Kila kinachotokea katika maisha yako kina sababu ya kutokea

Kila kinachotokea katika maisha yako kina sababu ya kutokea

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,438
Kijiko alizaliwa mjini, kijana msafi sana kwa muonekano. Alimaliza masomo na kupata ajira, alifanikiwa kufungua na biashara ya maduka ya chakula. Kijiko hakua na shida ya pesa ya kula ingawa hakua tajiri.

Alikua kwenye mahusioani na binti mmoja mwajiriwa katika ofisi ya serikali. Binti alipomfahamisha Kijiko habari za uja uzito, Kijiko alimfahamisha kuwa atakua tayari kulea mtoto lakini hayuko tayari kuishi kuoa. Yule binti alimpenda sana Kijiko lakini ilimbidi akubali matokeo.

Kijiko alikutana na binti mwingine, walianza mapenzi, sababu ya Kijiko kutomuoa huyu alikuja kugundua alikua na mtoto wa miaka minne, Kizito alisema haoi mtumba.

Kijiko alimpata binti amemaliza form six, binti alikua mrembo sana, huyu dada aliolewa harusi kubwa na Kijiko. Baada ya miaka mitano ya ndoa bila ya mtoto waliamua kumuachia Mungu maisha ya ndoa yaendelee.

Kijiko aligundulika ana maradhi ya saratani. Aliugua na tiba ilimaliza pesa zake za akiba. Safari za kwenda India kwenye matibabu. Ikifika wakati ilibidi wauze nyumba ya mwisho ili wagharamie safari. Mke wa Kijiko aligoma kabisa, alimwambia Kijiko live “ukifa utaniacha na nini”?

Mama wa mtoto wa kwanza wa Kijiko aligharamia safari baada ya kuuza alivyonavyo kumtibu baba wa mtoto wake. Kijiko alitamka kabla ya kufariki, alijuta kumuacha mke mwema kwa sababu za uja a.

Kila kitu katika maisha kinakutokea kwa sababu.
 
Ni kweli na majuto huja baadae ila sio lazima itokee hivyo

Unaweza pia kumuoa huyo mwenye mtoto na baadae akawa mwiba, akawa anamwona mwanae (uliyemkuta naye) ni bora kuliko watoto uliozaa nae, na akawa anamjali mwanae na kuwanyanyasa watoto wako ilihali aliyezaa naye mwanzoni hata hajui alipo

Maisha hayana formula na hayako static

Muhimu kuliko yote ni kumwomba Mungu akupe Mke / Mume sahihi.
 
Ni kweli na majuto huja baadae ila sio lazima itokee hivyo

Unaweza pia kumuoa huyo mwenye mtoto na baadae akawa mwiba, akawa anamwona mwanae (uliyemkuta naye) ni bora kuliko watoto uliozaa nao, na akawa anamjali mwanae na kuwanyanyasa watoto wako ilihali aliyezaa Nate mwanzoni hata hajui alipo

Maisha hayana formula na hayako static

Muhimu kuliko yote ni kumwomba Mungu akupe Mke / Mume sahihi.
Kama kila anae dondosha DNA yake akibeba mzigo wake hatukua ná matatizo kama haya.
 
Kijiko alizaliwa mjini, kijana msafi sana kwa muonekano. Alimaliza masomo na kupata ajira, alifanikiwa kufungua na biashara ya maduka ya chakula. Kijiko hakua na shida ya pesa ya kula ingawa hakua tajiri.

Alikua kwenye mahusioani na binti mmoja mwakiriwa katika ofisi ya serikali. Binti alipomfahamisha Kijiko habari za uja uzito, Kijiko alimfahamisha kuwa atakua tayari kulea mtoto lakini hayuko tayari kuishi kuoa. Yule binti alimpenda sana Kijiko lakini ilimbidi akubali matokeo.

Kijiko alikutana na binti mwingine, walianza mapenzi, sababu ya Kijiko kutomuoa huyu alikuja kugundua alikua na mtoto wa miaka minne, Kizito alisema haoi mtumba.

Kijiko alimpata binti amemaliza form six, binti alikua mrembo sana, huyu dada aliolewa harusi kubwa na Kijiko. Baada ya miaka mitano ya ndoa bila ya mtoto waliamua kumuachia Mungu maisha ya ndoa yaendelee.

Kijiko aligundulika ana maradhi ya saratani. Aliugua na tiba ilimaliza pesa zake za akiba. Safari za kwenda India kwenye matibabu. Ikifika wakati ilibidi wauze nyumba ya mwisho ili wagharamie safari. Mke wa Kijiko aligoma kabisa, alimwambia Kijiko live “ukimfahamisha utaniacha na nini”?

Mama wa mtoto wa kwanza wa Kijiko aligharamia safari baada ya kuuza alivyonavyo kumtibu baba wa mtoto wake. Kijiko alitamka kabla ya kufariki, alijuta kumuacha mke mwema kwa sababu za uja a.

Kila kitu katika maisha kinakutokea kwa sababu.
Kwahio kwamba kumtosa single maza ndio kumuacha mke mwema? 😂😂😂
 
Back
Top Bottom