Kikwete, zungumza na Kagame!!

Haswaa...fedheha kubwa kweli! Afu jana si umesikia kauli ya waziri wao wa mambo ya nje? Alisema...' wao hawatawafukuza watz kama alivyofanya JK''... Baadhi ya watz wenyewe walikuwa wanalia Jk amalize hili swala kwa mazungumzo. Nafikiri Jk aliongozwa na Jazba ktk kufanya maamuzi yake..
c.c Lukolo ,Uda
ukimya wa Kagame baada ya hotuba ya JK ni fedheha kwa Taifa
 
haya mambo ya kagame vs jakaya yanakuzwa mno....

kama kawaida ya watz, hawana ya maana ya kujadili na sasa wanataka kujenga mlima kutoka kwa kichuguu...bloody stupid ------!!!

arrrrrrrrrrrrrrrrgggggggggggggggggghhhhhhhhhhhhh!!!!!!!!!!!
 
Kwenye suala la wahamiaji haramu, nadhani watu wameligeuza tu na kulifanya lionekane ni suala linalotokana na ugomvi wa JK na Kagame. Lakini hoja ya JK kwenye suala la wahamiaji ilikuwa ni kukithiri kwa ujambazi katika mkoa wa Kagera. Na kulingana na taarifa alizozipata ilikuwa ni kwamba ujambazi huo unasababishwa na wahamiaji haramu ambao wengi wao ni wanyarwanda na ndiyo walikuwa na silaha za kufanyia uvamizi. Ndiyo maana JK akawataka waondoke. Inaewezekana nyuma ya agizo hilo kulikuwa na bifu lake na Kagame, lakini kile kilichotoka kinywani mwake kilihusu kukithiri kwa ujambazi.
 
haya mambo ya kagame vs jakaya yanakuzwa mno....

kama kawaida ya watz, hawana ya maana ya kujadili na sasa wanataka kujenga mlima kutoka kwa kichuguu...bloody stupid ------!!!

arrrrrrrrrrrrrrrrgggggggggggggggggghhhhhhhhhhhhh!!!!!!!!!!!
Hoja yako ni nini sasa?
 
Hii ndio demokrasia kutofautiana ila tu msigombane sawa uliyoongea ila rejea swali la awali kwa nini JK ndio aanze na sio PK amwombe kuhusu nini alichokosea???amani unadhani inapatikana kwa jinsi hiyo???kwa nini JK an nafasi nzuri ya kumwomba au kuanzisha mazungumzo na sio PK???JK hana cha kupoteza kuliko kagame hata kama atahamishia mizigo yake toka nje kenya.huwo ni wivu wao Uhuru,M7 na Kagame baada ya kuona China na USA wanafanya ziara zao TZ.kimewauma.
 
Wewe ni mtu wa ajabu sana sina hakika kama unaelewa wakunjane ugenini maraisi???wapi uliona hiyo??watu mnajaribu kila njia kumfanya JK kakosea lakini wapi ukweli umeishadhihirika.
 

Wacha pumba, sijaona kibaya alichokiongea JMK, angalau hapo kwenye mkutano alivyoyaongea pangetokea wakuu wengine wakampinga pia ingeleta maana. Wengi waunge mkono, huyo mnyalukolo akae kimya mbele ya wanamme wenzake halafu akifika kwao aanze kuongea ujinga. Hafai huyo, anaogopa kuongea mbele ya wanaume.
 
Wewe ni mtu wa ajabu sana sina hakika kama unaelewa wakunjane ugenini maraisi???wapi uliona hiyo??watu mnajaribu kila njia kumfanya JK kakosea lakini wapi ukweli umeishadhihirika.
Ebu fikiria , Kagame ameishafika nyumbani kwake..anakaa na kutafakari sana...na kuibuka na kauli ya ...'hit him at right time'...ebu fikiria tena kipindi kile wako huko ughaibuni ...kwa uchungu aliokuwa nao, Kagame, angetoa kauli gani....Kama siyo kauli ambayo ingefanya JK kurushia konde!!
 
Vonix, naona kuna mahali unakwepa hoja. Hoja yangu hapa ni kwamba kwa kuwa Kagame anaamini katika matumizi ya nguvu, na JK anaamini katika mazungumzo, basi na awe wa kwanza kuinitiate mazungumzo kama njia nzuri ya kumaliza migogoro. Hivi unafikiri wakiendelea kutupiana maneno hivi kama wanavyofanya mwisho wa siku itakuwaje?
 
Last edited by a moderator:
Nakubaliana na wewe Faiza, kama Kagame angejibu kitu hapo kwenye mkutano, pengine usuluhishi ungepatikana hapo. Lakini kitendo cha kunyamaza na kwenda kusemea nyumbani kumeufanya mgogoro uwe mpana. Lakini kwa kuwa Kikwete ndiye aliyemchokoza mwenzake, basi amuombe wazungumze yaishe.
Mwisho ninataka kukuchallenge FaizaFoxy, Kagame siyo mnyalukolo.
 
kwanza unauhakika gani kwamba hawakuzungumza kabla....kwanini umekuwa mwepesi wa kuhukumu. unaweza kutuhakikishia kuwa hawakufanya mazungumzo kabla na yakashindikana...
alafu pia kumbuka matamko ya Kagame yalifanyika katika public wala sio kwa njiia za simu. watanzania wote tumesikia kauli za kagame n sote tulioneshwa kukerwa kwa kauli izo. huoni kitendo cha raisi kuweka wazi kinachoendelea kati yao ni ujasiri wa hali ya juu kuwahi kutokea na kuwaondolea wananchi maswali yasiojibika...
mleta bada umekurupuka...
 

Kamchokoza nini? awe asiwe Mnyalukolo ndio hao hao tu, hawasadifiki.
 
huyu kama ni mtz ni -------- wa kwanza. Kikwete doesnt need to talk to that useless kagame. Ni ushauri ulitolewa. its either you take it or you leave it. wewe mtu ni mjinga tena msaliti wa kwanza. huna akili kabisa weeewe.
I liked your level of reasoning!
 
Well nilitarajia pia mtizamo wa aina hii. Naona unapenda kuzungumza kwa kuhisia. Labda ame, pengine ame..... Mimi nimeandika kutokana na context. Kama Kikwete angekuwa amezungumza na Kagame akashindwa kumsikiliza angetuambia kwenye hotuba, kwamba nilipoona mwenzangu ameanza maneno, nilijaribu kuongea naye na akaonekana kutokujali na kuendelea kuyasema..... Na angetuambia level waliyofikia katika mazungumzo yao ya kumaliza huo mgogoro. Lakini hakutuambia hivyo. Sasa ni kwa vipi unataka mimi niamini nisichokijua? Kama una ushahidi kwamba JK aliongea na Kagame ulete na si kuleta story za labda....
 

hakuna haja ya kumbembeleza mwanaume mwenzako hapa! yani JK amuombe radhi PK, kwa kosa lipi? kama vipi ngoja kwanza wahamiaji-haramu warudi kwao kwanza then mazungumzo yatafuata kama kagame ataomba iwe hivyo!
 
Vijana wa Bavicha tangu Slaa amuunge mkono Kagame mmeamua na nyinyi Kujiunga naye!

Siasa za namna hii sio healthy kwa ustawi wa Taifa...

huu uzi sio wakuendelezea vata vya masalia vilivyoshindwa, wanaomuunga mkono kagame huku ni watumwa wa kagame kuja kujaribu kumwosha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…