Kikwete siyo safi! - yes I said it!

Kikwete siyo safi! - yes I said it!

Wajamameni tulalamika mno, kama mchangiaji mmojawapo aliyebainisha hapo juu, JK ni reflection wa watanzania. Mambo anayoyafanya ni utashi wetu sisi tuliomuweka madarakani. Ni kama George Bush amareflect wamarekani walivyo. Haiwezekani tukapata raisi ambaye hatakuwa na reflection ya kwetu sisi. Watanzania wengi hatupendi kufanya kazi ni kulalamika tu, kila mtu mission town, hatujui kusoma alama za nyakati,kila mtu najitahidi kuwafisadi kwa nafasi yake!!! ni aibu hata kusimulia mawaziri wanatafuta academic intellectual kwa gharama yeyote kila mtu anajua Matayo hana PhD, Nchimbi,Nagu et al list ni ndefu lakini ndo mawaziri wetu!!. BWM alipokuwa madarakani aligundua ni aina gani ya watu mizigo anayoiongoza, akamua kujifanyia biashara ikulu, kuna mkutano mmoja Johanesburg BMW alimua kuwakilishwa na jamaa fulani kutoka Ghana.baada ya kuona TZ tupo kwenye usingizi wa pono..nafikiri watanzania walio wengi tupo tu kwa sababu ya kuwepo. Wale wenye macho hawataki kubeba torchi, wanaachia vipofu watuongoze. Wenye uchungu tujikite kwenye siasa tupole uongozi basi....hainiingi akilini Mbuge kukaa miaka 40!! Mzindakaya et al inamaana hakuna zaidi ya yeye kwenye hilo jimbo, akifa ndo mwisho wa uwakilishi wa wadanganyika hao. Tusilalamike tufanye kitu..mimi wewe na yeye kama tuna machungu na hii mchi yenye neema. Mungu bariki Tanzania
 
Halafu ninachoshindwa kuelewa ni pale baadhi ya watu wanaoonekana kuwa wana akili walipompigia debe Kikwete. Walioona nini kwake? The guy couldn't even dare to debate Mbowe and others. Yes he was the front runner and all...but why avoid debating if you are confident in your abilities? Instead he embarked on a cross-country promises tour where he promised a bunch of stuff that I lost track of and none of which have been delivered so far! A lot of people who were firmly behind him then are now his staunch critics. Where were these people before to ask him the same questions they are asking him now when some if not the same issues/ questions existed before he took over the presidency? I guess that charm, likable personality, and good looks duped and mesmerized them into believing that he was the real deal without having him to answer the tough questions. They say hindsight is 20/20...so I wonder if they had to do it again if they'll support him the way they did in '05...
 
Ushirombo, wenzio wameanza kufanya kitu, la maana na wewe kudandia treni hilo! Binafsi nimechoka kulalamika..
 
Kuna hii theory pia kwamba watz tunapenda kusifia watu wanaopaa kimaisha kiajabujabu, mtu anaporomosha majumba harakaharaka, tunamchekea, mshikaji anafanya TRA anapiga deal za kukwepesha kodi, tunamshangilia, mtu akifake receipt ofisini anasifika. Mtu akirudisha imprest ambayo hakutumia tunamshangaa na kumcheka. Na huu ndio ufisadi wenyewe tunaongelea, je ndio tuseme watz tunapenda ufisadi au namna gani?

Kitila,

Swali hili hata mie najiuliza sana. bongo wasanii wanasifiwa. Watu wa town mission wanaonekana ndio wanafaa. Argument ya Nyani ni kubwa kweli. Hata hapa Marekani, weusi watamsifia mtu mwenye utajiri wa kuuza madawa zaidi ya kusifia mtu anayefanikiwa kwa kusoma au kufanya kazi ngumu.

Ingawa bado sijakubaliana kabisa na argument ya Nyani ila nimeanza kidogo kuquestion kuwa labda waafrika tuna issues ambazo bado sijazijua vizuri!
 
Nadhani hapa mnaibua mambo muhimku sana "Kwanini Kikwete alichaguliwa?" ni swali muhimu sana katika mjadala huu.

Unajua Mwanakijiji hilo ni swali muhimu sana. Hata kabla ya kumchagua mtu inabidi watu waulize hilo swali: kwa nini tukuchague wewe. Na si swali ambalo linajibiwa kwa kutoa mi ahadi kibao. Nichagueni mimi kwa sababu ninajuana na wafadhili na nitawajengea daraja na barabara za rami.
 
