Kwa muda mrefu sana nimeona Kagasheki na mchungaji Msigwa wamekuwa mstari wa mbele kupiga vita ujangili wa Tembo unaofanywa sehemu mbalimbali za nchi wanasiasa na vigogo wengine wakihusishwa. Nimesikitishwa sana kuona mkuu wa kaya hajachukua hatua zozote stahiki kupambana na janga hili. Ikumbukwe kuwa, utalii ndo eneo pekee tunalopata fedha ya kigeni maana madini yote yana wenyewe.
Mheshimiwa rais, naomba uwaunge mkono wapambanaji hawa wa ujangili. Tafadhali ingilia kati, paza saiti yako na vitendo vifuate. kama ulivyofanya kwa wahamiaji haramu natamani niuone tena mkono wako.
Mheshimiwa rais, naomba uwaunge mkono wapambanaji hawa wa ujangili. Tafadhali ingilia kati, paza saiti yako na vitendo vifuate. kama ulivyofanya kwa wahamiaji haramu natamani niuone tena mkono wako.