Kila kukicha watu wanaibiwa akiba ya pesa yao na hawa scammers kama Qnet, Scatec, eKyalinda, Mr.Kuku, Global motion Alliance nk

Kila kukicha watu wanaibiwa akiba ya pesa yao na hawa scammers kama Qnet, Scatec, eKyalinda, Mr.Kuku, Global motion Alliance nk

Kuna jamaa wanaitwa earnjet, nao walipiga pesa wakasepa
 
Na wengi wanaondokeza hayo mambo ni wanawake wakishapigwa ndo wanashtuka
 
Watu wanapigwa kutokana na ujinga wao wenyewe
Nchi hii inawajinga wengi sana sana

Ova
 
Ila nadhani hivi vyombo vya habari credible ndio vinaingiza watu mkenge zaidi angali Mr. Kuku na Kalynda wote wanatumia zile channels unazoziamini kukupiga.

Najua wanapata matangazo lakini pia wao wanajukumu la kufanya due diligence. Jamii inaviamini sana hivi vyombo.
 
Tatizo nao hawana uwezo wa kiakili kuweza kufanya critical thinking and analysis.
 
Mtoa mada umeileta hii hoja ki masihara lakini huo ndio ukweli mtupu, mie nafikiri elimu yetu sio nzuri tena kwa muda mrefu sasa. Mie naishi huku ughaibuni, nilishangaa sana siku moja jamaa rafiki yangu sana ambae nimesoma nae form 1 - 4 ila yeye alikua ana akili sana na tulimuita genius. Yeye yupo bongo na muajiriwa wa shirika kubwa hapo dar la umma. Siku moja kaniletea message ndeeefu eti anaulizia vipi ajiunge na hao Qnet eti anataka aweke kama 2m tshs atapata double ya hio pesa na ushee, na akakazia watu wengi sana ofisini kwao wamepiga pesa kupitia hao jamaa. Nilimuonya tu asithubutu ataliwa vihela vyake hivyo vya akiba vyote.Sijui kama alinisikia ila nilichogundua ambacho na wewe mtoa mada umekiongea Watanzania wengi ni wapumbavu na wanaamini kupata utajiri kupitia short cut...wanasahau kua hakuna Free Lunch popote pale duniani. Na hizi dini na hawa manabii wa uongo akina Masanja ndio janga la kitaifa kabisa. Yaani waseme wafungue mipaka leo ya East Afrika wabongo ndio watakuwa watumwa maana wenzetu Kenya, Uganda, rwanda na wengineo wametuzidi kimaarifa na akili. Wabongo wanaendekeza sana ujinga ujinga na kuamini upumbavu mwingi wa hawa manabii wa uongo.
 
Wenye kujua, kumezuka matangazo mengi kuhusu mikopo kwa njia ya simu. Je, wenye kujua hii mikopo ni kweli au ni utapeli tu?
 
Jiongeze

Ukiitwa kwenye fursa wewe ndo fursa

Ukiomba mkopo ukaambiwa tuma hela ya fomu jua unaliwa

Ukiomba mkopo ukaambiwa toa kiasi fulani ndo upate jua unaliwa

Afu wajinga mmekuwa wengi
 
Mkopo wa kweli labda wale branch tu ndio wanatoa, nyingine sina hakika
 
Ahsante lakini serikari inayaona yote ila imekaa kimya wengine wanatumia majina ya wakubwa
 
Wenye kujua, kumezuka matangazo mengi kuhusu mikopo kwa njia ya simu. Je, wenye kujua hii mikopo ni kweli au ni utapeli tu?
Yes,kuna Branch,Umoja loan wote wanakopesha,ila umoja loan ni service charge yap ni kubwa sana, almost 35%
 
Back
Top Bottom