Kitila,

Swali hili hata mie najiuliza sana. bongo wasanii wanasifiwa. Watu wa town mission wanaonekana ndio wanafaa. Argument ya Nyani ni kubwa kweli. Hata hapa Marekani, weusi watamsifia mtu mwenye utajiri wa kuuza madawa zaidi ya kusifia mtu anayefanikiwa kwa kusoma au kufanya kazi ngumu.

Ingawa bado sijakubaliana kabisa na argument ya Nyani ila nimeanza kidogo kuquestion kuwa labda waafrika tuna issues ambazo bado sijazijua vizuri!

Hii ndio changamoto sasa kwa kizazi chetu ku-prove kwamba hivyo sivyo tulivyo. Hizi kelele zinazopigwa humu msizidharau hata kidogo. Siku moja mtakuja kukumbuka jinsi mtandao ulivyoleta mapinduzi ya kifikra kwa kuwaunganisha watu walio sehemu mbalimbali duniani, waliootoa maoni yao kwa uhuru na uwazi bila hofu yoyote ile. Pole pole fikra hizo za kimapinduzi zitapenyeza ktk jamii na mabadiliko yataanza kutokea. Tuweni na subira.
 
Kwa upande wangu naona tatizo ambalo bado tunalo siyo Tanzania tu bali hata sehemu nyingi za Afrika ni masalia ya mawazo ya kikoloni. Wakati watu weusi wa Marekani wanahangaika na masalio ya mawazo ya kitumwa sisi tuliokuwa chini ya wakoloni bado tunahangaika na mawazo hayo.

a. Kiongozi yuko sawa wakati wote. Wakati wa ukoloni haikuwa kawaida kwa mtu kumkosoa "Bosi" au hata kumpinga kiongozi kwani unaweza kuitwa kwa DC (bomani) na kupigwa viboko!

b. Huwezi kufanikiwa hadi kiongozi abariki. Utaona kuwa watu wengi waliopata ahueni ya maisha wakati wa ukoloni walifanya hivyo kwa baraka za wakoloni wenyewe. Ndiyo historia ya kina Mungai n.k Wale waliofanya kazi kwa wazungu n.k walipewa ahueni ya aina fulani na hata wakati wa uhuru ulipofika walikuwa tayari wamepewa a jump start ukilinganisha na wengine.

c. Viongozi waliokwenda kinyume na wakoloni walionesha uhuru wa mawazo. Kitendo cha Nyerere kurudisha suruali ambayo alijua haikupatikana kwa uhalali ilikuwa ni ishara ya kwenda kinyume na mawazo ya "mzungu". Kitendo cha Bi. Rosa Parks kugoma kwenda nyuma ya basi, alikuwa anakwenda kinyume na mawazo ya "Mweupe"; kitendo cha Gandhi kuendelea na maandamano licha ya vitisho toka Mwingereza kilimfanya aende kinyume na mtawala.

Ni hilo la tatu ndilo linalotokea sasa hivi katika Tanzania na limeanza kwa watu binafsi. Tutapiga hatua kubwa pale ambapo sekta binafsi itaweza kusupport vyama vya upinzani hadharani bila woga wa kuadhibiwa na watawala. Tutakapofikia kuona Kampuni ya Bia inadhamini au inachangia CCM na vyama vya upinzani (kwa ajili ya maslahi yake) au wafanyabiashara wakubwa wanaonekana hadharani na kushiriki harambee za wapinzani basi mnyororo wa mwisho utakuwa umeanza kukatika.

Sasa hivi CCM imeanza kupogeza kukamata (loosing the grip) watu binafsi jambo ambalo huko nyuma lilikuwa halifikiriki. Leo wana CCM wanaweza kutoa hisia zao mbele ya vyombo vya habari badala ya "vikao vya chama". Huku tunakokwenda asasi, makampuni n.k yatalazimika kuchukua uamuzi wa kutolazimika kuibariki CCM kwa kuhofia kuwa CCM itawaadhibu.

Watu walipomchagua Kikwete sababu kubwa ni kuwa walikuwa na matumaini kuwa atakuwa tofauti na atawaongoza. Lakini wengi (bila ya shaka hata yeye mwenyewe) hakutarajia kuwa katika kuongoza huko atatakiwa afanye maamuzi magumu na ya haraka na wakati mwingine ya kuthubutu zaidi. Hadi hivi sasa bado hajafanya kitu hicho na amekuwa "mbembelezaji Mkuu"!

Suala la BoT kwa mfano, hivi kwanini hamjajiuliza terms of reference za uchunguzi zinaanzia mwaka 2005? tu na siyo nyuma ya hapo? Ukweli ni kuwa nyuma ya hapo kuna IPTL, Dege, Rada n.k!!
Sasa hivi watu wameanza kutambua kuwa uongozi siyo lele mama na kuongoza watu milioni karibu 40 siyo mambo ya kishkaji!
 
