Kikwete: Tutawajibu wanaotusema!

Kikwete: Tutawajibu wanaotusema!

Hahahahaaaaa

Hii si aliitihoa kwa Prof. Jay Kwenye ndio mzee.

Wasanii bana. Anyway tuliyataka wenyewe. 2010 hiyoo tutampa tena, nahisi sasa wanafunzi watapelekwa practical mwezini.
 
...Jakaya, ambaye alikuwa anarejea kutoka ziara ya takribani wiki mbili kwenye nchi za Jamaica, Cuba na Trinidad na Tabago ambako alihudhuria mkutano wa Jumuiya ya Madola, alisema hatishwi na maneno yaliyozungumzwa kwa kuwa watu waliozungumza wanajulikana wanatoka upande gani.

”Japo bado sijapata taarifa vizuri kuhusu yote yaliyozungumzwa katika kongamano hilo; siwezi kushangazwa sana, lakini ninakwenda kupata taarifa kamili na kujadiliana na wenzangu kisha nitajibu mambo yote yaliyokuwa na maana na yale ambayo hayana maana na yaliyosemwa kwa chuki, tutayapuuza tu,” alisema Rais Kikwete.

Rais Kikwete alisema hashangazwi na hali iliyotekea kwa kuwa binadamu wanatofautiana kimtazamo, lakini akasisitiza kuwa anachojali zaidi ni dhamana aliyonayo kwa umma.

"Asilimia 15 watakupenda, asilimia 15 nyingine watakuchukia na asilimia 70 iliyobaki watabaki wanaangalia upepo unaelekea wapi hivyo tusubiri kuna maamuzi tutafanya,” alisema Rais Kikwete.


Kumbe mtu yeyote anayekukosoa yuko kinyume chako? Sasa umma si ndio unaopiga vita juu ya ufisadi na kumwambia achukue maamuzi magumu? Sidhani ni sawa kila mtu katika umma apaze sauti juu ya jambo hilohilo, wapo wanaoweza kusema lakini wakaitikiwa na umma?

Si sawa kufikiri kila anayetofautiana nawe katika jambo fulani yuko kinyume nawe katika kila kitu. Nionavyo mimi, kama anawajua wasemaji wako upande gani siku zote inaelekea hakuna neno jema analotazamia kutokea upande ule. Negative attitude hiyo haimsaidii mtu kujikosoa. Asilimia hizo ni sawa as psychological relieving factots to anybody under catastrophic circumstances, lakini hiyo 70% yenye kufuata upepo could be detrimental, depending upepo huo umepigiwa hesabu ya namna gani. However it may be a motivating formula.

Makamba, sikumbuki kama kuna siku alikubali kwamba wakubwa zake wamekosea lolote. Yule kwa kawaida yake ni vocal, anayependa kumfurahisha aliye juu yake at any cost. Ndiyo maana akipelekwa kwenye kampeni huwa ni chanzo cha maangamizi ya chama chake na often hurudishwa nyumbani asiharibu zaidi, ndipo wanatumwa wenye kujua namna ya kuongea na watu kwa lugha inayoeleweka. Otherwise yeye ni askari wa amri saa zote na kila mahali. Sio yote aliyoyasema ni sawa, ila anayo haki ya kuongea atakavyo. Tatizo ni pale anapowaziba wenzake midomo wasiongee ila yeye tu.

Mwaka 2010 ni mgumu japo JK bado atapeta tu, haimaanishi kwamba atapeta kwa sababu kafanya vizuri saaana, ila kwa sababu ni jadi ya watanzania wa CCM kuhakikisha mtu amnamaliza vipindi viwili vya miaka daladala. Sasa hivi kuna watanzania wengi wenye uwezo wa kuongoza nchi, ni suala la nani akae leo na nani akae kesho tu. Kuna vipaji vingi ila havionekani sababu ya kutunga sheria ili kuwazuia wengine wasiinue kuonyesha vipaji vyao. Kama ingekuwa marekani ambako mtu yeyote anao uhuru kujaribu bahati yake kwa namna yoyote bora akubalike, amani ingeongezeka zaidi bila shaka. lakini hakuna kizuri kisichokuwa na kasoro, barabara ndeeefu haikosi kona ati. Tusubiri majibu yake JK.

