Kila kitu kilishapangwa

Hii inaitwa dejavu yaani unayoyapitia yalishaandikwa na huwezi yabadilisha.
Kuna wakati yanaweza kukutokea kama ndoto hivi. Kidini tunaiita ilham.
Ukiamini juu ya hili maisha hayatakupa stress sana.
Utapambana ukikosa utasema si risk yangu.
Sasa wale wazee wa kufosi ndio wataenda mpaka kwa sangoma trying to fix it. Itawork kwa muda tu lakini kwakua hukuandikiwa hivyo itarudi kwenye hali yake ya kawaida.
 
Mmmhh na sio qadar ?
 
Doctor hapa penyewe umetulisha matango pori. Inawezekana vipi upange hayo yote wakati unakua hauna ufahamu wowote?
 
Hakuna angependa atengeneze masikini.
Mafanikio ni consistency ya jumla maamumizi madogomadogo...yaliyofanyika vizuri...ndio hupelekea mafanikio


Vilevile.....umasikini hivyohivyo....ukitaka kuamini

Fuatilia mataji walivyo wengi kuna tabia flan wanashea


Vilevile hata kwa masikini hivyohivyo
 
I know najua mimi huwa na Acces hizo energy kwa kuwaza kuProject concious na Meditation throgh different mudras Na nimefanya mambo mengi kuwezekana ikiwa pamoja na kupata information ya mambo yaliyoshindikana kabisa..

So nakuelewa sana ukisema hivyo kwa sababu Proof ninayo hata mimi..
Kuna Power na Energy kubwa sana ambayo binadamu tukiijua kuitumia kwa only 50% Tutakuwa watu tusioshikika hata robo
 
Ni story ndefu mkuu!
Not According to science
 
safuher

Hiyo ni qadar Sheikh, kwa lugha ambayo ni wengi wataielewa inaitwa predestination.

Hili somo ni gumu sana Sheikh.

Na nina kauchovu fulani, ngoja kakiondoka kidogo inshaallah nitachangia ndugu yangu.

Ila kitu ambacho watu tunabidi tufahamu ni kwamba Mungu hakuchagulii maisha yako yawe hivi ama vile. Bali Mungu yeye alishaona maisha yako yatakuwaje kuanzia A mpaka Z. Ameshaona machaguo yetu yatakuwaje. Kipi tutachagua na tukichagua mustakabali wetu utakuwaje. Kipi hatutokichagua na mustakabali wetu wa maisha utakuwaje anafahamu. Yeye hivyo ameshaviona.

Mathalani; ameshakuandikia kwenye kitabu kuwa mtu A atamuua mwenzake mtu B kwa kumchoma na kisu. Suala si kwamba Mungu amekuandikia alishapanga umuue mwenzako kwa kumchoma kisu, hapana! Bali yeye alishaona na kujua kuwa mtu A atamuua mtu B kwa kumchoma na kisu.

Kwa lugha nyepesi ya kisasa tutasema Mungu yupo nje ya muda. Sisi viumbe wake tumo ndani ya muda. Na muda ni matukio.

Hivyo matukio yetu yoote na machaguo yetu Mungu alishayaona. Ili kuonyesha uungu wake kitabu kimeshatangulia na maisha yetu yote ameshayaona hivyo kila kitu kuhusu sisi kilishaandikwa kutokana na machaguo yetu ya kwetu sisi wenyewe. Elimu ya Mungu ni kubwa sana haya mambo ni mazito mno!
 
Sasa mkuu ,mbona binadamu asilimia zote wana mipango mizuri ,ila asilimia kubwa mambo yanaenda tofauti?
Mambo unayopanga sasa ni tofauti na mambo uliyoyapanga kabla hujaja duniani..
Kinachozungumziwa ni Kuwa mipango yote mpaka hatima yako..
Tayari ulikwisha ipange kabla ya kuja duniani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…