Nadhani hapa mnaibua mambo muhimku sana "Kwanini Kikwete alichaguliwa?" ni swali muhimu sana katika mjadala huu.

Walimchagua kwa sababu ni "kijana", mtanashati na supposedly ni mtu wa watu.

Rais Kikwete sio mtendaji bali ni mwanasiasa.
 
watu walimchagua Kikwete kwa vile walimpenda na walimuamini. Hadi hivi sasa bado wanamuamini na wale wapiga kelele watachoka kwani yeye anajitahidi kwa kadiri ya uwezo wake kuliongoza taifa katika neema. Uchaguzi ulishaisha mwaka 2005 kilichobaki ni kusubiri tu.

asanteni.
 
alichaguliwa kwasababu kulikuwa hamna "choice" nyingine ya maana kwa wakti ule.....i doubt kama by 2010 kutakuwa na mtu upande wa ushindani ambaye atakuwa tayari for the job!!! its sad to say, but its a fact.
 
YNIM,

Huu inawezekana kuwa ni ukweli na hata mie nakubaliana nawe katika hilo. Hata hivyo hili ni swali kubwa zaidi ya general election! Je hata CCM kulikuwa hakuna mwingine anayefaa zaidi yake? Kama huyu ndiye anafaa basi ccm ni mbovu zaidi kuliko hata hao washindani!
 
alichaguliwa kwasababu kulikuwa hamna "choice" nyingine ya maana kwa wakti ule.....i doubt kama by 2010 kutakuwa na mtu upande wa ushindani ambaye atakuwa tayari for the job!!! its sad to say, but its a fact.

Huo ndio ukweli ambao wengi hapa hawataki kuusikia. Wanatakia kusikia JK aliiba kura.

Kwa Watanzania ninaowajua mimi na baadhi ninawaona hapa JF, tusitegemee maajabu. Wanaothamini maadili na uongozi bora ni wachache mno. Wengine wanasema tu kwasababu hawana uhusiano na wanaoongoza au hiyo nafasi ya ulaji hawajaipata.

Kujituma kama Nyerere ni wito mkubwa mno, nina uhakika Tanzania ya leo wengi wetu hatuwezi hata kuwajibika kwa asilimia 20 ya alivyokuwa Nyerere.

Mimi nimewaona wasomi wengi sana wa TZ huku majuu na uzalendo wao fake, wakifika nyumbani ndio viongozi wa dhuluma, utawala mbovu na ufisadi. Huwa nashika tama, hivi kweli ni hawa jamaa ambao tulikuwa tunashinda nao kwenye vijiwe?

Mnaweza kumpaka JK mtakavyo lakini huenda ni reflection ya Watanzania wa leo, huenda ni bora kuliko sisi wengi hapa na labda ndio maana alichaguliwa kwa asilimia 80.

I wish tungelikuwa na rais mwingine mchapa kazi, lakini tutamtoa wapi kama Watanzania wenyewe ndio hawa wa JF maneno mengi, vitendo sifuri. Sisemi kila mtu, kuna watu wachache ambao maneno na matendo yao vinafanana lakini wengi wetu mmmhhhh!! mungu saidia.
 
Huo ndio ukweli ambao wengi hapa hawataki kuusikia. Wanatakia kusikia JK aliiba kura.

.....
I wish tungelikuwa na rais mwingine mchapa kazi, lakini tutamtoa wapi kama Watanzania wenyewe ndio hawa wa JF maneno mengi, vitendo sifuri. Sisemi kila mtu, kuna watu wachache ambao maneno na matendo yao vinafanana lakini wengi wetu mmmhhhh!! mungu saidia.

Mhhhh Mtanzania,

Wakati ambao JF inajiandaa kuweka mikataba yote ya serikali kuanzia Loliondo ya mzee Mwinyi mpaka huu uliosainiwa juzi ufaransa bado wewe unasema kuwa vitendo sifuri.

Kusema kuwa watu wanataka kusikia kuwa JK aliiba kura is very low of you. JK ameexplode peke yake. Kama unamshauri, naomba umwambie kuwa asiendelee kuwa na mind set hiyo unayoiweka hapa kuwa watanzania maneno mengi na hakuna vitendo.

Watu wamechoka na ugumu wa maisha na mifumuko ya bei inayoendelea huko bongo. Fukuto linalokuja ni kubwa sana. Just mark my words. Tanzania imebadilika sana na nimeanza kuamini kuwa labda saa ya ukombozi kweli imefika.