Leka
 
Heheee Chaguo la Mungu siyo?

Wa-Anglican na Kizazi cha Nguruwe nasikia ndiyo tulimchagua Kikwete.

Asante yake kajawa Waislaam kwenye CCM na serikali yake.

Hahaaa, Pengo!!! Eti chaguo la Mungu. Sijui alikuwa akimaanisha Mungu yupi?

Maswala mengine heri ukae kimya kuliko uropoke.

Tumaini, usiwe na shaka. Mnataka Muislaam, huyo hapo mnaye. Au kwa kuwa alichaguliwa na Wa-Anglican?

NB: Kwa huku Tabora, hata awekwe NYANI wa CCM, Nguruwe wa CCM, Fisi wa CCM, nk so longer ni CCM basi atashinda. Minyamwezi bwana, huwa napata hamu ya KUI-hasi ili kizazi kipotee milele. Utafikiri siyo mijukuu ya Mirambo na Isike.


Mweh!! taratibu taratibu Sikonge tutafika tu,
Inatakiwa nyie wachache mnaoweza kuchambua pumba na mchele muwasaidie wanyamwezi wenzenu kuachana na mawazo mgando vichwani mwao kwamba bila CCM hakuna maisha.
Lakini nakumbuka kama uchaguzi wa 1995 Tabora palichemka sana hapo kwani siku hizi imekuwaje?
usikate tamaa mkuu endelea kuwaelimisha wanyamwezi, labda uanze kuwakumbusha historia yenu wanaweza wakaelewa,.
 
Rais naye hajibu hoja,ishu ya msingi hapa kutuambia ni mambo gani wewe na serikali yako mnaweza kujivunia na kwamba umefikia wapi na maisha bora...si kuanza kutoka nje ya topic na kulalamika kuwa ni chuki.
Tatizo Rais wetu hakubali challenge na anataka aonekane yupo right kwa kutufanyia usanii...km anaongoza watoto vile. Halafu makamba anataka watu wakae kimya kwasababu hayo mamlaka yamewekwa na Mungu.
Makamba anamwelewa vema Boss wake (JK). Nampongeza kwa hiloo...

JK ameonyesha naye ni muungajii mkono na huenda ni archtecht wa mipasho, mapigo, majungu, fitina na nk.

Tusimlaumu makamba wala mama SS. Wanaimba wimbo wa Boss wao.
 
kikwete .....huna jipya kwa watz? elimu,maisha,kilimo...vyote umefulia
 
Wanyamwezi wana msemo wao mmoja, "Kuzikana Nsazi ni Kunia Lifi' yaaani ukitaka nzi wasikufuate wewe kunya mavi waachie! Kazi kweli kweli!

Heheee Chaguo la Mungu siyo?

Wa-Anglican na Kizazi cha Nguruwe nasikia ndiyo tulimchagua Kikwete.

Asante yake kajawa Waislaam kwenye CCM na serikali yake.

Hahaaa, Pengo!!! Eti chaguo la Mungu. Sijui alikuwa akimaanisha Mungu yupi?

Maswala mengine heri ukae kimya kuliko uropoke.

Tumaini, usiwe na shaka. Mnataka Muislaam, huyo hapo mnaye. Au kwa kuwa alichaguliwa na Wa-Anglican?

NB: Kwa huku Tabora, hata awekwe NYANI wa CCM, Nguruwe wa CCM, Fisi wa CCM, nk so longer ni CCM basi atashinda. Minyamwezi bwana, huwa napata hamu ya KUI-hasi ili kizazi kipotee milele. Utafikiri siyo mijukuu ya Mirambo na Isike.
 
