Nakubaliana na wewe kwamba maamuzi ya vita siku zote hufanywa na mamlaka za juu. Na pengine wananchi hatuna namana ya kupinga hilo. Lakini tuna nafasi ya kusema na uongozi wetu ili upunguze huo uwezekano wa nchi kuingia vitani. Bado hali yetu ya kiuchumi ni ngumu sana, hatustahili hata kuiota hiyo vita. kama tutaruhusu hizi chokochoko za maneno ziendelee tutaishia kupigana. Ndiyo ilivyokuwa kati ya Nyerere na Idd Amini, naona sasa inataka kutokea hivyohivyo na Rwanda. Wakati sisi tupo busy kupigana na kila jirani yetu wenzetu wa Kenya wanazidi kujenga uchumi imara. Kabla ya Vita na Idd Amini Tanzania ilikuwa ndiyo nchi imara kiuchumi AFrica Mashariki, lakini baada ya ile Vita tulishuka ghafla na kuanza kujishindwa kabisa. Tunataka tuwe wa mwisho kiuchumi katika Africa mashariki? Hatutaki vita sisi.
Ninaamini ningekuwa mimi, ningempigia simu Kagame kumuuliza kwamba nimesikia kwenye vyombo vya habari kwamba ananisema vibaya. kwani ushauri wangu ulikuwa na ubaya gani? Kama hakuupenda ushauri wangu basi namwomba radhi na ninaomba yaishe. Kwani JK angesema hivyo ingekuwaje? Si mazungumzo ya kwenye simu tu?K
ama Kagame angemjibu hovyo, bado JK angekuwa na nafasi ya kuwasiliana na kiongozi mwingine wa Africa kumtaka azungumze na Kagame na kumweleza nia yake ambayo ilikuwa imelenga kumaliza mgogoro na kwamba yeye JK hakujua kama wazo lake hilo lingemuumiza Kagame. Hivi ukisema hivyo unakuwa umeshuka thamani kiasi gani? Kama yeye JK anaamini katika mazungumzo na anamtaka Kagame ashuke na kuzungumza na waasi wake, ni kwa vipi yeye JK asiwe tayari kuzungumza na Kagame ambaye hawajawahi kuwa na ugomvi naye?
Kwahakika mimi bado naona JK ana nafasi ya kumuomba mwenzake kagame ili wayamalize kwa amani badala ya hii hali inayoendelea sasa ambayo inatishia usalama wa nchi hizi mbili. Tayari tuna uadui na Malawi, hatuhitaji kuwa na uadui na Rwanda tena. Hatujiulizi ni kwanini sisi tu ndiyo tunakuwa na maadui kila upande?