Endelea kuwa tu dismissive wa kinachoendelea. Bro Jay 4 ameshauri wana ccm kusoma alama za nyakati. Nchi imebadilika hii ohhh hooooo!
 
Kaka Mtanzania
Naona umetoa a bitter pill to swallow tena bila a drink of water. Sina comments za kuongeza on top, ila "nimegundua" kwamba jamii ya kitanzania ni shabiki sana ya uzembe,usanii,uzushi na pia ufisadi....yaani ukiwa mtumishi wa umma na kufanya mambo hayo, basi wewe ndio unaonekana HERO. Ukiwa mwajibikaji na playing by the rules basi wewe ni fala na bwege la kutupwa. Hoja kwamba uongozi ni reflection ya watz wenyewe mie nakubaliana nayo.
 
Mhhhh Mtanzania,

Wakati ambao JF inajiandaa kuweka mikataba yote ya serikali kuanzia Loliondo ya mzee Mwinyi mpaka huu uliosainiwa juzi ufaransa bado wewe unasema kuwa vitendo sifuri.

Kusema kuwa watu wanataka kusikia kuwa JK aliiba kura is very low of you. JK ameexplode peke yake. Kama unamshauri, naomba umwambie kuwa asiendelee kuwa na mind set hiyo unayoiweka hapa kuwa watanzania maneno mengi na hakuna vitendo.

Watu wamechoka na ugumu wa maisha na mifumuko ya bei inayoendelea huko bongo. Fukuto linalokuja ni kubwa sana. Just mark my words. Tanzania imebadilika sana na nimeanza kuamini kuwa labda saa ya ukombozi kweli imefika.

Endelea kuwa tu dismissive wa kinachoendelea. Bro Jay 4 ameshauri wana ccm kusoma alama za nyakati. Nchi imebadilika hii ohhh hooooo!

Mwafrika wa Kike,

Leo nenda idara yoyote ya serikali, nenda mashuleni, nenda hospitali, nenda kwenye NGOs za kusaidia jamii, nenda TRA, utakumbana na unyama unyama kuliko uadilifu na kazi bora, je hao nao ni wanasiasa? Je hao nao ni CCM?

Si ajabu watu wanatoka hapa JF na kuandika maneno makali, wanarudi ofisini kwao, wanaendeleza hayo hayo tunayoyapigia kelele kila siku hapa.

Tuna kazi kubwa sana ya kuisafisha jamii ya Tanzania. Mahali pa kuanzia ni sisi wenyewe popote tulipo na hasa kwenye utumishi wa umma kule nyumbani, vinginevyo ni yale yale ya maneno mengi, lakini matendo matupu.
 
Mnaweza kumpaka JK mtakavyo lakini huenda ni reflection ya Watanzania wa leo, huenda ni bora kuliko sisi wengi hapa na labda ndio maana alichaguliwa kwa asilimia 80.

..hupimwa kwanza kwa kufuata vigezo vilivyokubalika na kufaulu!

..hupigiwa kura baada ya kutumiwa,na si kabla!

..hudumu kwa siku nyingi,bila kulalamikiwa!

..hakimkatishi tamaa mtumiaji kukitumia!

..hutumiwa na wengi tena na tena!

..jirani akitumia humwambia mwenzake naye akijaribu!

..huhadithiwa vizuri mitaani!
 
Soma limeeleweka Mtanzania.... nakubaliana na wewe
 
Mwafrika wa Kike,

Leo nenda idara yoyote ya serikali, nenda mashuleni, nenda hospitali, nenda kwenye NGOs za kusaidia jamii, nenda TRA, utakumbana na unyama unyama kuliko uadilifu na kazi bora, je hao nao ni wanasiasa? Je hao nao ni CCM?

Si ajabu watu wanatoka hapa JF na kuandika maneno makali, wanarudi ofisini kwao, wanaendeleza hayo hayo tunayoyapigia kelele kila siku hapa.

Tuna kazi kubwa sana ya kuisafisha jamii ya Tanzania. Mahali pa kuanzia ni sisi wenyewe popote tulipo na hasa kwenye utumishi wa umma kule nyumbani, vinginevyo ni yale yale ya maneno mengi, lakini matendo matupu.

Mtanzania,

Unategemea nurse wa hospitali ya musoma awajibike vizuri wakati mabosi wake kuanzia daktari hadi waziri wa afya ni wezi tu na wababaishaji? Kila kinachoendelea huko chini ni matokeo ya failure ya uongozi wa juu kwenda chini.

