ni siku nyigi sana sijaingia humu kuchangia ila leo naomba niseme haya mapema hii,
kwanza wanajukwaa wengi tunakosa hekima sana, nashangaa kuon awatu wana mzodoa mdada wa watu ili hali kasema analokutana nalo. Jiulize hivi wewe unayemkejeli je ndugu zao wote wameolewa?? je wameolewa na wanaume wa kweli?? na je wanao nao wameolew?? je wameolewa na wanaume wa kweli?? mkeo uliyemuoa umemuoa kwasababu u mwanaume wa kweli ana just kwasababu mkeo ama gf wako hakuwa na option nyingine?? nashangaa sana kuona wengine mnasema vby tena ni wanaume ilihali hawajijui kama ni wao wana semwa hapa ama la. Yumkini wewe unasema kadoda ndiye uliye mtongoza na akagundua kwamba umri wako ni mdogo kuliko wake.acheni kejeli na heshimuni hisia za wenzenu, pia pendeni kufanyika msaada kwa mwingine kuliko kufanyika husuda.
kwako dada mzuri mtoa mada, as i can tell, kwa umri wako pia wapo wanaume ambao watakufaa zaid kuliko hawa under age unao kumbana nao. sitaki kuamini kwamba wanaume wote above 35 ni married na sitaki kuamini kwamba wote above 35 hakuna ambaye hatafuti mwenza. nafikiri utofauti upo kwenye mawindo tu mnayopitia, like swala hula nyasi fupi na hivyo hufanya simba awinde kwenye nyasi fupi kwani anajua chances za kukutana na swla ni kubwa.
angalia maeneo ambayo wewe unawapatia hao unaowasema je ni vyuoni, ama kazini, bar, kwenye gari, mitandaoni ama nyumba za ibada?? kisha angalia maeneo hayo wengi wa dwellers humo ni watu gani?? huenda wewe ni mtu wa kwenda bills sana sasa huko wategemea ukakutane na mtu kama
Mr Rocky ama
Dark City?? ama wewe ni mtu wa mitandaoni zaid wategemea huko ukutane na wanaume wepi zaid ya akina
Mentor,
mzabzab et al??( sorry hapa namaanisha kiumri na ni mfano tu)
hivyo tathmini hayo kwanza na sikushauri kwa umri huo umdate mwanaume ambaye ni -2yrs kwako. atakusumbua period manake ndoa sio mchezo wa matusi tu ni zaid ya hapo. na hao wa 30 ni wanaume wazuri but ni wazuri kwa wa rika lao and not kwa wale waliowazidi umri.