Walichosema Membe na EL ndicho sahihi and in fact ndicho kilichotakiwa kusemwa na JK yeye kama Amiri Jeshi Mkuu!.
Kazi ya jeshi ni kulinda nchi na mipaka yake 24/7. Nchi jirani inajimegea pande la Tanzania kwa kuhamisha mpaka halali huku Amiri Jeshi wetu akiponda maraha kwenye trips bila kusema chochote na badala yake anafunguka pale tuu alipokutana na she wa Malawi ndipo anapojitangaza yeye ndie Amiri Jeshi!.
Mpaka halali ni katikati ya Ziwa Nyasa, Baada ya kushindwa vita kuu ya Kwanza, Waingereza waliipoka Tanganyika ule mpaka na kuukabidhi kwa Malawi. Ilitakiwa ile siku tunapata Uhuru na mpaka urudishwe, haukurudishwa hadi sasa Wamalawi wanajiona ni halali yao na wamejiapiza kufa nao!.
Msimamo wa EL na Membe ndio msimamo thabiti, mpaka ni pasu pasu na hakuna mjadala wala diplomasia chini ya hapo!.
Kwa vile tayari kuna dhana ya "Dhaifu" kushindwa kufanya maamuzi magumu na kuopt kubembeleza, na tumesha subiri mpaka halali kwa kipindi cha miaka 50, hatuwezi kushindwa kuvumilia miaka miwili na nusu iliyobakia ambapo nchi itatwaliwa na amiri jeshi ambaye sio dhaifu ataurudisha mpaka halali mahala pake!.
Niungeni mkono 2015 kwe CCM asimame ama EL, ama Membe tupate ukombozi wa kweli wa pili wa Mtanzania!.
Pasco.