Jamani si mlisema yeye ni chaguo la Mungu!! Mpaka wengine mkamwita "Tumaini lililorejea"

Nimependa Msomi Ulimwengu alivyomchachambua!!!
 
alipima akili alipokuwa huko,hahhaaaahhaaaa mamaaaaaaa haahahahahahahha
alidanganywa majibu aliyopewa,
 
alipima akili alipokuwa huko,hahhaaaahhaaaa mamaaaaaaa haahahahahahahha
alidanganywa majibu aliyopewa,

Edson nakuunga mikono yote miwili na miguu yote miwili pia. Hawa doctors wamemwongopea majibu kabisa kabisa otherwise wangemweleza hali halisi I guess angeweza hata kuparalyse. Ila sasa one thing ni kwamba hao madaktari wanasymphasize sana na watanzania, I'm sure wanakosa majibu kwamba ubongo wenye uwezo mdogo kama huo unawezaje kuongoza nchi? POLE YETU KUBWA WATANZANIA.
 
Bongo presidaa ambaye hakukoselewa kwa sana wakati hakiwa madarakani ni Mzee Mchonga manake ulikuwa ukiingia katika 18 zake lazima ukione cha mtema kuni. Lakini waliopita baada ya mchonga mbona pamechimbika, kali kuliko zote ni taasisi ya Mwl. Nyerere ambayo imejaa wastaafu ambao miaka yote wamekula bata na kusahau watanzania sasa kunakaribia magharibi wanashtuka na kuanza kutetea watanzania kinafiki ili makaburi yao yasipigwe mawe.

Kubwa kwao ni kukosoa wakiwa nje wakati wao ni sehemu ya yote wanayokemea leo, ananyanyua mdomo mtu kukemea uongozi wa kupeana kishkaji lakini anasahau atashavu alokula ni kutokana na ushkaji huo huo. Mie ningependekeza taasisi ya Mwl. Nyerere wastaafu wote wangekaa pembeni kupisha mawazo mapya ya vijana ambao sio waoga kama hao wazee. Hakuna raisi aliyewahi kuteua mashemeji zake kuwa viongozi kama Nyerere lakini wamekauka kama hawajui kuwa mfumo mzima wa CCM haufai toka ulipoasisiwa na waasisi wake na wao ni sehemu.
 





RAIS WA TANZANIA JM KIKWETE JANA AMEONYESHA UWEPO MDOGO KATIKA KUJIBU HOJA ANAZOAMBIWA,
AKIWA KAANA KWAMBA AMEWASHWA MOTO KWENYE MFUKO WA SURUALI JK ALINGAKA KUHUSU MASWALI ALIOPEWA NA WAANDISHI AMBAYO YANA UKWELI HALISIA KUHUSU HOJA WALIZOTOA WAH BUTIKU NA WENZAKE

RAIS ALIISHIA KUJIBU KIHUNI 155....155.....70 5.....ALAFU ANAAGA KWA ALAMA YA DOLE...MMH SIDHANI RAIS ANAITAJI KUKASIRIKA KWENYE UKWELI...NI KWELI AMETAMKA ANAENDA KUSHUGULIKIA HOJA NA KUZIJIBU LEO HII NATAMKA RAIS KIKWETE HANA KICHWA CHA KUWAJIBU WAKINA BUTIKU...ATACHEZA NA HAO HAO WAKINA SITTA ANAOWACHEZEA NA WAFANYABIASHARA WAKE WA MADAWA YA KULEVYA ANAO WALINDA...LAKINI NAWAAHAKIKISHIENI MAJIBU ATAKAYOTOA YATAZIDI KUMWONYESHA JINSI ALIVYOKUWA KILAZA KWA KUKUMBATIA wafanyabishara matapeli,,,kisa pesa zao zinatunza CHAMACHA MAJAMBAZI....VERY BAD

wah sana natumaini tutasikia kama si kuweka hadharani nawahakikishia zile nondo za wale wazee hazijibiki kila sehemu wamegongeleanyundo...jk akimbii pale...akawahaadaae hao hao waandishi wake na matapeli wake.....
 