Hapa amerika, wasomi wengi wamekubaliana kuwa corporate culture inakuwa determined sana na viongozi wa juu na ndio maana maCEO wanalipwa pesa nyingi kampuni zao zinapofanya vizuri.

Kwa kweli sitegemei kupata service nzuri toka kwa daktari wangu wa wilaya anayelipwa laki 1 kwa mwezi huku waziri wa afya akiwa na nymba ya milioni mia tano!

Kwa kweli sitegemei mfanyakazi wa TRA wa songea vijijini akawa na moyo wa kufanya kazi wakati bosi wake ameshirikiana na Rostam Azizi kukwepa kodi ya mabilioni ya shilingi...

Serikali ikiwa mbofu mbofu kama hii ya Kikwete kila kitu hadi vijijini kitakuwa kibovu tu.
 
Hivi Mtanzania.. hivi hayo unayoyasikia yanaendelea tanzania yametoka mbinguni? Hiyo orodha imezua kasheshe hivyo je kile tutachofanya wiki ijayo si ndio kitawachanganya watu. Si wote wanataka wasimame jangwani majina yao yatajwe kuwa wanafanya kitu!
 
Mtanzania,

Unategemea nurse wa hospitali ya musoma awajibike vizuri wakati mabosi wake kuanzia daktari hadi waziri wa afya ni wezi tu na wababaishaji? Kila kinachoendelea huko chini ni matokeo ya failure ya uongozi wa juu kwenda chini.

Hapa amerika, wasomi wengi wamekubaliana kuwa corporate culture inakuwa determined sana na viongozi wa juu na ndio maana maCEO wanalipwa pesa nyingi kampuni zao zinapofanya vizuri.

Kwa kweli sitegemei kupata service nzuri toka kwa daktari wangu wa wilaya anayelipwa laki 1 kwa mwezi huku waziri wa afya akiwa na nymba ya milioni mia tano!

Kwa kweli sitegemei mfanyakazi wa TRA wa songea vijijini akawa na moyo wa kufanya kazi wakati bosi wake ameshirikiana na Rostam Azizi kukwepa kodi ya mabilioni ya shilingi...

Serikali ikiwa mbofu mbofu kama hii ya Kikwete kila kitu hadi vijijini kitakuwa kibovu tu.

Mwafrika wa Kike,

Hapo ndipo tunapotofautiana, wengine tunaamini kwamba ni lazima tutimize wajibu wetu kabla hata ya kuangalia kama mtu mwingine anatimiza wajibu wake.

Fisadi anaiba mamilioni kwasababu anaona mshahara wake hautoshi, daktari naye anaiba malaki kwasababu anaona mshahara wake hautoshi, nurse naye anamwacha mama mja mzito anakufa kwasababu mshahara wake hautoshi. Wote hawa ni kitu kimoja, hawana tofauti yoyote. Hata yesu alisema toa kibanzi kwenye jicho lako kwanza kabla hata ya kuthubutu kuangalia jiko la mwingine.

Kitu nilichojifunza kwa nguvu zote huku nje ni umuhimu wa kutimiza wajibu wangu, kisha kujua kutetea haki yangu mpaka dakika ya mwisho. Je nina haki gani ya kutetea haki yangu huku mimi mwenyewe nimenyang'anya haki ya mtu mwingine?

Sisi tunaona akina Karamangi, JK, Lowassa ndio mafisadi lakini kwa mama mjamzito anayekufa kitandani kwasababu tu ameshindwa kutoa rushwa kwa Mkunga, huyu Mkunga ndio fisadi namba moja. Kwa
msichana wa mlimani ambaye anafelishwa kwasababu tu ameshindwa kutoa mwili wake ili mwalimu achezee, huyo mwalimu ndio fisadi namba moja, kwa mfanyabiashara anayefilisiwa kwasababu tu kakataa kumpa hongo mtu wa TRA, huyu TRA ndiye fisadi.

Sawa haya mapambano yanaweza kuharakishwa kama utawala wa juu utatimiza wajibu wao, lakini mapambano haya yatafanikiwa zaidi kama Watanzania tutabadilika na kuthamini haki ya mtu mwingine. haki ambayo inatakiwe umpe mbaya wako sawa na kipenzi chako. Kama tutajenga culture ya kuthamini kazi badala ya bla bla nyingi. Culture ya kujua kwamba ukiiba elfu kumi ni sawa tu na kuiba milioni kumi, wote ni wizi na inatakiwa ulaaniwe. Kinyume chake wote sisi tutakuwa mafisadi tu.
 
Back
Top Bottom