubebe kivyao vyao!! Ukiangalia sehemu fulani tayari nilishajenga hoja hiyo kuwa kwa wao kumuweka JK katika orodha ya mafisadi walifanya strategic mistake...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…