NB:
- Naona hapa ameongea kama aliyeingia madarakani kwa kufanya mapinzuzi vile. Kutoka 85% waliompenda hadi 15% na wafukuza upepo 70%

_ Hii kupenda kusafiri hata kabla hajatatua hili ni kweli kuwa linatokana na kula miguu ya mtetea wa keinyeji?

- Ni kweli kuwa sikio la kufa halisikii dawa? kelele zilizokwisha masikioni kuwa misururu ya rais ni mikubwa kupita kiasi bado haisikii au ndio kuwa ni kula nchi kwa kwenda mbele? Fikiria kwa mataifa 195 duniani kama kila moja likipeleka Denmark watu 60 kama msafara wake, basi huo mkutano utakuwa na watu 11,700. Jamani huwaga tunajipima kulingana na uwezo wetu?

=== Sijui, labda ni chuki binafsi==

Chuki Binafsi nani akuonee chuki JAKAYA? hakuna wa kukudhuru kaka yangu, ila madamu umepewa kazi ya wananchi basi watumikie watanganyika wanyonge waliokuchagua tena kwa mbembwe na nderemo za ajabu as if nchi ndo inapata uhuru, leo hii unawataka kuwasariti? ni kosa gani walilookufanyia? hawakuchukii hata kidogo nachoamini mimi hakuna mtanganyika mwenye chuki binafsi juu yako ila tunataka mambo yaende sawa na ni wewe pekee ya kuyasawazisha, we ndiyo baba yetu, sasa ukiogopa KUCHUKUA MAAMUZI MAGUMU sisi watanganyika maskini tukasemee kwa nani?

Kinachotakiwa ni kushughulikia mambo muhimu (National Key issues) ambayo unayajua fika ila tu umaamua kuyaweka pending, mambo ambayo mi naona ni dk 15 tu, ita press conference chukua hatua, sisi wananchi na dola tupo nyuma yako brother na hata katiba ishakupa mamlaka tangu zamani mbona - hakitaharibika kitu, watose tu msife wote.

Mwisho tunakupenda sana raisi wetu ila ukiendelewa kuwalea marafiki zako basi tena SISI WAZANAKI KUNA MSEMO TUNAITA " MALI GANYANJAA...
 
Mambo ya Politiki za bongo ni uvundo mtupu...Kwani huyo JK hataki watu wamwambie kuwa anatokota wakati mchezo ndio unaanza?? Si mlikuwa mnataka Raisi mwenye sura nzuri ndio huyo sasa....
 
Mlimchagua wenyewe sasa mnalia na kusaga meno! Kudadadeki!

Hata 2010 tutamchagua tena. Hakuna mwingine kama Kikwete. Hii ndiyo design ya viongozi tulionao TZ na ndiyo wanapendwa na watu. Wenye wivu waginyonge!!! TZ tunamtaka rais kama huyu, rais kama Mzee ruksa ili tule kivulini, shauri yako kama mfwereji wa maji haupitii kwako, wenziyo sasa ni mkao wa kula mpaka 2015. Safari hii tunajitahidi kuinvest ili yasije yakatukuta yale yaliyotukuta baada ya Mzee ruksa kuondoka maana hatukutegemea kuwa mifwereji yetu ya maji itafungwa ghafla. Watu walitucheka lakini sasa tumerudi kwa nguvu mpya. Pole sana kama huna baba, mama, mjomba au shangazi kwenye system ya ufisadi, maana maisha yako yatakuwa magumu walau kwa miika sita ijayo.

Kuhusu swala la umeme tusha zoea kwani mgao umeanza leo?? Wewe kama unataka umeme nenda kariakoo kajinunulie kagenerator ka mchina na mtaani kila mtu atakujua kuwa mambo yako poa. Ila kusema usubiri TANESCO (RIP) ni kama ndoto ya mwenda wazimu!!!
 
