GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Watu ni mtaji mkubwa sana katika kuleta mabadiliko yo yote yale ya kijamii.
Haijalishi watu wako na utayari kiasi gani, pasipo kiongozi wa "kulianzisha", matamanio yao yatasalia ndotoni.
Wakati mwingine, si lazima watu wajue kuwa wanao uhitaji, lakini itamlamzimu kiongozi kujua uhitaji wa watu wake, kutafuta ufumbuzi na kuwashawishi waukubali.
Nilishangazwa na nilichokutana nacho hivi karibuni.
Nilikuwa nikisafiri kwa gari la abiria kwenda mkoa fulani. Nilianza safari saa kumi na mbili Asubuhi.
Saa moja Asubuhi, tulifaulishiwa kwenye gari jingine kwa sababu nililokata tiketi halikuwa likifika nilikokuwa nikienda. Hapo ndipo kimbembe cha changamoto kilipoanza.
Tulikaa pale kusubiria hilo gari tulilofaulishiwa lijaze abiria ndipo liondoke. Tulipiga moyo konde hadi lilipojaza abiria, kwenye saa mbili Asubuhi. Lakini hata baada ya kujaza abiria, liliendeleq kusubiria kwa ajili ya kupakia watakaosimama.
Abiria walilalamika sana, lakini si konda wala dereva aliyewasikiliza. Badala yake, walikuwa wakiwajibu kwa kejeli.
Kipindi chote hicho, mimi nilikuwa kimya, nikijisomea zangu kama asiye na haraka japo nilitamani kufika mapema niendako.
Kwa kawaida, mimi si "muongeaji". Huwa nazungumza pale ninapoamua.
Ilipofika saa tatu Asubuhi, niliamua kuuvunja ukimya. Nilinyanyuka nikimfokea dereva na konda, nikiwataka wanirudishie nauli yangu nikapande gari jingine.
Lengo langu halikuwa kuwahamasisha abiria wenzangu, lakini hawakuacha kuhamasika.
Nilipomfikia konda, nilijikuta namkwida shati ili anirudishie hela yangu. Abiria wenzangu nao wakawa kama wamempata kiongozi. Baadhi walianza kushuka, kwamba wameghairi kusafiri na hilo gari hivyo warudishiwe nauli, huku wengine wakiwa wamenyanyuka na kuja kusimama kando yangu wakinisaidia kufoka, na wakiwa kama vile wanasubiria konda ajibu kwa fujo ili wamfanyie "fujo" itakayomstahili. Eti walikuwa wanasubiri konda ajibu kwa shari ili wampige😀
Kuona hali hiyo, dereva na konda walijishusha, na kuamua kuondoa gari.
Lilipotufukisha stendi, tulishuka na mimi nikakata tiketi ya gari jingine kwa ajili ya kunifikisha kituo cha mwisho. Hapo napo kukawepo mchezo unaofanana na niliokutana nao kituo tulichotoka.
Nilikatiwa tiketi ya mabasi ya Kampuni fulani, na nikaambiwa gari lingekuja hapo stendi baada ya muda mfupi.
Lakini masaa matatu baadaye, bado nilikuwa nipo hapo stendi. Kulikuwa na abiria kadhaa ambao nao walikuwa wamekata tiketi kwenye hiyo Kampuni, na walikuwa wanaenda uelekeo mmoja pamoja nami. Cha ajabu, magari kadhaa ya hiyo Kampuni yalipita hapo, lakini hatukuruhusiwa kupanda, ingawa yalikuwa yakielekea nilikokuwa nikienda.
Nililazimika kufanya kama nilivyofanya Asubuhi. Nilimfuata wakala kwa ukali, na kumwamuru anirudishie nauli yangu. Abiria niliokuwa nikisubiri nao usafiri, hawakubaki nyuma. Walipaza sauti zaidi baada ya kumpata "kiongozi"
Kelele zetu zilizaa matunda. Tuliondoka ndani ya nusu saa, baada ya kusubiria kwa zaidi ya masaa matatu.
Kama tungeendelea kukaa kimya, "tungeshinda" pale stendi.
Kuwa "aggressive" wakati mwingine kunasiadia.
Kiongozi anahitajika kila mahali.
Simba wanaye kiongozi. Hata ng'ombe wanaye kiongozi wao.
Kunapotokea hali ya hatari, mnyama kiongozi hupita mbele ya wenzake kwa ajili ya kukabiliana na adaui. Akishindwa kuwa mbele kipindi cha hatari, huipoteza nafasi ya uongozi.
Watu hawahitaji kuambiwa jinsi ya kufanya, bali wanataka kuona ufanyavyo. Ukianzisha, watakuunga mkono kwa ajili ya kumalizia ulichokianzisha, hasa kama kina "manufaa" kwao.
Kwa kuhitimisha, kiongozi anapaswa kuwa na ufahamu wa kinachohitajika, na ujasiri wa kuchukua hatua sahihi itakayowaamsha "wafuasi" wake.
Ikiwa una sifa hizo, basi wewe ni kiongozi. Usiwaangushe watu wako!