Kila Graduate anatakiwa kusema "NO" Wakati Huu

Kila Graduate anatakiwa kusema "NO" Wakati Huu

Gwamanga

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2021
Posts
223
Reaction score
434
Graduate Usipokuwa na nguvu, uwezo wa kusema NO kwa herufi kubwa Kitaa, Mafanikio utaishia kuyasikia kwenye Televisheni, Binafsi Mimi ni Graduate kutoka chuo kikuu cha Dodoma nina miaka miwili toka nimehitimu mafunzo yangu. Kimsingi kanuni ya kuishi mtaani kwa uzoefu wangu inahitaji kusema NO mara nyingi zaidi ya kusema YES Fatilia visa hivi na mikasa unionee neno NO lilivyo mhimu kwa Graduate yoyote yule ili kuyaelekea mafanikio yake baada ya chuo, Hasa kwa wale waliojiajiri kwenye Biashara.

Imagine mimi ninapofanyia biashara kuna mchizi mmoja mlevi alitaka kunichukulia poa kumbe hakujua nami nilikuwa namlia target, alianza kujifanya rafiki yangu, mara vichomi vikaanza leo Jero, kesho buku, nikasema huyu atanizoea siku ya siku akaja anataka anipige mzinga wa buku Tano, Aaaaaaah nikamkaushia Tangu hapo Ameanza kuniheshimu na kuithamini Biashara yangu, Graduate ukicheka na nyani utavuna mabua, kumbuka hata mtaani wale washikaji ambao huwahi kumaliza Bumu mapema na kuanza kuomba Buku za karibu huku pia wapo.

Imagine Mtu anakuletea vyeti vyake vyote ili umpe mkopo, then mnakubaliana harafu siku ya rejesho hatokei na huna cha kumfanya kwani mlikopesheana kishikaji hii inatukutana Graduate wengi maana unakuta unataka uishi kulingana na status yako wakati vyanzo hamna au vikiwepo havitemi ipasavyo hivyo mkopaji akija na riba ya asilimia 30 unawaka tamaa.

Imagine wanawake wakijuwa wewe ni graduate pia unamiliki biashara wanavyojisogeza mwanangu wakati naanza biashara hii kitu ilinitesa sana nusra nifunge chimbo langu kwa kula faida mpaka mtaji, nilibadilika mpaka nilipokalishwa chini na wazazi wangu, Graduate kuwa na kiasi la sivyo utabebesha watoto wa watu mimba, mtaani utaoa bila kutarajia au utaukwaa umeme, Mitaani pisi kali pia zipo na zinafelisha sana kwenye biashara utakuwa kama mimi kula faida na mtaji, Jichunge "Pisi Kali kama Fisi kali zinakula mpaka mifupa".

Imagine ukifungua chimbo la biashara hao waganga wakienyeji watakavyojisogeza kwako mimi kwenye chimbo langu aiseeee, kirrruuuuuuuh walikuja kama waganga sita hivi kwa mda tofauti na sitori zao, mara mvuto, chuma ulete, nyota na Bahati, Graduate MTAA una mambo mengi Usishangae kassimu kuwa Mganga, Jichunge.

Imagine mpaka Mtoto wa jirani yako utamsikia anasema Digrii za siku hizi kama matako kila mtu anayo, Mtoto wa Dada yako utamsikia anasema Mimi siendi shule Ajira zenyewe hakuna kwani waliosoma wapo wapi situnakula wote Mtori? Inauma Mpaka Baba na Mama utawasikia wanasema Janeth kamwite yule Ngo'mbe Aje anywe chai, Graduate sisi mtaani yanatukuta mengi, Shati ninalolivaa mpaka sasa limeshapauka kama la ngoswe penzi kitovu cha uzembe kwani ni Mwaka wa pili sijalibadili Any Way Kuwa na Nguvu ya kusema NO mimi si kama Wanichukuliavyo nitachukua hatua na kuyaelekea mafanikio anza kubadilika.

Imagine kaka zenu huku tunaitwa Wakusoma, Madigrii na Wasomi uchwara, wanaotuita ni wale tunaobeba wote zege wakati tunatumika kama saidia fundi, ni wale washikaji zetu tuliowaacha darasa la saba kwa kuwaita majina ya vilaza, ngumbalo au feliya, Hao ndio wanaotuita majina hayo tukiwa tunabeba mizigo masokoni au tukiwa tunapakia mifuko ya cement kwenye magari makubwa Ama kweli kutangulia sio kufika Tusipokuwa na uwezo wa kusema NO, No itabaki kuwa No.

UBALIKIWE MTU WA MUNGU.
 
Akili yako ndio ilikua aiko sawa saiv ndio inaanza kupandisha oil kidogo!!!!
 
Big up sana mwanangu, geaduate mwenzangu!
Kijana mwenzio pia napambana haswaaaa!!
 
Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Back
Top Bottom