Kuna tabia ambayo imeanza kujengeka kwamba watu fulani wakisema kitu dhidi ya utawala wa awamu ya nne wana wivu kwa vile ni majeruhi wa siasa za mchakato wa 2005 ndani ya CCM. Kwa maana nyingine “wajeruhi’ hao hawapaswi kusema jambo lolote dhidi ya serikali ya JK kwa vile aliwashida na hivyo hawana zuri la kusema juu yake! This is very ridiculous. Badala ya kujibu hoja wakuu hawa wanatuingiza kwenye “uke wenza” maana wake wenza ndio wanakuwa na majibu kama haya.

Kwa mfano hata kama kina Mzee Butiku na Warioba walikuwa kwa Dr. Salum katika mchakato wa 2005 kuna ubaya gani kumshauri Rais kukisafisha chama chake na serikali kuachana na mafisadi? Nani hasiyeona kwamba sasa hivi CCM imekamatwa na kikundi cha watu fulani wenye maslahi binafsi? Rais na Makamba wake wajibu hoja sio mambo ya uke wenza!
 
wanamkakati wa kikwete wanakosea sana wanapobadili mwelekeo wa vita dhidi yao kwa kuanza kuhalalisha mafanikio ya awamu ya nne ..kuwa yanazidi ya mwalimu ....someni gazeti la Subash Patel -TAZAMA ...Mtanielewa.....

nafikiri ni bora watetezi wa kikwete wangejielekeza kujibu hoja....badala badala ya kuangalia sura .....ya mtoa hoja...kosa hilo hata jk jana amelifanya..pale alipowaambia waaandishi kuwa "mnajuwa hao wanaotuo tuhuma wanatoka upande gani..."...ukichambua kauli kama hiyo inabariki makundi ...ina maana bado kuna WAO na SISI..thats a big mistake!!
 
Kwa kauli za jana za rais mwenye dhamana ya kuongoza wadanganyika alikosea amedhihilisha bado ana chuki na wapinzani wake kisiasa ndani ya CCM ambao wana mwambia ukweli ulio wazi kuwa urafiki na urais hautakiwi.
 
wanamkakati wa kikwete wanakosea sana wanapobadili mwelekeo wa vita dhidi yao kwa kuanza kuhalalisha mafanikio ya awamu ya nne ..kuwa yanazidi ya mwalimu ....someni gazeti la Subash Patel -TAZAMA ...Mtanielewa.....

nafikiri ni bora watetezi wa kikwete wangejielekeza kujibu hoja....badala badala ya kuangalia sura .....ya mtoa hoja...kosa hilo hata jk jana amelifanya..pale alipowaambia waaandishi kuwa "mnajuwa hao wanaotuo tuhuma wanatoka upande gani..."...ukichambua kauli kama hiyo inabariki makundi ...ina maana bado kuna WAO na SISI..thats a big mistake!!

I agree with you man. Hawa wamekosa hoja. Mwalimu alimaliza ngwe yake kwa mafanikio ndio maana analiliwa na wananchi aliowapenda na waliompenda na anakumbukwa hadi leo na ataendelea kukumbukwa nchini hadi nje ya nchi. Kuanza kulinganisha mambo ya Kikwete na Mwalimu ni kumtusi tu Mwalimu bila sababu za msingi.

Inapaswa hao waandishi wa magazeti wamshauri Rais vizuri badala ya kupalilia makundi.
 
Hivi mlitegemea ajibu nini zaidi ya alichokijibu? ni ukweli usiopingika kuwa hata yeye anaona jinsi mambo yanavyomelema. si rahisi hata kidogo akafurahia mashmbulizi. ila kale kamsemo ka chuki binafsi kamenikumbusha yule mwanamziki ali hachoki mzee wa farasi. hahahahahahahahahah
 
Back
Top Bottom