...Jakaya, ambaye alikuwa anarejea kutoka ziara ya takribani wiki mbili kwenye nchi za Jamaica, Cuba na Trinidad na Tabago ambako alihudhuria mkutano wa Jumuiya ya Madola, alisema hatishwi na maneno yaliyozungumzwa kwa kuwa watu waliozungumza wanajulikana wanatoka upande gani.
âJapo bado sijapata taarifa vizuri kuhusu yote yaliyozungumzwa katika kongamano hilo; siwezi kushangazwa sana, lakini ninakwenda kupata taarifa kamili na kujadiliana na wenzangu kisha nitajibu mambo yote yaliyokuwa na maana na yale ambayo hayana maana na yaliyosemwa kwa chuki, tutayapuuza tu,â alisema Rais Kikwete.
Rais Kikwete alisema hashangazwi na hali iliyotekea kwa kuwa binadamu wanatofautiana kimtazamo, lakini akasisitiza kuwa anachojali zaidi ni dhamana aliyonayo kwa umma.
"Asilimia 15 watakupenda, asilimia 15 nyingine watakuchukia na asilimia 70 iliyobaki watabaki wanaangalia upepo unaelekea wapi hivyo tusubiri kuna maamuzi tutafanya,â alisema Rais Kikwete.